Habari Kali
Loading...

WASTARA: NAMPA BOND NAFASI YA KUNIOA!

WASTARA Juma Issa Abeid amekiri kuzidiwa na hisia za kuwa na mwenza kutokana na ukweli kwamba damu yake bado changa, hivyo suala la kuolewa halikwepeki huku akimpa nafasi kubwa msanii mwenzake, Bond Bin Sinan endapo atakidhi vigezo na masharti.

Wastara Juma Issa Abeid akiwa na Bond.
Akifungulia ‘koki’ ya maneno mbele ya paparazi wetu kwa njia ya simu mwanzoni mwa wiki hii, Wastara ambaye kwa sasa yuko bize kusaka ubunge nyumbani kwao Morogoro Vijijini, alisema hawezi kudanganya kwamba ataishi bila kuwa na mume kwa kuwa amekamilika kimaumbile.
“Mimi ni mwanamke, nimekamilika tena nakula na ninashiba. Damu bado changa. Nikisema siwezi kuolewa, nitakuwa nadanganya. Nimekaa muda mrefu kwa sababu kila mwanaume anayenihitaji ananitamani tu.
“Bond namuona ni mwelewa. Lakini nimempa sharti la kutonigusa hadi siku ya ndoa. Kama atakidhi na hayo mengine ambayo ni siri yetu, niko tayari kuolewa naye,” alisema Wastara.

ESTER AZIDI KUTESWA NA TUMBO LA BIA!

KUNENEPEANA! Kuvimbiana na kuongezeka kwa ukubwa wa tumbo kunazidi kumpa wakati mgumu msanii ‘anayechungulia’ katika gemu la uigizaji, Ester Kiama kufuatia kusongwa na madai kuwa ‘amebugia kijusi’ (mjamzito) huku Kulwa Kikumba ‘Dude’ akidaiwa kuwa baba kijacho.

Msanii ‘anayechungulia’ katika gemu la uigizaji, Ester Kiama.
Akikutanisha ‘lips’ na paparazi wetu hivi karibuni, Ester alisema licha ya kuwaeleza watu kwamba ukubwa wa tumbo lake unatokana na utumiaji wa vinywaji vyenye ngano (kama bia) na uvivu wa kufanya mazoezi, lakini wao wamekuwa wakimkomalia kuwa ni mimba.
“Watu wengi wanasema nina mimba. Wengine wanakwenda mbele zaidi wakinipongeza kwa kumbebea mimba ya Dude. Yaani napata wakati mgumu,” alisema Ester.

BAADA YA KUACHANA NA MUMEWE, ROSE NDAUKA APEWA ONYO NA FAMILIA!

Staa wa filamu Bongo, Rose Ndauka.

STAA wa filamu Bongo, Rose Ndauka hivi karibuni amewekwa chini na familia yake na kupewa onyo kuhusu wanaume pamoja na maadili.
Kwa mujibu wa chanzo, Rose aliambiwa maneno mengi na familia yake ikimtaka ajirekebishe na haswa ajitume zaidi katika kazi zake anazofanya.
“Familia yake imeamua kumuweka chini na kumwambia mengi kuhusu maisha haswa ikimtaka ajirekebishe tabia yake kwa ujumla,” kilisema chanzo.
Rose alipotafutwa kuweka wazi juu ya hili, alifunguka;
“Kila familia ina utaratibu wake, kwahiyo mimi kuwekwa na familia na kupewa onyo wala siyo suala la ajabu.”

BAADA YA MSANII WOLPER KUKIRI YEYE NI FREEMASON, WENYEWE FREEMASON WAMJIA JUU!

KATIKA toleo lililopita la gazeti hili, ukurasa wake wa pili kulikuwa na habari yenye kichwa; Wolper: Mimi ni Freemason kwa muda mrefu sasa.
Sasa, baada ya habari ile kutoka, kuna madai kwamba, wenyewe Freemason wameingiwa na wasiwasi juu ya kauli ile lakini chanzo kikitoa kauli mbili tofauti.
Chanzo chetu kililiambia gazeti hili kuwa, baadhi ya wanachama wa taasisi hiyo wameshtushwa na maneno ya Wolper kama yana ukweli wowote.
“Yaani kule Freemason, baachi ya wanachama wanasema Wolper alikurupuka kusema vile. Lakini hawajasem alikurupuka kwa sababu si Freemason au hakutakiwa kukiri,” kilisema chanzo.
Jumatatu iliyopita, Amani lilimpigia simu mwanachama mmoja wa taasisi hiyo ambaye yupo ngazi ya uongozi na kuzungumza naye kuhusu Wolper lakini alikata simu bila kutoa majibu.
Wolper mwenyewe alipotafutwa kwa simu na kuulizwa kama anajua ameibua kizaazaa hicho, alijibu ndivyo sivyo:
“Mimi niko mbali na mji jamani. Nina mishemishe f’lani hivi. Unajua nataka kutoa filamu. Nitakuja siku moja hapo Global kuomba udhamini wa filamu hiyo.”
Staa wa filamu Bongo, Jackline Wolper.
Sasa, baada ya habari ile kutoka, kuna madai kwamba, wenyewe Freemason wameingiwa na wasiwasi juu ya kauli ile lakini chanzo kikitoa kauli mbili tofauti.
Chanzo chetu kililiambia gazeti hili kuwa, baadhi ya wanachama wa taasisi hiyo wameshtushwa na maneno ya Wolper kama yana ukweli wowote.
“Yaani kule Freemason, baachi ya wanachama wanasema Wolper alikurupuka kusema vile. Lakini hawajasem alikurupuka kwa sababu si Freemason au hakutakiwa kukiri,” kilisema chanzo.
Jumatatu iliyopita, Amani lilimpigia simu mwanachama  mmoja wa taasisi hiyo ambaye yupo ngazi ya uongozi na kuzungumza naye kuhusu Wolper lakini alikata simu bila kutoa majibu.
Wolper mwenyewe alipotafutwa kwa simu na kuulizwa kama anajua ameibua kizaazaa hicho, alijibu ndivyo sivyo:
“Mimi niko mbali na mji jamani. Nina mishemishe f’lani hivi. Unajua nataka kutoa filamu. Nitakuja siku moja hapo Global kuomba udhamini wa filamu hiyo.”

HUYU NDIYE MSANII WA BONGO ALIYEKIRI KUTESWA NA MAPENZI KWA SABABU YA UNENE WAKE!

Mtangazaji wa ITV / Radio One, Farhia Middle.
MTANGAZAJI wa ITV / Radio One, Farhia Middle amesema tangu aujue ulimwengu wa mapenzi hajawahi kukutana na mwanaume mwaminifu na kwamba kila mara amekuwa akilizwa na mapenzi jambo ambalo husababisha kujiona mwenye mkosi.
Akipiga stori na gazeti hili hivi karibuni, mtangazaji huyo alisema licha ya baadhi ya watu kumsifia kuwa ni mrembo kwa sura na umbo, lakini amekuwa akikutana na balaa la kuumizwa na mapenzi kwa kusalitiwa ama kunyanyaswa na wanaume.
“Yaani huwezi amini, wakati mwingine huwa najiuliza kwa nini mimi? Mbona kila mwanaume ninayempata sidumu naye. Kama siyo msaliti basi ni yule mwenye mfumo dume na hulka za kunyanyasa. Najiona kama nina mkosi,” alisema Farhia.

PICHA ZA ZISIZO NA MAADILI ZA MREMBO HUYU ZAMUUA BABA YAKE!


Loredana Chivu ni mwanamitindo nchini RomaniaBaba mmoja amejiua baada ya kuona picha za uchi zamwanawe wa kike katika jarida la Playboy nchini Romania.
Loredana Chivu alirarua ukurasa uliokuwa na picha yake akiwa 'amepos' katika jarida hilo la Playboy na punde babake alipogundua kuhusu picha hizo, alizongwa na mawazo na hata kumkana mwanawe.
Kwa mujibu wa mtandao wa Mirror, msichana huyo mwenye umbo la kuvutia alisema, '' babangu aliacha kuongea na mimi na kuonekana mwenye hasira sana''.

"alipogundua kuwa picha hizo zilikua zangu, alijitenga sana na kujaribu kunitenga na mimi''.
Nilidhani labda angesahau na sikudhani hata siku moja angejitoa uhai. Loredana Chivu anasema anajuta sana kwani babake hakuwahi kuongea naye baada ya kupata picha zake.
Mwanamitindo huyo Loredana Chivu mwenye mamia ya picha akiwa nusu uchi kwenye akaunti yake ya Instagram, alikuwa na uhusiano wa karibu sana na babake lakini alisema yote hayo yalibadilika baada ya babake kuona picha zake akiwa nusu uchi.
Alipokwenda kumtembelea babake miezi michache baadaye, baada ya kuamua kwamba kimya kilikuwa kimeendelea kwa muda mrefu sana, alishtuka sana kumpata babake akiwa amejitoa uhai
"nilipata akiwa na kamba shingoni akiwa ananing'inia chumbani''.

Loredana,anayeishi nchini Romania, anasema kuwa tangu kifo cha babake, amekuwa akiwaza na kuwazua kwamba aliamua kujiua kwa sababu ya mgogoro kati yetu na hasa kuhusu picha zangu zilizoziona kwenye jarida la Playboy.
''Najuta sana kwamba hakuwahi kupata muda wa kuzungumza na babangu kuhusu yaliyotokea''.

''Hakuwacha ujumbe wowote kabla ya kujitoa uhai, siku zote tulikuwa na uhusiano mzuri lakini yote yalibadilika baada ya baba kuona picha zangu nikiwa uchi. Bado inaniuma sana na singemtakia mtu yeyote kupatwa na kama yaliyonikuta''.


-BBC SWAHILI

MJUE MODEL MKALI MWENYE FOLLOWERS WENGI SANA HUKO INSTA

Anaitwa Kathy...kutoka CUBA




HIVI DADA ZETU MNAPOPIGA PICHA KAMA HIZI MNAKUA MNATAKA NINI??!! WATAZAME HAWA



 

 

UJAUZITO UMENIVURUGA SHEPU YANGU, TIWA SAVAGE

Mwanamuziki wa Nigeria,  Tiwa Savage.
Lagos Nigeria
MWANAMUZIKI Tiwa Savage wa Nigeria amelalamika kwamba ujauzito alio nao hivi sasa umevuruga shepu yake hasa kutokana tumbo kujitokeza.
Tiwa Savage akiwa na mumewe Tunji ‘Teebillz’ Balogun.
Mrembo huyo ambaye anategemea kumzalia mtoto  mumeweTunji ‘Teebillz’ Balogun, amesema kwenye akaunti yake ya Instagram kwamba pamoja na kufurahia hali hiyo, ujauzito una changamoto zake.
“Wakati wote unatamani uzae mtoto umwona na unakuwa unafurahi wakati anapojitingisha tumboni na unapofahamu kwamba sasa amelala.”Ni safari ya kufurahisha tangu ujauzito hadi mwisho wake,” aliandika.

HII NDIO KAULI YA SALAMA JABIR NA SOLO THANG KWENDA KWA MASHABIKI WA ALI KIBA NA DIAMOND!

SalamaUpinzani unaokuzwa na mashabiki kati ya Diamond Platnumz na Ali Kiba kwenye mitandao ya kijamii umepelekea Mastaa wa Tanzania kuanza kujitokeza hadharani na kuwaweka mashabiki hawa sawa kwa kuamini wamevuka mipaka kwenye ushabiki.
Mtangazaji wa TV show ya Mkasi Salama Jabir na msanii mkongwe bongoflevani Solo Thang ni miongoni mwa waliozipaza sauti zao June 30 2015.
Kupitia kwenye ukurasa wa twitter Salama Jabir aliandika ‘Wabongo tumekua wakosoaji mpaka wasanii wanajishtukia, hakuna “zuri kabisa” kwenye macho yetu… tuwaache wasanii wawe “Wasanii” nadhani!
.‘Jana tulikua tunaongea na wana job, Ali Kiba hakuwa mtu wa vioo vikali, yeye alikuwa anatoa audio kali na video ya Mwananchi kamaliza, zama zimebadilika mpaka anakwea pipa kwenda kutoa kideo kikaaali tushukuru, kapendeza, rangi nzuri! mengine tuyaache..’  kauli ya Salama Jabiri
.Upinzani huo ulioanzishwa na makundi yanayojiita (TeamAliKiba na TeamDiamond) yalimkwaza pia mkongwe wa Hip Hop Solo Thang na kuandika..’Ukiweka habari au picha au muziki wa msanii muyu mashabiki  wa yule wanakutukana!  kwanini? ? hii burudani tu isiwe uhasama, tujivunie sanaa yetu..’
solo 1
Solo Thang

ROSE MUHANDO AMWAGA MACHOZI BAADA YA KUFANYIWA HAYA!

Brighton Masalu ROSE Muhando, aliye mwimbaji Injili Bongo, amejikuta akimwaga machozi yaliyojaa uchungu huku akitumia kama dakika 45 kuelezea wazi mateso na manyanyaso ambayo anayapitia kwa sasa ikiwemo kuhusishwa na tuhuma za utapeli na ‘kubwia unga’, Risasi Jumamosi linakupa stori kamili!
Mwimbaji Injili Bongo, Rose Muhando.
ILIKUAJE?
Mwandishi wetu alimtafuta mwimbaji huyo juzi kwa njia ya simu kutoka mkoani Dodoma yaliko makazi yake lengo likiwa kujua maendeleo yake kikazi ndipo kukaibuka mapya mengi.Rose alianza kuporomosha lawama dhidi ya watu wanaomzushia mambo yasiyo ya kweli juu yake:

MSIKIE MWENYEWE
“Aah, mimi nipo tu (Dodoma) nimekaa kimya kwa sababu si mtu wa majibizano na malumbano, nimepakwa uchafu wa kila aina na kutukanwa huku wanaonitukana ni Wakristo wenzangu na mbaya zaidi hadi wachungaji wananisakama kwa maneno makali, nikaona kukaa kimya ni hekima.”

TUENDELEE
Rose alisema, alichukua uamuzi wa kuachana na dini yake ya zamani (Uislamu) na kujiunga na Ukristo kutokana na kuguswa na mafundisho yake baada ya kuhubiriwa upendo wa kweli lakini kwa sasa anakutana na maumivu na kusalitiwa huku wakisahau mema anayofanya kwa kutangaza Injili.

HUYU HAPA TENA!
“Wakristo wamenifundisha ugaidi na ukatili, ndugu zangu ni Waislamu, kila siku hawaachi kunisuta kutokana na matusi ninayotukanwa na Wakristo wenzangu, nakuwa sina cha kusema, kubisha nashindwa, kumkufuru Mungu nashindwa, nabaki kuugua moyoni kwa kiwango kisichotamkika.”

MATUSI YANAHUSU NINI HASA?
“Unakuta mtu amekualika kwenye tamasha. Kwa bahati mbaya ama kwa kusahau ratiba au kuingiliana majukumu, unaposhindwa kufika, inasambazwa kuwa umetapeli. Unapelekwa polisi wakati mwingine nakuwa nimewasiliana na mhusika juu ya kutofika, namuuliza nimrudishie pesa yake au kama ataandaa tamasha jingine nihudhurie, unashangaa maneno ya utapeli yanaibuka,” alisema Rose.

KILIO CHAANZA!
Rose alishindwa kuhimili kiwango cha maumivu ya moyo na kujikuta akiangua kilio hali iliyomlazimu mwandishi kupata wakati mgumu kumtuliza.

“Oke, nikatukanwa kuwa natumia unga. Ngoja nikuulize. Ingekuwa natumia unga, hivi kweli ningeweza kutunga nyimbo, kuimba na kujituma kwa namna hiyo? Nakuuliza, ninge.... (kilio kikubwa).
AKAENDELEA
“Niliowaamini ndiyo wamenigeuka, wamenitumia kwa muda mrefu na wakati mwingine kwa kunifanyisha kazi ambazo sikuwa nazitaka lakini wameona haitoshi, ni haohao waliniteka na kunipeleka porini na kunitishia maisha. Mungu atajibu na mbingu zitasimama (safari hii kwa kilio cha juu zaidi).”

ENDELEA NAYE
“Wengine wamekuwa wakinitaka kimapenzi (akataja jina), lakini kwa kutumia pesa zao nikikataa wananitishia maisha, wana wake na watoto, nabaki najiuliza kwani mimi ni kafara ya waume za watu? Eeh? Kweli jamani? Nimepelekwa porini, nikapigwa, nikaoneshwa mambo ya ajabu kweli, ili nitoe penzi kwa nguvu, yote hayo nasingiziwa makubwa na kunenewa mabaya, nina moyo wenye nyama, naumia.

“Nimewakosea nini walimwengu? Tatizo ni kuimba? Hivi hawa Wakristo hawaoni kwamba nimekuwa biashara yao nzuri kwa kuimba nyimbo nyingi zinazopendwa na wengi? Hawalioni hata hilo? Nitende wema gani wa kupitiliza hapa?”
YOTE TISA, KUMI HII HAPA!
“Wameninyang’anya vitu vyangu vingi ikiwemo vya ndani, viwanja, na wote ni waume za watu walionitongoza na kuwakataa, wengine nilifanya nao kazi kwa ukaribu, mfano... (akataja jina) na wametumia nafasi hiyo kunipokonya vitu hivyo na wanajua kwa undani uhalali na umiliki wake. Hii ni haki kweli?

“Watu wanaposikia tu Rose Muhando tapeli sasa waelewe napitia mateso magumu yanayoumiza mno, wasisikie tu naimba hivi na kudhani nina furaha ya maisha, nateseka nafsini! (kilio cha kwikwi).
AWEKA NUKTA
Katika kumalizia mazungumzo na mwandishi wetu, Rose alisema: “Waniache na safari yangu ya kumtumikia Mungu, ninachojua yeye (Mungu) atashughulika na watesi wangu na kila nafsi itayaonja mauti.”
Risasi Jumamosi linafanya juhudi za makusudi kuwasaka watu waliotajwa kwenye sauti ya Rose ili kuwasomea madai yake. Endelea kusoma Magazeti Pendwa ya Global Publishers.   

LICHA YA KUJIFUNGUA UZURI WA AUNT PALEPALE

MWANDISHI WETU KIWANGO! Tofauti na watu wengine ambao maumbile yao hubadilika mara baada ya kujifungua, kwa staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel hali imekuwa tofauti, uzuri na umbo lake limebaki vilevile.
Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel akiwa na mwanaye.
Akizungumza na wahariri sambamba na waandishi wa Global Publishers nyumbani kwake Mwananyamala jijini Dar, Aunt alisema kilichomfanya asinenepe kupita kiasi na kuharibika mwili ni mazoezi sambamba na kufuata ushauri wa vyakula anaopewa hivyo mwili wake kubaki vilevile.
“Nachukia ubonge nyanya, namshukuru Mungu pia kwani wengi wakijifungua huwa wananenepa hovyo lakini kwangu mambo yamekuwa tofauti. Niko vilevile, nafikiri pia ni kutokana na kufuata ushauri mzuri wa kula chakula niliopewa,” alisema Aunt.
Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel.
Mbali na kutobadilika, Aunt alisema kwa sasa muda mwingi anautumia kuwa nyumbani na ubavu wake, Moze Iyobo wakimlea mtoto wao tofauti na zamani alipokuwa na misele ya usiku katika viwanja tofauti vya starehe.

SKENDO YA FREEMASON YAMGANDA WOLPER! NYUMBANI KWAKE KWAJAA UREMBO WA FREEMASON


Stori: Gladness Mallya na Musa Mateja
BAADA ya hivi karibuni kunaswa akiingia katika jengo lao, staa mwenye mvuto kunako gemu la filamu Bongo, Jacqueline Wolper amezidi kugandwa na skendo ya Jamii ya Siri (Secret Society) ya Freemason akidaiwa kuishi kwa masharti ya taasisi hiyo huku nyumba yake ikiwa imejaa vitu vinavyodaiwa kuwa vya ‘Ki-freemason’.

Staa mwenye mvuto kunako gemu la filamu Bongo, Jacqueline Wolper.
Akizungumza na gazeti hili, ‘dada’ wa kazi wa Wolper ambaye kwa sasa ameacha kufanya kazi kwake huku akiomba hifadhi ya jina lake, alisema mbali na vitu hivyo, staa huyo anaishi kwa masharti makali kwani kila siku anaamka saa kumi alfajiri na wakati huo anamzuia dada huyo asiamke.
“Akiamka (Wolper) saa kumi hiyo alikuwa akinikataza nisiamke, sikuwahi kujua huwa anafanya kitu gani akiamka na kwa nini alikuwa akinikataza, ukweli maisha yake anaishi kwa masharti ya ajabuajabu nahisi ni Freemason,” alisema dada huyo.
Michoro inayodhaniwa kuwa niya kifrimason.
Dada huyo alitaja kuwa nyumbani kwa mwigizaji huyo, Mbezi Beach jijini Dar, kumesheheni mapambo kibao ya Kifreemason ambayo huyatunza na kuyalinda kama binadamu hali ambayo ilikuwa ikimpa wakati mgumu kwani hakuwahi kuona mambo kama hayo maishani mwake.
Dada huyo alitoa picha za vifaa vya ndani kama saa, picha za ukutani vyenye alama zinazodaiwa kuwa za Freemason pamoja na picha ya mwili wa Wolper ambayo imechorwa alama zinazodhaniwa kuwa ni za jamii hiyo ya siri.

Na huu ukiwemo.
Baada ya kupata habari hizo, paparazi wetu alimtafuta Wolper ambaye alijibu kwa kifupi;
“Ni kweli huwa naamka saa kumi lakini ni kwa ajili tu ya kufanya mazoezi, kuhusu hayo mengine napenda tu picha na vitu vyenye nembonembo sasa mimi sijui kama ndizo za Freemason.”

SLIM AANGUA KILIO GARI LIKIENDA KWA MTALAKA

MUIGIZAJI mahiri wa filamu, Slim Mbegu ‘Slim’ hivi karibuni aliangua kilio akiwa Mahakama ya Mwanzo Magomeni baada ya kushuhudia gari alilopewa zawadi yeye na mkewe aliyetengana naye, Asia Morgana likivutwa kwa Break Down kusogezwa eneo hilo.
Muigizaji mahiri wa filamu, Slim Mbegu ‘Slim’.
Wawili hao walikuwa na shauri mahakamani hapo wakigombea gari hilo kila mmoja akidai ni mali yake halali, lakini hatimaye mwanamke alishindwa na hivyo Slim kuamriwa kulipeleka kortini ili liweze kukabidhiwa kwa wenyewe, lakini akashindwa kwa kushindwa kulifanyia matengenezo madogomadogo ya kulifanya litembee.
Gazeti hili liliongea na Asia aliyemshukuru Mungu kwa kuweza kupata gari lake alilodai kusumbuliwa kwa muda mrefu na aliyekuwa mumewe, wakati Slim alisema hana la kusema zaidi ya kumuachia Mungu kila kitu.

MLELA: NIMEPATA MTOTO KWA BAHATI MBAYA!

YUSUF Godfrey Willard Mlela, muigizaji nyota wa filamu Bongo, alipata mtoto kwa bahati mbaya baada ya ‘kuuza mechi’ kwa msichana ambaye hakuwa na malengo naye kimaisha, lakini amelazimika kumhudumia kijana wake kwa kila kitu muhimu.
muigizaji nyota wa filamu Bongo, Yusuph Godfrey Willard Mlela.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, alisema alikutana na msichana huyo ambaye alikataa kumtaja jina kama rafiki wa kawaida, lakini akajikuta akishiriki naye bila kinga na siku hiyo hiyo akapata ujauzito ambao pia alishindwa kumshinikiza kuutoa kwa vile anatambua ni kitu kibaya.
“Ilikuwa ni bahati mbaya, unajua mwanamke wa kumuoa ni yule ambaye mnazungumza na kupanga baada ya kujuana vizuri tabia.

WEMA AMKEJELI LINAH!

Imelda Mtema
NI shiida! Siku chache baada ya msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Esterlina Sanga ‘Linah’ kulalamika juu ya kitendo cha Wema Sepetu ‘Madame’ kumchukua aliyekuwa bwana’ake Nangari Kombo, muigizaji huyo ameibuka na kutoa maneno yanayoashiria kejeli, kuwa aache presha, kwani zile ni picha tu!

Staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu ‘Madame'.
Katika gazeti la Risasi Jumamosi, toleo lililopita, iliripotiwa na kuchapishwa habari na picha zilizomuonyesha Madame akiwa amepozi kitandani na kijana huyo, aliyepata umaarufu baada ya kuingia ndani ya eneo la kuchezea katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam mwaka 2010, wakati wa mechi kati ya Brazil na Taifa Stars na kumkumbatia kiungo nyota wa mabingwa hao wa zamani wa dunia, Kaka.
Lakini Risasi Mchanganyiko lilipotaka kujua maoni yake juu ya shutuma hizo, Wema alisema kupiga picha na Nangari hakumaanishi mapenzi, kwani yeye ni mtu wa watu na picha kama hizo hupiga na marafiki zake wengi tu, hivyo Linah asiwe na shaka naye hata kidogo.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Esterlina Sanga ‘Linah’.
“Nilipiga naye kama ninavyoweza kupiga na marafiki wengine kama akina Martin Kadinda, Petit Man na wengineo. Sina uhusiano naye wa kimapenzi, naomba aamini kuwa ni rafiki tu wa kawaida,” alisema Wema na kuibua maswali juu ya aina ya uswahiba wa kawaida wa kupiga picha kitandani na mpenzi wa mtu!

MAI AMCHOKONOA LINAH, BAADA YA WEMA KUMCHUKULIA BWANA WAKE

Gladness Mallya KATIKA kinachoonekana kama kumchokonoa nyota wa muziki Estalina Sanga ‘Linah’, mtangazaji maarufu Bongo, Maimartha Jesse ‘Mai’ ameunga mkono kitendo cha Wema Sepetu kumchukua mpenzi wa Mbongo Fleva huyo Nangari Kombo.
Mtangazaji maarufu Bongo, Maimartha Jesse ‘Mai’.
Mai aliweka picha ya Wema akiwa na Kombo kwenye ukurasa wake wa Instagram na kumpongeza kwa kumpata ingawa watu mbalimbali walimponda mtangazaji huyo kwa maneno makali wakimlaumu kwa kufurahia mwenzake kuporwa bwana.
Gazeti hili lilipomtafuta na kumuuliza kuhusu kisanga hicho, Mai alisema; “Jamani Wema naye ni binadamu na ana haki ya kuwa na mpenzi, mimi sijui hizo habari kwamba amemchukua mwanaume wa Linah, nilimpongeza kwa sababu ni mdogo wangu, kwa kumpata mpenzi kwani mjini mwanamke ukionekana kila siku uko peke yako wanakufikiria vibaya na kuongea maneno mengi ya ajabu.”

MREMBO: DUDE AMENIZALISHA, KANITELEKEZA


Gladness Mallya na Andrew Carlos
Mrembo aliyejitambulisha kwa jina la Ester Eliakim, mkazi wa Kinyerezi, Dar ameibuka na kueleza kwamba alizaa na staa wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ ambaye baadaye alimtelekeza yeye na mwanaye Cleopatra (mwenye miezi 11).

Ester akiwa na mtoto aliyezaa na Kulwa Kikumba ‘Dude’.
Akizungumza na paparazi wetu, Ester alisema mara ya kwanza alikutana na Dude katika mchezo wa Bongo Dar es Salaam alikokuwa akicheza kama askari na wakaanzisha uhusiano wa kimapenzi tangu mwaka 2008.
Waliendelea na uhusiano wao wa siri huku Dude akimtaka awe msiri ili kuilinda familia yake jambo ambalo alikubali.
Mwaka jana alipata ujauzito na kumweleza Dude ambaye alikubaliana naye na akawa anamhudumia, lakini kwa sharti la  kumtafuta kijana na kumfanya mpenzi kivuli ili awe ndiye aliyempa mimba, kwani ikijulikana ni wake itakuwa ni shida kwa mkewe Eva.

“Nilikubaliana naye maana hii ilikuwa ni mimba kama ya nne, nyingine tatu nilitoa, ilibidi nifanye hivyo.
“Baada ya mtoto kuzaliwa niliyembambika alipomuona tu alikataa nilipomueleza Dude akakataa kunihudumia, kodi ilipoisha alinitumia hela nusu.

“Kila ninapowasiliana naye, ananipiga chenga niko tayari kupima DNA kwa sababu nina uhakika 100% mtoto ni wa Dude,” alisema Ester.Gazeti hili lilimtafuta supastaa Dude, lakini hakupokea simu wala kujibu sms alizotumiwa zaidi ya kuandika “Niko kwa Benard Membe, nipigie baadaye.”

Shilole Achekelea..Awashukuru BASATA kwa Kumsamehe Sakata Lake la Picha Chafu Akiwa Jukwaani

Shilole
Shilole a.k.a Shishi bybee sasa anaweza kupata usingizi mnono bila mawazo, sababu lile sakata la kusambaa kwa picha zake chafu zilizopigwa wakati akitumbuiza nchini Ubelgiji mwezi uliopita hatimaye limemalizika vizuri.

Sakata hilo ambalo lilifika hadi bungeni ambapo Naibu Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia alisema serikali ililiagiza Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA kufanya naye mahojiano ili serikali iweze kuchukua hatua.

Muimabji huyo wa ‘Nakomaa na JIji’ ameelezea furaha yake baada ya kusamehewa na BASATA alipoenda kutoa maelezo.


  • “Leo nimeenda BASATA kwasababu waliniita juzi, kwahiyo nimeenda kusikiliza wito wao, tumeongea nashukuru wamenielewa tumeongea tumeelewana basi hakuna tena ambacho kitu kina tatizo tena hapo kwasababu wale ni wazazi wanatakiwa kumkanya mtu kama mtoto labda” Alisema Shishi bybee



  • “Tumeelezana pale nini kifanyike nini kisifanyike na kila kitu ambacho kinahusiana na tasnia ya sanaa. Nimewaelezea situation ilivyotokea wamenielewa wameniambia pia niwe mwangalifu katika mavazi, of-course ni kweli kitu kama hicho kinaweza kutokea kwahiyo sisi ni binadamu, nimeshukuru sana kwasababu wameweza kunielewa, basi ni hivyo tu nina furaha kwaajili ya hiyo kitu.” Alimaliza Shilole.


Source: EATV.TV

Ali Kiba na Jokate Wazidiwa na Uzito wa Penzi..Sasa Wajianika na Kujiachia Wazi na Kuualika Ulimwengu Kwenye Dunia yao Mpya

ALI KIBA NA JOKATE
Alikiba na Jokate Mwegelo wanaendelea kukusogeza karibu katika muungano wao wa hivi karibuni. Wawili hao wanaonesha kuelemewa na uzito wa penzi lao kiasi cha kuanza kujiachia na kuualika ulimwengu kwenye dunia yao mpya.

Jokate amepost picha Instagram akiwa na hitmaker huyo wa Chekecha na kuandika:All The Best Chèr.

Mashabiki wanaonekana kuufurahia uhusiano huo na wengine wanasema wanapenda kuwa pamoja.


  • “Oooh wowww nina vyo wapenda hadi raha , yani couple yenu ina vutia sana , maana nyiote wazuri alafu mna jitambuwa , na atakae kuwa kinyume na hili ata kuwa hawatakii wema , maana wana damu tuliumbiwa tuwe wawili ili kusaidiana mambo mengi katika maisha, so nawapendeni sana @jokatemwegelo ,@officialalikiba , nawaombea sana Mungu azidi kuwa lindia mausiano yenu , mufike kwenye malengo mazuri zaidi, msisikilizi ya walimwengu hawana mema hawana mema,” ameandika alinezinta.
Older Posts
© Copyright ZEE LA UDAKU | Designed By Code Nirvana
Back To Top