Siku tano baada ya Rais Jakaya Kikwete kusema kuwa tamko la Jukwaa la Wakristo (TCF) kuwataka waumini wao kupigia kura ya ‘hapana’ Katiba Inayopendekezwa lilikuwa la hasira, viongozi hao wamejitokeza tena na kusisitiza kwamba msimamo wao huo utabaki kama ulivyo.
Katika
tamko pamoja walilolitoa jana baada ya kukutana juzi mjini Dodoma,
viongozi hao wamemtahadharisha Rais Kikwete kuwa kuendelea kupigia debe
Katiba Inayopendekezwa na kuruhusu Mahakama ya Kadhi, kunaweza
kulitumbukiza Taifa katika machafuko na hali ikiwa hivyo Serikali ndiyo
itakayolaumiwa.
Tamko
hilo limesainiwa na viongozi walewale waliosaini lile la awali la Machi
12, mwaka huu ambao ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania
(CCT), Askofu Dk Alex Malasusa, Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu wa
Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa na
Mwenyekiti wa Kanisa la Pentekoste Tanzania (CPCT), Askofu Daniel Awet.
Tamko lao hili hapa:
Sisi,
Maaskofu kutoka TEC, CCT na CPCT tumekutana leo tarehe Machi 30, 2015
hapa Dodoma ili kuomba kwa pamoja juu ya mgawanyiko unaodhihirika wa
dini za Kikristo na Kiislamu kutokana na muswada wa Mahakama ya Kadhi.
Maaskofu
tuliokutana hapa hatuna hasira na wala hatuongozwi na hasira wala
mihemko katika kufikia maamuzi tunayofanya kama ambavyo wengine
wanavyotutafsiri.
Tunafikia
maamuzi yetu baada ya maombi na sala na tunasukumwa na upendo kwa
wananchi ili kujenga taifa lenye umoja, amani, utulivu na maelewano.
Pia
tumekuja kufuatilia kwa kina Muswada wa Marekebisho ya Sheria
Mbalimbali ya 2014 unaopendekeza, pamoja na mambo mengine, marekebisho
ya Sheria ya Tamko la Sheria za Kiislamu la mwaka 1964.
Muswada
huu unapendekeza kuanzishwa Mahakama ya Kadhi ambao utawasilishwa
Bungeni April 01, 2015 kwa hati ya dharura na hivyo kuufanya umma wa
Watanzania kutokujua maudhui yaliyomo katika muswada huo wakati bado
hoja zetu za msingi tulizopeleka kwenye Kamati ya Katiba na Sheria ya
Bunge na kwa Waziri Mkuu hazijajibiwa.
Tangu
tulipokutana Machi 10, 2015 ambako tulitoa tamko letu kuhusiana na
Mahakama ya Kadhi na Katiba Inayopendekezwa, tumekuwa tukiendelea
kutafakari juu ya yale tuliyokuwa tumesema katika matamko yetu
mbalimbali na jinsi amani na utulivu wa nchi yetu vinavyoendelea
kumomonyoka siku zinavyokwenda.
Kwanza
tumeshangazwa na tabia ya viongozi wa serikali ya kuitisha na kuendesha
mikutano wanayodai ni ya viongozi wa dini lakini isiyo rasmi. Machi 03,
2015 Waziri Mkuu aliitisha mkutano kupitia Mchungaji mmoja ambapo
hakuna hata kiongozi mmoja wa taasisi au Kanisa aliyeshiriki.
Jambo
la kushangaza ni kile kilichotokea Machi 28, 2015 ambapo Mhe. Rais
alishiriki kikao cha kikundi ambacho sio rasmi yaani Kamati ya Amani ya
Mkoa wa Dar es Salaam.
Tunasema
kamati hiyo siyo rasmi kwa sababu haina baraka za viongozi wa ngazi za
juu wa kidini wa Mkoa huo na haina mwongozo wa kazi zake.
Mikutano
ya jinsi hii kati ya serikali na wale ambao imewaona kuwa ndio viongozi
wa dini sio sahihi kwani viongozi wa dini wana taratibu zao za kualikwa
au kuwakilishwa katika mikutano na viongozi wa serikali au wa dini au
madhehebu mengine.
Tunawashauri
wanaohutubia na wanaoshiriki mikutano hii wajue kwamba washiriki hawana
uwezo wa kuamua au kukubaliana na jambo lolote kwa niaba ya viongozi
wao wa juu na pia viongozi husika wa serikali wasifurahi kwamba ujumbe
wao umewafikia viongozi wa dini kwani hao washiriki sio wawakilishi
rasmi na hawana uwezo wa kutoa maamuzi au kukubaliana juu ya jambo
fulani la kitaifa.
Pili, tumekuwa
tukifuatilia kwa karibu juu ya muswada wa Mahakama ya Kadhi na
tumebainisha dhahiri kwamba kile tulichokuwa tunasema kitatokea
kimeaanza kutokea bayana.
Yale
yaliyotokea kwenye semina kuhusu Mahakama ya Kadhi kwa Waheshimiwa
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Machi 29, 2015 ambao
ni wasomi, ni ishara ndogo sana ya kile kitakachotokea maeneo yote ya
nchi yetu. SERIKALI KWA NIA MOJA NA KWA SABABU TUSIZOZIJUA INAANZISHA VITA VYA KIDINI KATI YA WATANZANIA WAKRISTO NA WAISLAMU.
Tunashangazwa
kuona jinsi serikali inavyonuia jambo hili ovu litakaloleta balaa kwa
nchi yetu wakati huu wa kuelekea kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa
na baadaye Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Kutokana na mambo hayo makuu mawili hapo juu, sisi Maaskofu wa Jukwaa la Wakristo Tanzania tunatamka kama ifuatavyo :
1.Matamshi
ya Mhe. Rais akihutubia aliyowaita viongozi wa dini tarehe Machi 28,
2015 kuwa Mahakama ya Kadhi ni ya Waislamu wenyewe na serikali
haitajihusisha wala kugharamia yanakinzana na kile kinachoendelea
bungeni na nchini.
Hapa
tunajiuliza, endapo maneno ya Rais ni kweli, mbona Bunge linaendelea
kujadili kitu ambacho serikali haitajihusisha wala kukigharimia ? Kwa
mantiki hiyo, tunamtaka Mhe. Rais aagize muswada huu uondolewe Bungeni
na usijadiliwe tena kwa kuwa Utafiti wa Tume ya kurekebisha sheria
ulishaonyesha madhara ya uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi.
Vinginevyo, kuendelea kujadiliwa kwa muswada huu maana yake ni kwamba serikali inajihusisha na itagharimia mahakama hiyo.
2.Serikali
ijue kuwa endapo Wabunge wa dini za Kikristo na Kiislamu watapigana na
kisha baadaye wananchi nao wakafanya hivyo katika maeneo yao, SERIKALI ITAKUWA NDIYO CHANZO CHA MAPIGANO HAYO.
Kama
tulivyotamka hapo juu, kuhusiana na jambo hili tunamtaka Mhe. Rais
aiepushe nchi yetu na kuingizwa kwenye mapigano ya kidini ambayo
kuyadhibiti itakuwa vigumu sana (tafadhali rejea kinachoendelea huko
Nigeria).
Pia
tunamwomba Mhe. Rais akumbuke na kutafakari kile kilichotokea na
kinachotokea nchi ya Afrika ya Kati kati ya kundi la Seleka (Waislam) na
kundi la Anti Balaka (Wakristo).
3.Tunaamini
kuwa viongozi wa serikali wanafahamu viongozi rasmi wa dini na
madhehebu ya dini. Kwa mantiki hiyo tunawashauri viongozi wa serikali
waache kabisa kutumia vikundi visivyo rasmi kualika mikutano wanayodhani
kuwa itakubalika na waumini wa dini hizo. Mikutano yote ya jinsi hiyo
itakayoitishwa ni batili na maamuzi yake hatuyatambui na hatutayatambua.
4.Bado
Maaskofu tunasimamia Tamko letu la Machi 10, 2015 na tunawahimiza
Wakristo wajitokeze kwa wingi katika kujiandikisha katika Daftari la
Kudumu la wapiga Kura na zaidi wajitokeze kwenda kupiga kura ya HAPANA wakati wa kura ya maoni kwani Katiba inayopendekezwa ilifikia hapo kwa njia ya ubabe, ilikosa uadilifu na mbaya zaidi ni RUSHWA YA AHADI YA MAHAKAMA YA KADHI ya iliyotolewa na Waziri Mkuu kwa Waislamu wakati wa kupitisha Katiba Inayopendekezwa.
Tunafanya
hivyo kwa dhamiri safi kwa sababu ya imani yetu na kwamba sisi ni raia
wa nchi hii na tuna haki ya kueleza mawazo yetu bila woga kama Katiba ya
Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 inavyotupa haki.
5.Mwisho tunawaomba Wakristo wote waendelee kufunga na kuomba kwa ajili ya utulivu na amani ya nchi yetu.
Hizi ndio sehemu 12 zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, Bonyeza Hapa chini== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO CHAFU YA AGNESS MASOGANGE== >