Sisi
maaskofu na wachungaji kutoka makanisa mbalimbali tumeshtushwa na
kusikitishwa kwa taarifa ya ugonjwa wa Askofu na mtumishi mwenzetu
Josephat Gwajima ambaye tarehe 27/03/2015 alifika kituo cha polisi cha
kati kuitikia wito wa polisi uliomtaka kwenda kujibu shutuma za kutumia
lugha ya matusi kwa kardinali Pengo.
Tumepata
fursa ya kutafakari na kujadili kwa kina hali iliyompata Askofu
mwenzetu hasa baada ya kuzingatia kuwa Askofu Gwajima alifika polisi
akiwa mzima na mwenye afya njema lakini wakati wa akihojiwa na polisi,
hali yake ilibadilika ghafla kiasi cha kupelekea yeye kulazwa hospitali
ya TMJ akiugua tena kwenye wodi ya wagonjwa mahututi yaani (ICU) katika
chumba cha uangalizi maalum.
Maswali yetu makuu ni kitu gani kimempata mwenzetu? Tunajiuliza, je vyombo vya usalama vimekua sio sehemu salama kama zamani?
Tukiwa
bado tunatafakari hill, tumeshtushwa tena baada ya kupata taarifa ya
kuwa Wachungaji Wasaidizi wa Askofu Gwajima pamoja na walinzi wake
waliokuwepo hospitalini hapo kwa ajili ya kumuuguza nao pia wamekamatwa
kwa tuhuma za kutaka kumtorosha Askofu Gwajima.
Jambo
hili linashangaza zaidi maana wachungaji wale wale waliokuwa naye akiwa
mzima wa afya wakati anaelekea polisi ndio wale wale wanatuhumiwa
kutaka kumtorosha akiwa mgonjwa.
Ni
jambo la kushangaza na lisiloingia akilini kuwa wasaidizi hao wa
Gwajima walitaka kumtorosha wakati Gwajima kama angekua na nia hiyo
angekwisha fanya hivyo mana alikuwa na uwezo wa kutoroka alipokua Arusha
kwenye kikao cha Maaskofu wakuu wa makanisa ya Kipentekoste ambao
alipata taarifa za kuitwa Polisi.
Isitoshe Gwajima aliitikia wito na kwenda polisi mwenyewe kwa miguu yake bila kushurutishwa, wala hakufikishwa polisi kwa nguvu.
Swali:
Kama alikua anaona ugumu wa kutoroka wakati hakuna polisi anayemlinda
na huku akiwa mwenye afya tele, itakuaje rahisi kutoroshwa leo akiwa
mahututi na akiwa kwenye ulinzi mkali wa polisi? Mbona hii
inastaajabisha?
Jambo
jingine linalotupa shida ni kuhusu mlalamikaji wa kesi hii inayomkabili
Askofu Gwajima. Tumeelezwa na wasaidizi wa Askofu Gwajima kuwa pale
polisi walielezwa kuwa aliyefungua kesi hii sio Pengo ila mtu mmoja
aitwaye Aboubakar.
Kwa
ufahamu wetu juu ya sheria unatutuma kuamini kuwa Aboubakar sio MTU
sahihi wa kufungua kesi hiyo sababu hawezi kutuonyesha ameumizwa kiasi
gani na matamshi ya Askofu Gwajima.
Isitoshe,
Kardinali Pengo mwenyewe ametamka katika Ibada yake ya Jumapili hii ya
tarehe 29/03/2015 kuwa amemsamehe Gwajima, yupi tena mwenye uchungu wa
kumzidi Kardinali Pengo?
RAI YETU:
Rai
yetu ni kwamba, ni vizuri serikali pamoja na vyombo vyake vya usalama
vikatumia weledi katika kushughulikia mambo ya kidini na viongozi wake
kwani yanaweza kusababisha chuki dhidi ya serikali na pia kupelekea
mpasuko mkubwa wa kidini katika jamii yetu iliyo na historia nzuri ya
umoja na mshikamano na ushirikiano katika matukio yote ya kimaisha.
Tunaomba serikali isaidie kuondoa mkanganyiko huu na busara kubwa itumike ili kuepusha uvunjifu wa Amani katika jamii.
MAAMUZI YETU:
Jambo hili linazungumzika, maana hata hivyo tumeshaazimia kukutana na IGP ili kupata suluhisho juu ya jambo hili.
Kwa niaba ya maaskofu na wachungaji:
Mwenyekiti: Askofu Dr. Mgullu Kilimba
Katibu: Askofu Dr. Dramas Mukassa
Hizi ndio sehemu 12 zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, Bonyeza Hapa chini== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO CHAFU YA AGNESS MASOGANGE== >