Maajabu
ya Bagamoyo! Katika hali ya kushtua, familia yenye makazi yake,
Magomeni, Bagamoyo mkoani Pwani, imejikuta kwenye mauzauza baada ya
ndugu yao kufariki dunia huku akidaiwa kukohoa, kufumbua macho na
kuonesha dalili za kuwa hai, pamoja na kwamba daktari alithibitisha
kifo.
WAOMBOLEZAJI WATIMUA
Katika tukio hilo lililosababisha
waombolezaji kutimua mbio lililojiri Juni 28, mwaka huu, binti wa
familia hiyo, Tunu Shabani (36), alifariki dunia katika Hospitali ya
Wilaya ya Bagamoyo kutokana na kuumwa kichwa ghafla.
MUME ASIMULIA
Akizungumza na Amani lililofunga
safari kutoka Dar hadi Bagamoyo, mume wa Tunu, Iddi Ramadhani alisema
mkewe alianza kupata maumivu ya sikio baadaye kichwani ambapo
alimhamishia kwa wazazi wake maeneo hayohayo ya Magomeni kwa kuwa ni
karibu na hospitali.
Iddi alisimulia kuwa Juni 27, mkewe huyo
alipelekwa kwenye hospitali hiyo, akatundikiwa dripu lakini hali
ilizidi kuwa mbaya kiasi cha kuwekewa mashine ya kupumulia kabla ya
kuaga dunia alfajiri ya Juni 28.
“Baada ya daktari kuthibitisha kifo cha
mke wangu, ndugu tulikutana, tukaandaa mazishi kwa kuchimba kaburi na
shughuli ya kuandaa maiti kwa ajili ya mazishi tuliyopanga yafanyike saa
6:00 siku ya pili yake yaani Juni 29.
“Wakati wa kuosha maiti mara tukasikia sauti kasha ikafumbua macho, miguu yake ikajinyoosha na mwili ukawa na joto.
“Ilibidi tusitishe kumzika kwanza na kujaribu kumtafuta daktari,” alisema Idd.
Aliongeza kuwa, hali ya marehemu
iliendelea kuwatatiza kwa kuwa wataalam walishindwa kufanya chochote
hadi Juni 29, walishangazwa zaidi kuona maiti ikiwa inatoka jasho jingi
huku joto likiendelea kuwa vilevile.
SHEHE ANENA
Akizungumza na waandishi wetu, shehe
aliyekuwa akisimamia kuandaa maiti, Mtawa Adam (pichani) alisema kuwa
kwa mujibu wa taratibu za mazishi za Dini ya Kiislam, marehemu ambaye ni
mwanamke huoshwa na wanawake wenzake, kanuni ambayo mwili wa Tunu nao
uliipitia.
Shehe Adam alisema kuwa, kama kawaida
alimpima marehemu na kumshonea sanda huku akisubiria wanawake hao
wamalize kumuosha na kumuandaa ili yeye aingie kwa ajili ya kumnyosha
viungo, lakini kabla hawajamaliza, alishtushwa kuwaona wakitoka mbio na
kudai maiti imefumbua macho na kunyoosha mguu.
“Niliingia ndani na kumuona marehemu
ambapo wakati huo alikuwa amefumba macho, nilipomgusa alionekana wa moto
kama alikuwa hai, nikamtazama nyayo zake zilionekana ni nyeupe tofauti
na za marehemu ambazo huwa za njano.
“Nilimrekebisha mguu wake aliounyoosha,
lakini nikashangaa ukirudi tena kama ulivyokuwa awali na hata mapigo
yake ya moyo yalikuwa yakipiga mara moja baada ya dakika hata mbili,”
alisema shehe huyo na kuongeza kuwa aliwashauri wanafamilia wamuondoe
Tunu kwenye kitanda cha maiti na kughairi maziko huku daktari mwingine
akiitwa kumpima lakini naye alisema alifariki dunia.
UMATI WAJAA
Waandishi wetu, walishuhudia umati wa waombolezaji wakiwa wamezunguka eneo hilo ili kushuhudia kilichoendelea.
MAMA APANDISHA MASHETANI
Katika hali isiyo ya kawaida, mama mmoja alipandisha mashetani na kudai Tunu hajafa.
WAGANGA WANNE
Kwa mujibu wa ndugu mmoja wa familia
hiyo aliyeomba hifadhi ya jina lake, waliwaita waganga wa nne wa
kienyeji ambapo mmoja alifika na kudai Tunu alichukuliwa msukule lakini
alishindwa kumfanya awe hai.
Aidha, waganga waliobakia licha ya kufanya ndumba zao, Tunu hakuweza kuamka kama walivyodai awali.
Baba mzazi wa marehemu, Adam Hassan
akizungumza na waandishi wetu alisema Tunu hakuonesha dalili za kuwa hai
hivyo taratibu za mazishi zilifanyika kesho yake (Juni 30) na kuzikwa
katika Makaburi ya Kiwangwa, Bagamoyo.
Hizi ndio sehemu 12 zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, Bonyeza Hapa chini== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO CHAFU YA AGNESS MASOGANGE== >