Ndugu wanahabari kumekuwa na utaratibu wa habari zinazoupotosha umma wa Watanzania kuhusu chama chetu cha ACT-Tanzania.
Katika gazeti la mwanahabari toleo na 117 la tarehe 29/09/2014 katika
ukurasa wake wa mbele iliandikwa "MKAKATI WA KUKIPA NGUVU CHAMA CHA
KIPYA CHA ZITTO KABWE WAVUJA".
Act-Tanzania tunaeleza kuwa ni chama cha Watanzania wote kisichokuwa
na mmiliki wake na tunaunganishwa na misingi kumi ya chama pamoja na
Itikadi yetu ya demokrasia jamii.
Act-Tanzania tunatambua uwezo na mchango wa kisiasa na ujenzi wa
demokrasia ya vyama vyingi nchini uliotolewa na Mheshimiwa Zitto Kabwe
mbunge wa Kigoma Kaskazini.
Na kwamba kwa sasa ana kesi na chama chake mahakamani na tunaamini
atakapomaliza kesi hiyo mchango wake katika siasa za upinzani za
Tanzania ni muhimu sana.
Act-Tanzania tunaamini kwamba Mheshimiwa Zitto Kabwe ni mwanasiasa
mahiri na makini hivyo tunamkaribisha kwa moyo mkunjufu katika chama
mbadala Tanzania.
Na kuhusiana kwamba kuna mkakati wa kuipa nguvu Act-Tanzania ni
taarifa za kutunga kwani mikakati yetu ya kuimarisha chama na uenezi
wake ni mkubwa na mipango yetu inayotekelezwa kwa umakini na weledi
mkubwa.
Na Act-Tanzania tumejipanga kufanya siasa zitakazoleta mabadiliko
nchini na kasi yetu inatokana na juhudi na mshikamano wa viongozi wa
ngazi zote.
Aidha tunatumia eneo kubwa la mipango yetu ya kukieneza chama kwa
mfano kwa sasa tumemaliza ziara ya mikoa 12 na majimbo 68 hivi karibuni
iliyokuwa na mafanikio makubwa sana.
Pamoja na mambo mengine tulitoa maelekezo ya maandalizi ya uchaguzi
wa vijiji, vitongoji na serikali za mitaa tarehe 14/12/2014,
tukitekeleza azimio la kikao cha Halmashauri kuu kilichofanyika Singida.
Hivyo hakuna mkakati wa kuibeba ACT-Tanzania, Bali ACT-Tanzania inabebwa na umakini na weledi katika mipango yake.
Kuhusu Bwana Samson Mwigamba na Profesa Kitilia Nkumbo kujiunga na
Act-Tanzania hawa ni Watanzania na baada ya kufukuzwa na chama chao cha
zamani Act-Tanzania tuliona mchango wao bado unahitajika katika siasa
hapa nchini na kwa kuwa hakukuwa na kizuizi kwa wao kujiunga na
Act-Tanzania basi tuliwapokea na kwa sasa wanatumikia Act-Tanzania kwa
moyo wa kizalendo kabisa.
Kuhusiana na hoja ya kwamba kuna mamluki wa upinzani hizo ni siasa
nyepesi kwani unapofukuza wanasiasa mahiri ndani ya chama chochote na
wanapokosa fursa ya kufanya siasa pale walipofukuzwa hakuna dhambi ya
kushiriki siasa katika chama kipya cha siasa hapa nchini.
Mwisho tunawashukuru Watanzania wote wanaoendelea kutuunga mkono nchini kote.
Pia tunapenda kutoa tamko kwamba kwa mujibu wa maazimio ya kikao cha
Halmashauri kuu kilichokutana mjini Singida tarehe 25-26/7/2014
tunaendelea na maandalizi ya uchaguzi wa vijiji,vitongoji na serikali za
mitaa na maandalizi yetu yanaendelea vyema kabisa.
Lakini pia tunaheshimu uhuru wa kutoa habari waliotumia gazeti la
Mwanahabari lakini tumesikitishwa sana na wao kama chombo huru kushindwa
kutuhoji sisi kama chama baada ya kuwa na habari wanayoiita "MKAKATI WA
KUKIPA NGUVU CHAMA KIPYA CHA ZITTO KABWE WAVUJA".
Imetolewa Leo tarehe 01/10/2014
Na Mohammed Massaga
Katibu mawasiliano na Uenezi wa ACT-TANZANIA Taifa
Hizi ndio sehemu 12 zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, Bonyeza Hapa chini== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO CHAFU YA AGNESS MASOGANGE== >