Wakati hofu juu ya usalama wa watoto katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam ikizidi kutanda miongoni mwa wazazi na walezi, Polisi imekanusha kuwapo kwa matukio ya utekaji nyara watoto wanaosoma shule za msingi na kufanyiwa unyama ukiwamo ulawiti, kuuawa na hata kuchunwa ngozi.
Kwa
wiki kadhaa sasa, hofu juu ya matukio ya aina hiyo yalichangiwa kwa
kiasi kikubwa na taarifa za mitandao ya kijamii, ikielezea jinsi watoto
wanavyotekwa.
Kamanda
wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova akizungumza
jana, alisema hivi karibuni umezuka uvumi kutoka kwa watu mbalimbali
kwamba lipo kundi la wahalifu wanaotumia gari aina ya Toyota Noah yenye
rangi nyeusi kutenda uhalifu dhidi ya watoto.
Alisema
Polisi imefanya uchunguzi na mpaka sasa hawana taarifa yoyote ya mtoto
kutekwa au kufanyiwa madhara yoyote kwa mtindo wa utekaji nyara. Kwa
mujibu wa kamanda, polisi inamshikilia mtu mmoja kwa kuhusika kusambaza
uvumi huo.
“Polisi
imegundua kwamba huu ni uvumi ambao haujulikani chanzo chake hivyo
nawaomba wananchi kuachana na uvumi huo na kupuuza kwani unaleta hofu
katika jamii bila sababu za msingi na kuleta usumbufu kwa baadhi ya
watu,” alisema.
Alisema
Oktoba 3 mwaka huu saa 3.00 asubuhi, Vingunguti, mfanyakazi wa The
Guardian Ltd, Prosper Makame (34) akiwa na mkewe MaryStella Munis (30)
mfanyabiashara wa vyombo vya nyumbani walifika eneo la shule ya msingi
Kombo kwa ajili ya kuchukua fedha za vyombo wakiwa na gari aina ya Noah
yenye namba T 252 DAY rangi nyeusi na kuvamiwa na wananchi.
“Wakati
watu hao wakisubiri kuchukua fedha, ghafla walikuja zaidi ya wananchi
100 na kuzingira gari hilo huku wakipiga kelele wakidai kwamba ndilo
gari linaloteka wanafunzi. Lakini polisi walipata taarifa hizo mapema na
kufika eneo la tukio na kuwaokoa watu hao pamoja na gari lao,” alisema.
Kova
alisema Oktoba 13 saa 10.00 katika Kituo cha Polisi Tabata katika
Manispaa ya Ilala, uliibuka uvumi kuwa gari namba T 548 BUN aina ya Noah
nyeusi ambayo ni mali ya askari polisi wa kikosi cha Usalama
Barabarani, Inspekta Esther lililokuwa kituoni hapo, ndani yake kulikuwa
na vichwa vitano vya watoto wa shule ya msingi Mtambani.
“Kutokana
na uvumi huo wananchi walikusanyika kituoni hapo ili kushuhudia na
kuona hivyo vichwa vitano, ndipo mkuu wa kituo hicho alipoamuru gari
hilo kufunguliwa na kuwathibitishia wananchi kuwa habari hizo ni za
uongo na uvumi,” alisema.
Alisema
hali hiyo ya uvumi ni ya hatari kwa sababu wananchi kila wanapoona Noah
nyeusi wanaikimbilia na kuizingira kwa lengo la kufanya fujo.
“Polisi
tunasisitiza kuwa uvumi huu wa kuwepo kwa kikundi cha wahalifu ambao
wamekuwa wakiwateka watoto na wanafunzi siyo kweli hata kidogo na hivyo
wananchi wanatakiwa kuepukana na taarifa hizo ambazo zinaweza
kusababisha uvunjifu wa amani,” alisema.
Alisema
uchunguzi wa kubaini nani alieneza uvumi huo ulifanyika na kubaini kuwa
umeenezwa na Gilbert Stanley (32), mkazi wa Tabata ambaye alikamatwa.
Alipohojiwa, kwa mujibu wa kamanda, alikiri kueneza habari hizo na kudai aliambiwa na mtu mwingine ambaye alidai hamkumbuki.
Hizi ndio sehemu 12 zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, Bonyeza Hapa chini== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO CHAFU YA AGNESS MASOGANGE== >