Idadi ya watu waliokufa kutokana na ajali ya moto wa lori lililopinduka na kisha kulipuka baada ya watu kulivamia kwa lengo la kujipatia mafuta, imeongezeka na kufikia watano kutoka vitatu vya awali.
Hayo yamethibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova.
Alisema
katika ajali hiyo iliyotokea juzi usiku eneo la Mbagala, watu 16
walijeruhiwa baada ya kuungua maeneo mbalimbali ya miili yao.
Ajali
hiyo ilihusisha lori aina ya Scania lenye namba za usajili T 347 BXG
mali ya Moil Transporter lililokuwa likitarajiwa kusafirisha mafuta
kuelekea Kampala, Uganda likiwa na kemikali aina ya petroli lita 38,000
inayokadiriwa kuwa na thamani ya dola 36,000 (Sh milioni 60).
Aliwataja
waliokufa kuwa ni Hassan Mohammed (25), mkazi wa Mbagala Kimbangulile,
Masoud Masoud (33), Mohammed Ismail (19), Ramadhani Khalfan (36) na
Maulid Rajabu, wakazi wa Mbagala Charambe.
Majeruhi
waliotambuliwa ni Hamis Ally (35), mkazi wa Mbagala Kiburugwa, Rajabu
Selemani (28), mkazi wa Tandika, Idd Said (28), Janney Mathayo (25),
mkazi wa Mbagala Kizuiani, Mathayo Daniel (21), mkazi wa Mbagala
Charambe na askari polisi, Koplo Thomas aliyejeruhiwa na jiwe kwenye
paji la uso wakati akijaribu kuzuia vibaka kuchota mafuta kabla ya
kulipuka.
Alisema
majeruhi wengine 10 wamelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili na
Hospitali ya Wilaya ya Temeke wakiendelea na matibabu na wengi wao hali
zao siyo za kuridhisha.
Kamanda
Kova aliongeza kuwa, mbali ya kusababisha vifo na majeruhi, ajali hiyo
pia ilisababisha kuungua kwa nyumba ya kulala wageni iitwayo United
yenye vyumba 32, mali ya Deus Kasigwa (42), mkazi wa Mtoni Mtongani.
Moto huo uliteketeza pia maduka matano yenye vitu vyenye thamani ya Sh
milioni 197 na pipikipiki saba ziliteketea kabisa na moto.
Naye
Ofisa Uhusiano wa Hospitali ya taifa ya Muhimbili, Doris Ishenda
alisema majeruhi 11 wanaoendelea kutibiwa hospitalini hapo, huku
akiongeza kuwa, hali zao sio nzuri kwa kuwa waliunguzwa vibaya na moto
na kwamba madaktari wanaendelea kuwapatia matibabu.
‘’Majeruhi
wote wamelazwa katika wadi namba 22 ya Sewa Haji wanaendelea na
matibabu, lakini hali zao sio nzuri kabisa kwani waliungua sana,’’
alisema Ishenda.
Wakati
huo huo, Paulo Milanzi (35), mkazi wa Chanika katika manispaa ya Ilala
anayetuhumiwa kushiriki katika mauaji ya Ofisa Usalama wa Taifa,
Sylvanus Mzeru, amefariki dunia baada ya kupigwa risasi katika
majibizano na polisi.
Kova
alisema mtuhumiwa huyo alikuwa akitafutwa na polisi kwa muda mrefu
kuhusu matukio mbalimbali ya mauaji na unyang’anyi wa kutumia silaha
jijini Dar es Salaam na mikoa ya jirani.
via: mpekuzi
Hizi ndio sehemu 12 zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, Bonyeza Hapa chini== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO CHAFU YA AGNESS MASOGANGE== >