Siku
chache baada ya kifo na maziko ya aliyekuwa Mbunge wa Mbinga Magharibi
(CCM), Kapteni John Komba, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa,
amemlilia akieleza kuwa ni mtu ambaye alikuwa ‘muumini asiyeyumba wa
safari ya matumaini.’
Marehemu Komba ambaye alizikwa Jumanne iliyopita kijijini kwake Lituhi, anatajwa kuwa alikuwa rafiki wa karibu na Lowassa.
Katika
taarifa yake iliyotolewa kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam
jana, alisema moyo wake unabubujika machozi ya damu kwa kuwa marehemu
Komba alimshawishi agombee urais na amefariki dunia kabla hajampa jibu
la kukubali au kukataa.
Alisema Kapteni Komba alikuwa mmoja wa makamanda wa kuongoza harakati za kumshawishi ajitose kwenye kinyang'anyiro cha urais.
“Ulipaza
sauti bila woga kuelezea imani yako kwangu. Kapteni naumia sana
umeondoka bila ya kukupa jibu la kukubaliana na ushawishi wako au
la...kwa hakika Chama kimepata pigo.”
“Hivi
ni kweli sitasikia tena sauti yako Kapteni Komba! Mbona umeondoka bila
ya kuniaga ndugu yangu! Moyo wangu unabubujika machozi ya damu," alisema Lowassa katika taarifa hiyo.
Alisema siku tatu kabla ya Komba kukutwa na umauti, alimtumia ujumbe kupitia kwa wasaidizi wake akimwambia ‘Mwambie Edward akija aje kuniona mimi sijisikii vizuri.’
“Maneno
yako kwa mmoja wa wasaidizi wangu siku tatu kabla ya umauti kukupata,
yanazunguka akilini mwangu...Kapteni Komba, mimi na wewe tumepigana vita
nyingi kwa maslahi ya Chama na nchi yetu na tulishinda vita hivyo.
Lakini bado tulikuwa tunaendelea na mapambano ya kumnasua Mtanzania
katika umaskini,” alisema Lowassa.
Aliongeza: “Ni
nani asiyejua mchango wako katika ushindi wa chama chetu katika ngazi
zote. Nyimbo zako ndiyo adhana au kengele ya kuwakusanya waumini
(wana-CCM na wananchi), katika mikutano ya Chama. Komba ulikuwa nembo ya
chama chetu.”
Alisema Komba ameondoka, lakini ameacha alama katika ulimwengu wa siasa hususan katika Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Katika
taarifa hiyo, Lowassa alisema kwa kuwa alishirikiana na Komba kwenye
nyakati za matatizo na furaha, atashirikiana na Chama kuendeleza pale
alipoachia kutatua matatizo ya familia.
Kapteni
Komba aliyefariki dunia Februari 28, mwaka huu akiwa njiani kupelekwa
Hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam, alikuwa anasumbuliwa na maradhi
ya shinikizo la damu na mara kadhaa Ofisi ya Bunge ilimpeleka India kwa
matibabu. Pia alikuwa na tatizo la kisukari ambalo ndilo lililochukua
maisha yake.
Lowassa ametoa taarifa hiyo nzito akiwa ni miongoni mwa makada wa CCM wanaotajwa kuwania nafasi ya urais.
Wengine
wanaotajwa na ambao wameshajitangaza kujitosa kuwania nafasi hiyo ni
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda; Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika,
Steven Wasira; Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Bernard Membe; Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja na Naibu Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba.
Wengine ni Mbunge wa Nzega, Dk. Hamis Kigwangwalla na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye.
Wamo
pia Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu; Waziri wa
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta; Naibu Waziri wa Fedha,
Mwigulu Nchemba; Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Asha-Rose Migiro;
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Prof. Mark Mwandosya na
Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli.
Waraka Wenyewe:
Hivi
ni kweli sitosikia tena sauti yako Captain Komba! Mbona umeondoka bila
ya kuniaga ndugu yangu! Moyo wangu unabubujika machozi ya damu.
Maneno
yako kwa mmoja wa wasaidizi wangu siku tatu kabla ya umauti kukupata
kwamba “mwambie Edward akija aje kuniona mimi sijisikii vizuri”
yanazunguka akilini mwangu.
Captain
Komba, mimi na wewe tumepigana vita nyingi kwa maslahi ya chama na nchi
yetu… na tulishinda vita hivyo. Lakini bado tulikuwa tunaendelea na
mapambano ya kumnasua Mtanzania katika umaskini.
Komba
ulikuwa muumini usiyeyumba wa “Safari ya Matumaini”. Ulikuwa mmoja wa
makamanda wa kuongoza harakati za kunishawishi niwanie urais kupitia
chama chetu. Ulipaza sauti bila woga kuelezea imani yako kwangu.
Captain, naumia sana umeondoka bila ya kukupa jibu la kukubaliana na
ushawishi wako au la.
Kwa
hakika chama kimepata pigo. Ni nani asiyejua mchango wako katika
ushindi wa chama chetu katika ngazi zote. Nyimbo zako ndiyo adhana au
kengele ya kuwakusanya waumini (wana CCM na wananchi) katika mikutano ya
chama. Komba ulikuwa nembo ya chama chetu.
Komba
umeondoka, lakini umeacha alama katika ulimwengu wa siasa hususan
katika chama chetu. Daima nitakukumbuka ndugu yangu, naamini kabisa yale
mapambano utayaendeleza huko ulikoenda ambako sote tutakuja.
Nakuahidi
ndugu yangu, kama tulivyokuwa pamoja katika matatizo na furaha zetu,
mimi na chama chetu tutaendeleza pale ulipoachia kutatua matatizo ya
familia.
Namuomba Mungu anipe nguvu na moyo wa kuyafanya hayo. Pumzika kwa amani rafiki yangu, ipo siku isiyo na jina tutaonana.
Hizi ndio sehemu 12 zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, Bonyeza Hapa chini== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO CHAFU YA AGNESS MASOGANGE== >