Watu
watano wamefariki dunia papo hapo katika kijiji cha Shilabela, kata ya
Bwanga, wilayani Chato, mkoa wa Geita, baada ya kupigwa na radi wakati
wakiendelea na ibada ya Sikukuu ya Pasaka.
Tukio
hilo lilitokea juzi jioni kwenye Kanisa la Assemblies of God Tanzania
(AGT) na kujeruhi watu wengine 18 wakati wakiwa kwenye maadhimisho ya
sikukuu ya kufufuka kwa Yesu Kristo, Pasaka. Kati ya majeruhi hao, wanne
wamelazwa katika Zahanati ya Bwanga, wilayani Chato.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Geita, Joseph Konyo, jana alithibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kuwataja waliofariki ni Daud Merdad (20), Daud Lazaro
(20), Saimon Marco (15), Haile Shija (20) na Monica Sumuni (19).
Kamanda
Konyo aliwataja majeruhi watatu waliolazwa Zahanati ya Bwanga ni Mabula
Mathias (8), Fabian Ezekiel (10) na Edina Leonard (21).
Mganga
Mfawidhi wa zahanati hiyo, Deogratias John, alisema majeruhi 18
walipokelewa katika zahanati hiyo, lakini 14 walitibiwa na kuruhusiwa
kurejea nyumbani baada ya hali zao kutengemaa.
Akizungumzia
tukio hilo, Diwani wa kata hiyo, Mahobe Chiza, alisema ni kubwa na la
aina yake lililotokea wakati wananchi hao wakisherehekea sikukuu ya
Pasaka.
“Walikuwa
katika sikukuu ya Pasaka, lakini bahati mbaya mvua iliyokuwa ikinyesha
ilisababisha radi kupiga na kuwadhuru waumini hao,” alisema Chiza.
Naye
Mchungaji wa kanisa hilo, Deus Mhangwa, alisema kanisa lake limepata
msiba mkubwa wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya Pasaka, ambayo ni siku
ya kukumbuka kufufuka kwa Yesu Kristo baada ya kusulubiwa msalabani.
“Kila
nafsi itaonja mauti, lakini tukio hili limewaachia simanzi kubwa
waumini wa kanisa pamoja na wananchi kutokana na kupotea kwa nguvu kazi
ya kanisa na taifa kwa ujumla,” alisema Mchungaji Mhangwa.
Hizi ndio sehemu 12 zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, Bonyeza Hapa chini== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO CHAFU YA AGNESS MASOGANGE== >