Natambua
umuhimu wa watu kukutana sehemu mbalimbali na kubadilishana mawazo,
haijalishi ni eneo gani ambalo litatumika. Wapo ambao stori zao
huzipigia baa na wengine maskani tu.Huko ndiko tunakojadili mambo kadha
wa kadha yanayogusa maisha yetu ya kila siku. Mimi nadhani ni jambo la
msingi sana kwani naamini watu zaidi ya mmoja wanapokutana na
yanayozungumzwa yakawa ni yenye maana, ni lazima yatakuwepo mabadiliko
chanya kwa wahusika.
Lakini
pamoja na yote hayo, nimegundua kuna baadhi ya wanaume wanapokuwa
kwenye mazungumzo kama hayo huingia pia katika kuzungumzia maisha yao ya
kimapenzi na baya zaidi ni kwamba, badala ya kuzungumzia mambo mazuri
huingia kwenye kuzianika kasoro walizonazo wapenzi wao. Jamani huu si
ulimbukeni uliopitiliza?
Yaani
wanafanya hivyo wakiwa na imani kwamba eti kwa kuzieleza kasoro hizo,
wenzao watawasaidia katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo yao. Unaweza
kumsikia jamaa akisema mbele za watu;
“Unajua kuna kitu kinaniumiza kichwa sana washikaji, mpenzi wangu hayajui kabisa mapenzi, yaani nikiwa naye faraha naona kama niko na gogo vile!” Labda nikuulize wewe msomaji, kwa mtu mwenye busara anaweza kweli kuanika kasoro hiyo kwa wenzake?
“Unajua kuna kitu kinaniumiza kichwa sana washikaji, mpenzi wangu hayajui kabisa mapenzi, yaani nikiwa naye faraha naona kama niko na gogo vile!” Labda nikuulize wewe msomaji, kwa mtu mwenye busara anaweza kweli kuanika kasoro hiyo kwa wenzake?
Mimi
mwenyewe naamini katika ushauri nikitambua kuwa, kupitia ushauri
ninaoweza kuupata kutoka kwa watu wangu wa karibu naweza kupata mwanga
wa kufanya maamuzi sahihi lakini siamini kama kupitia vikundi vyenye
mchanganyiko wa watu naweza kupata ushauri mzuri hasa ninapokuwa na
matatizo yanayohusu maisha yangu ya kimapenzi.
Jamani,
mapenzi ni mambo ya siri hivyo ni vema yakaheshimiwa na ifike wakati
basi tuchuje yale ambayo tunastahili kuyanadi mbele za watu kuhusu
wapenzi wetu na mengine yabaki kuwa siri ya wewe na mpenzi wako. Hapo
ndipo heshima ya penzi inapopatikana.
Yako
mambo mengi ya mpenzi wako yasiyostahili kusemwa mbele za watu, lakini
muhimu kabisa ni masuala yote yanayohusu tendo la ndoa, kasoro za
kimaumbile hasa za mwili, uwezo wa kuelewa mambo na elimu hasa inapokuwa
ya chini. Migogoro ya ndani, hitalafu za kitabia na dhiki
mnazokabiliana nazo hazitakiwi kabisa kutoka nje ya kuta za chumba
chenu.
Athari
za kutoa siri za ndani zipo nyingi, uchunguzi unaonesha kwamba sababu
nyingi za kusalitiana na kuvunjika kwa uhusiano wa kimapenzi hutokana na
kuvuja kwa siri za ndani za wapenzi.
Ikiwa mwanaume atatangaza jinsi mpenzi wake asivyotosheka na tendo la ndoa au namna mkewe anavyoongoza kwa usaliti sina shaka wafitini watapata pa’ kuanzia.
Ikiwa mwanaume atatangaza jinsi mpenzi wake asivyotosheka na tendo la ndoa au namna mkewe anavyoongoza kwa usaliti sina shaka wafitini watapata pa’ kuanzia.
Hivi
kuwaambia washikaji zako kwamba mpenzi wako hajui mapenzi unataka wao
wamfundishe au unataka wakushauri uachane naye? Ukishamuacha je? Labda
nikufahamishe tu kwamba, wapo marafiki zako ambao wanaweza kukushauri
uachane na mpenzi wako lakini baada ya kumuacha wao wakamchukua.
Niseme
tu kwamba, kama mpenzi wako si mtundu wala mbunifu suluhisho si
kumtangaza kwa wenzako bali wewe ndiye utakuwa na jukumu la kumuelekeza
katika hili na lile na mwisho wa siku naamini atakuwa bora zaidi.
Ni hayo tu kwa leo. Niwatakie mwaka mpya wenye mafanikio.
Ni hayo tu kwa leo. Niwatakie mwaka mpya wenye mafanikio.
Hizi ndio sehemu 12 zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, Bonyeza Hapa chini== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO CHAFU YA AGNESS MASOGANGE== >