Kiongozi wa waasi wa ADF, Jamil Mukulu (menye shati jeupe).
Waasi wa Allied Democratic Forces (ADF).
Raia wakikimbia mapigano dhidi ya ADF.
JEESHI la polisi nchini limefanikiwa kumtia mbaroni kiongozi wa kundi
la waasi wa Allied Democratic Forces (ADF) wa nchini Uganda, Jamil
Mukulu, ambaye amekamatiwa nchini Tanzania.
Mukulu aliyekuwa akiongoza waasi hao katika mauaji wa halaiki katika
nchi za Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) tangu miaka ya
1990, alikamatwa nchini Tanzania mwanzoni mwa mwezi huu akitokea
mashariki mwa DRC.
Vyombo vya habari nchini Uganda vimethibitisha kutiwa mbaroni mtu huyo
ambaye kundi lake linatuhumiwa kufanya mauaji ya watu 300 tangu mwezi
Oktoba mwaka jana hadi sasa huko DRC.
Mukulu ametiwa mbaroni kwa ushirikiano wa polisi wa Tanzania na wenzao
wa Uganda. Hata hivyo, jeshi la Uganda limesema kuwa haliwezi
kuthibitisha kuwa mtu aliyetiwa mbaroni ni Jamil Mukulu hadi
atakapofikishwa nchini humo na kuchukuliwa vipimo vya vinasaba vya DNA.
Kwa muda mrefu polisi ya Uganda ilikuwa imetoa amri ya kutiwa mbaroni
kiongozi huyo wa waasi wa ADF mwenye umri wa miaka 51 kwa tuhuma za
kufanya mauaji ya kigaidi na kuiomba Interpol iisaidie kumkamata.
Mukulu aliyekuwa muumin wa kanisa Katoliki kabla ya kuhamia Uislam,
alianzisha kundi hilo la ADF mnamo miaka ya 1990, kwa ajili ya kupingana
na serikali ya Uganda.
Tangu hapo amekuwa akiongoza waasi katika mapigano ambayo yamepoteza
maisha ya maelfu ya raia wa Uganda na DRC. Mukulu anakabiliwa na makosa
ya ugaidi na uhaini.
Taarifa ya Umoja wa Mataifa inasema mwaka 1998, waasi wa ADF walifanya
mauaji ya kinyama ya wanafunzi 80 walipokivamia chuo kimoja magharibi
mwa Uganda.
Mwezi Novemba mwaka jana waasi hao waliwaua watu zaidi ya 100 ikiwa ni mwendelezo wa mashambulizi ya kutisha Mashariki mwa DRC.
CHANZO: BBC SWAHILI
Hizi ndio sehemu 12 zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, Bonyeza Hapa chini== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO CHAFU YA AGNESS MASOGANGE== >