Treni
ya kisasa (Delux), kwenda Bara yenye mabehewa 22 ilianza safari yake ya
saa 30 kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma ikiwa ni tofauti ya saa sita
ikilinganishwa na safari ya treni ya zamani.
Kutokana
na tofauti hiyo, abiria walioanza safari kwa furaha na matumaini jana
saa tano asubuhi wanatarajiwa kufika Kigoma leo saa 11 jioni badala ya
saa tano usiku.
Hata
hivyo, abiria hao watalazimika kuingiza mikono yao zaidi mifukoni,
kutokana na kiwango kipya cha nauli kuwa Sh79,400 badala ya Sh75,700 za
awali kwa daraja la kwanza.
Huku
nauli za daraja la pili ikishuka kutoka Sh55,400 hadi Sh,47,600 zile za
daraja la tatu zimepanda kutoka Sh27,700 hadi Sh35,700.
Kwa
mtazamo wa haraka, mabehewa hayo yanavutia yakilinganishwa na yale ya
awali yaliyokuwa yamekithiri kwa uchakavu, yaliyokuwa yamejaa mende na
yenye milango na madirisha mabovu.
Mabehewa
hayo yana viti vya kutosha, huduma ya intaneti, swichi za umeme za
kuchajia simu na kuunganisha kompyuta na safari zake zimeongezeka kutoka
mbili hadi tatu kwa wiki.
Akizungumza
muda mfupi kabla uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli
Tanzania (TRL), Mhandisi Kipallo Kisamfu alisema wamelazimika kupandisha
viwango vya nauli kutokana na gharama zitakazokuwa zinatumika katika
uendeshaji wa treni hiyo.
“Licha
ya kuongeza kidogo kiwango cha nauli, dhamira yetu ni kuwapatia abiria
huduma safi na ya raha... kila msafiri atasafiri akiwa ameketi kwenye
kiti chake. Hakuna abiria atakayesafiri akiwa amesimama,” alisema na
kuongeza: “Treni inayozinduliwa leo inatumia mabehewa mapya 22
yaliyonunuliwa kutoka Korea Kusini na kichwa cha treni kiliundwa upya
kwenye karakana ya TRL iliyopo Morogoro mabehewa mapya yamegharimu
Serikali Sh28.6 bilioni.”
Kuhusu vituo vya ambavyo treni hiyo alisema itasimama kwenye vituo vikubwa ambavyo vingi ni vile vya miji, wilaya na mikoa.
Katibu
Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Dk Shabaan Mwinjaka aliwataka abiria kuwa
walinzi wa treni hiyo ili kuhakikisha usafiri huo unadumu.
“Kumekuwa
na tabia ya watu kujiamulia kuharibu mali za umma, ninawaomba abiria
mtakaopanda treni hii muwe walinzi wa wenzenu kwa sababu baadhi ya
abiria wamekuwa na tabia ya kuchora kwenye viti,” alisema Dk Mwinjaka.
Mmoja
wa abiria, Saida Roman alisema Serikali inahitaji kupewa pongezi kwa
hatua hiyo kwani hivi sasa abiria wanaotumia usafiri wa treni kutoka Dar
es Salaam kwenda Kigoma watasafiri kwa raha tofauti na ilivyokuwa
zamani.
-Mwananchi
Hizi ndio sehemu 12 zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, Bonyeza Hapa chini== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO CHAFU YA AGNESS MASOGANGE== >