DENTI wa Chuo cha Ubaharia (EMI) kilichopo Posta jijini Dar, Alpha Mohamed (18) aliyedaiwa kupigwa na Diwani wa Kata ya Sinza kwa ‘leseni’ ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Renatus Pamba, ‘Mr Simple’, bado yu hoi katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar.Denti ,Alpha Mohamed (18) anayedaiwa kupigwa na Diwani wa Kata ya Sinza kwa ‘leseni’ ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Renatus Pamba, ‘Mr Simple’.Alpha alidaiwa kupigwa Agosti 29, mwaka huu nyumbani kwa diwani huyo Sinza- White Inn, Dar ambapo chanzo cha kipigo hicho kilisemekana kuwa ni denti huyo kukutwa akipiga stori na binti wa diwani aliyejulikana kwa jina moja la Mage.
Ilidaiwa kwamba baada ya vipimo ilibainika kwamba denti huyo alipata maumivu makali kifuani na mgongoni baada ya kupigwa na fimbo pamoja na fagio.Haya ni majeraha ya mgongoni aliyopata Alpha Mohamed kutokana na kipigo cha Diwani.Chanzo chetu kilibaini licha ya Alpha kupelekwa katika Hospitali ya Palestina iliyopo Sinza jijini Dar lakini hali ilizidi kuwa mbaya kwani mara kwa mara amekuwa akitapika damu na kulalamika kupata maumivu makali maeneo ya kifua na kichwani huku akikohoa damu.
Ilisemekana kwamba kutokana na hali kuzidi kuwa mbaya, ndugu wa Alpha wamelazimika kupitisha karatasi ya michango mtaa mzima kumchangia fedha za matibabu ili kunusuru maisha yake.
Alipotafutwa mjomba wa Alpha, Aboubakari Ramadhani ili kujua afya ya Alpha, alisema bado haijatengemaa na amelazwa Mwananyamala.Ndugu na jamaa wa Alpha Mohamed wakisikitikia uenevu huo.“Hali yake ni mbaya, hatujui nini kitatokea. Familia ilifungua jalada la kesi lenye kumbukumbu KN/RB/7748/2014 SHAMBULIO hivyo tunaendelea kumtibu huku tukisubiri hatua za kisheria,” alisema Ramadhani.Baada ya habari ya tukio hilo kuripotiwa kwenye gazeti hili toleo Na 1145 lenye kichwa cha habari kilichosomeka;
DIWANI AMPA KIPIGO DENTI, wanahabari wetu walimtafuta diwani huyo ili kujua undani wa sakata hilo kwani naye alifungua mashitaka akidai Alpha alimbaka bintiye, lakini hakutoa ushirikiano.
Kwa nyakati tofauti, sakata hilo limeripotiwa katika vituo viwili tofauti vya polisi, Kijitonyama-Mabatini alikoshitakiwa diwani na Urafiki-Ubungo ambako diwani alimshitaki Alpha akidai alimbaka bintiye, Mage.
Hizi ndio sehemu 12 zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, Bonyeza Hapa chini== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO CHAFU YA AGNESS MASOGANGE== >