
Jacqueline Lepenza, akiwa na baba'ke.
Willy Lupenza, baba mzazi wa mtoto huyo mwenye umri wa miaka mitatu
na nusu, alisema marehemu mke wake, Anjela Osward (35) (pichani) alikuwa
amekwenda nyumbani kwao Ilembula mkoani Njombe kwa ajili ya ubatizo wa
binti yao huyo.Alisema katika hali ya kushangaza, siku ya ubatizo huo, Jacqueline alibatizwa peke yake pasipo watoto wenzake kupewa baraka hizo kwa sababu ambazo hazikueleweka.“Ndugu mwandishi, hili ni tukio ambalo sitalisahau katika maisha yangu, kwa sababu haiwezekani mtoto abatizwe peke yake halafu kwenye ajali, idadi kubwa ya watu wapoteze maisha lakini yeye anusurike.”
Alisema baada ya ajali, mtoto wake huyo alikutwa na watu waliojitokeza kuwasaidia majeruhi akiwa amelala juu ya bati la kuzuia matope kwenye tairi ya lori lililokuwa limebeba kontena huku akilia na matairi yakiendelea kuzunguka.
Alisema haelewi mtoto huyo alitokaje ndani ya basi hadi kwenye bati hilo la lori, kwani licha ya kukutwa mzima, lakini eneo hilo pia lilikuwa hatarishi kwa mwanaye ambaye alimpoteza mama yake aliyekuwa mmoja kati ya watu zaidi ya 50 waliofariki dunia.
...Akiwa na bibi yake.
Willy alisema Machi 11, mwaka huu alipata taarifa kwa njia ya simu
kutoka kwa shemeji yake ambaye yuko mkoani Iringa kwa shughuli zake za
kibiashara juu ya tukio hilo, baada ya yeye naye kuarifiwa na Jeshi la
Polisi Iringa baada ya kuokotwa kwa simu ya mkewe.Alisema baada ya kupigiwa na polisi waliofika katika eneo la tukio mapema, shemeji yake huyo alimpigia na kumjulisha juu ya mkewe kupata matatizo Mafinga.“Nilianza safari mara moja kuelekea huko, lakini nilipofika Morogoro nilipata taarifa za uhakika zilizoniaminisha kuwa mke wangu alikuwa amefariki dunia,” alisema.
Aliongeza kuwa aliendelea kufanya mawasiliano na ndugu kujua alipo mtoto, hadi alipoambiwa kuwa kulikuwa na mtoto mmoja aliyekuwa wodini (Hospitali ya Wilaya Mafinga), hivyo akaambiwa kama anaweza kuwatumia picha yake kwa njia ya mtandao ili waweze kumfananisha.
“Niliwatumia picha kwa Mtandao wa WhatsApp, kumbe siku ya ajali mwanangu alikuwa amevaa gauni ambalo aliwahi kulivaa siku za nyuma, na ndiyo picha niliyowatumia, walimtambua kirahisi na alipofanyiwa uchunguzi wa kidaktari ikagundulika kuwa hakuwa na matatizo yoyote kiafya,” alisema baba huyo.
Mamam wa Jacqueline, Anjela Osward enzi za uhai wake.
Kufuatia kufika Mafinga na kuutambua mwili wa mke wake, aliomba mwili
huo kutopelekwa sehemu yoyote ili urudishwe nyumbani kwao Ilembula kwa
mazishi yaliyofanyika katika Kijiji cha Mwambaga.Kuhusu hali ya mtoto
kwa sasa, Willy alisema anaendelea vizuri na anamshukuru Mungu pamoja na
madaktari na polisi walioshiriki katika tukio hilo ambalo mwanaye huyo
alipona kimaajabu.Ajali hiyo ilihusisha lori aina ya Scania namba T 689 APJ mali ya Cipex Company lililokuwa likiendeshwa na Maka Sebastian (26) na basi aina ya Scania namba T 438 CED mali ya Majinja lililokuwa likiendeshwa na Baraka Gabriel (38).
Hizi ndio sehemu 12 zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, Bonyeza Hapa chini== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO CHAFU YA AGNESS MASOGANGE== >