Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima jana alizimia na kisha kukimbizwa hospitali wakati akihojiwa Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.
Gwajima
ambaye alijisalimisha kituoni hapo saa 8:22 jana mchana akiitikia wito
wa polisi uliomtaka kufika kutokana na tuhuma za kutoa lugha chafu dhidi
ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama
Polycarp Kardinali Pengo.
Waandishi
wetu waliokuwa kituoni hapo wanaeleza kuwa walimuona Gwajima akitolewa
kutoka katika chumba cha mahojiano akiwa amebebwa.
Kwa
mujibu wa waandishi hao Gwajima ambaye alikuwa amebebwa na maofisa wa
polisi alipelekwa moja kwa moja kwenye gari aina ya Noah kwa ajili ya
kumpeleka hospitali.
Tukio
hilo lililotokea majira ya saa 3:16 usiku lilikuja katika kipindi
kisichozidi dakika saba tangu askofu huyo alipoonekana akiwa
ameshikiliwa na wasaidizi wake kuelekea msalani huku yeye mwenyewe akiwa
amejishika kichwa.
Wakati
akipelekwa hospitali, msafara wake ulikuwa ni wa magari mawili mojawapo
likiwa ni aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba za usajili PT 1848 na
Noah yenye namba za usajili T 215 BEM.
Akizungumza
na mwandishi wetu kituoni hapo, mwanasheria wa askofu huyo, John Mallya
alisema wakati wakiwa katika mahojiano, alisema anahisi kizunguzungu na
baadaye akaishiwa nguvu na akawa amefumba macho.
Mallya
alisema baada ya hali hiyo kutokea, polisi walimchukua na kisha
kumpeleka katika hospitali ya Jeshi la Polisi iliyoko Kurasini, Dar es
Salaam.
Wakati
Mallya akiwasiliana na mwandishi majira ya 4:30 usiku alisema kuwa
walikuwa wakifanya mchakato wa kumuhamishia katika hospitali ya TMJ
kutokana na yake kutokuwa nzuri.
“Siwezi kujua tatizo ni nini na siwezi kuzungumza chochote kuhusu hilo maana hayo ni mambo ya kitabibu” alisema Malya.
Ilipotimu
saa 4:41 Waandishi wetu ambao nao walifika katika hospitali hiyo ya
Jeshi la Polisi walishuhudia Gwajima akitolewa katika hospitali hiyo ya
Jeshi la Polisi na kisha kupakizwa katika gari maalum la kubebea
wagonjwa lenye namba DFP 6309.
Wakati
hayo yakitokea taarifa nyingine zilizotufikia zilidai kuwa; kwa muda
wote akiwa katika mahojiano, Gwajima alikuwa hajala chochote hali ambayo
iliibua wasiwasi kwamba huenda ilichangia kubadilika kwa afya yake.
Polisi
mmoja aliyekuwa katika chumba cha mahojiano aliwaeleza waandishi wetu
kwamba Askofu Gwajima alipoteza fahamu muda mfupi baada ya kuhojiwa
kuhusu mali anazozimiliki.
Awali
wakati Gwajima alipowasili kituoni hapo mchana kabla ya kuhojiwa
alizungumza na waandishi wa habari ambapo alikiri kutoa lugha chafu
dhidi Kardinali Pengo.
Gwajima
ambaye alifika kituoni hapo saa 8:22 mchana alisema kauli yake hiyo
ambayo imesambaa kwenye mitandao ya kijamii aliitoa kutokana na
Kardinali Pengo kuwageuka wenzake ambao ni Baraza la Maaskofu Tanzania
linalounganisha Wakatoliki, Pentekoste na Jumuiya ya Kikristo Tanzania
(CCT) kukubaliana kwa pamoja kuwa hawataki Mahakama ya Kadhi.
Alisema
maaskofu wote walikubaliana kuhusu tamko hilo na kisha kulisaini lakini
anamshangaa Kardinali Pengo ambaye pia alisaini kuwageuka.
“Mimi
kama kiongozi wa kiroho nikaona nimkemee kiongozi mwenzangu wa kiroho
aache mambo ambayo si mazuri. Hakuna maneno ya kashfa ambayo nimeyatoa.
Niliyotoa ni neno la Mungu linalotumiwa kumwongoza mtumishi wa Mungu,” alisema Gwajima.
Alisema anashangaa kuitwa polisi kwani hajatukana polisi na ndio sababu akaitika wito na kufika.
Gwajima
alifika polisi akitembea kwa miguu kutokana na foleni kali iliyokuwepo
barabarani huku akiwa ameongozana na Mwanasheria wake John Malya pamoja
na baadhi ya wachungaji, waumini wa kanisa hilo na wengine waliotajwa
kuwa ni walinzi wake.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Kamishna Suleimani Kova
alisema Mchungaji Gwajima ametii amri ya Jeshi hilo kama alivyotakiwa.
Kova
alisema baada ya kufika kituoni hapo alielekezwa kwenda kumuona Mkuu wa
Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam SACP Costantine Massawe.
Akitaja
tuhuma zinazomkabili Mchungaji Gwajima, Kova alisema ni pamoja na
kumkashifu na kumtukana hadharani kiongozi wa Kanisa Katoliki Kardinali
Pengo.
“Taratibu
za kuhojiwa zimeshaanza kwa mujibu wa sheria na mtuhumiwa atapewa haki
zote anazostahili ikiwemo kuwa na ndugu yake wa karibu, rafiki
anayemwamini au wakili wake. Kama ilivyokawaida utakusanywa ushahidi
kutoka pande zote za shauri hilo ili kubaini ukweli wa jinsi tukio hilo
lilivyotokea,” alisema Kova.
Kova
alisema baada ya hapo hatua nyingine za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni
pamoja na kupata maoni ya kitaalamu na ya kisheria ili kuhakikisha
kwamba haki inatendeka.
“Ili
ufanisi upatikane katika upelelezi wa shauri hili ni muhimu kupata
ushirikiano kutoka kwa kila atakayetakiwa kulisaidia Jeshi la Polisi
kukamilisha haraka upelelezi wa shauri hilo ambalo limepata mvuto mkubwa
kwenye jamii,” alisema Kova.
Hizi ndio sehemu 12 zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, Bonyeza Hapa chini== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO CHAFU YA AGNESS MASOGANGE== >