Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametaja hatua saba ambazo Serikali yake imeanza kuzichukua ama inakusudia kuzichukua ili kukabiliana na msongamano wa magari katika Jiji la Dar Es Salaam.
Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa msongamano wa magari ni ishara ya
ubora wa maisha ya wananchi na ustawi wa Watanzania kwa sababu miaka 20
ama hata 10 iliyopita, Jiji la Dar Es Salaam halikuwa na msongamano.
Hata hivyo, Rais Kikwete ameonya kuwa, kama ilivyo katika miji yote
mikubwa duniani, ni jambo lisilowezekana kumaliza tatizo la msongamano
wa magari katikati ya Jiji la Dar Es Sslaam (Central Business District),
hasa kwa kutilia maanani kuwa hakuna shaka kuwa watu wataendelea
kununua magari na huwezi kuvunja nyumba zote katikati ya Jiji ili
kupanua barabara.
Rais Kikwete ameyasema hayo , wakati akizindua rasmi Barabara kisasa
ya Mwenge -Tegeta kwenye Barabara ya New Bagamoyo Road.
Amezitaja hatua hizo za kukabiliana na msongamano wa magari katika Mji wa Dar Es Salaam kuwa ni pamoja na ujenzi wa njia ya Mabasi Yaendayo Kasi (DART), ambao awamu yake ya kwanza inakaribia kukamilika pamoja na uanzishwaji wa huduma za kisasa za usafiri wa treni katika maeneo mbali mbali ya jiji hilo.
Amezitaja hatua hizo za kukabiliana na msongamano wa magari katika Mji wa Dar Es Salaam kuwa ni pamoja na ujenzi wa njia ya Mabasi Yaendayo Kasi (DART), ambao awamu yake ya kwanza inakaribia kukamilika pamoja na uanzishwaji wa huduma za kisasa za usafiri wa treni katika maeneo mbali mbali ya jiji hilo.
Hatua ya tatu ambayo Rais Kikwete ameitaja ni kujengwa kwa barabara za juu kwa juu (flyovers) katika maeneo ya TAZARA na Ubungo, yenye msongamano wa watu wengi, na ujenzi wa barabara 12 za kuzunguka Jiji (Ring Roads)
na nyingine za kuunganisha maeneo ya jiji hilo kama vile upanuzi wa
Barabara ya Uhuru kuwa njia mbili kila upande badala ya njia moja ya
sasa.
Aidha, Rais Kikwete amezitaja hatua nyingine kuwa ni ujenzi wa Daraja
jipya la Salender ambalo litapitia baharini, usafiri wa kivuko kipya
kutoka Bagamoyo hadi Dar Es Salaam na ujenzi wa miji midogo ya kisasa
inayojitegemea katika maeneo ya Kigamboni, Mabwepande na Luguruni.
Rais Kikwete amesema kuwa baadhi ya hatua hizo zinazochukuliwa ama
zinalengwa kuchukuliwa na Serikali zimekuwa zinakabiliwa na siasa nyingi
za kupinga miradi hiyo kutoka kwa baadhi ya viongozi na wanasiasa
nchini ambao amewaita “watu wenye upeo mfupi”.
Akizungumza wakati wa akizindua rasmi Barabara ya Kisasa ya
Mwenge-Tegeta ambayo ni sehemu ya Barabara ya New Bagamoyo Road, mjini
Dar Es Salaam iliyo na urefu wa kilomita 12.9 imegharimu kiasi cha Sh.
bilioni 77.85, fedha ambazo zimetolewa na Serikali ya Japan kupitia
Shirika lake la Maendeleo ya Kimataifa la JICA. Serikali ya Tanzania
imechangia asilimia 7.64 katika gharama za ujenzi wa Barabara hiyo.
Rais Kikwete amefanya uzinduzi huo katika eneo la Makutano ya Kambi
ya Jeshi ya Lugalo na Barabara ya Kawe katika sherehe iliyoshuhudiwa na
mamia ya wananchi. Alikuwa ni Rais Kikwete ambaye aliweke jiwe la msingi
la ujenzi wa Barabara hiyo Aprili 4, mwaka 2011.
Barabara hiyo ni awamu ya kwanza ya ujenzi wa Barabara itokayo
Makutano ya Barabara ya Kawawa, Kinondoni hadi Tegeta. Ujenzi wa awamu
ya pili wa kilomita 4.3 kati ya Mwenge na Makutano ya Barabara ya
Kawawa, unatarajiwa kuanza wakati wowote baada ya mipango yote ya ujenzi
huo kukamilika.
Barabara hiyo ya Mwenge-Tegeta inalenga kupunguza msongamano wa
magari katika eneo la kaskazini mwa Dar Es Salaam na pia ni sehemu ya
bararaba kuu inayounganisha Jiji la Dar Es Salaam na Mkoa wa Pwani,
kupitia Wilaya ya Bagamoyo, na kuunganisha mikoa hiyo na mikoa ya
kaskazini mwa Tanzania.
Akizungumza kwenye sherehe hiyo ya uzinduzi wa Barabara hiyo
iliyojengwa na Kampuni ya Konoike kutoka pia Japan, Balozi wa Japan
katika Tanzania, Mheshimiwa Masaki Okada amesema kuwa ujenzi wa barabara
hiyo ulichelewa kukamilika mwaka jana, kama ilivyopangwa, kwa sababu ya
wajenzi kukabiliwa na matatizo ya mafuriko makubwa yaliyotokea mwaka
2011.
Mbali na kutaja misaada mingi katika sekta ya miundombinu na hasa
barabara ambayo imefadhiliwa na Japan katika miaka mingi iliyopita,
Mheshimiwa Okada amesema kuwa Japan sasa iko tayari kuanza ujenzi wa
Barabara ya Gerezani-Bendera Tatu, Dar Es Salaam, utakaogharimu Sh.
bilioni 18.5, msaada kutoka Japan.
Aidha, Balozi huyo amewaomba radhi Watanzania kutokana na ucheleweshaji wa kuanza kwa ujenzi wa barabara ya juu kwa juu –flyover-
katika eneo la TAZARA, Dar Es Salaam, ambao utagharimu Sh. bilioni 53
ambazo zinatolewa na Serikali ya Japan kupitia Shirika la Maendeleo ya
Kimataifa la JICA.
Amesema kuwa ujenzi huo umechelewa kwa sababu makandarasi wa Kijapan ambao walitakiwa kujenga flyover hiyo wanakabiliwa na kazi nyingi huko nyumbani za kujenga upya miundombinu iliyoharibiwa na tetemeko na kimbunga cha Great East Japan Earthquake and Tsunami, kilichotokea Machi 2011 na kusababisha uharibifu mkubwa mno.
Aidha, amesema kuwa wajenzi hao pia wanalazimika kufanya kazi usiku
na mchana ili kukamilisha miundombinu ya kuiwezesha Japan kuandaa
Michezo ya Olimpiki ambayo imepangwa kufanyika nchini humo mwaka 2020
Hizi ndio sehemu 12 zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, Bonyeza Hapa chini== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO CHAFU YA AGNESS MASOGANGE== >