Sheria hii ni muhimu duniani kote na ndio maana hata Tanzania ilikuwa inangojea kupata sheria ya kuongoza masuala ya mitandao yaani Cyber Law kutokana na uhalifu wa aina mbalimbali wa masuala ya mitandao.
Sifa
kuu ya sheria ya kuongoza masuala ya mitandao ni kuweka bayana makosa
ya mitandaoni na pia kuyatolea adhabu. Sheria hii inayopitishwa kwa
dharura madhara yake ni:
Moja, Kifungu
7 (2b): Mpokeaji wa ujumbe (receiver) anaweza kushtakiwa kwa kosa la
kupokea ujumbe ambao sheria imeufanya kuwa wa jinai. (Mfano: Mtu
akikuforwadia ujumbe, ukiupokea na wewe umefanya kosa la jinai).
Pili, Kifungu
21(1): Mtumia mtandao wa Intaneti yeyote hayuko salama kwani mtoa
huduma wake analazimika kutoa habari zake kwa serikali pale
zitakapohitajika (kwa lazima).
Tatu, Kifungu
8: Itakuwa ni kosa la jinai kama mtu ataweka wazi nyaraka za siri za
serikali hata kama ni nyaraka ya kusaidia nchi kwa ujumla (Mfano:
Matumizi mabaya ya mali ya umma).
Nne, Kifungu
14: Picha yoyote yenye mwelekeo unaoweza kuonekana kama ‘mchafu
kingono’ inaweza kupelekea mtu kufungwa hadi miaka 10 au kulipa milioni
30; Sasa kama mtu kaweka picha yake Instagram ambayo sio ya ponografia
lakini ‘ikatafsiriwa’ hivyo. Sheria haijatafsiri ponografia!
Tano, Kifungu
23: Je, ulijua kuwa ‘kusababisha maudhi ya hisia’ kwa mtu mwingine ni
unyanyasaji na unaweza kufungwa kifungo kisichopungua mwaka mmoja?
Sita, Rejea
adhabu ya ibara mbalimbali: Sheria hii kila kosa linaweza fanya mtu
afungwe kifungo hadi cha maisha na kulipa pesa hadi zisizohesabika kwani
hakijawekwa kikomo cha juu cha adhabu bali kikomo cha chini tu kwa
Kiingereza “not less than”
Saba, Sheria
haijaeleza vizuri suala la kutumia jina lisilo lako kwenye mtandao na
hivyo mtu anaweza kushitakiwa kama kuna mtu mwingine mwenye jina kama
hilo katika maisha halisi.
Nane, Serikali
kupitia waziri husika ndio ina mamlaka ya kusema jambo lililowekwa
kwenye mtandao ni la kweli, uongo au la kupotosha. Kumbuka hata ESCROW,
EPA walisema ni uwongo; ni wangapi katika mtandao wangeshtakiwa kiuonevu
kwa hili?
Tisa, Kifungu
22: Ukiweka ujumbe katika mtandao na ukaufuta au kuuboresha, kama
ukishtakiwa kwa kuweka ujumbe huo unaweza kuhukumiwa pia kwa adhabu ya
kuuboresha au kuufuta. Ni mara ngapi unafuta ‘status’ zako za WhatsApp?
Unaweza shtakiwa kwa kuchelewesha ushahidi kisa tu ulifuta na hamna mtu
anayeweza kujua ulifuta kwa kusudi au la.
Kumi, Mkuu
wa kituo cha Polisi chochote kile nchini anaweza kuagiza wewe umpatie
simu/laptop yako au taarifa zako zote (kwenye email, chats) au hata
vifaa vyako au ofisi yako kwa ajili ya upelelezi bila oda ya Mahakama.
Kumi na moja,
Kifungu 31 (3a): “As soon as practicable” the law states. Askari Polisi
wakichukua vitu vyako wanaweza kukupatia listi ya vitu walivyovipokea
muda watakaoona kwao inawezekana kufanya hivyo. Jiulize, inaweza chukua
muda gani?
Kumi na mbili, Kifungu
31-35 & 39-45: Kama wewe ni Blogger au mtoa huduma ya mtandao, pale
unapobaini kosa ukalitoa na uko katika mikakati ya kuitaarifu mamlaka
husika (Kama sheria inavyosema), askari naye anaweza kwa wakati huohuo
akaja kukagua na kuchukua vitu vya kazi zako, hivyo sheria inakinzana
yenyewe kwa yenyewe. Blogger yuko sawa kisheria na askari yuko sawa
kisheria.
Je, sheria hii ikisainiwa na Rais Jakaya Kikwete tutapona?
DAVID Kafulila
Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi)
Hizi ndio sehemu 12 zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, Bonyeza Hapa chini== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO CHAFU YA AGNESS MASOGANGE== >