WAJUKUU wa marehemu Sabina Ngalu (77) wameibua kutuko makaburini kufuatia kuzama ndani ya kaburi la marehemu huyo na kugoma kutoka wakidai kwamba mpaka walipwe shilingi laki moja (100,000), Uwazi lina mkanda mzima.
Tukio hilo la aina yake lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita katika Kitongoji cha Nyamwanza Kata ya Sima wilayani Sengerema mkoani Mwanza muda mfupi baada ya mwili wa marehemu kuwasili eneo la mazishi kwenye shamba lake ukitokea Kanisa la Roman Katoliki Parokia ya Yesu Kristo Mfalme la mjini Sengerema.
Sababu za wajukuu hao kung’ang’ania ndani ya kaburi hilo walitaka wapewe ng’ombe mmoja au pesa hizo taslimu kwa mjibu wa mila na desturi za kabila la Kisukuma jambo ambalo lilipingwa na baadhi ya wanandugu waliodai mila hizo zilipitwa na wakati.
Kufuatia wajukuu hao kuendelea kugomea ndani ya kaburi, kaka wa marehemu, Enosi Ngalu alikwenda kukata fimbo na kuwashukia kisha kuwacharaza viboko wote huku nao wakisisitiza hawatoki mpamka ‘kieleweke’.
Baadhi ya wajukuu walioonja joto la jiwe ya kuchapwa viboko ni Andrea Mabula, Sabina Bukuru, Johari Bukuru, Asha Bukuru, Faida Bukuru, Yuves Petro, Semeni na kiongozi wao, Enos Ntilaga.
Kitendo cha wajukuu hao kuendelea kugoma kutoka kaburini kilimchefua Padri Nicodemus Mayalla ambaye pia ni Paroko wa Parokia ya Yesu Kristo Mfalme, Sengerema ambaye aliamua kuondoka eneo la maziko huku akiwataarifu polisi kuhusiana na vurugu hizo.
Kufuatia hali hiyo, mmoja wa waombolezaji alizama mfukoni na kutoa kiasi hicho cha pesa na kuwapa ndipo walipokubali kutoka dani ya kaburi hilo ili mazishi yaendelee.
Ili kuonesha alikerwa na kitendo hicho, Padri Mayalla ambaye kwa wakati huo alikuwa amewekwa chini na baadhi ya ndugu wakimsihi kutosusia mazishi hayo, aligoma kurejea kaburini kuongoza ibada ya mazishi.
Baada ya vuta nikuvute, hatimaye Padri Mayalla alikubali kuendelea na ibada lakini aliwataka wajukuu hao kurudisha pesa waliyochukua na kuwaomba radhi wana mtaa huo na ndipo yeye aweze kurudi kaburini.
Wajukuu hao waliitwa mbele ya padri huyo na mbele ya wana mtaa, wakaomba samahani ikiwa ni pamoja na kurudisha kitita hicho cha pesa paroko huyo naye akarejea kaburini na kuongoza ibada ya mazishi.
Hata hivyo, wakati ibada ikiendelea polisi zaidi ya wanne kutoka Kituo cha Polisi Sengerema wakiwa na bunduki aina ya Sub Machine Gun (SMG) na mabomu ya machozi walifika eneo la tukio ili kuhakikisha amani na utulivu vinatawala.
Cha kushangaza, saa baada ya kutoka makaburini, wajukuu hao waliwahi nyumbani kwa marehemu, Mtaa wa Mlimani, Kata ya Nyatukala wilayani Sengerema na kuanzisha timbwili jingine kwa kuficha chakula na vyombo vya kupakulia wakidai warudishiwe pesa yao waliyoirejesha makaburini kwa shinikizo la baba paroko.
Baada ya timbwili hilo kukolea, mmoja wa wafiwa alizama mfukoni na kutoa shilingi laki moja na kuwakabidhi wajukuu hao ambao walirudisha chakula jikoni na taratibu za waombolezaji kupata chakula ziliendelea.
Hizi ndio sehemu 12 zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, Bonyeza Hapa chini== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO CHAFU YA AGNESS MASOGANGE== >