KAMA hakuwahi
kutoa sadaka, huu ndiyo muda wake! Staa wa sinema za Kibongo, Aunt
Ezekiel Grayson anadaiwa kukinukisha nyumbani kwa Wema Isaac Sepetu
baada ya kunusurika kufumaniwa na mume wa mtu, Moses Peter Iyobo a.k.a
Moze Iyobo ambaye ni densa wa Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Habari zisizokuwa na shaka zinadai kwamba tukio hilo lilijiri
Jumapili iliyopita nyumbani kwa Wema, Kijitonyama, Dar ambapo Aunt
alisababisha tafrani iliyosababishwa na mke wa mwanaume huyo aliyetajwa
kwa jina la Mwengi Ally.
Kwa mujibu wa mashuhuda wetu waliokuwa wakizungumza kwa kupokezana,
Mwengi alidai kwamba Aunt amekuwa akitembea na mumewe huyo hivyo
timbwili lilianzia nyumbani kwa Aunt, Mwananyamala A jijini Dar.
Ilidaiwa kwamba, huku Aunt akiwa hajui hili wala lile, ghafla
waliibuka wasichana saba na kumuanzishia mwigizaji huyo.Mashuhuda hao
walidadavua kwamba katika kujinusuru na kipigo ambacho alihisi akiwa
peke yake, angeumizwa Aunt alikimbilia nyumbani kwa shoga yake, Wema.
Ilidaiwa kwamba wasichana hao hawakuishia hapo kwani walimkimbiza
Aunt hadi wakamuona akiingia kwa Wema ambapo walipofika getini
walikutana na meneja wa msanii wa Bongo Fleva, aitwaye Mirrow, Petit Man
ambaye walimuomba amtoe Aunt ili wamshikishe adabu ajifunze kukaa mbali
na waume za watu.
Ilisemekana kwamba katika tafrani hiyo getini, Wema alitoka na
msichana wake aitwaye Careen lakini Aunt hakutoka ambapo waliwaambia
wasichana hao kuwa Aunt hawezi kutoka na isitoshe wa kulaumiwa ni Moze
Iyobo kwani yeye ndiye anayedaiwa kumtongoza Aunt na kuanza kuchati naye
hadi mkewe akanasa meseji zao za mapenzi.
Baada ya kujazwa data hizo, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Mwengi
ili kupata maelezo ya kina kuhusiana na ishu hiyo ambapo alikiri kwenda
kwa Aunt na Wema lakini hakufanikiwa kumpata Aunt kwani kama
angemkamata, maafa yangetokea.Mwengi alisema kuwa siku ya tukio aliitwa
na Aunt maeneo ya Mlimani City, Dar na akamwambia aende na mtoto
akamfanyie shopping.
Alisema baada ya kuambiwa hivyo hakuwa na hiyana kwani alijua kuwa ni
kama mama yake mkubwa na shoga wa mpenzi wa baba yake mkubwa ambaye ni
Diamond, kumbe nyuma ya pazia kulikuwa kuna kitu kingine
kimejificha.“Niliporudi nyumbani, mume wangu aliniambia nimpige picha
kwa kutumia simu yake, nilipoifungua ndipo ikaingia meseji kutoka kwa
Aunt.
“Nilipoisoma ile meseji nikagundua kuwa walianza kuchati muda mrefu
kuhusu mapenzi yao, ndipo nikakusanya jeshi langu na kumfuata nyumbani
kwake nikamshikishe adabu, amshukuru Wema kumficha maana sipati picha
kwa jambo ambalo lingetokea. Ingekuwa mwisho wake wa kupora waume za
watu,” alisema Mwengi.
Alipotafutwa Aunt na kuulizwa juu ya sakata hilo, alijibu kwa kifupi:
“Sina muda mchafu wa kuongea halafu nimelala, kwa sasa niache
nipumzike.”
Hizi ndio sehemu 12 zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, Bonyeza Hapa chini== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO CHAFU YA AGNESS MASOGANGE== >