Habari Kali
Loading...

Dereva Wa Bajaji Asimulia Jinsi Magaidi 10 Walivyonaswa Morogoro Wakiwa Na Silaha Msikitini...Imamu Awakana 'Magaidi' Hao

Mbinu Za Kumfikisha Kileleni Mwanamke Mwenye Makalio Makubwa Kwa Haraka, Bonyeza Hapa chini== >

Siku moja baada ya Jeshi la Polisi kukamata watu tisa waliokuwa na milipuko, sare za jeshi na silaha za jadi msikitini mkoani Morogoro, imebainika kuwa walikamatwa saa tatu kabla ya kutoka kwenye eneo hilo na kwenda kutekeleza azma yao.
 
Ingawa haijajulikana kuwa watu hao walikuwa waende wapi, habari hizo zimebainisha kwamba walipanga kuondoka saa 11 alfajiri, lakini polisi wakawakamata saa nane usiku.
 
Mwandishi wetu alivyofika kwenye Kijiji cha Chikago, Kata ya Kidatu wilayani Kilombero, alibaini kuwa watu hao walifika kwenye msikiti huo – Masjid Salah Al–Fajih – saa nne usiku na kuingia ndani huku wenyeji wakiwa hawapo.
 
Ilibainika kuwa katika msikiti huo wa Sunni kuna watoto wanne wenye umri kati ya miaka 12 na 16 huwa wanalala, lakini wakati wahalifu hao wanafika hawakuwapo.
 
Watoto hao ambao hawakutaka kutaja majina yao, walisema wakati watu hao wanaingia msikiti hapo, wao walikuwa wameenda kutafuta chakula cha usiku.
 
“Tulivyorudi tulikuta kuna watu wamelala kwenye mikeka, tukawasalimia ‘assalam alaykum’ wakatuitikia. Hatukuendelea kuwasemesha kwa sababu tulijua watakuwa wageni wa Imamu wa msikiti.
 
"Kwa mbele kuna mlango huwa tunaufunga wakati tukitaka kulala, lakini siku hiyo tulipotaka kuufunga ili tulale walitukataza wakasema kuwa wataondoka alfajiri kwa hiyo tusiufunge,” alisema.
 
Watoto hao walisema kati ya mazungumzo machache waliyoweza kufanya na watu hao, walibaini kuwa baadhi wanatoka Kilimanjaro, Tanga, Arusha na Singida.
 
Walisema kabla ya kufika asubuhi, majira ya saa nane usiku walifika polisi kwenye msikiti huo na kuwakamata vijana hao.
Dereva wa bajaji aliyewapeleka  Msikitini: Alphonce Maurus ambaye ni dereva wa bajaji aliyewapeleka watu hao kwenye msikiti huo, alisema juzi majira ya saa tatu usiku akiwa Kidato kwenye eneo lake la kusubiri abiria, watu 11 walifika hapo wakihitaji usafiri.
 
Alisema kati ya watu hao, yeye aliwabeba watano akiwamo Hamad Makwendo ambaye aliuawa alipokuwa akijaribu kupambana na askari.
 
Maurus alisema baada ya kuwapakia watu hao pamoja na Makwendo aliyekuwa mwenyeji wao, wengine sita walipanda kwenye bajaji nyingine na kuwafuata hadi kwenye msikiti wa Sunni ulio kwenye kijiji hicho.
 
Alisema wakati wote wa safari yao, mwenyeji wao ndiye alikuwa akizungumza kuelekeza njia huku wengine wakiwa kimya.
 
Maurus alisema watu hao walikuwa wamebeba mabegi, lakini hakuweza kujua ndani kulikuwa na nini.
 
“Tulivyofika pale msikitini tuliukuta uko wazi, wao wakaingia ndani,” alisema.
 
Alisema usiku Makwendo alitoka akiwa na bajaji akienda kuchukua watu wengine na walipofika njiani ndipo wakakutana na askari.
 
“(Makwendo) alishuka kwenye bajaji akawa anakimbia na askari wakamkimbiza, alivyofika sehemu akadondoka, alivyodondoka kuna askari alikuwa anamkimbiza alivyojaribu kumkamata, akachomoa sime akamkata shingoni na kwenye mkono.
 
“Yule askari akapiga kele wenzake waliokuwa nyuma wakampiga risasi yule jamaa kisha wakampakia kwenye gari lao wakataka kuondoka naye.
 
“Kutokana na zile kelele wananchi walijaa wakawaambia askari wasipomshusha yule mtu watachoma gari moto, na kweli wakafanikiwa kumshusha wakampiga na kumchoma moto,” alisema.
 
Maurus alisema baadaye askari walimshika na kumtaka awapeleke kwenye eneo walipo watu wengine.
 
Mwenyekiti wa kitongoji Mweyekiti wa Kitongoji cha Ikera, Kata ya Kidatu, Mohamed Libaha, alisema siku ya tukio hilo, majira ya saa 8 usiku, askari walifika nyumbani kwake na kumuhoji kama ana taarifa za wageni walio kwenye kitongoji chao.
 
Alisema baada ya kuwaambia kuwa hawana ugeni wowote, polisi waliwakamata watu hao na kiongozi wa msikiti huo, Ustaadh Maulid Sultani.
 
Katibu wa msikiti huo, Mohamed Manze, alisema wao kama viongozi na waumini wa msikiti huo hawakuwa na taarifa zozote za ujio wa watuhumiwa hao, na kwamba katika msikiti huo wapo vijana wanne ambao huwa wanalala na kujisomea hapo.
 
Alisema siku ya tukio watuhumiwa hao walifika msikitini hapo majira ya saa nne usiku ambapo tayari ibada ya mwisho ilikwishafanyika na waumini kutawanyika.
 
Manze alisema walitumia mwanya huo kuingia na kujihifadhi bila taarifa zozote kwa uongozi wa msikiti huo jambo ambalo ni kinyume na utaratibu za msikiti huo.
 
Alisema wao kama waumini wa msikiti huo hawakupendezwa na suala hilo na kwamba limewachafua na kuwaharibia sifa waumini na msikiti wao.
 
Chanzo cha askari kujua siri ya watu hao Manze alisema hivi karibuni kwenye eneo hilo mtu mmoja alikamatwa akihusishwa na matukio ya ugaidi yaliyotokea mkoani Arusha na mapango ya Amboni mkoani Tanga.
 
“Baada ya lile tukio wananchi waliweka ulinzi shirikishi, ikawa kila kitu wanawaambia polisi,” alisema.
 
Ummul-Khayr Sadir Abdul Machi 30, mwaka huu vyombo vya usalama vya Kenya vilitangaza kumkamata Mtanzania Ummul-Khayr Sadir Abdul (19) na wenzake wawili raia wa Kenya wakiwa mpakani mwa taifa hilo na Somalia, wakidaiwa kuwa njiani kwenda kujiunga na kundi la Al-Shabaab.
 
Taarifa kutoka kwa Kamishna wa Polisi Jimbo la El –Wak nchini Kenya, Nelson Marwa, ilisema Mtanzania huyo alijieleza kuwa ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afrika kilichoko nchini Sudan.
 
Wasichana wengine waliokamatwa pamoja na Ummul-Khayr, ambaye anaelezwa kuwa kiongozi wao, ni Maryam Said Aboud na Khadija Abubakar Abdulkadir.
 
“Hawa wasichana watatu inaaminika kuwa walikuwa wanakwenda Somalia kupata mafunzo ya kigaidi na baadaye kufanya mashambulizi ya kujitoa mhanga,” alisema Kamishna Marwa.
 
Alisema ingawa nyaraka za wasichana hao zote zinaonyesha kuwa ni wanafunzi, lakini bado walibanwa kwa maswali kuhusu sababu inayowapeleka nchini Somalia.
 
Alisema raia hao wawili wa Kenya, mmoja ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mount Kenya kilichopo Thika, Jimbo la Kiambu na mwingine ni mwanafunzi wa Sekondari ya Burhania iliyopo Malindi, Kilifi.
 
“Serikali imepata taarifa kuhusu watu wanaokusanya watu kutoka Afrika Mashariki ili wakajiunge na makundi ya ugaidi nchini Somalia, wakala wetu wa usalama wamepata taarifa hizo na kufanikisha kukamatwa kwa wasichana hao,” alisema Kamishana Marwa.
 
Ummul-Khayr alimaliza madarasa ya Quran Zanzibar na baadaye alipata elimu yake ya juu katika Shule ya SOS kabla ya kujiunga na elimu ya Chuo Kikuu nchini Sudan.

Hizi ndio sehemu 12 zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, Bonyeza Hapa chini== >


Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO CHAFU YA AGNESS MASOGANGE== >

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Newer Posts Older Posts
© Copyright ZEE LA UDAKU | Designed By Code Nirvana
Back To Top