Mwigizaji Wema Sepetu amewataka watu wanomsakama kwa maneno waache apumzike kufanya hivyo kwani yeye ni binadamu kama ilivyo kwa wengine na anaumia kama wanavyoumia wengine.
Wema ambaye alikuwa akizungumzia ujumbe
aliouandika hivi karibuni katika mtandao wa Instagram kuhusu kutopata
mtoto, anasema kuna watu hawajali maumivu yake ndiyo maana kila kukicha
wanamkashifu.
“Watu hao hawawezi kutafuta jema langu na
kunisifu, kazi yao kunisanifu na kunikashifu kwa vitu wasivyovifahamu
wala kuwa na ukweli navyo.Nimevumilia mengi namna sasa imetosha,”
anasisitiza dada huyo aliyewahi kuwa Miss Tanzania na kuongeza kuwa kwa
sababu hiyo, hivi sasa hasomi magazeti ya aina yoyote akiogopa kuharibu
‘hali ya hewa ya siku’ husika, kwani watu hawajali wanaandika chochote
bila kufikiria madhara gani.
Akizungumzia tuhuma za kuwalipa fedha waandishi wa
habari ili aandikwe kwa lengo la kupata ‘Kiki’ mwanadada huyo
anasema hayana ukweli wowote na kuongeza kuwa kama kuna anayefanya
hivyo hana akili.
Anasema haoni sababu ya kutoa fedha ili aandikwe
ilhali kuna watu kazi yao ni kuangalia anafanya nini na kumuandika,
ingawa amekiri kuwa anawafahamu baadhi ya waandishi kama binadamu.
Anasema watu wakimuona yupo karibu na watu hao wanaamini anawapa fedha wamuandike, kwa lengo la kumpaisha jina lake.
“Niliwahi kuwa mrembo mkubwa tu, natambulika na
watu wengi, mwigizaji, naendesha kipindi katika runinga, kwa kila hali
lazima nitaandikwa tu, lakini siyo kwa kuwapa watu fedha ili wanichafue
eti... nakuza jina , hapana jina langu ni kubwa tayari, ” anasema Wema.
Mkali huyo wa filamu ikiwamo ile inayosubiriwa kwa
hamu ya ‘Day after Death’ aliyoigiza na mwigizaji mahiri wa nchini
Ghana, Van Vicker, anasema anahitaji kuwa na wakati wake binafsi, lakini
kutokana na kuwa na jina hana hiyo nafasi kwani kila anachokifanya
kinafuatiliwa na jamii, hivyo katika hali kama hiyo hakuna haja ya
kulipa fedha aandikwe.
Kuhusu siasa Wema anasema yeye ni shabiki mkubwa
wa CCM, ingawa kuna baadhi ya vitu vinamkera na inabidi vifanyiwe kazi
ili kujiimarisha.
Anasema anaupenda utendaji wa Rais Jakaya Mrisho
Kikwete kutokana na vitu vingi alivyofanya katika kipindi cha miaka 10
aliyokuwa madarakani na ingekuwa amri yake angerudi tena.
Hizi ndio sehemu 12 zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, Bonyeza Hapa chini== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO CHAFU YA AGNESS MASOGANGE== >