Mtindo wake wa majivuno na kujisifia ni
kati ya vitu vilivyomfanya achukiwe na wengi, hali ambayo mwenyewe
aliiona kama sifa kubwa ambayo ilisababisha kujiita Mr Misifa.
Kwa sasa utafanya kosa kubwa kama utaacha
kulijumuisha jina la Abdul Abass Sykes, lililoibuka miaka ya 2000,
ambalo lilizaa ‘Dully Sykes’ kama mmoja wa wakongwe kunako tasnia ya
Muziki wa Bongo Fleva.
Vibao kama Salome, Leah, Hi, Mr Misifa, Nyambizi, Bijou, Julietha na Bongo Fleva ndivyo vilivyochangia kumfanya kutambulika na kutamba sokoni.
Mkongwe huyo sasa anatamba na Kibao cha Shuka, ambaye pia ni mmiliki wa Studio ya Dhahabu Records iliyopo Tabata Bima jijini Dar.
Championi Jumatatu linakupa zaidi baada ya kumkalisha mkali huyo kilingeni.
Hivi karibuni ulitoa wimbo mpya, mashabiki wameupokeaje?Vibao kama Salome, Leah, Hi, Mr Misifa, Nyambizi, Bijou, Julietha na Bongo Fleva ndivyo vilivyochangia kumfanya kutambulika na kutamba sokoni.
Mkongwe huyo sasa anatamba na Kibao cha Shuka, ambaye pia ni mmiliki wa Studio ya Dhahabu Records iliyopo Tabata Bima jijini Dar.
Championi Jumatatu linakupa zaidi baada ya kumkalisha mkali huyo kilingeni.
Dah! Kwanza naomba niwashukuru mashabiki wangu ambao wamekuwa chachu ya maendeleo kwenye kazi zangu za muziki, huwezi amini ‘single’ niliitoa hewani Jumatatu iliyopita na kusambaza video siku ya Ijumaa lakini matumaini ni makubwa, kwa sababu wengi wameshaisikiliza na ninatumaini kupata ‘feedback’ nzuri.
Hata hivyo kuna kazi yangu ambayo nitaiachia hewani ‘soon’ nimefanya na Diamond na msanii flani hivi wa mbele ‘amazing’ ila siwezi kumtaja kwani ni mapema mno halafu nataka iwe ‘surprise’ kwa mashabiki wangu.
Ile project ya wimbo wa kumuinua Chid Benz, iliishia wapi?
Tayari wimbo upo ambao uliimbwa na Diamond na AY, mimi nilihusika katika kuutengeneza kama ‘produza’ tu na mashabiki wameupokea vizuri sana.
Chid Benz ni ndugu yetu, ndiyo maana tulianzisha ile project kwa ajili ya kuhakikisha anaachana kabisa na matumizi ya madawa ya kulevya, huu ni mwanzo tu, bado kuna mengine tutayafanya kwa ajili yake.
Studio yako inasaidiaje kuwainua wasanii wachanga?
Aisee kwa sasa nimesimama kufanya hizo shughuli za kuinua vipaji vya wasanii chipukizi kwa sababu kama ni kuwasaidia nimeshawasaidia sana lakini wengi wameniangusha.
Muda huu naangalia zaidi mambo yangu ya msingi, umri unaposonga na majukumu yanaongezeka! So acha nifanye yangu kwanza lakini sitaacha kuwasaidia kwa kuwa na mimi nilitokea huko, najua changamoto wanazokutana nazo.
Kifo cha baba yako kiliathiri vipi kazi zako?
Kiukweli kuondoka kwa mzee kwangu ni pigo kubwa sana, alikuwa ni zaidi ya rafiki yangu na mara kwa mara alikuwa akinishauri, kunionya na kunionyesha njia sahihi pale ninapokwenda tofauti. Lakini hilo naomba tusiliongelee sana maana kazi ya Mola haina makosa.
Vipi umewahi ‘kutoka’ na staa mwe-nzako?
Ha! Ha! Haaa! No, sijawahi ‘kudeti’ na staa na wala sitarajii, maana hao mastaa wenyewe sijaona hata wa kudeti naye.
Hata hivyo mimi bado sijaoa, lakini nitakapompata ‘wife material’ nitaoa tu, hata hivyo nina watoto wanne na kila mtoto ana mama yake. Mwanangu wa kwanza anaitwa Titho Sykes, naishi naye nyumbani kwangu.
Kitu gani unakichukia kwenye muziki?
Kikubwa zaidi ambacho ninachukia ni wivu na chuki zisizo na msingi baina ya wasanii. Hapa napenda kuwashauri wasanii wenzangu tupendane, pia ushirikiano ni muhimu kama tunahitaji kazi zetu zifike mbali zaidi.
Tujifunze kupitia kwa wenzetu lakini tukiendekeza mambo hayo, mafanikio yataendelea kuwa ya mtu mmoja-mmoja na siyo muziki kwa ujumla.
Unamzungu-mziaje Diamond hapa alipofikia?
Nichukue nafasi hii kumpongeza kwa mafanikio makubwa aliyoyafikia, kupitia yeye natumaini muziki wetu umejulikana zaidi kimataifa na nchi nyingi zimetujua kuwa nasi tunaweza.
Naamini amesaidia kufungua njia kwa wengine na utaona hata sasa kila msanii anataka kazi yake iwe kwenye ubora, jambo linalofanya tuzidi kupiga hatua.
Pia napenda kuipongeza kampuni yenu (Global Publishers Ltd) na ‘media’ mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanya kazi kubwa kusapoti kazi zetu za nyumbani! Siwezi kuwasahau pia mashabiki wangu ambao kwa namna moja au nyingine wamenifikisha hapa nilipo, lakini hata washikaji zangu wote ninawapenda, maana sina bifu na msanii hata mmoja.
Hizi ndio sehemu 12 zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, Bonyeza Hapa chini== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO CHAFU YA AGNESS MASOGANGE== >