TAASISI
ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR),imesema vijana wenye
umri wa kuanzia miaka 30 na kuendelea, wanaongoza kwa kutumia dawa za
kuongeza nguvu za kiume.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana,Mkurugenzi wa
NIMR,Dk.Mwele Malecela alisema kwa sasa tatizo hilo ni kubwa ambalo
linawakumba vijana wengi hususan barani Afrika.
Alisema
hali hiyo,imesababisha vijana hao kutafuta dawa za kuongeza nguvu za
kiume aina ya Mundex,ili waweze kupunguza ukubwa wa tatizo hilo.
“Vijana
wengi wenye umri wa kuanzia miaka 30 na kuendelea wana matatizo ya
upungufu wa nguvu za kiume, jambo ambalo limewafanya kutafuta dawa za
kuongeza nguvu ili waweze kuzitumia na kupunguza ukubwa wa tatizo.
“Tangu
tugundue dawa hii, idadi kubwa ya wanaokuja kununua ni vijana hasa
wenye umri wa miaka 30,hali ambayo inaonesha wazi kuwa tatizo hili
linakua kwa kasi,”alisema Dk Mwele.
Alisema
kipindi kilichopita, matatizo hayo yalikuwa yanawapata wanaume wenye
umri wa kuanzia miaka 50 na kuendelea, lakini sasa hivi ni tofauti
kabisa ambapo vijana wenye umri huo ndiyo wenye matatizo hayo.
“Miaka
iliyopita tatizo hili lilionekana ni la watu wazima wenye umri wa
kuanzia miaka 50 na kuendelea,sasa hivi ni tofauti kabisa ambapo
matatizo hayo yameshamiri kwa vijana, jambo ambalo limewafanya kutafuta
dawa ndani na nje ya nchi ili waweze kujitibia,”alisema.
Alibainisha
kuwa taasisi hiyo kwa kushirikiana na tiba mbadala walifanya utafiti na
kubaini kuwa dawa ya Mundex inaweza kuwasaidia kupunguza ukubwa wa
tatizo.
Taasisi hiyo,pia imebaini idadi kubwa ya wanawake wakiwamo watoto, wana matatizo ya uvimbe tumboni(Fibrous) hasa kwa waafrika.
Alisema dawa hiyo imethibitishwa kisheria na kwamba inaweza kutumika mahali popote kwa sababu haina madhara kwa binadamu.
Alisema
kutokana na hali hiyo,wanaweza kuitafuta katika ofisi zao za kanda ili
waweze kuinunua na kuitumia, jambo ambalo linaweza kuwasaidia.
“Tulifanya utafiti na kubaini kuwa dawa ya Mundex ina uwezo wa kupunguza tatizo la upungufu wa ngufu za kiume.
“Kwa sababu imethibitishwa kisheria, kila mmoja mwenye matatizo anaweza kuitumia ili iweze kumsaidia,”alisema.
Alisema
kwa sasa inaonekana tatizo hilo ni kubwa ambalo linaongezeka siku hadi
siku, hali hiyo inaweza kuwaathiri wanaume wengine kupata matatizo hayo.
Alisema
kutokana na hali hiyo, wameiomba Serikali kuwaongezea fedha ili waweze
kufanya utafiti ambao utaweza kubaini chanzo cha tatizo hilo na tiba
zaidi inayowafaa ili kuwatibia wataopata matatizo.
Akizungumzia kuhusu uvimbe, Dk.Malecela alisema tatizo hilo ni kubwa linalowafanya wagonjwa kufanyiwa upasuaji.
“Sasa
hivi hadi watoto wanafanyiwa upasuaji kwa ajili ya uvimbe,hali ambayo
inaonyesha wazi kuwa tatizo hilo ni kubwa linahitaji nguvu ya
ziada,ikiwamo kufanya utafiti ili kupata ufumbuzi,”alisema.
Alisema
taasisi yake,ina watalaamu na wasomi wa kutosha ambao wanaweza kufanya
utafiti wa kiwango cha juu na cha kimataifa ambacho kinaweza kuwajengea
imani kwa jamii na watanzania kwa ujumla.
Alisema
mpaka sasa, wameweza kujenga uhusiano na vyuo vikuu mbalimbali ndani na
nje ya nchi ambavyo vimeweza kuwatuma wanafunzi kwenda kupata mafunzo
kwa njia ya vitendo.
Alisema
miongoni mwa tafiti ambazo ziliwafanya wafanikiwe ni pamoja na utafiti
wa majaribio ya chanjo ya ukimwi na malaria nchini.
Alisema
katika utafiti wa chanjo ya ugonjwa wa Ukimwi, taasisi hiyo ilishiriki
katika tathmini ya upatikanaji wa dawa za kupunguza makali ya na
majaribio ya tiba ya virusi vya HSV-2(Herpes Simplex Virus2) katika
kupunguza maambukizi ya Ukimwi.
“Pia tulifanikiwa kupata dawa ya usugu ya kurefusha maisha kwa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi(VVU).
“Tulifanikiwa kufanya uchunguzi wa vimelea vya Ukimwi katika maziwa ya mama anayenyonyesha,”alisema.
Alisema,
licha ya kufanya tafiti hizo wana changamoto mbalimbali zinazowakabili
ikiwa ni pamoja na ukosefu wa rasilimali fedha, hali ambayo inafanya
washindwe kufanya tafiti za mara kwa mara.
Alisema
mpaka sasa wana miundombinu mibovu pamoja na uhaba wa ofisi katika
kituo cha Hospitali ya Taifa Muhimbili(MNH) na Tanga ambapo wanatumia
majengo ya kupangisha ambayo gharama zake ni kubwa.
Alisema
mkakati uliopo ni kuhakikisha wanafanya tafiti mbalimbali zenye tija
ambazo zitaweza kuisaidia Serikali kutatua matatizo yaliyopo nchini.
Hizi ndio sehemu 12 zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, Bonyeza Hapa chini== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO CHAFU YA AGNESS MASOGANGE== >