Kufuatia
tishio la ugaidi la kuipiga miji mikubwa ya Tanzania, Dar es Salaam na
Mwanza, kupitia ujumbe uliosambaa kwenye mitandao ya kijamii, majeshi ya
ulinzi yamesema yameimarisha ulinzi nchi nzima.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Ernest Mangu, alipoulizwa na mwandishi
wetu jana, alithibitisha kuwa jeshi hilo linazo taarifa za uwekezako wa
kuwapo kwa ugaidi.
Alisema hata hivyo kuwa tayari wameshajizatiti na wameshatoa maelekezo kwa polisi waliopo mikoa yote nchini kuimarisha ulinzi.
Alisema kwa sasa wanaendelea kufuatilia kwa undani zaidi taarifa walizonazo kama ni za kweli au la.
“Baada
ya kupokea taarifa hizi (bila kusema chanzo chake), tumejiimarisha na
tumeshatoa maelekezo kwa polisi wetu waliopo mikoa yote wachukue
tahadhari kwenye maeneo yao,” alisema na kuongeza:
“Kila
taasisi ya usalama imepata ujumbe huu wa uwezekano wa Tanzania
kushambuliwa na magaidi, kila mmoja anafuatilia kama ni kweli au
uongo,” alisema.
Mangu
amewaomba wananchi watoe ushirikiano kwa vyombo vya usalama pale
wanapohisi tofauti kwenye maeneo yao ili hatua ziweze kuchukuliwa mapema
kabla ya hatari.
Tishio
hilo kupitia ujumbe uliosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, lilienea
jana katika mitandao mbali mbali na Jeshi la Polisi limethibitisha
kupata ujumbe huo.
Moja ya ujumbe uliozagaa kwenye mitandao ya kijamii ni ule unaosomeka:
"The Australian, UK and US governments have issued an enhanced terrorist alert for Uganda.
"Al Jazeera TV have intimated possible attacks in Mwanza and Dar es Salaam in Tanzania.
For
information, James Ferdinand of UNAS Security and ATN Officer at the
Philippines Embassy in Nairobi, Kenya, can be contacted. Friend please
forward this sms to all your friends in Dar and Mwanza"
Ujumbe huo kwa tafsiri yake unanaanisha kuwa;
"Serikali za Australia, Uingereza na Marekani zimetoa tahadhari ya kufanyika kwa matukio ya ugaidi nchini Uganda.
"Televisheni ya Al Jazeera imetoa tahadhari ya uwezekano wa kuwapo kwa mashambulizi katika miji ya Mwanza na Dar es Salaam.
Kwa
taarifa James Ferdinand wa Shirika la Usalama la UNAS na Ofisa wa
Ubalozi wa Filipini jijini Nairobi, Kenya, wanaweza kutafutwa kwa
ufafanuzi.
"Rafiki tafadhali sambaza ujumbe huu kwa marafiki zako wote wa Dar es Salaam na Mwanza".
Wakati
Mangu akitoa tahadhari hiyo, Msemaji wa jeshi hilo, Advera Bulimba,
juzi katika taarifa yake, alisema wameimarisha ulinzi kwenye maeneo yote
yakiwemo yale ya kuabudia ambapo huwa na mkusanyiko ambao magaidi
wamekuwa wakiitumia kufanya mashambulizi yao.
Maoni ya Wadau
Miongoni
mwa wadau waliozungumzia tishio hilo ni aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa
Chama cha Wanachi (CUF) Julius Mtatiro, anayesema ana wasiwasi ndani ya
nchi kuna kundi la watu linalojiandaa na matukio ya kigaidi, kutokana na
mfululizo wa matukio ya kupora silaha kutoka kwa polisi.
Alisema
jeshi la polisi pekee halitaweza kukabiliana na hatari hiyo kutokana na
matukio ya hivi karibuni katika mikoa ya Tanga na Pwani, kuonyesha
kuzidiwa kiasi ambacho ilibidi kuomba msaada kutoka Jeshi la Wananchi
(JWTZ), kukabiliana na makundi ya watu wanaodaiwa kuwa zaidi ya
majambazi.
“Uvamizi
wanafanyiwa askari wetu, wanauawa na kuporwa SMG’s, napata shaka kuwa
kuna kundi liko mahali linakusanya silaha taratibu na kujiandaa na
uvamizi mahali,” alisema Mtatiro.
Alisema
kutokana na magaidi kugeukia vyuo vikuu kama sehemu za mashambulizi,
serikali inapaswa kuweka ulinzi mkali ili visishambuliwe.
Alisema
kwa mtazamo wake anaona bado nchi inakabiliwa na ulinzi wa kuamini
Mungu kutokana na maeneo ya vyuo kuwa rahisi kupitisha silaha hadi
mabwenini.
“Utachoka
pale ukiingia Mabibo Hostel na kitu chochote utapitisha tu. Hizi ni
hostel na vyuo ambavyo vinalindwa na askari wa makampuni binafsi wasio
na silaha au wakiwa na silaha duni," alisema.
Naye
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dare s Salaam, Dk. Benson Bana, alisema
serikali inatakiwa kuchukua hatua za haraka na kuacha tabia ya kupuuza
kila jambo wanalosikia.
“Suala
la ugaidi ni jambo zito ambalo huwezi kuliacha hivi hivi tu, tumeona
wenzetu Uganda walivyochukua hatua na sisi tusizembee tuhakikishe ulinzi
unawekwa kila mahali," alisema.
Alisema
suala la ugaidi halitoki nje ya nchi pekee kwani hata ndani kuna
uwezekano kuna watu wanaotumika na lazima tufikie mahali tuweze
kutambuana ili iwe rahisi kuzuia jambo baya.
Leo wakristo Tanzania wanaungana na wenzao duniani kusherehekea sikukuu ya Pasaka.
Siku
tatu zilizopita, wanamgambo wa Kisomali walifanya shambulizi Chuo Kikuu
cha Garissa, kilichopo nchini Kenya na kuwaua watu 147.
Wanamgambo
hao ambao wakati wakivamia kampasi ya chuo hicho, walikuwa wameficha
nyuso na kujifunga milipuko kwenye miili yao na silaha, walirusha
maguruneti na kumimina risasi dhidi ya wanafunzi.
Shambulizi
hilo lililodumu takriban saa 15, awali lilifanyika bila kuchagua lakini
baadaye baadhi ya Waislam waliachiwa na kuelekeza mashambulizi kwa
Wakristo.
Hizi ndio sehemu 12 zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, Bonyeza Hapa chini== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO CHAFU YA AGNESS MASOGANGE== >