Wachimbaji wadogo wa dhahabu mkoani Shinyanga, maarufu 'manyani', wamekufa katika machimbo madogo ya Kalole wilayani Kahama, baada ya kufukiwa na kifusi usiku wa kuamkia jana.Vifo hivyo vilitokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Akizungumza
kwa simu, Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya alisema wachimbaji
hao walikumbwa na mauti hayo baada ya kuingia ndani ya mashimo hayo kwa
njia ya panya kwa lengo la kutafuta mawe yenye dhahabu.
Mpesya
alisema wachimbaji hao ni wale ambao huingia mashimoni kuiba mawe hayo,
baada ya muda kumalizika wa kufanya kazi ambayo kwa kawaida huishia saa
12.00 jioni.
Baada ya hapo, imeelezwa ndio watu hao 'manyani' huvamia mashimo hayo nyakati za usiku kwa kuiba mawe hayo.
Katika
tukio hilo, Mpesya alisema wachimbaji hao wote 19 waliingia kwenye
mashimo manane, ambayo yameunganika kwa chini, walikufa baada ya mashimo
hayo kuanza kubomoka kutokana na mvua hiyo.
Mkuu
huyo wa wilaya alisema baada ya ajali hiyo, kazi ya kufukua ilifanyika
ambapo maiti 19 waliopolewa ingawa kutokana na hali ya unyevu kwenye
mashimo hayo yanayoendelea kutitia, wamelazimika kusimamisha ufukuaji.
“Unajua
hawa ndugu zetu ni wale wachimbaji wasiokuwa na mashimo ambao muda
ukiisha wa kazi huingia kwenye mashimo hayo bila kuangalia usalama na
ndivyo ilivyotokea kwa wachimbaji hao,” alisema Mpesya na kuongeza kuwa
maiti 17 kati 19 wametambuliwa na ndugu zao.
Katika
jitihada za kutafuta wengine, tayari wameomba mashine za kufukua kutoka
katika mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu pamoja na zile za kunyonya maji.
Mpesya
alisema idadi inaweza kuongezeka baada ya kazi ya kufukua kukamilika
kwa kuwa hawawezi kujua kama maiti hao 19 ndio hao hao waliokuwemo ndani
ya mashimo hayo.
“Tunasubiri
wenzetu kutoka mgodi wa Bulyanhulu waje waone kwanza mitambo ipi ambayo
inaweza kutumika kufukua mashimo hayo, kwa kuwa ufukuaji wa kienyeji
tuliokuwa tukiutumia tumeusimamisha kutokana na mashimo hayo kuendelea
kutitia,” alisema Mpesya.
Machimbo
hayo yako katika Kijiji cha Kalole katika Kata ya Lunguya katika
Halmashauri ya Msalala. Ni moja ya migodi ya wachimbaji wadogo
wanaokisiwa kufikia 30,000 na tayari wengi wao wamejipatia mamilioni ya
fedha kwa uchimbaji huo wa kienyeji, ingawa hali hiyo ni hatari katika
maisha yao wakati wa mvua za masika.
Hizi ndio sehemu 12 zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, Bonyeza Hapa chini== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO CHAFU YA AGNESS MASOGANGE== >