Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limeviweka chini ya ulinzi na kuvifanyia uchunguzi vituo vitatu vilivyokusanya watoto 115 kutoka mikoa 13 nchini kwa lengo la kuwapatia mafunzo ya dini ya Kiislamu.
Vituo hivyo vyote vipo katika eneo la Nkuhungu, lililopo katika Manispaa ya Dodoma.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime, alisema wanafanya
uchunguzi katika vituo hivyo kutokana na kuhusika kuendesha vituo vya
kulelea watoto bila kusajiliwa na hatarishi.
“Jana (juzi) saa sita usiku tulifanya upekuzi katika vituo vitatu,
katika kituo cha kwanza tukafanikiwa kukuta watoto takribani 63, kati
yao 46 chini ya miaka 18.
“Katika kituo cha pili tulikuta watoto 40, kati yao walio chini ya
umri wa miaka 18 walikuwa 12, kituo cha tatu tuliwakuta watoto saba,
kati yao wenye umri chini ya 18 ni watano,” alisema Misime.
Alisema katika idadi ya watoto wote hao, 63 wana umri wa chini ya miaka 18 na wengine 52 umri wao ni miaka 25.
Alisema watoto hao wote ni wanaume na wengi wanatoka katika Wilaya ya
Kondoa ambao ni 50 na watoto 26 wanatokea katika Wilaya ya Dodoma
Mjini, Chamwino na Mpwapwa.
“Watoto wanaosalia wanatokea mikoa ya Kagera, Dar es Salaam,
Kilimanjaro, Zanzibar, Tanga, Tabora, Singida, Pwani, Lindi, Mtwara,
Geita, Mwanza na Manyara,” alisema Misime.
Alisema watoto hao walikutwa usiku wakiwa wamechanganywa bila kujali umri wao, jambo ambalo ni hatarishi.
“Uchunguzi
unaendelea na yeyote atakayeguswa na ushahidi kuwa amekiuka sheria
atafikishwa mahakamani, ikiwepo wazazi walioruhusu watoto hao
kuwa katika uangalizi ambao si wa kutosha kama Sheria ya Mtoto ya mwaka
2009 inavyoelekeza,” alisema Misime.
Mwandishi wetu jana alifika katika moja ya nyumba hizo ambayo iko
eneo la Nkuhungu CCM katika Manispaa ya Dodoma inayohifadhi watoto
takriban 60 na kushuhudia watoto hao wenye umri kuanzia miaka mitatu na
kuendelea wakiendelea na shughuli zao na wengine wakinywa uji.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya majirani walisema wameanza kuwaona watoto hao tangu mwishoni mwa mwaka jana.
Mmoja wa jirani hao, Mama Naomi, alisema siku zote amekuwa akiwaona
watoto hao wakishinda hapo na hajawahi kuwaona wakienda shule kusoma.
“Chakula na kuni za kupikia huwa wanaletewa na walimu wao,
wanajipikia wenyewe, wale watoto wadogo kazi yao ni kuosha vyombo,”
alisema Mama Naomi.
Wakizungumza katika eneo hilo, baadhi ya watoto hao walisema wapo hapo kwa ajili ya kupatiwa mafunzo ya dini ya Kiislamu.
Walipoulizwa kama wanaenda shule kutokana na wao kuwa na umri mdogo,
watoto hao walijibu kuwa baadhi yao wanasoma elimu ya msingi na wengine
sekondari.
“Mimi nimetoka Kondoa lakini nilipokuja hapa nimeandikishwa Shule ya
Msingi Nkuhungu, nikimaliza kusoma dini hapa huwa nakwenda shuleni,”
alisema mmoja wa watoto hao.
Akizungumzia tukio hilo, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustapha
Rajab, alisema hakuna dhambi yoyote kwa watoto hao kulelewa katika kituo
hicho.
“Hayo ni mafunzo katika madrasa ambazo zilianza zamani ulimwenguni
kote, polisi haina mamlaka ya kufunga madrasa, labda kama watakuta kuna
tatizo lolote la kuhatarisha amani,” alisema Rajab.
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Betty Mkwasa, alisema
amesikitishwa na hali ya mazingira katika eneo hilo ambayo hayafai
kuishi binadamu wa kawaida na kuahidi Serikali itachukua hatua za kisheria.
Hizi ndio sehemu 12 zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, Bonyeza Hapa chini== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO CHAFU YA AGNESS MASOGANGE== >