Stori: Haruni Sanchawa na Makongoro Oging’
Mvua kubwa iliyonyesha ambayo haijawahi kunyesha ndani ya Jiji la Dar es Salaam kwa kipindi cha miaka kumi, imeacha vilio na umaskini mkubwa kwa wakazi wake, imebainika.
Timu ya Uwazi kipindi chote cha mvua ilikuwa mitaani na kubaini kuwa
hadi juzi watu zaidi ya kumi walipoteza maisha kutokana na mvua hiyo na
baadhi ya miili iliyopatikana haijatambulika na ndugu zao na
waliotambuliwa wameshazikwa na kuacha vilio.Mvua kubwa iliyonyesha ambayo haijawahi kunyesha ndani ya Jiji la Dar es Salaam kwa kipindi cha miaka kumi, imeacha vilio na umaskini mkubwa kwa wakazi wake, imebainika.
Aidha, waandishi wetu walishuhudia jeshi la polisi likitoa maiti moja katika Mto Msimbazi uliyoko Magomeni jijini Dar es Salaam, hata hivyo haikuweza kutambuliwa hivyo kuaminika kuwa ilisombwa na maji kutoka mbali.Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Kipolisi ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova aliliambia Uwazi kuwa maiti kadhaa zilikuwa zimehifadhiwa Hospitali ya Muhimbili na ndugu walikuwa hawafahamiki na kuwataka waliopotelewa na ndugu zao kwenda kuzitambua.
Waandishi wetu katika mitaa mbalimbali jijini Dar es Salaam, walibaini athari kubwa za maji yaliyoingia katika majumba ya watu hasa maeneo ya Jangwani, Kigogo, Kinondoni na wakazi wake kuachwa wakiwa hawana makazi ya kuishi, hivyo familia kusambaratika.
Maeneo ya Jangwani ilionekana kama kisiwa kwani nyumba nyingi zilizingirwa na maji na kuhamwa na wakazi wake, huku wengine wakilalamika kuwa wamepoteza mali zao ambazo zimesombwa na maji na mbwa wa polisi walitumika kusaka maiti.
Neema Laulence mkazi wa Magomeni Makuti, alisema kuwa kutokana na mvua hiyo, watu wamekosa makazi baada ya nyumba zao kujaa maji, hata hivyo alisema serikali haipaswi kulaumiwa kwa sababu viongozi wa mkoa wamejitahidi sana kuelimisha wanaoishi mabondeni ili wahame lakini wamekuwa wabishi.
Abdallah Hamis alisema: “Mvua hii ni kubwa na haijawahi kutokea na walioathirika wajilaumu wenyewe maana serikali ilishatoa viwanja Mabwepande lakini baadhi yao waliviuza na kurudi mabondeni.”Naye Mwanaisha Hamisi maarufu kwa jina la mama Kabang, alisema serikali itumie nguvu kuwahamisha watu wanaokaa mabondeni kwa sababu wanapofariki taifa linapata aibu.
“Ni aibu serikali kushindwa kuwadhibiti watu wanaong’ang’ania kuishi mabondeni. Iwahamishe kwa nguvu,” alisema Mwanaisha.Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Dk. Agnes Kijazi akizungumzia hali ya mvua nchini alisema: “Maeneo ambayo hali ya mvua inaweza kuyaathiri zaidi na kukumbwa na vimbunga ni pamoja na kanda ya kati, nyanda za juu kusini magharibi, magharibi mwa nchi na maeneo ya ukanda wa Pwani hivyo wananchi wachukue tahadhari.”
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik alisema anasikitishwa na kitendo cha baadhi ya watu kuilaumu serikali wakati miaka mingi imekuwa ikiwahimiza wanaoishi mabondeni kuhama.
“Ukweli ni kwamba safari hii hatuwapi hifadhi kwa sababu wamekuwa jeuri na pia baadhi yao wameishitaki serikali mahakamani, sasa tufanye nini?” alihoji.
Hizi ndio sehemu 12 zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, Bonyeza Hapa chini== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO CHAFU YA AGNESS MASOGANGE== >