Dustan Shekidele, Morogoro LA haula! Mwanamke aliyefahamika kwa jina moja la Asha, mkazi wa Mtaa wa Area Six, Kata ya Kichangani mkoani hapa ambaye alikuwa kwenye swaumu ya Mfungo wa Ramadhani, amejikuta akilazimika kutengua swaumu na kumpa kichapo mwanaume aliyeiba futari na kiti chake cha plastiki alichokuwa amekalia nje ya nyumba akipika futari hiyo.
TUKIO KAMILI
Tukio hilo la aina yake, lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo wakati paparazi wetu anawasili kwenye eneo la tukio, alikuta kasheshe bin tafrani ikiendelea. Mbali na mwanamke huyo, wananchi wenye ghadhabu nao walikuwa wakimshikisha adabu mwanaume huyo huku wakidai ni mwizi.
MAELEZO YA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo, awali mwanamke huyo alikuwa nje ya nyumba yake akipika futari huku akiwa amekalia kiti hicho.
Akiomba kuachiwa baada ya kupewa kichapo kikali.
“Ghafla si akapata udhuru uliomlazimu aingie ndani. Akaacha futari
ikitokota jikoni. Amefanya yake kule ndani, akakumbuka ameacha futari
jikoni, akatoka.“Kufika! Kwanza akaona futari imepungua. Sasa ile
anataka kukaa, kiti nacho hakipo. Akashangaa.”ATAFUTA KITI, AMWONA NACHO MTU
Chanzo kiliendelea kudai kuwa, mwanamke huyo alianza kukisaka kiti chake sehemu mbalimbali nyumbani hapo lakini bila mafanikio. Alipotupa macho mbali na nyumbani, akamwona nacho huyu mwanaume amekibeba akitambaa zake.
“Ndipo mama bila kujali swaumu, akaingia ndani. Akachukua kirungu na sime na kumfukuza mpaka akamkamata na kuanzia kumwangushia kipondo huku jamaa akikitupa kile kiti kichakani kwa lengo la kupoteza ushahidi,” kilisema chanzo hicho.
WANANCHI WAINGILIA KATI
Baadhi ya wananchi wanaoaminika kuwa na hasira kali nao waliamua ‘kununua’ kesi hiyo ambapo na wao walichukua silaha mbalimbali, yakiwemo mawe na kuanza kumbonda mwanaume huyo mpaka damu chapachapa.
Anayedaiwa kuibiwa futari akimpiga kwa hasira.
BODABODA NUSURA WAMTOE UHAI, WAMVUNJA MGUUBaadhi ya madereva wa bodaboda walipomwona mwanaume huyo anazidi kuchakaa uso kwa kipigo, badala ya kumwokoa, waliingilia kati na kutaka kumchoma moto lakini wasamaria wema walipinga kitendo hicho na kumuokoa kwa kumkimbizia kwenye Kituo cha Polisi cha Nanenane kilicho jirani na eneo la tukio.
Hata hivyo, wakati akikimbizwa polisi, bodaboda hao waliamua kumgonga na pikipiki kwa makusudi na mmoja wao alifanikiwa kumvunja mguu.
MAMA MWENYE FUTARI
Alichonifanyia siyo haki kabisa, kama alikuwa na njaa, angeniambia, ningempakulia futari akala kuliko kuniibia.