Ni mambo ya kushangaza sana ambayo yamenaswa na Gazeti la Uwazi katika Kisiwa cha Mafia Mkoa wa Pwani ambapo mwanamke mmoja aitwaye Mwasiti Ally wa Kijiji cha Kanga, amewafungia wanaye watatu kwa miaka kumi ndani ya chumba kimoja kwa madai kuwa ni wagonjwa wa akili.
Uwazi
lilipata habari hizi kupitia kwa watu waishio Mafia na kuamua kufunga
safari hadi kisiwani humo kufuatilia tukio hilo la aina yake.
Baada
ya kufika Mafia mjini, Uwazi liliendelea na safari ya umbali wa
kilomita 40 kutoka mjini hadi kwenye kijiji hicho kwa ajili ya
kuthibitisha madai hayo ya kushangaza.
Kabla
ya kuzungumza na mama huyo, Uwazi lilibahatika kuwapata majirani ambapo
mmoja wao alisema watoto hao ambao ni baba mmoja, mama mmoja, walianza
kuwa katika hali ya kushangaza kiakili mwaka 2001.
“Alianza
mtoto mmoja ambaye ni wa kwanza kuzaliwa. Cha ajabu, kila mwaka
mwingine akafuatia hadi wa tatu. Jambo hilo liliishangaza familia na
hata sisi majirani,” alisema jirani mmoja.
Naye mama mzazi wa watoto hao akizungumza na Uwazi alisema: “Ni kweli watoto wangu hawa wana matatizo ya akili, hawako sawa. Nateseka nao sana.
“Ilikuwa mwaka 2001, binti yangu mkubwa, Muhadia Juma (pichani) ndiye alianza, tukajaribu kumfikisha hospitali lakini hakuwa vizuri.
“Ilikuwa mwaka 2001, binti yangu mkubwa, Muhadia Juma (pichani) ndiye alianza, tukajaribu kumfikisha hospitali lakini hakuwa vizuri.
"Mwaka 2002 akafuatia mdogo wake aitwaye Ally Juma. Nikashangaa ni nini?
“Nikiwa nahangaika nao hawa, mwaka 2003 akafuatia mdogo wao, anaitwa Mzee Juma. Nilizidi kuchanganyikiwa kabisa.”
“Nikiwa nahangaika nao hawa, mwaka 2003 akafuatia mdogo wao, anaitwa Mzee Juma. Nilizidi kuchanganyikiwa kabisa.”
Mwanamke
huyo alisema amejaliwa kuzaa watoto saba, watatu ambao wote ni wakubwa
ndiyo wamepatwa na matatizo ya akili na wanne ambao ni wadogo wapo sawa
na wameolewa wakiendelea na maisha yao ya ndoa.
Akiendelea
kuzungumza na Uwazi, mwanamke huyo ambaye ni mjane alisema baada ya
kuona hali inazidi kuwa mbaya alianza kutafuta watu wa kumsaidia ambapo
alizunguka kwa waganga mbalimbali wa kienyeji akiamini wanaye hao
wamerogwa.
“Nimehangaika
sana ndugu mwandishi lakini kikubwa kwa watoto wangu wana matatizo ya
akili hadi hivi sasa nimekwishafika sehemu mbalimbali, ikiwemo Hospitali
ya Wilaya ya Mafia lakini hakuna mafanikio,’’ alisema mama huyo.
Hata
hivyo, aliongeza kusema kuwa tangu mwaka 2003 aliona imeshindikana na
watoto hao wanazidi kufanya mambo ya ajabu ikiwemo kuwaogopa watu,
kuchekacheka, kula kwa fujo na kutojijali pia kukimbilia eneo la
baharini.
Mwasiti
alisema muda wote huo alikuwa akiishi nao nyumba moja lakini ilipofika
mwaka 2005 aliamua kuomba msaada kwa watu ili wajengewe kijumba chao
waweze kuishi humo wenyewe ambapo ilimlazimu awafungie ndani hadi hivi
leo.
Wote
wamebadilika na kuwa na afya mbaya huku kucha za mikononi na miguuni
kurefuka sana, nywele zimekua ndefu kiasi cha kutisha na sura zao
kuonekana kama za misukule na kuwa kama walemavu wa miguu. Lakini mama
mtu anatoa sababu ya kuwafungia:
“Sababu kubwa ya kuwafungia ndani tangu mwaka 2005 ni usalama wao. Niliamini kwa kuwaachia tu wangeweza hata kupotea.
“Sababu kubwa ya kuwafungia ndani tangu mwaka 2005 ni usalama wao. Niliamini kwa kuwaachia tu wangeweza hata kupotea.
“Miezi ya hivi karibuni nilishanga sana kumwona Muhadia ana ujauzito, aliyempa ni Mzee ambaye kidogo bado anajiweza kinguvu."
Mama huyo alisema baada ya kubaini Muhadia kupata ujauzito, familia ilijitahidi kuwa naye karibu hadi siku ya kujifungua ambapo alijifungua mtoto wa kiume na kupewa jina la Hassan Abdallah (Abadallah si baba).
Mama huyo alisema baada ya kubaini Muhadia kupata ujauzito, familia ilijitahidi kuwa naye karibu hadi siku ya kujifungua ambapo alijifungua mtoto wa kiume na kupewa jina la Hassan Abdallah (Abadallah si baba).
Inadaiwa
kuwa, siku ya uchungu wa Muhadia, familia ilishirikiana na uongozi wa
kijiji wakafanikiwa kumpeleka katika hospitali ya wilaya ambapo
alijifungua salama.Baada ya kujifungua, Muhadia alirudishwa kijijini
lakini baada ya siku 21, mtoto Hassan alifariki dunia na kuzikwa
kijijini hapo.
Naye
mjumbe wa mtaa aliyejitambulisha kwa jina la Mzee Seleman alipoulizwa
kuhusu hali ya familia hiyo alisema ni kweli mjane huyo amekuwa akiishi
na watoto hao kwa shida sana zaidi ya miaka kumi sasa tangu walipoanza
kupata matatizo.
“Watoto
wale wanamsumbua sana mama yao, wamekwisha changiwa fedha kwa ajili ya
matibabu ya matatizo waliyonayo lakini hadi leo hakuna mafanikio kama
unavyowaona,’’ alisema mjumbe huyo.
“Inawezekana
wakipata msaada hata kama akili hazitakuwa sawa lakini afya zao
zitaimarika kwani kwa sasa kila kitu wanafanyia mlemle ndani, ikiwemo
kujisaidia.
“Hakuna mtu mwingine anayeweze kuingia katika chumba walichofungiwa zaidi ya mama yao mzazi tu,” alisema mjumbe huyo.
“Hakuna mtu mwingine anayeweze kuingia katika chumba walichofungiwa zaidi ya mama yao mzazi tu,” alisema mjumbe huyo.
Kwa
hali ya familia hiyo, kunatakiwa nia ya makusudi kwa serikali, taasisi
na watu binafsi kwenda kutoa elimu za kijamii ikiwemo kuishi na watu
wenye ulemavu na kadhalika, kwani inaonekana elimu bado ni tatizo kwa
eneo hilo kiasi kwamba, kuwafungia wagonjwa hao ndani haionekani kama ni
suala linaloweza kumfikisha mtu kwenye nyombo vya sheria.
Ushahidi
wa uduni wa elimu unaonekana hata kwenye kujua mambo muhimu. Mfano,
mwanamke huyo hajui tarehe, mwezi na mwaka wa kuzaliwa mtoto wake hata
mmoja kati ya watoto wote saba!
Chanzo: Gazeti la Uwazi/Gpl
Chanzo: Gazeti la Uwazi/Gpl
Hizi ndio sehemu 12 zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, Bonyeza Hapa chini== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO CHAFU YA AGNESS MASOGANGE== >