MWANZILISHI wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania, Prashant Patel, amefungua maombi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam akiomba mshirika wake, Hashim Ludenga, azuiliwe kuendelea kuendesha mashindano hayo yanayotarajiwa kufikia kilele chake Oktoba 11, mwaka huu.
Patel
amewasilisha maombi hayo katika hati ya dharura kupitia wakili wake,
Benjamin Mwakagamba, akidai Lundenga ana mpango wa kuendesha mashindano
hayo kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, kinyume cha sheria na
bila hata kumtaarifu.
Anaomba
mahakama itoe zuio dhidi ya Lundenga, la kuendesha mashindano hayo hadi
shauri lake la msingi aliloliwasilisha litakaposikilizwa na kutolewa
uamuzi.
Katika
kesi yake ya msingi, Patel anadai pamoja na mambo mengine, utekelezaji
wa makubaliano ya Februari 20, 2012 na malipo ya Sh milioni 19 ambayo
hayajalipwa kwa mujibu wa mkataba na faida nyinginezo ambazo
zimejitokeza hadi Septemba 23, mwaka huu.
Shauli
hilo limepangwa kutajwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Frank Moshi
leo, na Lundenga ametakiwa kuwasilisha utetezi wake ndani ya siku 21, na
akishindwa kufanya hivyo, mahakama itaendelea kutoa hukumu dhidi yake.
Katika
hati ya kiapo inayounga mkono maombi yake, Patel anadai kuwa yeye
pamoja na Lundenga ndio waanzilishi, waongozaji na waendeshaji wa
mashindano ya Miss Tanzania na wamekuwa katika hali hiyo kwa miaka 20
sasa, tangu mashindano hayo yaliyoporuhusiwa tena mwaka 1994.
Kwa
kipindi chote hicho, wamekuwa wakisaini makubaliano ya namna ya
kuendesha mashindano hayo na mara ya mwisho walisaini makubaliano
Februari 20, 2012.
Hata hivyo, Lundenga alikataa kusaini makubaliano kwa mwaka 2013 na 2014 na ameshindwa kumlipa fedha zake Sh milioni 19.
Patel anadai badala yake Ludenga ameshirikiana na wadhamini wengine kuendesha mashindano hayo.
Kwa
mujibu wa makubaliano, Lundenga pia alipaswa kulipa pauni za Uingereza
30,000 kama malipo ya kibali kwa mwendeshaji wa shindano hilo duniani,
Miss World, deni ambalo limekuwa la muda mrefu, hivyo kuchafua hadhi
yake.
Patel
anadai kuwa Ludenga alipelekewa taarifa na wakili wake kulimaliza suala
hili bila kushirikisha hatua za kisheria, lakini alikaidi na kukataa.
Hivyo Patel anadai kuwa hakuwa na njia nyingine zaidi ya kulipeleka
suala hilo mahakamani.
-Mpekuzi
Hizi ndio sehemu 12 zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, Bonyeza Hapa chini== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO CHAFU YA AGNESS MASOGANGE== >