Habari Kali
Loading...

Gwajima Aligeuka MFALME Baada ya Kuachiwa Kwa Dhamana Isiyo Na Masharti...Wafuasi Wake 15 Nao Waachiwa, Mwandishi Atiwa Mbaroni

Mbinu Za Kumfikisha Kileleni Mwanamke Mwenye Makalio Makubwa Kwa Haraka, Bonyeza Hapa chini== >

Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya TMJ, Dar es Salaam akiwa chini ya ulinzi wa polisi, ameachiwa huru kwa dhamana katika kituo cha Polisi cha Oysterbay baada  ya  kufikishwa  kituoni  hapo kwa kutumia baiskeli ya wagonjwa (wheelchair)  kuhojiwa kwa mara ya pili.
 
Askofu Gwajima, alipandishwa kwenye baiskeli hiyo, baada ya kupelekewa na mmoja wa wafuasi ambaye alikuwa amevalia mavazi ya kichungaji.
 
Wakati akipelekwa katika gari Askofu Gwajima, alionekana akigugumia kutokana na maumivu makali ambayo haikujulikana mara moja chanzo chake.
 
Baada ya wafuasi wake kukamilisha taratibu zote, ilipofika saa 6:15 mchana, gari la polisi aina ya Land Cruiser lenye namba za usajili KX 06 EFY liliwasili hospitalini hapo.
 
Gari hilo, lilikuwa na askari wanne, mmoja akiwa ni ofisa wa polisi aliyekuwa amevalia sare za askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na wengine wakiwa wamevalia kiraia.
 
Asakari hao ambao walikuwa wamebeba bunduki walikwenda moja kwa moja wodini na baadae kutoka pamoja na kiongozi huyo wa kiroho.
 
Baada ya muda kidogo, askari hao walishuka chini na ilipofika saa 06:34 chana, gari nyingine ndogo aina ya Yutong MG 6 Turbo yenye namba STL 110 iliwasili eneo hilo ikiwa na askari mmoja.
 
Ilipofika saa 6:45, Askofu Gwajima alishushwa katika lifti ya hospitali hiyo, akiwa anasindikizwa na zaidi ya watu wanne, huku yeye akiwa amekaa kwenye baiskeli hiyo na kupandishwa moja kwa moja kwenye gari la polisi.
 
Akiwa anainuliwa kwenye kiti na kupandishwa katika gari, Askofu Gwajima alionekana akikunja uso na kufungua mdomo kama mtu anayegugumia kutokana na maumivu makali.
 
Baada ya kutoka hospitalini, msafara huo ulielekea moja kwa moja Kituo cha Polisi cha Oysterbay.
 
Alifikishwa kituoni hapo saa 6:55 na kupelekwa chumba kilichokuwa kimeandikwa ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kinondoni.
 
Alipofika mlangoni alikutana na ofisa mmoja, ambaye jina lake halikutambuliwa mara moja, alimuaru asubiri ili wakili wake afanye taratibu za dhamana.
 
“Subiri hapa mfanye taratibu za dhamana mkishamaliza hakikisha Alhamisi (kesho) unaripoti Central Polisi (kituo kikuu cha polisi Dar es Salaam),”alisikika ofisa huyo akisema.
 
Wafuasi  Wakusanyika.
Wakati taratibu za dhamana zikiendelea, wafuasi wa Askofu Gwajima waliendelea kukusanyika eneo hilo kwa madai kuwa wanamsubiri kiongozi wao.
 
Wakiwa wamekusanyika makundi makundi, huku wengine wakiwa wameshikilia makaratasi yenye maandishi na picha ndogo kwa ajili ya kusaidia udhamini kama ukihitajika.
 
Ilipofika saa 8:00 mchana, gari aina ya Toyota Land Cruiser yenye namba za usajili T 631 AHD iliingia kituoni hapo na muda mfupi ikaondoka na Askofu Gwajima.
 
Baada ya kuonekana akiwa ndani ya gari hilo, wafuasi wake walianza kushangilia na kuimba “tumeshinda, tumeshinda tumeshinda…yesu, yesu, yesu…” huku wakiikimbilia gari kwa nyuma na ndipo gari hiyo ilisimama nje kidogo ya kituo hicho.
 
Gari hiyo, ilizingirwa na wafuasi wake huku waandishi wa habari nao wakitafuta upenyo wa kuzungumza ambapo askofu huyo alitamka maneno machache akisema. “viongozi wa dini wawe wa kweli na wasimamie ukweli na uwazi daima,” alisema Gwajima.
 
Baada ya kuondoka wafuasi wake walitembea kwa miguu kutoka Oysterbay hadi Kawe lilipo Kanisa la Ufufuo na Uzima, huku wakiimba nyimbo za kumsifu Mungu.
 
Naye mwanasheria wa Askofu Gwajima, John Mallya alisema mteja wake ameachiwa kwa dhamana isiyo na masharti.
 
“Mteja wangu, ameachiwa kwa dhamana isiyo na masharti na tumeamua akapumzike nyumbani kwa kuwa hali yake ya kiafya bado si nzuri,” alisema Mallya.
 
Awali kabla yakuchukuliwa na polisi hospitalini,daktari aliyekuwa akimtibu, Dk. Fortunatas Mazigo, alisema Askofu Gwajima asingeweza kuruhusiwa kutoka hospitalini jana kwa sababu hali yake haikuwa ya kuridhisha.
 
“Hatutarajii kumruhusu leo bado hayuko vizuri,endapo atahitajika kuripoti polisi tutampa kibali cha muda na atapaswa kurudi hospitalini kwa sababu hajaweza kutembea, labda kwa msaada wa watu ingawa anaendelea vizuri tofauti na ilivyokuwa juzi,” alisema Dk. Mazigo.
Mwandishi atiwa mbaroni
Jeshi hilo lilimkamata mwandishi wa Habari wa Kituo cha Televisheni ya Tumaini, Bw. Frank Godfrey, kinachomilikiwa na Kanisa Katoliki kwa kosa la kupiga picha.

Licha ya kuwaeleza polisi kuwa yeye ni mwandishi wa habari, askari waliendelea kumvuta ndani ya kituo hicho kwa nguvu jambo ambalo lilisababisha waandishi wengine kupiga kelele.

Kutokana na hali hiyo, baadhi ya waandishi waliingia ndani kufanya mazungumzo ya kutaka kuachiwa kwa mwenzao na  wengine waliendelea kupiga kelele ndipo polisi waliamua kumwachia na kutolewa amri kwa waandishi wote wa habari kuondoka eneo la kituo hicho na kukaa mbali.

Amri hiyo ilipingwa vikali na waandishi na kuwaeleza polisi umuhimu wa wao kuwepo eneo hilo.

"Nimesema ondokeni, kama mnasema kazi zenu ni muhimu, nasema ondokeni na mkakae mbali na hapa,"
alisema Kamanda mmoja wa polisi aliyekuwa na nyota tatu ambapo askari waliokuwa na silaha za moto, waliwafuata waandishi hao ili waondoke eneo hilo.

Kuachiwa watu 15 waliokamatwa
Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limewaachia watu 15 ambao wanatuhumiwa kutaka kumtorosha Askofu Gwajima.

Akizungumzia jambo hilo, Mchungaji wa Kanisa hilo Yekonia Bihagaza ambaye ni miongoni mwa waliokamatwa, alisema jeshi hilo lilianza kuwaachia watu 12 na jana wakaachiwa watatu  waliokuwa wamebaki kituoni.

"Hatujui Jeshi la Polisi lilitukamata kwa kosa gani, tunasubiri siku ya kupelekwa mahakamani," alisema.

Naye Mchungaji Frederick Fusi, alisema haki imeshinda uovu kwani sababu iliyowafanya wakamatwe ambapo wao ni watumishi wa Mungu ambao wanapambana katika ulimwengu wa roho na wanasubiri kupeleka mahakamni wakajue kosa lao.

Maskofu  Wakutana  na  IGP  Mangu.
Katika hatua nyingine, maaskofu na baadhi ya wachungaji wa makanisa ya Kipentekoste walioandamana na viongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, walifika Kituo Kikuu cha Polisi Kati kwa ajili ya kukutana na maofisa wa polisi ili kuzungumzia suala hilo.
 
Msafara wa viongozi hao, uliongozwa na Mchungaji Samwel Ndege wa Kanisa la Ufufuo na Uzima.
 
Kikao cha viongozi hao na maofisa wa polisi kilianza saa 4 asubuhi na kilidumu kwa zaidi ya saa moja, huku waumini wengine wakiendelea kusubiri nje. Hata hivyo, waumini hao walifukuzwa na polisi waliokuwa doria.
 
Maaskofu walipotoka nje ya kikao hicho, waliwaeleza waumini wao kwamba wanapaswa kwenda kuonana na Mkuu wa Jeshi hilo (IGP), Ernest Mangu.
 
Mchungaji Ndege, akiongozana na wenzake saba walifika makao makuu ya polisi saa 7 mchana.
 
Kikao chao na IGP Mangu kilikuwa cha ndani, huku waandishi wakizuiwa kuingia ndani.

Hizi ndio sehemu 12 zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, Bonyeza Hapa chini== >


Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO CHAFU YA AGNESS MASOGANGE== >

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Newer Posts Older Posts
© Copyright ZEE LA UDAKU | Designed By Code Nirvana
Back To Top