Habari Kali
Loading...

PICHA CHAFU YA MGOMBEA URAIS YAIBULIWA!

Mwandishi wetu
NIkama kumekucha! Tayari mbinu za kuchafuana na kupakana matope miongoni mwa wanasiasa waliojitokeza kugombea urais kupitia chama kimoja cha siasa zimeanza kujitokeza baada ya hivi karibuni kuibuliwa kwa picha ya mgombea mmoja wa chama hicho aliyetangaza nia akiwa na hawara ndani ya chumba cha hoteli.

Kuibuliwa kwa picha hiyo kumekuja siku chache kufuatia mgombea huyo kutangaza nia huku akianika kipaumbele chake endapo atapata ridhaa ya wapiga kura kuingia ikulu.
MUDA WA PICHA
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichotinga katika Ofisi za Global Piblishers, Bamaga-Mwenge, inadaiwa kuwa, mheshimiwa huyo (jina tunalo) na mwanamke huyo ambaye si mke wake, walipiga picha hiyo muda mrefu lakini kutokana na duru za kisiasa za uchaguzi mkuu mwaka huu, picha hiyo inaonekana kuwa ‘keki’ kwa wapinzani wake.

“Unajua hii picha ni ya muda mrefu. Mheshimiwa alipiga akiwa na uhusiano na huyu mrembo. Sasa mheshimiwa alipotangaza nia tu, wabaya wake wakaona hapa ndiyo penyewe, wakaiibua ili itumike kwenye kampeni yake ya urais kama chama chake kitampitisha yeye kugombea,” kilisema chanzo hicho.
ENEO LA PICHA
Ilizidi kudaiwa kuwa, picha hiyo ilipigwa ndani ya hoteli moja maarufu iliyopo Mwananyamala jijini Dar es Salaam na mpigaji alikuwa mwanamke huyo ambaye hakujulikana jina akitumia simu yake ya mkononi kwa kuishika kwa mkono wake wa kulia (selfie).

SI MKE WAKE
Chanzo kilisema kwa sababu mheshimiwa huyo wa kutoka Kanda ya Ziwa ana mke na watoto na anaheshimika katika jamii, kupiga picha ya namna hiyo kunamuondolea sifa ya kuwa rais wa Tanzania.

“Ingekuwa picha yenyewe ni mheshimiwa na mke wake, sidhani kama wabaya wangeitumia lakini sasa si unajua maadili ya Kiafrika. Nadhani hata wenzetu nje, huwezi kuwa na mke halafu ukawa na hawara wakakupa cheo kikubwa kama cha urais wa nchi,” kilisema chanzo hicho.
HALI ILIVYO KWA SASA
Tayari baadhi ya wagombea wa urais kupitia vyama mbalimbali wameanza kuwalilia baadhi ya wenzao kwamba, wameanza kucheza rafu katika safari ya kinyang’anyiro cha kuusaka urais kwa kuwatafutia skendo chafu, za zamani na mpya ili wachafuke katika jamii na kuonekana hawafai kukabidhiwa ikulu, Oktoba mwaka huu.

ORODHA YA WAGOMBEA
Mpaka sasa, mbali na Chama Cha Cuf ambapo wameshamtaja Profesa Ibrahim Lipumba kugombea urais mwaka huu,  wanachama wenye nguvu walioonesha nia ya kugombea nafasi hiyo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni Edward Lowassa, Benard Membe, Frederick Sumaye, Samuel Sitta, Makongoro Nyerere, Mwigulu Mchemba, Lazaro Nyalandu, January Makamba ambapo baadhi yao picha zao zimetumika ukurasa wa mbele wa gazeti hili.

Story ya wanawake wa Rombo kukodi wanaume Kenya kuwaridhisha kimapenzi yatinga bungeni, wanaume wataka waombwe radhi

Habari iliyoandikwa kwenye gazeti la Mwananchi juzi yenye kichwa cha habari ‘Wanawake wa Rombo wakodi wanaume kutoka Kenya’ imeibukia bungeni leo.

Habari hiyo iliandikwa kutokana na kauli aliyoitoa mkuu wa wilaya ya Rombo, Lembris Kipuyo, aliyedai kuwa kutokana na wanaume wa wilaya hiyo kuwa walevi wa kutupa, wake zao wamekuwa wakikodi wanaume kutoka Kenya ili kuwaridhisha kimapenzi.

“Tatizo la ulevi wilayani Rombo na matumizi ya pombe zisizokuwa na viwango ni kubwa sana na linahitaji nguvu kulikabili,” alisema mkuu huyo wa wilaya. “Imefikia wakati wanaume wengi wanashindwa kumudu kufanya tendo la ndoa na kuwalazimu kukodi wanaume kutoka nchi jirani ya Kenya kwaajili ya tendo hilo.”

Akiuliza swali kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, mbunge wa Rombo, Joseph Selasini (CHADEMA), amesema habari hiyo imesababisha madhara makubwa katika jimbo lake.

Selesani amesema habari hiyo imewadhalilisha wanaume wa Rombo na wanaiomba serikali iwaombe radhi kwa kilichoandikwa.

Amesema kutokana na habari hiyo wanaume wengi wameanza kuwatilia mashaka wake zao kuwa huenda ‘wamekuwa wakichepuka’ na wakenya na hivyo kusababisha maelewano hafifu ndani ya ndoa.

Akijibu swali hilo, mheshimiwa Pinda alisema binafsi hajaisikia taarifa hiyo kwahiyo hatoweza kuomba radhi hadi pale atakapolifuatilia.

Mwigulu awaomba radhi wanafunzi elimu ya juu baada ya kutopewa Pesa zao za mkopo!

SIKU moja baada ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kile cha St Joseph vyote vya   Dar es Salaam kuanza mgomo kutokana na kukosa fedha za kujikimu, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amewaomba radhi.

 Nchemba aliomba radhi bungeni jana baada ya Mbunge wa Viti Maalum, Ester Bulaya (CCM) kuomba muongozo, akihoji sababu za Serikali kushindwa kupeleka fedha hizo vyuoni.

 “Mheshimiwa Spika, naomba nipewe mwongozo ni kwa sababu gani serikali imeshindwa kupeleka fedha huku ikijua wazi kwamba wanafunzi hao ni watoto wa masikini,

Katika taarifa yake, Nchemba alisema kutokana na kuchelewa huko aliwaomba radhi wanafunzi ambao wanasoma kwa kutegemea mkopo wa serikali huku akizitaka mamlaka husika kuhakikisha fedha hizo zinawafikia wanafunzi mara moja. Alisema  Hazina imekwisha kuidhinisha fedha hizo.

 “Juzi hazina ilikamilisha miamala ya fedha ambazo zinahitajika katika vyuo hivyo na mamlaka zinazohusika zilipaswa kufikisha fedha hizo jana kwa wahusika (wanafunzi),” alisema Nchemba na kuongeza:

 “Ni muda mrefu migomo haijatokea kutokana na ukweli kuwa mtiririko wa utoaji wa fedha haukuwa na matatizo. 

 “Hakuna hata wa kulikuza suala hili kwa sababu msingi wake ulikuwa ni wa halali lakini kwa sasa limepatiwa ufumbuzi,” alisisitiza.

 Kuchelewa kutolewa fedha hizo za mkopo kumesababisha wanafunzi wa vyuo hivyo kugoma kuanzia juzi  hadi watakapopewa fedha hizo za kujikimu.

Bulaya katika taarifa yake alisema wanafunzi zaidi 7,000 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) juzi waligoma kuingia darasani kwa sababu ya kukosa fedha za kujikimu huku wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo cha Mtakatifu Joseph kilicho Mbezi, Dar es Saam wakisimamishwa masomo.
Mwisho

FLAVIANA MATATA AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUMBUKUMBU YA WALIOFARIKI MV BUKOBA

Waliofika kanisa katoliki la Mt. Francis, lililopo Nyakahoja-Mwanza, na kushiriki misa maalum ya kumbukumbu ya kuzama kwa meli ya Mv. Victoria. Misa ya kumbukumbu ikiendelea. Wakifuatilia misa ya kumbukumbu.
Wakiweka mauwa kwenye kaburi.Flaviana Matata akiongea neno.Sheikh akiomba dua maalum kwa ajili ya kuwakumbuka marehemu wa ajali ya meli ya MV. Bukoba....wakipiga picha ya pamoja kwenye kaburi....wakipiga picha ya ukumbusho.
Na Johnson James, Mwanza
ALFAJIRI ya Mei 21 mwaka 1996 – siku kama ya leo -- ni tarehe ambayo Tanzania ilipatwa na msiba mzito ambapo zaidi ya watu 600  walifariki baada ya meli ya MV Bukoba iliyokuwa ikifanya safari zake kutoka mjini Bukoba kwenda jijini Mwanza  kuzama katika Ziwa Victoria ambalo liko katika eneo la nchi za Kenya, Uganda na Tanzania.
Mwanamitindo maarufu nchini na duniani,  Flaviana Matata,  wakati wa msiba huo alikuwa na umri wa miaka minane,  alikuwa mmoja wa waombolezaji waliofika kwenye misa maalumu ya kuwaombea marehemu waliofariki katika ajali hiyo  alimpoteza mama yake mzazi meli hiyo ilipozama maeneo ya Bwiru jijini Mwanza  ikiwa na jumla ya abiria wapatao 800.
Katika misa iliyofanyika kwenye kanisa  Katoliki huko  Nyakahoja jijini Mwanza, mwana mitindo huyo wa kimataifa  amesema:  “Leo ni siku ambayo sitaisahau kwani ni siku ambayo mama yangu mzazi alifariki kwa kuzama majini na meli ya MV Bukoba  katika Ziwa Victoria hivyo niungane na wenzangu waliopoteza ndugu zao katika ajali hiyo ambao ilitwaa maisha ya Watanzania wengi.”
Aidha, katika misa hiyo iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini, wasanii  na vikundi mbalimbali kama Zalendo na Bongo Ride ambao wamewasha mishumaa kwenye makaburi  ya marehemu yaliyoko kitongoji cha Igoma jijini Mwanza.
Matata amesema kuwa anaiomba serikali kuhakikisha kuwa vyombo vyote vya majini vinakuwa salama ili kudhibiti ajali za majini  ambazo zimekuwa zikitokea mara kwa mara.
Flaviana aliongozana na dada yake, Grace Matata,  na mshindi wa Big Brother Africa, Sultan Idriss,  ambaye alikuwa kivutio cha wengi katika kumbukumbu hiyo.

Rais kikwete Atembelea Maeneo Yaliokumbwa na mafuriko-Dar


RAIS Jakaya Kikwete jana alitembelea   maeneo mbalimbali ya  Dar es Salaam  ambayo yameathirika na mafuriko kutokana na mvua inayoendelea kunyesha.

Ziara hiyo ilianzia  katika daraja linalotenganisha  Mbagala Kuu na Mtoni Kijichi katika Wilaya ya Temeke na kumalizia katika Daraja la Jangwani   katika Wilaya ya Ilala.

Rais Kikwete baada ya kuona daraja linalotenganisha Mbagala Kuu na Mtoni  Kijichi, alitoa agizo kwa Jeshi la Ulinzi wa  Wananchi Tanzania (JWTZ) kuweka daraja la muda katika  eneo hilo huku ujenzi ukiendelea.
 
Hata hivyo Rais Kikwete alipotembelea katika Daraja la Jangwani aliwataka wahandisi   kutumia  maarifa  kuondoa taka zinazosababisha madaraja hayo kuziba ili maji yaweze kupita kwa urahisi.

“Katika eneo hili tuliwaambia watu wahame lakini walikataa sasa tutafanyaje. Inabidi wahandisi mtumie maarifa ya kutoa taka zilizoziba katika madaraja haya ili maji yasipite juu ya daraja bali yaweze kupita chini kwa urahisi.

“Nimeanza ziara yangu ya kuangalia madhara yaliyotokana na mafuriko na nimeanzia  katika eneo la Mbagala na Jangwani.
 
“Kesho (leo) nitamalizia katika eneo la Mkwajuni na Tegeta na hapo ndipo nitakapotoa hitimisho  la athari za mafuriko   Dar es Salaam,” alisema Rais Kikwete.

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia  Mjema, alisema imepokelewa msaada wa Sh bilioni 250 kutoka  Benki  ya  Dunia  kwa ajili ya kutengenenezea daraja la Mbagala Kuu na barabara kwa kiwango cha lami.

Alisema daraja hilo pamoja na barabara vitatengenezwa  kwa   miezi mitatu hadi minne.  

Naye Mhandisi wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Eliseus Mtenga, alisema   itatafutwa  mashine itakayotoa taka zote zilizoziba katika daraja la Jangwani maji  yaweze kupita kwa urahisi.

Watu Watano Wathibitishwa Kufariki Dunia Jijini Dar es Salaam Kutokana na Mafuriko

JAMHURI YA MUUNGANO WATANZANIA
WIZARA YA MAMBO YANDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
PRESS RELEASE
08/05/2015
WATU WATANO WATHIBITISHWA KUFARIKI DUNIA JIJINI DAR ES SALAAM KUTOKANA NA MAFURIKO
Watu watano wameripotiwa kupoteza maisha jijini Dar es Salaam kutokana na athari za mafuriko kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha jiji. Mvua hizo zinazonyesha kwa siku tatu mfululizo zimesababisha vifo vya watanzania hawa katika maeneo tofauti ya jiji la Dar es Salaam kama ifuatavyo:
Mnamo tarehe 06/05/2015 majira ya saa moja kamili usiku huko maeneo ya Magomeni Kinondoni jijini Dar es Salaam mtu mmoja jina SHABAN S/O IDD, Miaka 73, Mkazi wa Manzese alisombwa na maji ya mto ng’ombe alipokuwa akijaribu kuvuka mto huo. Mwili wake ulipatikana siku iliyofuata 07/05/2015 akiwatayari amekwishafariki dunia na umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala.
Kifo kingine kilitokea tarehe 07/05/2015majira ya  saa sita kamili mchana huko maeneo ya Mwananyamala Mbuyuni Kata ya Mwananyamala, OysterBay, Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo mtu mmoja aitwaye MASUMBUKO S/O DOUGLASS @ LIMAMU, Miaka kati ya 50-55, mkazi wa Mwananyamala Mbuyuni, alianguka na kufariki dunia ghafla wakati anatoa maji yaliyoingia nyumbani kwake. Uchunguzi wa awali umebaini kuwa marehemu alikuwa na tatizo la ugonjwa wa kifafa hivyo wakati akihangaika kutoa maji, ugonjwa huo ulimpata na kuanguka kwenye maji na kufariki dunia baada ya kukosa msaada wa haraka. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala kwa uchunguzi.
Mtu mwingine mwanaume RASHIDI S/O HASSAN, Miaka 36, Mkazi wa maeneo ya Mvuruhani Pemba Mnazi Kigamboni jijini Dar es Salaam alizama katika mkondo wa maji unaoelekea baharini tarehe 06/05/2015. Mwili wake ulipatikana tarehe 07/05/2015 ukiwa unaelea majini umbali wa mita 500 toka eneo alilozama.
Kifo kingine kimetokea tarehe 06/05/2015 huko Yombo Makangarawe ambapo mtoto aitwaye GLORIA D/O MREMA, mwaka mmoja na miezi mitatu alipotea baada ya watoto wenzake kumuacha wakati wakicheza pamoja. Juhudi za kumtafuta zilifanyika bila mafanikio hadi mwili wake ulipopatikana ukiwa unaelea majini katima mto mzinga akiwa tayari ameshapoteza maisha.  Mwili umehifadhiwa katika Hospitali ya Temeke
Kifo kingine kimetokea tarehe 08/05/2015 saa moja kamili asubuhi huko maeneo ya Kinondoni Mkwajuni, Kata ya Mkwajuni Wilaya ya Kinondoni ambapo mtu mmoja mwanaume ambaye jina lake halikufahamika mara moja anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka (40-45) mkazi wa Kinondoni Mkwajuni, alikutwa amefariki dunia. Mwili umehifadhiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi.
Pamoja na vifo hivyo kuripotiwa, pia mtu mmoja ajulikanae kwa jina la MABULA S/O MOSSES, Miaka 65, Mkulima, Mkazi wa Vingunguti,  Buguruni wilaya Ilala amevunjika mguu wake wa kulia sehemu ya chini ya goti baada ya kuangukiwa na ukuta wa Godown la FIDA S/O HUSSEIN lililopakana na nyumba yake. Pia ukuta huo umesababisha uharibifu wa vitu mbalimbali. Majeruhi amepekwa Hospitali ya Amana kwa matibabu.
Katika kata ya Mchikichini, taarifa ya mafuriko inaonyesha takribani nyumba 60 hadi 70 zimefunikwa na maji hadi juu ya mapaa ambapo wakazi wake tayari walikuwa wamehama kufuatia agizo la Serikali kuwa wahame maeneo hayo. Pia takribani watu 30 hadi 35 wamejihifadhi katika shule ya Srkondari Mchikichini.
Katika Kata ya Jangwani, zipo nyumba zinazokadiriwa kufikia 90-100 zimefunikwa na maji hadi juu ya paa. Wakazi takribani 250-300 walihama mapema kufuatia taarifa hiyo ya Serikali. Aidha watu wanaokadiriwa kati ya 25-30 nao wamejihifadhi katika Shule ya Sekondari Mchikichini.  
Aidha, maeneo yaliyoathirika zaidi kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha ni Keko, Chang’ombe maduka mawili, Yombo Vituka, Vingunguti, Africana, Msasani Bonde la Mpunga, Eneo la Jangwani, Manzese, Kigogo, Mburahati, Boko Basihaya, na maeneo mengine ambayo taarifa zake bado hazijapokelewa
Barabara zinazounganisha katikati ya Jiji na pembezoni zimeharibika na hivyo kusababisha kutolewa maelekezo barabara hizo kufungwa ili kupunguza madhara ambayo yangeweza kutokea.
Aidha, madaraja mbalimbali yameharibika h
ivyo kukata mawasiliano kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine. Kwa mfano daraja la linalounganisha Mbagala na Mtoni Kijichi maarufu kama njia ya ng’ombe. Daraja lingine ni lile la Kinyerezi ambalo halipitiki baada ya kusombwa na maji.
Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Serikali limejiandaa kwa hali ya dharura itakayojitokeza. Pia Jeshi la Polisi limejipanga kukabili foleni kwa kuhusisha askari wa vikosi mbalimbali ili kukwamua tatizo hilo ambalo limesababishwa na uharibifu wa miundombinu.
Aidha nawataka wananchi wote kuchukua tahadhari ya hali ya juu hasa wale waishio maeneo ambayo ni mikondo ya maji au watumiaji barabara zinazopitiwa na mikondo hiyo. Wananchi wanaombwa kutoa taarifa za mapema na haraka pindi wanapoona au kugundua kuna maeneo au jambo  linalohatarisha maisha yao na ya watu wengine.
NB: Wakati huo huo zimepokelewa taarifa za kupatikana kwa miili ya watu watatu waliofariki ambayo inafanyiwa uchunguzi katika hospitali mbalimbali jiji Dar es Salaam ili kujua kama vifo hivyo vimetokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha jiji. Taarifa kamili zitatolewa kuhusu wajihi wa watu hao na wako katika hospitali gani
 
S. H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM

Mafuriko Yaua Watu Jijini Dar, Nyumba Kibao Zafunikwa...Katapila latumika Kuokoa Watu


Mvua kubwa iliyonyesha kwa siku mbili mfululizo tangu juzi imesababisha vifo vya watu watano huku mamia wakikosa makazi baada ya nyumba zao kubomolewa. 
 
Mvua hiyo iliyofikia kipimo cha milimita 132.5 kwa mujibu wa vipimo vilivyofanywa katika kituo cha Shule ya Msingi ya Maktaba, ilisababisha barabara kujaa maji na nyingine kuharibika na madaraja kadhaa kukatika.
 
Mkurugenzi Mkuu wa Hali ya Hewa, Dk Agnes Kijazi alisema jana kwamba kipimo hicho cha mvua ni cha juu mno kulinganisha na kile cha wastani ambacho ni kati ya milimita 16 na 30.
 
“Kwa takwimu za mwezi Mei, kiwango hiki hakijawahi kufikiwa kwa miaka 10 iliyopita.” Alipotakiwa kufafanua miezi mingine, Dk Kijazi alisema hakuwa na takwimu kwa kuwa alikuwa nje ya ofisi.
 
Awali, Dk Kijazi alitoa taarifa ikisema mifumo ya hali ya hewa inaonyesha kuwa “hali ya mvua inatarajiwa kuendelea katika baadhi ya siku hadi Mei 20, mwaka huu”.
 
“Mamlaka inaendelea kushauri wakazi wa maeneo hatarishi pamoja na watumiaji wa bahari kuchukua tahadhari,” alisema Dk Kijazi.
 
Watano wafa
Kutokana na mafuriko hayo, watu watano wakiwamo watoto wawili, walipoteza maisha baada ya kusombwa na maji.
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick alisema waliopoteza maisha ni watoto wawili na mzee mmoja ambao majina yao hayajafahamika.
 
“Mtoto mmoja (2) alisombwa na mafuriko katika eneo Machimbo ya Makangarawe na mzee mmoja alifariki jana baada ya mvua kunyesha na kujaa ndani ya nyumba yake. Mtoto mwingine ambaye bado hajapatikana alisombwa na mafuriko pia,” alisema Sadick.
 
Hata hivyo, habari zilizopatikana baadaye zilisema kuwa waliopoteza maisha ni watu watano.
 
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alimtaja mtu aliyefariki dunia kuwa ni Shabani Idd (73) mkazi wa Manzese.

Katika eneo la Mbezi Luis, Mto Mbezi ulifurika, hali iliyosababisha nyumba zilizojengwa kandokando ya daraja hilo kufunikwa na maji.
 
Mkazi wa eneo hilo, John David alisema hali ilikuwa mbaya zaidi jana asubuhi kwani maji yalifurika na kujaa barabarani na kusababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji.
 
Alisema wakazi walio karibu na mto huo walichukua tahadhari tangu juzi na kuhama makazi yao.
 
“Haikuwa rahisi kwa wao kuendelea kukaa hapa wakati wanafahamu hali kama hii ingetokea. Tangu jana jioni familia zinazoishi huko ziliondoka, lakini vitu vyao vimesombwa na maji na nyumba moja imesombwa pia,” alisema David.







GOOD NEWS: Bodi ya Mikopo Ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Yaanza Kupokea Maombi ya Mikopo Kutoka Kwa Wanafunzi Kwa Mwaka Wa Masomo 2015/2016


Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) jana (Ijumaa, Mei 1, 2015) imetoa mwongozo kwa wanafunzi wahitaji wanaotarajia kuomba mikopo na ruzuku kwa ajili ya mwaka wa masomo 2015/2016 unaotarajiwa kuanza miezi michache ijayo.

Kwa mujibu wa mwongozo huo, ambao unapatikana katika tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz), waombaji wote wamepewa takribani miezi miwili kuwasilisha maombi yao kuanzia Jumatatu, Mei 4, 2015 hadi Jumanne, Juni 30, 2015.

Aidha, wanafunzi wote wahitaji wa mkopo na ruzuku wanapaswa kufanya na kuwasilisha maombi yao kwa njia ya mtandao kupitia mfumo maalum (Online Loans Application and Management System) ulioanzishwa na HESLB kwa ajili ya kupokea maombi hayo. Mfumo huo unapatikana kupitia tovuvi ya Bodi au kwa kufungua kiunganishi chake (http://olas.heslb.go.tz).

Pamoja na mambo mengine, mwongozo huo unafafanua kuwa waombaji wa mara ya kwanza (First Time Applicants) wanapaswa kulipa ada ya maombi ya Tshs 30,000/- kwa na kisha kutumia namba ya muamala (Transaction ID) kuingia katika mtandao na kuanza kujaza fomu za maombi.

“Waombaji wa mara ya kwanza wanapaswa kulipa ada ya maombi ya Tzs 30,000/- ambayo inalipwa mara moja tu na haitarudishwa kwa nia ya M-Pesa,” inasema sehemu ya mwongozo huo uloiotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo.

Aidha, mwongozo huo umesisitiza kuwa wanafunzi wenye mikopo na wanaoendelea na masomo katika taasisi mbalimbali za elimu ya juu hawapaswi kuwasilisha maombi tena.

Bodi imewasihi waombaji na wadau wengine kuusoma na kuuzingatia muongozo huo wakati waote wanapofanya na kuwasilisha maombi.

HESLB ilianzishwa kwa sheria ya Bunge na 9 ya mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi Julai, 2005 ili, pamoja na majukumu mengine kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji waliodahiliwa katika taasisi za elimu ya juu. 
 
Aidha, jukumu jingine la Bodi ni kudai na kukusanya mikopo yote iliyotolewa kwa wahitimu wa taasisi za elimu ya juu kuanzia mwaka 1994 wakati Serikali ilipoanza kukopesha wanafunzi.

Taasisi Ya Kiislam Yatishia Kuandamana Nchi Nzima......Yaipa Serikali Siku 15 Kufungua Madrasa na Kuwaachia Huru Masheikh Waliokamatwa

Jumuiya na Taasisi za Kiisalam nchini, imetoa tamko na kuipa serikali siku 15 kabla ya kufanya maandamano nchi nzima kuelekea Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakidai kufunguliwa kwa madrasa zilizofungiwa kwa kuhusishwa na kutoa mafunzo ya ugaidi.

Masharti mengine ni kuachiliwa huru au kwa dhamana masheikh na maimamu waliokamatwa wakituhumiwa kutoa mafunzo na mazoezi ya kigaidi.

Maeneo ambayo madrasa hizo zaidi ya 10 zimefungwa ni katika mikoa ya Kilimajaro, Dodoma na Mtwara.  Tamko hilo pia lilisema jeshi hilo linawatuhumu kwa kukusanya watoto na kuwafundisha elimu ya dini katika mazingira yasiyofaa na kuwapo kwa taarifa za watu wenye milipuko misikitini na kujihusisha na ugaidi.

Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Sheikh Musa Kundecha, alisema jeshi hilo limekuwa likiwakamata watu hao usiku na kuwapeleka katika vituo vya polisi, na kuwahoji.

Alisema jeshi hilo limekuwa likifanya kazi za maofisa wa ustawi wa jamii na elimu, kufanya ukaguzi katika maeneo ambayo watoto hao wanafundushwa elimu ya dini ya kiislamu.

“Mkakati wa operesheni hii unakiuka utu, haki za binadamu, kikatiba na ni uchochezi dhidi ya Waislamu kuwafanya wachukiwe na jamii, tunawatunza yatima katika maeneo jirani na madrasa na kuwapa elimu ya kidini siyo kosa, tunatimiza wajibu wa kidini. Wajibu wa serikali ni kutulinda, lakini tunawekwa katika mazingira ya hatari,” alisema Kundecha.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Isaac Nantanga, alisema ulifanikiwa utafiti, kabla ya  jeshi hilo kuchukua hatua za kufunga baadhi ya madrasa na kuwakamata watu hao.

“Katika maeneo ya mikoa hiyo ni kweli kuna suala hilo, na watoto ambao wana umri wa kuwa shule walikutwa pale, hivyo tukataka kufahamu na yajulikane mafunzo wanayopewa,” alisema Nantanga.

Alisema kuendelea kushikiliwa kwa baadhi ya watu waliokamatwa na kunyimwa dhamana kunatokana na jeshi hilo kutojiridhisha au kutokamilika kwa taratibu za dhamana.

“Pale mtuhumiwa atakapoachiwa, ni lazima polisi wajiridhishe kabla ya kumpatia dhamana mtuhumiwa. Hadi hivi sasa, kama wizara hatujapokea tamko lolote kuhusu jambo hili, tunasubiri kupokea rasmi tamko, na tutaliweka mezani na kulifanyia kazi,” aliongeza.

LAANA KUBWA HII...!! MAHAKAMA KUU YAKUBALI OMBI LA VYAMA VYA MASHOGA KUSAJILIWA !

Mahakama Kuu ya Kenya.
Katika hatua ya kushitua, Mahakama Kuu nchini Kenya imesalimu amri mbele ya mashinikizo ya watetezi wa vitendo vichafu vya ulawiti, usagaji, ushoga na kusema kuwa sasa watu wanaojihusisha na vitendo hivyo vya uasherati wanaweza kusajili mashirika ya kile kinachodaiwa ni kutetea haki zao za kibinadamu.
Majaji watatu wa mahakama hiyo wameiamuru Bodi ya Kusimamia Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGOs) kulitambua na kulisajili shirika moja ambalo awali mahakama hiyo ilizuia lisajiliwe kwa sababu za kimaadili na kidini.
Jopo hilo la majaji Isaac Lenaola, Mumbi Ngungi na George Odunga limedai kuwa, katiba ndio marejeo ya kila kitu nchini Kenya na kwamba serikali haitakiwi kuzingatia mafundisho ya kidini katika maamuzi yake ambayo kwa mujibu wa majaji hao, maamuzi hayo yananyima kundi fulani la watu uhuru wao.
Uamuzi huo umechukuliwa huku mashinikizo ya nchi za Magharibi dhidi ya nchi za Afrika ya kuzitaka zitambue rasmi vitendo hivyo vichafu yakizidi kupamba moto.
Nchi za Magharibi yametishia kuzinyima misaada nchi za Afrika iwapo hazitatambua rasmi vitendo vya ulawiti na usagaji.
Hatua ya Mahakama Kuu ya Kenya imechukuliwa pia katika wakati huu wa kukaribia ziara ya Rais Barack Obama wa Marekani nchini Kenya ambaye ni mtetezi mkuu wa vitendo hivyo vichafu.
CHANZO: IRAN SWAHILI

YULE MWANAJESHI ALIYEWASHIKISHA "ADABU" MAJAMBAZI WALIOTAKA KUMPORA SILAHA,...RAIS KIKWETE AMTUNUKU NISHANI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akimvalisha  Cpl Laura Philip Mushi  Nishani ya Ushupavu wakati wa utoaji wa Nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano.
Koplo Laura Mushi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ni miongoni mwa Watanzania 42 waliotunukiwa nishani na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu juzi Dar es Salaam.
Laura alitunukiwa Nishani ya Ushupavu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Katika hafla hiyo Rais Kikwete alitunuku Nishani ya Kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Daraja la Pili, la Tatu na la Nne, Nishani ya Muungano Daraja la Pili na Nishani ya Ushupavu.
Kabla ya kupokea nishani hiyo, ilielezwa kwamba usiku wa Machi 14 mwaka huu, Koplo Laura , akiwa kwenye kituo chake cha ulinzi, alivamiwa na kundi la majambazi waliomkaba kwa kamba na kumburuza kwa lengo la kutaka kumuua na kupora bunduki aliyokuwa nayo ikiwa na risasi 30.
Ilielezwa kwamba wakati majambazi hao wakimburuza kutoka katika lindo lake, Koplo Laura alijitahidi na kufanikiwa kudhibiti kamba hiyo isimnyime pumzi kwa kuwa walikwisha mfunga shingoni, huku akipambana kuzuia asinyang’anywe bunduki aliyokuwa nayo na kufanikiwa.
Alifanikiwa kuidhibiti kamba hiyo na kisha kuifikia chemba ya risasi ya bunduki na kuweza kufyatua risasi nne huku akiburuzwa.
Hali hiyo iliwafanya majambazi hao kumwachia na kukimbia, hivyo kuokoa maisha yake na silaha aliyokuwa nayo.
“Kitendo hicho kimeonyesha ushupavu, uzalendo na heshima ya hali ya juu kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania na wanawake wote nchini,” alisema mshereheshaji wa shughuli hiyo.
Akizungumza baada kupokea tuzo hiyo, Koplo Laura alisema: “Sikutarajia kupata nishani hii, imenitia moyo, nguvu na morali zaidi wa kufanya kazi kuilinda nchi yangu, pia kuonyesha kwamba inawezekana kila palipo na juhudi. Ninamshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa kutambua mchango wangu.”
Katika hafla hiyo, watu wengine wa kada mbalimbali wakiwamo wanasiasa, watumishi wa umma pia wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wastaafu na majaji wastaafu walitunukiwa nishani.
Kupitia nishani hizo, Rais Kikwete pia amemkumbuka marehemu Brigedia Jenerali Moses Nnauye aliyekuwa Katibu wa Oganaizesheni wa CCM na mwasisi wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), aliyetunukiwa Nishani ya Kumbukumbu ya Muungano Daraja la Tatu.

GOOD NEWS: Majambazi Matatu (3) Yauawa na Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma


JESHI  la Polisi Mkoani Kigoma limefanikiwa kuuwa majambazi watatu baada ya kurushiana risasi na kukamata silaha mbalimbali za kivita.

Akizungumzia tukio hilo ofisini kwake Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kigoma,Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Frednand Mtui alisema kuwa majira ya saa nane usiku katika eneo la  mto kahabwe mpakani mwa Wilaya ya Kakonko na Kibondo, askari Polisi wakiwa doria walirushiana risasi na majambazi ambao idadi yao haijajuikana na kufanikiwa kuwauwa majambazi watatu.

Alisema wamefanikiwa kukamata silaha moja aina ya AK.47 yenye namba 10363 ikiwa na risasi 11 ndani ya magazine na risasi 22 za SMG ndani ya mfuko wa rambo pamoja na mabomu 2 ya kutupa kwa mkono .

Kamanda Mtui alisema kuwa aina ya mabomu waliyokutwa nayo majambazi hao ni offensive handgrenade namba Y.3PM-2 na jingine ni aina  ya deffensive handgrenade ambalo namba zake hazisomeki.

''Leo ilikuwa ni siku ya mnada hivyo inaonekana majambazi hao walijipanga kwenda kupora mali na pesa katika mnada wa leo,tunawashukuru raia wema kwa kutoa taarifa mapema na kufanikiwa kuwanasa majambazi hao na kuwauwa''alisema Kamanda Mtui

Alisema maiti za majambazi wote watatu ambao majina yao hayajafahamika ila wote wana umri kati ya miaka 25-35 zimehifadhiwa katika Wilaya ya Kibondo na upelelezi wa tukio hilo unaendelea.

Askofu Pengo: Nasumbuliwa na uti wa mgongo, Watanzania Chagueni Rais Masikini

Hatimaye Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amewatoa hofu Watanzania kuhusu afya yake kwa kueleza kuwa anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa uchunguzi wa matatizo yake ya uti wa mgongo.

Kardinali Pengo pia amegusia nafasi ya urais katika Uchaguzi Mkuu ujao kwa kuwataka watanzania kumchagua rais fukara kuliko anayetafuta nafasi hiyo kwa rushwa.

Alitoa kauli hiyo katika mahafali ya Saba ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph, Dar es Salaam jana.

Alisema maradhi ya uti wa mgongo ambayo yamekuwa yakimsumbua kila yaligundulika Agosti mwaka 2013 baada ya kufanyiwa uchunguzi wa afya, Ujerumani.

“Hospitali ya Ujerumani ndiyo waligundua kuwa nyuzi mbili ndani ya uti wa mgongo zimechanika zinabana mashipa ya neva, kwa hiyo zikawa zinanisababishia maumivu ya mgongo.

“Kule Ujerumani walizirudisha katika nafasi yake lakini kwa bahati mbaya hawakufunga huku wakitegemea kuwa mambo yatakwenda vizuri kwa njia ya kawaida.

“Lakini kwa sababu ya kurukaruka nikajiona kama nimepona ila baada ya muda kidogo maumivu yasio ya kawaida yalirudi tena,” alisema kiongozi huyo wa kiroho.

Alisema maumivu yalipozidi Juni mwaka jana alisafiri kwenda Hospitali ya Manipal, Bangalore, India kwa uchunguzi zaidi.

“Walinihudumia vizuri na kwa sasa naendelea vizuri … kwa wale wanaojali uhai wangu nilipokwenda mara ya mwisho kwenye uchunguzi waliniambia kila kitu kimekaa kwenye nafasi yake.

“Madaktari walinielezea kuwa nisishangae maumivu ya mara kwa mara kwa sababu operesheni ilikuwa kubwa.

“Kwa sababu operesheni ya sasa itachukua muda kati ya miaka miwili hadi mitatu niweze kujisikia mzima kabisa. Kwa sasa naendelea vizuri sina tatizo zaidi,” alisema.

Kuhusu Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu, Kardinali Pengo alisema ni kitu kibaya kama viongozi wanaowania nafasi ya urais wanatoa rushwa.

“Uongozi wa Taifa hauwezi kununuliwa kwa gharama yoyote… wanaoelekea kutoa rushwa baadaye watataka sisi wananchi tulipe zile gharama ambazo walikuwa wametugawia katika kutoa rushwa, afadhali waache kabisa.

“Ni vizuri tupate rais anayekuwa fukara lakini anayependa nchi yetu na hatatudai gharama ya kumchangua kama si hivyo gharama inaweza kuwa kubwa ikatusababishia matatizo,” alisema.

Kardinali Pengo pia alizungumzia matukio ya ugaidi na kuwataka wanaosambaza ujumbe fupi wa vitisho kuacha mara moja tabia hiyo kwa vile inawaweka wananchi katika hofu.

“Wanaweza kusababisha taharuki na mikanganyiko na kuleta madhara kwa wengi kwa kitu ambacho hakipo.

“Kama kuna hofu ya usalama sehemu yoyote inabidi tuwaachie wataalamu wa usalama waweze kuishughulikia kwa namna wajuavyo,” alisema.

Hata hivyo, aliitaka serikali kupitia Idara ya Usalama kuwa ya kwanza kuwahakikishia wananchi kuwa hakuna matukio hayo amani na utulivu viendelee kuwapo.

Pia aliwashauri wahitimu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Josesph kuwa wasisome kwa ajili ya kuajiriwa na serikali tu.

“Kuna nafasi za wataalamu wa sayasi na sanaa za kujiajiri katika chuo hiki … Chuo kikuu kizuri ni kile kinachoandaa wanafunzi kujiajiri,” alisema.

Mkuu wa Chuo hicho, Padre Aru Raji alisema chuo kinazidi kupanuka na mwaka huu kinatarajia kufungua Chuo Kikuu Sumbawanga na Chuo cha Afya na Tiba, Boko, Dar es Salaam.

Msaidizi Wa Gwajima Afikishwa Mahakamani...Aachiwa Kwa Dhamana Hadi Mei 4 Mwaka Huu !


Msaidizi wa Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, George Mzava, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
 
Mzava (43), mfanyabiashara na mkazi wa Ilala, Dar es Salaam, alifikishwa  mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka ya kukutwa na bastola ya kiongozi huyo na risasi kinyume cha sheria.
 
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka, alimsomea Mzava mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi, Wilfred Dyansobera, baada ya mshitakiwa huyo kujisalimisha.
 
Mzava akisindikizwa na wakili wake, Peter Kibatala, alifika mahakamani hapo ili kusomewa mashitaka yanayomkabili katika kesi iliyofunguliwa Ijumaa iliyopita, ambayo washitakiwa wenzake watatu, akiwemo Gwajima, walisomewa mashitaka yao.
 
Washitakiwa wengine katika kesi hiyo, ambao walisomewa mashitaka yanayowakabili Ijumaa na kuachiwa kwa dhamana ni Askofu Msaidizi Yekonia Bihagaze na Mchungaji Geoffrey Milulu.
 
Katika kesi hiyo, washitakiwa wote wanne wanakabiliwa na mashitaka matatu.  Gwajima anakabiliwa na shitaka la kushindwa kuhifadhi silaha na risasi anazomiliki kihalali katika usalama huku wengine wakidaiwa kukutwa nazo kinyume cha sheria.
 
Akimsomea mashitaka yanayomkabili Mzava, Kweka alidai Machi 29, mwaka huu, katika Hospitali ya TMJ, Mikocheni A, jijini Dar es Salaam, mshitakiwa huyo na wenzake, Bihagaze na Milulu, walikutwa na bastola aina ya Bereta bila  kuwa na kibali au ruhusa kutoka katika mamlaka zinazohusika.
 
Katika shitaka la pili, Mzava na wenzake hao wanadaiwa siku hiyo wakiwa hospitalini hapo, walikutwa na risasi tatu za bastola na 17 za bunduki aina ya shotgun bila kuwa na kibali au ruhusa kutoka mamlaka zinazohusika.
 
Mshitakiwa huyo alikana mashitaka hayo, ambapo Wakili Kweka alidai upelelezi haujakamilika na kuomba shauri hilo kuahirishwa hadi tarehe nyingine kwa kutajwa.
 
Hakimu Dyansobera alitoa masharti ya dhamana kwa kumtaka mshitakiwa kutia saini dhamana ya sh. milioni moja na kuwa na mdhamini mmoja mwaminifu atakayetia saini dhamana ya kiasi hicho.
 
Mshitakiwa alitimiza masharti hayo, hivyo aliachiwa kwa dhamana hadi Mei 4, mwaka huu, kesi itakapotajwa.

MEMBE: HAKUNA MTANZANIA ALIYEUAWA AFRIKA KUSINI


Waziri wa Mambo ya  Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,  Bernard Membe akitoa tamko.
…Akisisitiza jambo.
Sehemu ya wanahabari na wageni wengine waliofika kwenye hafla hiyo.
WAZIRI wa  Mambo ya  Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema kuwa hakuna  Watanzania waliouawa nchini Afrika Kusini kutokana na machafuko yanayoendelea nchini humo.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Membe amesema kuwa serikali itawarudisha watu 21 tu ambao wamepata matatizo ya kuvamiwa  na ambao wako Ubalozi wa Tanzania wakiwa wamehifadhiwa.
 

Alisema kuwa serikali kamwe haitamrejesha Mtanzania yeyote  ambaye atatumia machafuko hayo yanayoendelea nchini humo kama njia ya kurudi Tanzania, kwani wapo Watanzania wengi wako huko na hawana vibali vya kuishi nchini humo.
Vilevile, alisema kuwa jambo ambalo serikali inasubiri kwa sasa ni kupata ruhusa kutoka ubalozi huo ili kuwarejesha Watanzania hao  waliokubali kurudi nyumbani.
Membe amekanusha  taarifa zilizokuwa zikiripotiwa kwenye mitandao ya kijamii  na baadhi ya vyombo vya habari  vikidai kuwa Watanzania watatu wamefariki kutokana na machafuko hayo.  Alisema Watanzania hao watatu wamefariki kutokana na magonjwa na si kwa sababu ya machafuko hayo
 

Amewataja watu hao kuwa ni Athumani China ambaye amekufa kutokana na kupigwa na wananchi wenye hasira baada ya kumpora mzawa wa huko.  Mwingine ni Ally Mohamed aliyefariki kutokana na kifua kikuu, na mwingine aliyefia gerezani.
Waziri huyo amewataka Watanzania waishio nje ya nchi kupendana na  kuwa pamoja ili matatizo kama hayo yanapotokea iwe rahisi kwa serikali kutoa msaada.

AIBU! ASKOFU KKKT APIGA MIMBA MBILI NJE YA NDOA!


Joseph Ngilisho, Arusha
Aibu! Peace Sylvester (36), mkazi wa Kijenge Juu jijini hapa amefungua madai mazito kwenye Kituo Kikuu cha Polisi, Arusha  kwa majadala mawili,  AR/RB/4404/2015 KUTISHIA KUUA KWA MANENO na AR/RB/5290/2015 KUTELEKEZA FAMILIA dhidi ya Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe, Kagera, Benson Bagonza.

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe, Kagera, Benson Bagonza.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda jijini hapa katikati ya wiki iliyopita, Peace alidai Askofu Bagonza ni mzazi mwenzake kwa kuzaa naye watoto wawili, Piana Bagonza (6) na Bariki Bagonza (3) lakini akadai amemtelekeza hivyo kuwa na maisha magumu katika kuwalea watoto hao.
AANIKA HISTORIA NDEFU
Peace alisema alianza kufahamiana na askofu huyo mwaka 2006 mjini Karagwe, Kagera akiwa ni muumini wa kanisa hilo akimtumikia Mungu kwa kuimba kwaya ya kanisa.
Alisema katika kuonana mara kwa mara na askofu huyo ndipo uhusiano ukaanza lakini kwa makubaliano ya kutunza siri.

“Askofu aliniambia ana mke lakini ananipenda na anataka kuwa na uhusiano na mimi. Aliniahidi kunisaidia masuala mbalimbali iwapo nitamkubalia.“Baada ya muda niliamua kumkubalia, tukawa na uhusiano na tulikuwa tunakutana mara kwa mara. Ilipofika mwaka 2008 nikapata ujauzito wa mtoto wa kwanza,” alisema Peace.
AHAMIA ILEMELA, MWANZA
Mwanamke huyo aliendelea kudai kuwa, baada ya kupata ujauzito, askofu huyo aliamua kumhamishia Ilemela mkoani Mwanza  na kumpangishia chumba ambapo mwaka 2009 alijifungua mtoto wa kike, Piana.

AHAMIA ARUSHA
Peace aliendelea kudai: “Mtoto wangu alipofikisha umri wa miaka miwili, yaani mwaka 2010, askofu  alinihamishia hapa Arusha na kunipangia chumba eneo la Kijenge Juu na kunitafutia kazi kwenye Hoteli ya Safari (New Safari Hotel). Hii hoteli inamilikiwa na KKKT.” Alisema: “Askofu alikuwa akija hapa Kijenge kumsalimia mtoto na kumwachia matumizi mbalimbali huku akisisitiza kutunza siri zaidi.”

Peace anayedai kutelekezwa pamoja na watoto na Askofu Benson Bagonza.
ANASA MIMBA YA PILI
“Ilipofika mwaka 2011 nilipata ujauzito mwingine wa askofu ila cha kushangaza nilipomfahamisha aliniambia hataki kusikia taarifa hizo.“Niliweka msimamo wa kutotoa ujauzito na yeye akasitisha huduma mbalimbali ikiwemo fedha za malipo ya chumba alichonipangia.

“Alianza kunipigia simu na kunitisha kuniachisha kazi aliyonitafutia hotelini bila kupewa malipo yoyote. Alikuwa akinitumia watu mbalimbali kunitishia maisha. “Kutoka na hali hiyo nililazimika kumtafuta kiongozi mmoja wa ngazi ya juu kanisani na kumwambia jinsi askofu alivyonitelekeza kwa zaidi ya miaka minne bila kunihudumia nikiwa na watoto wake wawili.
“Hata hivyo, kiongozi huyo aliniambia atalishughulikia suala langu, lakini hadi sasa hakuna kinachoendelea na nikimkumbusha amekuwa akinijibu kwa ukali na kunikatia simu.”
WATOTO HAWAENDI SHULE
Peace alisema: “Kwa sasa naishi kwa shida na watoto. Hawaendi shule baada ya kukosa ada.”

Watoto anayedai kutelekezwa nao.
ASKOFU NA IJUMAA WIKIENDA
Akizungumza kwa simu na gazeti hili huku akihifadhiwa sauti, Askofu Bagonza alikiri kumtambua Peace kama mzazi mwenzake ila alisema si kweli kama hamtumii matumizi.“Mbona fedha huwa namtumia labda ameamua kunichafua tu. Hata juzi nimemtumia shilingi 250,000 iweje asema simhudumii?” alisema askofu huyo na kukata simu.

Kwa upande wake, Peace alipoulizwa kuhusu kutumiwa kiasi hicho cha fedha, alisema: “Fedha  hizo nilizipokea kutoka kwa wakala wa M-Pesa baada ya jambo hilo kulifikisha kwenye vyombo vya dola (polisi).”Taarifa zilizolifikia gazeti hili wakati linakwenda mitamboni zilieleza kuwa mwanamke huyo ameitwa Karagwe kwenda kuongelea suala hilo.
Older Posts
© Copyright ZEE LA UDAKU | Designed By Code Nirvana
Back To Top