Habari Kali
Loading...

CCM YAMTAKA JK AWATIMUE KAWAMBWA, CHIZA, MALIMA...SOMA ZAIDI

Mbinu Za Kumfikisha Kileleni Mwanamke Mwenye Makalio Makubwa Kwa Haraka, Bonyeza Hapa chini== >
Mawaziri


MAWAZIRI watatu wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete wapo katika wakati mgumu baada ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Nape Nnauye, kutangaza rasmi kuwa atahakikisha wanachukuliwa hatua za kuwajibishwa kutokana na kushindwa kutekeleza majukumu yao.

Wakati Nape akitaka mawaziri hao watimuliwe, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulhaman Kinana, amesema kuwa mawaziri hao watawekwa kiti moto katika kikao kijacho cha Kamati Kuu (CC), kwa lengo la kueleza ni hatua gani wanachukua katika kushughulikia matatizo ya Watanzania.

Mawaziri hao ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhandisi Christopher Chiza,  Naibu wake, Adamu Malima  na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa ambaye ametajwa kuwa sehemu ya matatizo katika kila wizara anayopewa kuiongoza.

Akizungumza jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma, Nape alisema hakuna sababu ya kukaa kimya wakati mawaziri hao wameshindwa kazi, hivyo ni vema wakawajibishwa ili kukiokoa chama chao.

Kuhusu Chiza na Malima, Nape alisema mawaziri hao wameshindwa kutekeleza wajibu wao kwani tangu walipochaguliwa kuongoza wizara hiyo hakuna hata siku moja ambayo wamefika Ruvuma kushughulikia matatizo ya wakulima wakiwamo wa korosho, tumbaku, mahindi  na mpunga, ambapo katika mikoa mbalimbali nchini imekuwa ikilalamikia sekta ya kilimo lakini wenyewe wamekaa kimya bila kuchukua hatua zozote.

“Katibu Mkuu leo ni bora nikazungumza haya ya mawaziri ambao wamepewa dhamana ya kuwatumikia Watanzania. Nimeuliza hapa Ruvuma Waziri wa Kilimo na naibu wake walishawahi kufika mara ngapi kushughulikia matatizo ya wakulima. Jibu lake, hakuna hata siku moja wamefika.

“Hii inaleta tabu, wakati wakulima wanahangaika na pembejeo za kilimo, ukosefu wa soko na malipo ya fedha wanazodai serikalini mawaziri wenye dhamana wapo mjini wanafunga tai na suti. Hawafikiri kuhusu matatizo ya wakulima,” alisema.

Aliongeza kuwa yupo tayari kupoteza nafasi yake lakini hawezi kuvumilia hali hiyo ikaendelea na kutumia nafasi hiyo kumuoma Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, ahakikishe wanachukuliwa hatua na ikiwezekana waitwe CC wahojiwe.

Alisema karibu Tanzania yote wakulima wamekuwa na matatizo mengi na wamekuwa wakilalamikia wizara hiyo na yeye ni shahidi wa hayo yanayoendelea kutokea na ili kukinusuru chama hicho mawaziri walioshindwa kazi wawajibishwe.

Alisema kuwa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika imepewa dhamana ya kuwatumikia Watanzania asilimia 80, ambayo ni wakulima lakini waliopewa jukumu hilo hawataki kufanya kazi zao.

“Wananchi naomba mnilinde, lakini niseme ukweli. Niseme nisiseme…mawaziri ambao tumewapeleka jikoni wameshindwa kupika chakula, tunasubiri sebuleni lakini chakula hakiji. 


Wanatukwamisha, ni bora wakaondoka kama wameshindwa kazi.
“Katibu Mkuu mimi nikija, sipo tayari kuona CCM inakuwa chama cha upinzani bungeni kwa sababu tu ya hawa wenzetu wachache ambao wanafanya makusudi na uzembe katika kutekeleza wajibu wao,” alisema Nape.


Wakati kwa Dk. Kawambwa mbali ya kushindwa kuongoza Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi naye anatakiwa kuchukuliwa hatua kutokana na mkataba aliouingia na makandarasi wa ujenzi wa barabara ya kutoka Namtumbo hadi Tunduru mkoani Ruvuma.

Nape alisema anamshukuru  Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, kwa kumfukuza mkandarasi huyo aliyemtaja kwa jina la Progressive ambaye ameshindwa kazi ya kujenga barabara hiyo.

Hata hivyo, kumfukuza mkandarasi huyo pekee haitoshi, hivyo aliyehusika kumpa mkataba anapaswa kuchukuliwa hatua kwani uchunguzi  unaonesha kuwa alishashindwa kazi na wakati anapewa mkataba huo Waziri husika alikuwa Dk. Kawambwa.

“Dk. Kawambwa amekuwa akitukwamisha CCM katika kutimiza wajibu wake. Hii barabara ya Namtumbo hadi Tunduru kushindwa kukamilika imeleta aibu kubwa na kututia fedheha. Hivyo lazima waliotoa mkataba wawajibishwe.

“Dk. Kawambwa huyu huyu ameshindwa kushughulikia matatizo ya walimu nchini na atambue kuwa tulimpa muda wa miezi sita na sisi tunahesabu, ukimalizika hatutaacha kuchukua hatua.

“Chama kitatumia wabunge wake kumuwajibisha. Hatuwezi kukaa kimya. Iwapo ninaonekana kama kero kwa kupigania masilahi ya nchi na watu wake, nipo tayari kuondoka na kwenda kujihusisha na kilimo. Maana mimi ndiye mpiga debe wa chama, nitakwenda kueleza nini kwa umma kutokana na ahadi zetu kukwama kwa sababu tu ya uzembe wa wachache ndani ya serikali?” alihoji.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa CCM, Kinana, alisema kuwa katika kikao kijacho cha Kamati Kuu (CC), kitakachofanyika Desemba mwaka huu chama kitamuandikia barua Rais Jakaya Kikwete ili mawaziri wake waje wajieleze mbele ya kikao kwa nini wasifukuzwe kwa kushindwa kazi.
VIA TANZANIA DAIMA

Hizi ndio sehemu 12 zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, Bonyeza Hapa chini== >


Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO CHAFU YA AGNESS MASOGANGE== >

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Newer Posts Older Posts
© Copyright ZEE LA UDAKU | Designed By Code Nirvana
Back To Top