POLISI mkoani Katavi inamshikilia mkazi wa kitongoji cha Ntumba, kijiji cha Mnyengele wilayani Mpanda, Deogratius Pastory (30) kwa kumjeruhi vibaya mkewe kwa kumkata mkono wake wa kushoto na kupasua tumbo la mpenzi wa mkewe kwa panga.
Mtu
huyo aliwatendea unyama huo baada ya kuwafumania mkewe aitwae Tabu
Nestory (20) na mpenzi wake wa kiume aitwaye Masaga Elias (28 wakifanya
mapenzi katika jiko la nyumbani kwake kijijini humo.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari alithibitisha mkasa huo.
Alisema tukio hilo ni la Machi 23, mwaka huu saa tano usiku katika
kitongoji cha Ntumba katika kijiji cha Mnyengele.
Akielezea
mkasa huo, Kidavashari alidai kuwa jioni ya siku hiyo ya tukio,
mtuhumiwa alimuaga mkewe Tabu kuwa anakwenda kijiji ambacho kiko umbali
mrefu kutoka kijijini hapo kwa ajili ya kuangalia shamba lao.
Inadaiwa
mtuhumiwa huyo alitumia baiskeli yake katika safari yake hiyo. Kwa
mujibu wa Kamanda Kidavashari, wakati mtuhumiwa huyo akiendelea na
safari yake ghafla baiskeli yake aliyokuwa akiitumia katika safari yake
hiyo iliharibika, wakati huo ilikuwa tayari imetimu saa tatu usiku .
“Kwa
sababu alikuwa bado amebakiza mwendo mrefu kufika alikokuwa akienda
aliamua kugeuza na kuanza kurejea nyumbani kwake, ambako alifika saa
tano usiku …na alipofika kwake alimkuta mkewe na mpenzi wake wakifanya
mapenzi katika jiko nyumbani kwake,” alieleza.
Inadaiwa
kuwa kitendo hicho kilimkasirisha mtuhumiwa, ambaye alimwamuru mkewe na
mgoni wake kuingia ndani, ambapo alimkamata mwanamume huyo na kumfunga
kamba mikononi, kisha akachukua panga na kumchana tumbo chini ya kitovu
hadi utumbo wake ‘ukamwagika’ nje .
Kwa
mujibu wa Kamanda Kidavashari, mtu huyo alitumia panga hilo alilotumia
kuchana tumbo la mgoni wake, kukata mkono wa kushoto wa mke wake.
Kidavashari
alidai kuwa majeruhi wote wawili, walikimbizwa katika Hospitali ya
Wilaya ya Mpanda mjini hapa, ambako wamewalazwa kwa matibabu, ambapo
mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara tu upelelezi wa awali wa shauri
lake utakapokamilika.
Hizi ndio sehemu 12 zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, Bonyeza Hapa chini== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO CHAFU YA AGNESS MASOGANGE== >