Wakati hali ya kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima, ikiwa tete kwa siku mbili mfululizo, Jeshi la Polisi na waumini wa Askofu huyo wanadaiwa kuvutana hospitali inayofaa kumpa matibabu.
Askofu
Gwajima, alizimia ghafla juzi majira ya saa 2: 45 usiku akiwa kwenye
chumba cha mahojiano katika Kituo cha Polisi Kati, baada ya kutuhumiwa
kumkashifu na kumtukana kiongozi wa kanisa la Katoliki Jimbo kuu la Dar
es Salaam, Mwadhama kadinali Polycap Pengo.
Hata
hivyo, mara baada ya kutokea tukio hilo, Askofu huyo alichukuliwa akiwa
katika hali ya kuzirai na kuanza kuzungushwa katika hospitali tofauti
wakati waumini walitaka apelekwe Hospitali ya TMJ Mikocheni, Jeshi la
polisi lilitaka apelekwe hospitali za Jeshi na Muhimbili.
Tukio
hilo ambalo mwandishi wetu alilishuhudia, lilianza majira ya saa 3:00
usiku alipopoteza fahamu hadi majira ya saa 8:00 usiku ambapo
walikubaliana apelekwe Hospitali ya TMJ ambako anaendelea kupatiwa
matibabu.
Hali ilivyokuwa polisi kati.
Baada
ya kuwasili kituoni hapo majira ya saa 8:15 alasiri, alikwenda moja kwa
moja katika chumba maalumu kilichoandaliwa kwa ajili ya kuhojiwa
tuhuma zinazomkabili.
Mahojiano
rasmi yalianza majira ya saa 8:45 mchana. Ilichukua muda wa saa saba
ndani ya chumba hicho, na ilipofikia saa 1.05 usiku, hali ya Askofu
Gwajima ilibadilika ghafla.
Baadhi
ya askari na viongozi wenzake walionekana kujaribu kutumia njia
mbalimbali ikiwamo kumpeleka chooni ili kumrudisha hali yake ya kawaida,
lakini ilishindikana.
Aliporudi ndani, aliishiwa nguvu na kupoteza fahamu kitu ambacho kilizusha taharuki ndani ya ukumbi huo.
Chanzo cha kuzimia.
Taarifa
kutoka ndani ya kikao hicho kilieleza, hali yake ilibadilika ghafla
baada ya kuanza kuhojiwa kuhusu mali anazomiliki ikiwamo helikopta
aliyoinunua hivi karibuni.
Aidha
mambo mengine aliyotakiwa kueleza ni uhusiano wake na wanasiasa
mashuhuri pamoja na akaunti anazomiliki na njia anazopata pesa.
“Mahojiano
yalikwenda vizuri, lakini ilipofikia zamu ya kumhoji mali anazomiliki
na ile helikopta aliyonunua, ghafla alibadilika na kuanza kutoka jasho
kwa wingi na kuzimia,” kilisema chanzo hicho.
Akithibitisha
jambo hilo, Mchungaji Yekonia Behanaze alikiri kuwepo kwa maswali hayo,
lakini alilalamikia namna alivyokuwa akihojiwa na askari hao kwamba
haukufuata hali ya kibinadamu.
“Unajua
hawakuwa na misingi mizuri ya kupata maelezo, walihojia mambo mengi
sana hata yale tuliyoamini yangekuwapo tuliona hayakuzingatiwa badala
yake iliegemea umiliki wa vitu,” alisema Mchungaji Behanaze.
Atembezwa akiwa Amezimia.
Baada ya kuzirai aliondolewa ndani ya chumba hicho ili kumuwahisha hospitali kwa ajili ya kupata matibabu.
Hata
hivyo, kulitokea mabishano makali kati ya polisi na viongozi wa kanisa
hilo, ambapo upande wa polisi ukitaka kumpeleka katika Hospitali za
serikali, viongozi hao waling’ang’ania kwenda Hospitali ya TMJ.
Ilipofika
Saa 3:00 usiku, polisi walimchukua na kumuingiza katika gari lenye
namba T 215 aina ya Noah na kumpeleka Hospitali ya Kilwa Road
inayomilikiwa na jeshi hilo.
Hapo
alitibiwa kwa muda wa saa tatu na ilipofika saa 5:08 usiku alichukuliwa
na gari la wagonjwa lenye namba DFP 6309 na kupelekwa Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili.
Msafara
wote ulikuwa chini ya ulinzi mkali wa polisi, ambapo wakati akielekea
Muhimbili, msafara huo ulikatisha mitaa ya Kurasini, Kariakoo, Faya na
kuishia Hospitali ya Muhimbili majira ya saa 5:18, usiku. Hata hivyo,
pande mbili hizo kati ya polisi na waumini ziliendelea kushindana kuhusu
hospitali inayofaa kumtibia.
Wakiwa
Hospitali ya Muhimbili, viongozi wa kanisa hilo ndugu na jamaa wa
Gwajima waliendelea kushinikiza kuondolewa hapo ili apelekwe TMJ ambako
walidai ndipo alipokuwa daktari wake.
Hata
hivyo, hoja hiyo ilipingwa na polisi wakiwaeleza Muhimbili ndiyo
Hospitali Kuu na watakubaliana nao endapo madaktari watashauri
kuondolewa kwa barua maalum.
Ilipofika
majira ya saa 6:00 usiku gari la wagonjwa kutoka Hospitali ya TMJ lenye
namba T 786 BYK liliwasili na kukaa tayari kumchukua.
Saa
7:00 usiku Askofu Gwajima alitolewa hospitalini hapo akiwa bado
amezirai na kuingizwa katika gari hilo na kumkimbiza Hospitali ya TMJ.
Katika msafara huo, magari yalipita mitaa ya Upanga, daraja la Selander,
Morocco na hatimaye hospitalini hapo na kulazwa wodi ya wagonjwa
mahututi (ICU).
Hali yake kwa sasa
Hata hivyo taarifa zilizopatikana kutoka Hospitali ya TMJ, zinaeleza bado hali yake si nzuri kutokana na kutorejewa na fahamu.
Kwa
mujibu wa daktari anayempatia matibabu, Dk. Photonatus Mazigo, hali ya
mgonjwa wake bado ni mbaya japokuwa kuna dalili ya kupata fahamu
taratibu.
“Kwa
ujumla hali ya mgonjwa siyo ya kuridhisha, hajazinduka tunachokifanya
ni kumpatia tiba ili arejee katika hali yake ya kawaida,” alisema Dk.
Mazigo.
Slaa, Baregu wafika hospitalini
Saa sita mchana, Katibu Mkuu wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibroad Slaa alifika
hospitalini hapo akiongozana na Mjumbe wa Kamati Kuu, Profesa Mwesiga
Baregu kumwona Gwajima.
Baada ya kumwona mgonjwa, Dk Slaa alizungumzia utata unaowapata watu wanaohojiwa na polisi, huku akisisitiza kuna vitu vinatakiwa kufanyiwa kazi, ikiwamo kubaini kuna nini.
Baada ya kumwona mgonjwa, Dk Slaa alizungumzia utata unaowapata watu wanaohojiwa na polisi, huku akisisitiza kuna vitu vinatakiwa kufanyiwa kazi, ikiwamo kubaini kuna nini.
Alisema sheria za kuhojiwa zipo wazi kuwa mtu
asihojiwe zaidi ya saa nane, vitu kama hivyo vinatakiwa kuzingatiwa
katika mahojiano.
“Nyinyi kama waandishi ndiyo kazi yenu kuangalia
kwa undani kuna nini kinaendelea katika haya mahojiano hadi mtu
anapoteza fahamu, siyo huyu hata kama kuna mwingine ilimtokea hali
hiyo,” alisema Dk Slaa.
Akizungumza hali ya mgonjwa kwa mtizamo wake,
alisema kuwa daktari anayemtibu hawajawafahamisha nini kimempata, lakini
kwa bahati mbaya hata mgonjwa mwenyewe hawezi kuzungumza na wao
hawakuweza kumuuliza chochote, hivyo hana la kusema.
“Angekuwa anazungumza, labda angeniambia
ilikuwaje, lakini hawezi hivyo sijapata lolote kutoka kwake wala
daktari,” alisema Dk SlaaHizi ndio sehemu 12 zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, Bonyeza Hapa chini== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO CHAFU YA AGNESS MASOGANGE== >