RAIS mstaafu wa awamu ya pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Abood Jumbe Mwinyi (94), yupo hoi baada ya kulazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili akisumbuliwa na maradhi ya moyo.
Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam jana, Ofisa Uhusiano wa Hospitali ya Muhimbili, Doris Ishenga, alisema Jumbe alipokewa hospitalini hapo tangu Oktoba 12, mwaka huu.
Amelazwa katika Taasisi ya Moyo baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kina.
Alisema kwa mujibu wa taarifa za madaktari za Kitengo cha Moyo hospitalini hapo, baada ya kumfanyia uchunguzi wamebaini Jumbe anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo hali inayobabishwa na kuwa na umri mkubwa.

“Ni kweli Alhaj Jumbe alifikishwa hapa Muhimbili tangu Jumamosi iliyopita na amelazwa katika wodi ya moyo akisumbuliwa na maradhi ya moyo.
“Unajua ugonjwa huu unawapata zaidi watu wenye umri mkubwa, madaktari wamesema hali yake si mbaya na wala si nzuri sana,” alisema.
Jumbe alikuwa Rais wa Zanzibar kuanzia mwaka 1972 hadi 1984 akishika nafasi hiyo baada ya kuuawa kwa aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, marehemu Abeid Aman Karume Septemba 5, 1972.
Alijiuzulu mwaka 1984 baada ya kutokea mfarakano wa kisiasa kati yake na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutokana na kile kinachoelezwa kuwa na msimamo wa kutaka mfumo wa Serikali tatu ili Zanzibar iwe na mamlaka yake kamili.
Baada ya kutoa msimamo huo, Jumbe alipata upinzani ndani ya Serikali na chama chake na kutakiwa ajiuzulu urais wa Zanzibar.
Baada ya uamuzi kutolewa kwenye vikao vya juu vya CCM, Jumbe aliachia nafasi hiyo ambayo ilichukuliwa na Ali Hassan Mwinyi mwaka 1984, ambaye baada ya mwaka mmoja alichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
chanzo: mtanzania
Hizi ndio sehemu 12 zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, Bonyeza Hapa chini== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO CHAFU YA AGNESS MASOGANGE== >