Watu wasiojulikana wamemuua Mwalimu Dionizi Ng’wandu wa Shule ya Sekondari Kagemu iliyopo nje kidogo ya Mji wa Bukoba na kumkata mguu mtu mwingine wakati wakifanya maombi kanisani.
Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Ijumaa
wakati mwalimu huyo pamoja na mwenzake aliyetambuliwa kwa jina moja la
Themistocles ambao ni waumini wa Kanisa la Pentecostal Asemblies of God
(PAG) walipoamua kuendelea na mkesha baada ya wenzao kuondoka.
Kwa mujibu wa Mchungaji wa kanisa hilo, Faustin
Joseph saa chache kabla ya mauaji hayo walikuwa wakifanya maombi wakiwa
kundi la watu wanne na ilipofika saa tano usiku waliondoka na kuwaacha
wenzao wawili.
‘’Tunao utaratibu wa kufanya maombi, ilipofika saa
tano usiku mimi na mwenzangu mmoja tuliondoka na kuwaacha wenzetu
wawili na ilipofika saa nane usiku nilipigiwa simu na majirani kuwa kuna
mauaji yamefanyika kanisani,’’ alisema mchungaji huyo.
Pia, mchungaji huyo alibainisha kuwa wauaji hao
hawakuchukua mali yoyote na kuwa siku chache kabla ya mauaji hayo watu
wasiojulikana walivamia kanisani hapo na kuiba viti pamoja na vitambaa
jambo alilosema liliwafanya waone umuhimu wa kuchukua tahadhari.
Akizungumzia mauaji hayo Mwenyekiti wa Makanisa ya
Kipentekoste mkoani Kagera, Crorwad Edward alisema tukio hilo
limewaletea mshtuko na kuwa wanajiandaa kutoa tamko kwa kuwa pia
yaliwahi kuwepo matukio ya kuchoma moto makanisa.
Akithibitisha kuwapo kwa mauaji hayo, Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Kagera, Henry Mwaibambe alisema muumini huyo ni Mwalimu
wa Sekondari ya Kagemu na kuwa majeruhi aliyekatwa mguu amelazwa katika
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa.
Pia, alisema kuwa tayari wameanza uchunguzi
kuhusiana na mauaji hayo aliyosema yamefanywa na watu wanne na kuwa
mtuhumiwa mmoja amekamatwa kwa ajili ya mahojiano na kuahidi kutoa
taarifa zaidi baadaye.
Hizi ndio sehemu 12 zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, Bonyeza Hapa chini== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO CHAFU YA AGNESS MASOGANGE== >