Kuna tetesi kuwa kuna kundi la watoto zaidi ya mia, wengine wakiwa na
miaka mitatu tu,wamekutwa kwenye misikiti mbali mbali ya mji wa dodoma.
Wengi wakitokea mikoa mbalimbali ya Tanzania.
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini, ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi
na Usalama, Betty Mkwasa alisema jana kuwa aliyoyaona katika kituo
hicho hayakubaliki.
“Kwanza watoto wanalala wengi, hakuna hewa ya kutosha, wanajipikia
wenyewe chakula na hawana uangalizi wa watu wazima,” alisema Mkwasa.
Alisema serikali haikatai dini yoyote kufundishwa kwa watoto bali
taratibu, kanuni, sheria pamoja na haki za mtoto lazima zifuatwe.
“Siwezi kujua walikuwa wanafundishwa nini lakini baada ya upembuzi
yakinifu utakaofanywa na wataalam ambao nimekuja nao, tutaweza
kuzungumza kama walifuata kanuni na utaratibu,” alisema.
Mwananchi ilipofika katika moja ya kituo hicho, jana asubuhi lilikuta
watoto hao wakicheza kwenye eneo hilo lililokuwa chini ya ulinzi wa
polisi waliokuwa na silaha za moto.
Watoto wengi walikuwa hawajavaa viatu na baadhi yao walisema kuwa viatu walivyokuja navyo kutoka makwao vimeshakwisha.
Bakwata
Sheikh mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Shaaban Rajabu alisema
wanakitambua kituo hicho kama ilivyo kwa vituo vingine vinavyofundisha
dini ya Kiislamu.
Sheikh huyo alipinga suala la watoto kukosa elimu, akisema wazazi wao wamehiyari vijana wao kusoma dini tu.
“Naomba ifahamike kuwa, wapo wazazi ambao wanapenda watoto wao wasome
dini tu na hata mimi nilisoma hivyo kabla ya kwenda nje kwa masomo zaidi
na kurudi,” alisema.
Alipinga suala la kusajiliwa kwa kituo akisema viko vituo vingi
havijasajiliwa hata katika dini nyingine, lakini havisumbuliwi na
kushangazwa kuona utaratibu wao unakuwa na shida.
Kwa upande mwingine alishauri Bunge kutunga sheria kali kwa ajili ya
kuvilazimisha vituo vyote kuwa na usajili ili viweze kufuatiliwa
kulingana na matakwa ya serikali.
Kwa upande wake, katibu wa Bakwata mkoani hapa, Hassan Kuzungu,
aliyeongozana na kamati hiyo, alieleza kusikitishwa na kitendo cha
mazingira waliyokuwapo watoto hao.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Nkhungu, Kasian Mponela alisema kuwa amekuwa akiwaona watoto hao, lakini hajui wanachojifunza hapo.
Alisema suala la kuangalia kama wanajifunza dini au mambo mengine sio
jukumu lake, kwani yeye anajua kila mtu anapanga mwenyewe matumizi ya
nyumba yake.
Hizi ndio sehemu 12 zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, Bonyeza Hapa chini== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO CHAFU YA AGNESS MASOGANGE== >