CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema vitendo vinavyofanywa na Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ni ukiukwaji wa Katiba na kanuni za chama hicho.
Aidha,
kimesema vitendo vinavyofanywa na Lowassa ni kampeni za wazi za urais
anazoendesha kabla ya muda kufika na hivyo kukiuka Katiba na kanuni za
CCM na kuonya kuwa kama ataendelea na kampeni hizo haramu atapoteza sifa
za kugombea nafasi ya urais.
Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alitoa ufafanuzi huo baada ya
waandishi wa habari waliopo katika msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana kutaka ufafanuzi wa kinachoendelea mjini Dodoma kwa
makundi tofauti kwenda kwa Lowassa kwa madai ya kumshawishi agombee
urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Nape akizungumzia suala hilo alisema, “Anachokifanya
Lowasa ni kuvunja kanuni na kiburi, ni matendo ya wazi ya kampeni, bila
shaka anajua adhabu yake. Matendo hayo yanaweza kumpotezea sifa za kuwa
mgombea kupitia CCM.”
Katibu
huyo wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa aliongeza kuwa Lowassa ni miongoni
mwa wanaCCM ambao walipewa adhabu na CCM mwaka mmoja uliopita kwa kuanza
kampeni kabla ya wakati na mpaka sasa bado wapo kwenye kipindi cha
uangalizi wakati vikao husika vikiendelea na tathmini dhidi yao.
Nape alisisitiza kuwa matendo yanayoendelea hivi sasa ni dhahiri kuwa ni kiburi kisicho na maana dhidi ya CCM.
“Lowasa
anajua utaratibu wa Chama katika kuwapata wagombea wake kwa ngazi
mbalimbali kuanzia udiwani mpaka urais hivyo kuendelea na matendo ambayo
yanatafsiri ya wazi kuwa ni kampeni ni kiburi cha wazi.
“Kwa matendo hayo ya Lowassa labda dhamira iwe ni kuomba ridhaa ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama kingine na si CCM.”
Nape
alisema ni vyema wagombea wa ngazi mbalimbali wakahakikisha
wanazingatia Katiba na kanuni za chama hicho ili wasiingie kwenye kundi
la kutokuwa na sifa ya kuomba ridhaa ya kugombea udiwani, ubunge na
urais.
“Tunaendelea
kukumbusha na kusisitiza kwamba wale wote wenye nia ya kugombea kupitia
chama chetu kuheshimu kanuni na tararibu za kupata ridhaa kugombea kwa
ngazi ya chama chetu,” alisema Nape.
Lowassa
amedaiwa kuwa amekuwa akitumia makundi mbalimbali kufanya kampeni
ambapo alianza na kikundi cha wajasiriamali jimboni Monduli mkoani
Arusha ambapo walienda nyumbani kwake kumuomba agombee.
Hatua
hiyo ilifuatiwa na mashehe 50 kutoka wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani
ambao nao walikwenda nyumbani kwa Lowassa Dodoma kwa lengo la
kumshawishi agombee urais.
Baadaye
walifuata wachungaji ambao nao walifunga safari hadi nyumbani kwa
Lowassa Dodoma na kusema wameamua kumuomba Lowassa agombee urais kwa
madai kuwa ana maono makubwa dhidi ya Tanzania.
Baadhi
ya wachungaji hao walimwambia Lowassa wanaamini kuwa yeye ndio chaguo
sahihi kwao na ndio maana wameamua kufunga safari na kumshawishi huku
wakieleza kuwa kila mtu ametumia nauli yake kufika Dodoma.
Kwa
upande wake Lowassa, akizungumza na wachungaji hao waliofika nyumbani
kwake, alisema anafarijika kuona makundi mbalimbali yakifika nyumbani
kwake kumshawishi agombee.
Alinukuliwa
na vyombo vya habari juzi akisema pia kuwa hakuna kundi ambalo
analituma au kulipa fedha kwa ajili ya harakati za kutaka kugombea
urais.
Hizi ndio sehemu 12 zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, Bonyeza Hapa chini== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO CHAFU YA AGNESS MASOGANGE== >