Kusambaa kwa taarifa za uwezekano wa kutokea kwa shambulio la kigaidi katika miji ya Tanzania, ikiwemo Dar es Salaam na Mwanza, kumesababisha baadhi ya taasisi muhimu kama vyuo vikuu na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kuchukua hatua za kujihami.
Taarifa
zilizotufikia jana zilieleza kuwa Tanesco na baadhi ya vyuo, vimeweka
taarifa ya tahadhari na kutoa masharti kwa wafanyakazi na wanafunzi, ya
namna ya kujilinda.
Mtandao
huu ulimuuliza Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Felchesmi Mramba, kuhusu
hatua hizo ambapo alikiri shirika hilo kuchukua hatua za ziada kujihami
na uwezekano wa shambulio hilo.
Mramba
alisema wamechukua hatua hizo za kiusalama baada ya kuwepo kwa tetesi
za uvamizi hasa baada ya kuwepo kwa tukio la nchi jirani ya Kenya,
ambako wanafunzi 148 waliuawa.
“Kutokana
na tishio hilo, tumeona ni vyema tuchukue hatua mapema… si lazima
yatokee ndiyo tuchukue hatua, tumeona ni vyema kujihami kwa kuimarisha
ulinzi katika vituo vyetu.
“Kuna
baadhi ya maeneo yetu ni maalumu na yakiwa na athari za kiusalama ni
hatari kwa nchi nzima... hivyo ni vyema tuchukue tahadhari kubwa maana
kunapotokea tatizo, huathiri nchi nzima,” alisema.
Vitambulisho
Alisema wamewaelekeza na kuwasisitiza watumishi wao kuimarisha ulinzi wao na katika maeneo ya kazi. “Kwa
kawaida tuna vitambulisho vya ofisi lakini kuna watu wengine walikuwa
hawavai, ila kwa sasa tumesema ni lazima kila mfanyakazi avae
kitambulisho wakati wote,” alisema.
Katika
Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IMF) hali ya ulinzi ilikuwa imeboreshwa,
ambapo kila mwanafunzi alitakiwa kuvaa kitambulisho chake awapo katika
maeneo ya chuo, ili mgeni yeyote atambulike kwa haraka.
Uongozi
wa chuo hicho ulichukua tahadhari kwa kuweka tangazo kumtaka kila
mwanafunzi achukue tahadhari pale anapoona mtu ambaye ana shaka naye au
kitu cha kutia shaka; pia taarifa hiyo iliwataka wanafunzi kuvaa
vitambulisho vyao.
Ukaguzi
Mramba
alisema mgeni yeyote atakayefika katika ofisi za shirika hilo kwa sasa
ni lazima akaguliwe na ajulikane anatoka wapi na anaingia ofisini kwa
sababu gani. Mbali na ofisini, alisema ukaguzi pia utafanyika kwa watu
wote wanaoingia kwenye mitambo.
“Tumeimarisha askari wetu ili kuhakikisha rasilimali za Tanesco ambazo ni za nchi zipo salama.”
Katika
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), katika lango kuu la kuingilia
ofisi mbalimbali za utawala, kumewekwa ulinzi na watu wote wanaoingia na
kutoka, wamekuwa wakikaguliwa kwa vifaa maalumu tofauti na huko nyuma.
Matangazo ya tahadhari
Aidha
UDSM, kama ilivyo IFM pia kumebandikwa tangazo lililotolewa na Kaimu
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho (Utawala), Profesa Cuthbert Kimambo,
likieleza kuwa hatua madhubuti zinachukuliwa na zitaendelea kuchukuliwa
katika kuimarisha ulinzi.
Alisema
kutokana na taarifa za tahadhari kuhusu matukio ya uhalifu yenye
taswira ya kigaidi katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu, ni jukumu la
kila mwana jumuiya ya chuo hicho kuwa macho kusaidia kuimarisha ulinzi
na usalama.
“Baadhi
ya hatua zinaweza kuleta usumbufu kwa wengi wetu. Taarifa zitatolewa
inapowezekana, lakini tunaomba uvumilivu na ushirikiano wenu ili
kuhakikisha usalama wetu,” ilisema taarifa hiyo ya Profesa Kimambo.
Hizi ndio sehemu 12 zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, Bonyeza Hapa chini== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO CHAFU YA AGNESS MASOGANGE== >