Habari Kali
Loading...

PICHA ZA SHOO KALI YA DIAMOND ALIYOFANYA ZANZIBAR! NI BALAAA...!!

Diamond and his female dancer


wcb female dancer

the best show
diamond and his fans

Wcb dances on stage

SABABU YA KWANINI MZIKI WA BONGO FLAVA NI MAARUFU KENYA KULIKO MZIKO WAO HIZI HAPA

 
As argued by pundits, Bongo Flava carries with it realistic overtures that identify with the common man’s struggles

Amidst the cacophony of city noise inside Mtwapa-bound matatu in Mombasa, or anywhere across Kenya, it is most likely that the music you will be blaring from the speakers is Bongo Flava.

Raga dance hall, despite being popular in Kenya, appeals slightly less than Bongo Flava, but stands slightly higher than indigenous music to Kenyan ears.
Artistes such as Diamond Platinumz, Lady Jay Dee, TID, Ali Kiba, Prof Jay, Ommy Dimpoz, TMK Wanaume and many others are household names in Kenya especially in Mombasa.
And even as the winds of fortune currently don’t seem to favour classic taarab, the modern taarab played by the likes of Mzee Yusuf, Hadija Kopa and co is quite at home in the coastal region, too.
In most Christian households, Rose Mhando, Christina Shusho, Boniface Mwaitege and the late Zedekiah form top shelf collections ever.
This is not to mention on the call back tunes on almost every cell phone in the country where Rose Mhando is among the leading .
Back in the days before Saida Karoli, Ray C and Mr Nice went into oblivion, they commanded great audiences and adoration on the Kenyan music scene.
These artistes simply awed Kenyan fans to the extent that bordered on madness.
Indeed, whenever they landed at JKIA, they received a reception befitting presidential welcome – complete with a red carpet and bouquets. 
Collectively, Bongo Flava’s popularity is not in the entrepreneurial side of music, but her aesthetic and artistic aptitude that has, like a bug caught East and Central Africa off guard.
Just take a look at a YouTube posting of Diamond’s performance in Eastern Congo or his concert at the KICC, Nairobi and perhaps you will understand what I am talking about.
It is at this point that we begin to seek answers so this particular question. Why are these lads and lasses such a big hit all over?
As argued by most pundits, Bongo Flava carries realistic overtures while the music by contemporary Kenyan musicians does not identify with the people, their problems, joy of realistic love – it is just far-fetched in nature.
Artistes such as Eric Wainaina and Kato Change are too alien to the local music industry to the extent that their main performances are outside Kenya.
Some who identify with the young generation like Prezzo are far too flamboyant for most people’s liking.
The attempted cloning of American hip hop done in Kiswahili has to a large extent ended up in a mere fiasco. In fact, not many take them seriously.
Though they may appeal to a certain section of the youth the standards that they exhibit does not catch the ear of mature listeners and apparently, the music is very abstract.
While watching EA Mseto by Mzazi Willy Tuva, on Citizen TV the other day, it was visible that the Tanzanian brand had a larger share than Kenyan content.
Artistes such as Diamond and Lady Jay Dee top the list of artistes with their realism and creativity.
Lady Jay Dee’s singles ‘Joto Hasira’ and ‘Yahaya’ off her ‘Nothing but the Truth’ album are a manifestation of creativity as she tries to address the social ills that surround her community.
Listening to Diamond who only burst on the scene four years ago one cannot help but admire the artiste; his stuff has a lot of pep and strikes as a very creative and hardworking youth.
It is therefore, not surprising that even in the 70s when Simba Wanyika and Les Wanyika dominated the airwaves in Kenya; it was a group that was made of mainly Tanzanians who had crossed over.
Economic hardships of that time had made it difficult for them to do their music back at home but that didn’t stop them from being a hit.
This artistic knack perhaps is the reason why best cartoonists, artists and musicians are mostly of Tanzanian origin.
It is accurate to note that on average Tanzanians are better at putting pen to paper and coming up with lyrics that appeal to the masses sung in soothing vocals.
Though it is worthwhile to admit that on the marketing front Kenyans seem to be making more money, this does not necessarily mean they are making better music.
In this regard, Uganda and Tanzania trounce Kenya. Kenyan artistes do not understand their audience and the economics behind marketing to them.
~Citizen

BREAKING NEWS: MSANII MWINGINE AFARIKI DUNIA...NI WA BONGO FLEVA

side boy
Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kuwa msanii chipukizi kwenye muziki wa Bongo fleva Side Boy Amefariki dunia.
Akizungumza na Lindiyetu.com mdogo wa marehemu Ally khamisi amesema yakua kaka yao marehemu Said Salum Hemed amefia Mkoani Lindi katika hospitali ya Nyangao, alikuwa anasumbuliwa na TB YA MIFUPA.
Marehemu aliimba nyimbo ya Hujafa Hujaumbika ambayo alimshirikisha BestNaso.

FIESTA YAWAPAGAWISHA WAKAZI WA SONGEA

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Recho akifanya makamuzi kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta usiku wa kuamkia leo katika Uwanja wa majimaji, Songea.
Recho akiwajibika yake jukwaani.
Mashabiki waliojitokeza katika Tamasha la Serengeti Fiesta 2014 Songea.
Msanii wa Bongo Fleva, Linah Sanga akiwa amekumbatiwa na shabiki wake.
Msanii wa Bongo Fleva, Linah Sanga akicheza na mmoja ya shabiki wake Ole Themba.
Mashabiki wakiendelea kupagawa na burudani.
Msanii wa Bongo Fleva, Mo music akitoa burudani kwa wakazi wa Songea.

UNAAMBIWA HIZI NDO NYIMBO 10 KALI ZAID NA ZENYE UJUMBE ZILIZOWAHI KUHIT TANGU BONGOFLAVA IANZE MWAKA 2000

http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2012/10/527577_279570612160791_1859187862_n.jpg

Muziki wa bongofleva umefanya mapinduzi sana kuanzia mwanzoni mwa miaka 2000 mpaka sasa, zifuatazo ndizo nyimbo bora za bongofleva zenye ujumbe ambazo hupaswi kuacha kuzisikiliza...

1. Dunia Njia, 
hii nyimbo iliimbwa na Bushoke ni moja ya nyimbo zenye ujumbe mzito kabisa , ukiiskiliza anaelezea maisha kwa ujumla, maisha baada ya kifo na matabaka yaliyomo katika jamii,..hupaswi kuacha kuisikiliza hii nyimbo itakufunza mambo mengi

2 Kazi Yake Mola, 
hii nyimbo imeimbwa na madee akishirikiana na mandojo na domokaya, kazi yake mola ni nyimbo inayohuzinisha kwa upande mmoja ila inafunza mambo mengi mnoo

3 Siku Hazigandi,

Malkia wa muziki wa bongofleva Jide akiwa katika ubora wake aliachia hichi kibao murua kabisa, achilia mbali midundo inayopatikana humu, ujumbe unaopatikana ni mkubwa sana unalenga kumfanya msikilizaji ajifunze kutokata tamaa katika maisha....

4 Ndio Mzee,
Professor J akiwa katika ubora wake alitunga hichi kibao ambacho kinakuelezea mustakabali mzima wa siasa na demokrasia ya kiafrika kwa kutumia lugha ya kiswahili, hii nyimbo inakufanya upate utashi mkubwa sana wa siasa za kiafrika na Tanzania....namshukuru Mungu nimebahatika kuisikia hii nyimbo

5 Darubini Kali,
Afande sele akishirikiana na Dogo ditto walitoa hichi kibao kilichomfanya Afande sele kuwa mfalme wa rhymes, kaongelea mambo mengi sana humu , ni moja ya nyimbo bora kabisa kuwahi kutungwa nchini Tanzania


6 Alikufa kwa Ngoma
Mwanafalsafa akishirikiana na Jide walitoa hichi kibao katika kipindi ambacho gonjwa la ukimwi lilikuwa tishio mno, aina ya ujumbe na uwasilishwaji wake kunaifanya hii nyimbo kuwa ya tofauti miongoni mwa nyimbo zote zilizokuwa zinaongelea kuhusu ukimwi,,,, hupaswi kuacha kutoiskiliza hii nyimbo

7 Mapenzi Kitu Gani,


huwezi ukazungumzia maisha ya mwandamu bila kuhusisha na mapenzi, MB DOGG akiwa katika ubora wake aliachia hichi kibao kujaribu kuonyesha uwalakini wa neno mapenzi, uhusiano wa utajiri, umaskini, umaarufu na mapenzi...ujumbe japo ni wa mapenzi lakini ni mzito mno....ni moja ya nyimbo bora kabisa za mapenzi hapa Tanzania


8 Elimu Dunia,

Daz baba aliachia kibao hichi ambacho ndani yake ujumbe wake unalenga kufundisha umuhimu wa elimu, hii nyimbo ni nzuri mno hupaswi kuacha kuisikiliza..

9 Sihitaji marafiki,

Farid kubanda nyimbo zake zote zina ujumbe mkali, ila ujumbe unaopatikana katika hii nyimbo ni wa kitofauti na wa kipekee,, kama nyimbo inavyojieleza "sihitaji marafiki'.......


10 Hii ndiyo Tanzania


Unataka kufahamu mambo ya Tanzania basi nenda kaisikilize hii nyimbo ya Roma mkatoliki inayoitwa "hii ndiyo Tanzania".........utapata ujumbe mzit sana aseee

Nadhani hizi ndizo nyimbo muhimu zaidi kwa Mtanzania yeyote kuisikiliza ....kama kuna ambayo imesahaulika au unalist yako hebu itaje hapa tuijadili.

Muigizaji Pastor Myamba apewa zawadi ya Tsh milioni 250 kwenye ndoa yake.

myamba
Hii imetoka kwenye instagram ya actor JB na inamuhusu muigizaji mwenzake wa bongomovie ambaye amefunga ndoa hivi karibuni.
Kwenye hiyo post taarifa ni kwamba pesa hizo hii ni moja ya zawadi alizopewa Pastor Myamba pamoja na mke wake baada ya kufunga ndoa yao.
Hii picha ni baada ya kukabidhiwa hizo pesa.

Capture
chanzo: millardayo

WAKO WAPI WAKINA MB DOG, Z-ANTO, KEISHA, PINGU, SPARK, DOGO JANJA NA WENGINE WALIYOJITOA TIP TOP??? ZIFAHAMU SABABU ZA WAO KUPOTEA KWENYE GAME..!!

Wako wapi MB Dog, Z-Anto, Keisha, Pingu, Spark, Dongo Janja na wengine waliowahi kujitoa Tip Top Connection? Kuna nini Tip Top, kwamba ukijiondoa tu huwezi kufanikiwa mbeleni? Kwanini ni wasanii wachache tu, tena anaweza kuwa Cassim Mganga peke yake ambaye baada ya kujiondoa kwenye himaya hiyo yenye makazi yake Manzese jijini Dar es Salaam, amefanikiwa kuwa na career ya kueleweka? Wengine wote, wamefeli.. big time. 
Kinachosikitisha zaidi ni kuwa wengi wakiondoka hutoa maneno ya kashfa na hivyo kujikuta wakinyea kambi. 
Hebu tuwaangalia hawa watatu, Dogo Janja, Z-Anto na MB Dog 
Dogo Janja 
Unakumbuka June 2012, kipindi Dogo Janja ameondoka Tip Top? Habari hiyo ilikuwa kubwa kiasi ambacho simu za Madee na Dogo Janja zilikuwa busy kwa interview. Kila pande ilikuwa ikiutupia lawama upande wa pili. 
Kama umesahau wacha tukukumbushe ilivyokuwa. 
Sababu zilizotajwa na Tip Top Connection ni kwamba Dogo Janja alilewa sifa na kuwa mtoro shuleni. Kwa mujibu wa interview aliyofanya na Bongo5, uonevu na dhuluma ndivyo vilivyomchosha Dogo Janja kuishi Dar es Salaam na kujiondoa kwenye himaya hiyo. 
Alisema tangu aje Dar es Salaam hakuwahi kusaidiwa chochote na Madee zaidi ya mambo ya muziki pekee huku kula, malazi na ada ya shule vikifanywa na rafiki yake Madee aitwaye Abdallah Doka ambaye (Dogo Janja) alikuwa akiishi kwake. 
Alisema kutokana na ngoma zake kujipatia umaarufu alikuwa akipata show nyingi nchini na zote alikuwa halipwi chini ya milioni moja. Kilichokuwa kinamsikitisha anasema ni kulipwa hela kidogo isiyozidi laki mbili na hivyo kumfanya aishi kwa tabu licha ya kuingiza hela nyingi za show. “Nilikuwa navumilia tu bro kwasababu kila nilipolalamika kuhusu mambo ya hela Madee alikuwa mkali sana,” aliiambia Bongo5. 
Dogo alidai ilikuwa inafikia wakati akifanya show za ukumbuni hulipwa elfu hamsini au chini ya hapo na wakati mwingine alikuwa halipwi kabisa. Alisema tamaa ilizidi kumwingia Madee kiasi cha kumnyang’anya kadi yake ya benki na kuanza kuchukua hela bila kujua password aliipata wapi. “Kuna wakati nilikuwa nataka kumtumia mama laki moja, Madee akanikataza eti kwakuwa watadhani nina hela sana,” alisema. 
Aliongeza kuwa kuna siku Madee alimpigia simu na kumwambia kuwa kaka yake wa Kibaha ameandaa show ya CCM na angemlipa shilingi laki moja. “Hivi kweli bro mimi ni mtu wa kufanya show ya laki moja?” alihoji. Hata hivyo aliamua kukubali ili kuepusha lawama. 
Baada ya show kumalizika alisema yeye na back up artist wake walirudishwa saa saba usiku wakati asubuhi yake alitakiwa kwenda shuleni kuchukua namba ya mtihani na kuandaa dawati la kukalia. Dogo Janja alisema kuwa ilimuuma sana kwakuwa muziki haujampa chochote licha ya Madee ambaye huwa hapati hata show kumtumia kimaslahi na hadi kufikia hatua ya kujenga nyumba yake. 
“Ni kama vile Madee alinipanda ili anivune,” alisema. 
Alifunguka kuwa hadi kufikia Tip Top watangaze kumfukuza alikuwa kwa Tundaman akipiga story na Madee akamuita kisha kuanza kumpiga na kwamba alichukua simu yake akaondoka nayo. “Jamaa alianza kujitumia meseji kutoka kwenye simu yangu kwenda kwake za matusi ama kuwa nataka kumroga. Jana nimemuonesha Milard hizo meseji na amesikitika sana.” 
Alisema kitendo cha kumwambia Madee kuwa amechoka na anataka kurudi nyumbani ndicho kilimfanya amfanyie yote hayo hadi kumwambia kuwa watahakikisha wanambania asifanye vizuri tena kwenye muziki. Pia amedai kuwa Madee aliwapigia simu wazazi wake ili wamkataze Dogo Janja asifanye interview na vyombo vya habari. 
“Wanajua nikiongea wataabika sana.” 
Baada ya drama zote hizo ndipo Ostaz Juma akaingia kwenye picha. Alimtumia nauli ya ndege rapper huyo kutoka Arusha kurejea Dar na akajiunga na Mtanashati Entertainment ambayo wakati huo ilikuwa na heshima kidogo. Dogo Janja alipewa maisha, akalipiwa ada ya shule na kutoa ngoma iitwayo Ya Moyoni aliyomshirikisha PNC. Haikupita muda, mambo yakaanza kutokota. 
Kwa mara nyingi Ostaz Juma alimfukuza na kumrejesha tena rapper huyo kwa madai kuwa hakuwa na nidhamu. Hata hivyo, imefika wakati ambapo Mtanashati Entertainment imekosa muelekeo na Dogo Janja anahisi meli inazama. Kuomba msamaha ili mambo yaende ni kitu kisichoepukika kwake kwakuwa ni kweli Dogo Janja wa ‘Mtoto wa Uswazi’ ft Godzilla amepotea kabisa. 
Z-Anto 
Ni ngumu kuamini ukubwa wa Z-Anto baada ya kutoa hit single yake ‘Binti Kiziwi’ ungekuja kuyeyuka kama barafu ikutanapo na jua kali. Enzi Binti Kiziwi inahit, hakuna msanii aliyekuwa na show nyingi kama Z-Anto. Hata hivyo, meneja wa Tip Top Connection aliwahi kudai kuwa kipindi hiki ndipo msanii huyo alianza kuota ‘majipu’ kwapani na kuanza pozi nyingi. Jambo hilo lilimkera Babu Tale kiasi cha kuamua kuifuta kabisa video mpya ya msanii huyo iliyokuwa inategemewa kumpeleka juu zaidi. Baada ya kuondoka Tip Top mpaka leo hii, Z-Anto si yule tena wa zamani na ukweli hali yake kimuziki ni mbaya. 
“Nililazimika kushuka kwa sababu hiyo. Lakini nilipokuja kuzigundua zile njia nikaweza kupenya na ngoma binafsi nilijisimamia mwenyewe kwa kila kitu ambayo ndio hiyo Kisiwa cha Malavidavi,” Z-Anto alikiambia kipindi cha Mseto cha Radio Citizen ya Kenya hivi karibuni japo alidai kuwa hadi leo Babu Tale anamtaka arejee kundini. 
“Mpaka kesho (Babu Tale) bado ananipenda. Hata ukimuuliza katika wasanii wake anaowapenda atatajwa wawili asishindwe kunitaja mimi.” 
MB Dogg 
Unazikumbuza Latifa na Si Uliniambia? Hizo ni miongoni mwa nyimbo bora za Bongo Flava za muda wote lakini yuko wapi MB Dogg? Kama ilivyokuwa kwa Z-Anto, naye baada ya kujitoa Tip Top, mambo yalienda mrama. Ilimchukua miaka mingi MB Dogg kuweka ‘ego’ pembeni na kukubali kuwa kweli amepotea na anaiihitaji Tip Top kiasi cha mwaka huu kuweka mambo sawa na Babutale. 
“Lakini kwa sasa nataka tumuangalie Mb Dogg kwa macho mawili,” Tale aliiambia Millaayo.com hivi karibuni. Mb Dogg ana kipaji watu wanaujua uwezo wa Mb Dogg, Mb Dogg sio kama amepotea hapana ila hana uongozi anahitaji promo ya nguvu tu akipata hiyo anarudi kupiga hela kama zamani.” 
Hata yeye mwenyewe MB hivi karibuni alikiri kuwa kufanya muziki bila kuwa na uongozi wa kukusimamia ni kazi bure. 
“Tip Top nilitoka na ndio kitu ambacho kilinirudisha nyuma sana,” MB Dogg aliiambia Bongo5 March 17 mwaka huu. 
“Pale nilikuwa nafanyiwa kila kitu, nilikuwa narekodi tu kazi yangu vitu vingine vyote wanafanya wao so baada ya kutoka na kujisimamia mwenyewe nikaanza kuyumba na kuhangaika huku na kule. Kwahiyo kitu ambacho nimegundua msanii bila management nzuri huwezi fika mbali asikwambie mtu. Msanii anahitaji kuongozwa, kushauriwa na mambo mengine. Sasa hivi nipo Tip Top tumeingia makubaliano mapya ya kazi ndio maana nashukuru Mungu ngoma yetu mpya ‘Umenuna’ inasonga kidogo kidogo mpaka kieleweke.” 
Kinachowaumiza zaidi wasanii walioondoka Tip Top ni kwamba wasanii waliosalia mathalani Madee, wameendelea kufanikiwa zaidi. Mwaka jana pekee, Madee anadai kuingiza zaidi ya shilingi milioni 150 kwa single yake moja tu ‘Sio Mimi’. Meneja wa Tip Top, Babu Tale akishirikiana na Said Fela ndio walio nyuma ya mafanikio ya Diamond Platnumz, kwahiyo ni wazi kuwa Babu Tale ni ‘hot cake’ kwa sasa na ndio maana wasanii wa Tip Top waliojiondoa wako radhi kumuomba msamaha ili warejee kundini. 
Swali ninalokuacha nalo msomaji ni Je! Haiwezekani msanii aliyejiondoa Tip Top kuwa na career yenye mafanikio? -Bongo5

STORY NA PICHA ZA MJENGO WA MH. TEMBA ALIYOKABIDHIWA HAPO JANA NA SAID FELLA..!! TAZAMA HAPA...!!

Kupitia akaunti ya Said Fella ambaye ni C.E.O wa MKUBWA NA WANAE FOUNDATION na meneja wa msanii Mh Temba, amefunguka na kusema anamkabidhi Mh. Temba mjengo wake ikiwa ni mjengo wa pili kumpatia kutokana na shughuli nzima ya muziki,
 
Temba akiwa kwenye mjengo wake
Said Fella aliweka picha hiyo hapo juu na kuambatanisha maneno haya"Wadau namshukuru mungu leo mchana nimemkabidhi mbabe wa mdomo nyumba yake ya pili hii ipo mbagara kirungule asante kwa mashabiki wetu wote wanao tuwezesha na vijana wengi kubadirisha maisha asante sana"  

RIPOTI: HIZI NDIO SABABU ZA BAADHI YA WATU KUCHUKIA MAFANIKIO YA DIAMOND...?? SOMA HAPA..

Watu wengine kamwe hawataweza kukusifu au kukubali kwa unachokifanya mpaka pale usipokuwepo kabisa.

 Ni ajabu kuwa watu wengine katu hawawezi kuona kile walichonacho; wakionacho pekee ni kile wasichonacho, ni kile wanachokosa. 

1466276_647113715310446_2016369392_n

Wakati mwingine inahitaji roho ya paka kuendelea na nguvu kufanya kile unachofanya wakati watu wanaendelea kukudhihaki. 

Zaidi ya muziki, kuna kitu gani kizuri kinachoitangaza Tanzania nje ya nchi kwa sasa? Tusaidiane kuuchambua ukweli huu unaomezeka kwa fundo la mate la kulazimisha kinywani.

 Ni lini mara ya mwisho Tanzania imefanya vizuri kimataifa kwenye soka? Hakuna habari njema zaidi ya kuendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu, iwe kwetu hata nje.

 Ni lini mara ya mwisho mkimbiaji riadha wa Tanzania ameshinda mbio zozote za kimataifa? Hakuna. 

Kimichezo ni kama bado tumeendelea kuwa wasindikizaji tu. Au umesahau jinsi Selemani Kidunda alivyodundwa mwaka 2012 kwenye mashindano ya Olimpiki? Ukitoa mwaka 2005 pale Nancy Sumari alipokuwa Miss World Afrika, ni lini mrembo yeyote wa Tanzania amewahi kuiletea sifa nchi yetu? 

Ni nini hasa kinachoweza kuifanya Tanzania kuipeperusha bendera yake kwenye jukwaa la kimataifa kwa sifa nzuri? Au labda kipindi hiki tumegeuka kuwa mabingwa wa biashara ya dawa za kulevya na Watanzania ndio wamekuwa vinara wa kukamatwa kila kukicha nchi za nje.

Angekuwepo Kanumba na zile jitihada alizokuwa akizifanya, labda tungesema Bongo Movies ilikuwa inaelekea kuwa njia nzuri ya kutupa heshima pia. Lakini tangu afariki, hakuna mwingine anayeonesha dalili za kufanya kile alichokuwa anakifanya na filamu zetu zimeendelea kuwa za nyumbani pekee.

Hivyo, ukiangalia kwa mifano hiyo, ni muziki pekee wenye matumaini ya kuliongezea ‘kiki’ jina la nchi yetu kwenye ‘google search’. Lakini kama muziki ndio unaonekana kuwa kitu muhimu kinachoitangaza Tanzania, mbona wale wanaofanya vizuri kwa kutuwakilisha nje tunawabeza?

Mpaka muda huu, ukimtoa AY, hakuna msanii mwingine wa Tanzania anayevuma kimataifa kama alivyo Diamond Platnumz. Amefanikiwa kiasi cha hivi karibuni kumshirikisha staa wa Nigeria Davido kwenye remix ya wimbo wake, Number 1 na video iliyogharimu si chini ya dola 25,000 iko mbioni kutoka. Amekuwa ni msanii mwenye kujituma, kutake risk na kutochoka kujaribu kufanya kile wengi wamekuwa wakikiogopa kufanya. Lakini bado kuna watu wengi hawaoni anachokifanya na wameendelea kumkejeli.


Wanasema hakuna binadamu aliye mkamilifu, lakini pamoja na kwamba unaweza kumnyonga mnyonge, ni vyema kukumbuka kumpa haki yake. Ni asili ya mwanadamu kuumizwa na mafanikio ya mtu mwingine, na ndio kinachotokea kwa Diamond. Ameendelea kufanikiwa kiasi mpaka anaanza kuwakera wengine. Si kosa kuchukia maisha na scandal zake, lakini si kosa pia kusifia kile anachoifanyia Tanzania.


Siwezi kubisha kuwa, mimi binafsi Diamond amekuwa akinikera kwa baadhi ya vitu (kama mimi pia ninavyokera wakati mwingine, nobody is perfect) lakini siwezi kuukataa ukweli kwamba Diamond ana kipaji, anajituma, anapendwa na anajua anachokifanya. Kubwa zaidi ya hayo, Diamond amekuwa mstari wa mbele kuitangaza Tanzania na Kiswahili pia lugha yetu adhimu kupitia nyimbo yake.


Ni jambo tunalolihitaji Watanzania kuwa na msanii wetu mkubwa mwenye hadhi na mafanikio kama ya P-Square. Pengine tusisahau ukweli huu kwamba ni mapenzi watakayoyapata wasanii wetu hapa nyumbani pekee ndio yatakayowapata mafanikio zaidi. Utafanikiwa vipi nje ya nchi kama nyumbani wanahate?


P-Square walikiri kuwa ni Wanaijeria wenyewe ndio waliowafanya wawe wakubwa kiasi hicho na kuwataka Watanzania pia wafanye hivyo kwa wasanii wao.


“Wanamuziki wenu wanafanya kile kile sisi tunachokifanya, mnaowaona watu hawa hapa?Mnaweza kuwafanya wawe wakubwa kuliko P-Square. Ukweli ni kwamba tunapromote muziki wa Africa. Waafrika huu ni muda wetu. Wamarekani nasema wanaogopa sasa hivi. 

Ningependa kuona mnaweka jitihada zaidi kwa wanamuziki wenu hapa. Nataka kuwaona wanakuja Nigeria na kuongoza concert. Hakuna mtu anayeza kufanya hivyo vizuri isipokuwa ninyi,” alisema Peter kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar, siku moja kabla ya show yao ya Leaders Club.


Diamond ni binadamu kama wengine. Anaumia anapoona anakosolewa hata katika mambo yasiyokuwa ya msingi. Kwa mfano hivi karibuni alihudhuria harusi ya Peter wa P-Square jijini Lagos, Nigeria. Inasemekana kuwa mwaliko huo aliupata kutokana na kuwa karibu na Iyanya aliyemshirikisha kwenye wimbo wake. Katika harusi hiyo, Diamond alipiga picha na Peter na kuiweka Instagram.

Platnumz-katika-harusi-ya-Peter-4Diamond akiwa na Peter Okoye

Inasemekana kuwa P-Square walipokuja Tanzania waliulizwa kama wanamfahamu Diamond na kwamba wakasema lahashaa, hawamjui. Cha ajabu suala hilo limegeuka gumzo na watu wamekuwa wakimkejeli Diamond kuwa kaumbuka. Jamani, kwani ni lazima Peter awe anamfahamu Diamond? 

Amfahamu kwa njia ipi? P-Square ni wasanii namba moja Afrika, unaweza kufikiria ni wasanii wangapi Afrika wenye level za Diamond wanaotaka walau kupata contacts zao? Ni wengi mno, na unadhani ni rahisi kuwapata? Na hata hivyo, wote tunajua harusi zinavyokuwa na pilikapilika, unahisi Peter alikuwa na uwezo wa kumkariri kila mtu aliyehudhuria harusi yake. Unadhani ilikuwa rahisi kwa Diamond kujitambulisha vizuri kwa Peter kiasi cha kumfanya amkumbuke? Ni ngumu.


Haya, jana Rais Jakaya Kikwete alisema kwenye semina ya fursa kuwa Diamond ni msanii mwenye nidhamu ya kazi ama kwa Kiingereza ni ‘work ethic’. Wengi wemepingana na kauli ya mkuu wa nchi kwa kuona kampa Diamond sifa asiyostahili.

Lakini kwanza tujiulize, ni nini maana na nidhamu ya kazi? Ni thamani iendanayo na uchapakazi, umakini na kujituma. Nidhamu ya kazi ni pamoja na kuwa ‘reliable’ kuwa na uwezo wa kuanzisha vitu na kutafuta ujuzi mpya. Kwa tafsiri hiyo, unaweza kumpiga Rais Kikwete kwa kusema Diamond ana nidhamu ya kazi? Maisha binafsi, scandal na ubinadamu, havina uhusiano wowote na nidhamu ya kazi. 



Sibishi kuwa wakati mwingine maisha ya Diamond hasa ya kimapenzi yamekuwa na sifa mbaya, lakini hiyo haiuondoi ukweli kuwa, ni msanii anayejituma sana. Tumkosoe pale ambapo anastahili kukosolewa na pia tumpe sifa pale anapostahili kusifiwa lakini sio kuhate pasipo na sababu za msingi.

Labda wengine wanamchukia kwasababu hupenda ‘kubrag’ kwa kupost picha za dola, cheni, saa, nguo ama viatu vya thamani kwenye Instagram? Kama ndivyo, basi nakumbuka kauli ya Joh Makini aliyoniambia hivi karibuni kuwa watu wengine wamekuwa na chuki kwa wenzao waliofanikiwa kwakuwa maisha kwao ni magumu.


“Ukichungumza kitu gani kinachosababisha haya mambo yote, utagundua kuwa watu wengi hawawezi kukidhi gharama za maisha jinsi ambavyo zinapanda. Huo ni mwanzo wa kuwekeana chuki kwenye kazi au mtu anakuwa anakusikia wewe kwa kitu ambacho unafanya, utagundua ni kwamba kwasababu yeye anashindwa kulipia bili zake za kila siku, hata kama hausikika kwa namna moja au nyingine kwenye kipato chake lakini unakuta tu mtu anakuwa na chuki binafsi. Tatizo bei ya mkaa,” alisema Joh.

Ina make sense hata hivyo. Unapogundua kuwa huduma ya maji imekatwa nyumbani na huna hela ya kulipa au mchana unapita mkavu bila ‘kupiga menu’ halafu kwenye Instagram unaona picha ya Diamond akiwa na buruguntu la dola za kimarekani, lazima kiroho kiume na unajikuta unageuka hater ghafla!!!

Tatizo ni bei ya Mkaa.

-BONGO5

HUU NDIO MJENGO MWINGINE WA DIAMOND PLATINUMZ AMBAO UPO KWENYE HATUA ZA MWISHO KUKAMILIKA...

Kijana anayefanya vizuri kwenye muziki wa Bongo Fleva Diamond Platnumz mambo si mabaya kwake baada ya kuonyesha mjengo wake mwingine wa hatari ambao bado upo katika ujenzi.  
 
Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram,Diamond jana ame-share picha ya nyumba hiyo na chini akatia neno..Shuka nayo.


''Toa kitu weka kitu...! Ndio tulivyo funzwa...stareh tunawaachia wajanja wa mji... #WCB #Wasafi for the Fkn Life!''

Haijajulikana mjengo huu uko maeneo gani wala umegharimu kiasi gani
ila inaendelea kudhihirisha mafanikio anayoendelea kuyapata Diamond.

RAY C ASHEREHEKEA MWAKA MMOJA WA KUACHA KUVUTA BANGI NA MADAWA MENGINE YA KULEVYA..

  
SEXY lady wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ amesheherekea mwaka mmoja na wenzake tangu alipoacha kutumia madawa ya kulevya ‘unga’.
Ray C akisherehekea na wenzake.
Wikiendi iliyopita Ray C alitupia picha kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram zilizomuonesha akiwa na wenzake katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar ambako huwa wanapata dozi ya madawa ya kulevya.
...Akizidi kuburudika baada ya kutimiza mwaka mmoja wa kuacha unga.
Aliandika: “Nawapenda sana hawa wenzangu wote, tuligundua tatizo tukasaidiwa na sasa tumepona na tunamshukuru Mungu...Tanzania bila madawa ya kulevya inawezekana.”

BINTI ALIYE DAIWA KUVUNJA NDOA YA BOB JUNIOR AKANUSHA NA KUSEMA HAYA...!!

 

Baada ya Blogs na Magazeti Kumwandika sana Ashley Toto  Mwanadada Kutoka Kenya Kuhusika na Kuvunjika kwa ndoa ya Bob Junior Amejitokeza na Kuandika haya kwenye Wall yake ya Facebook
"****JAMANI NIMECHOKA NA SKEDOLS ZA UONGO ILA NAAMINI HII NI MITIHANI NA INSHAALLAH YATAISHA***I HAVE NOTHING TO DO WITH HIM...." 

Tuliamua kumtafuta na kuongea nae na kusema kwa masikitiko kuwa Hana uhusiano wa kimapenzi na Bob Junior Bali wao ni marafiki tu wa Muda mrefu..Pia akasema huwa anamtafutia Show Sehemu mbali mbali ikiwemo Ujerumani anapoishi ..... So anasema amechoka kuandikwa kuhusu Bob Junior

Baby Madaha akanusha kutoa rushwa ya ngono kwa bosi wake wa Candy n Candy..


Msanii wa label ya Candy n Candy Baby Joseph Madaha amekanusha uvumi uliovumishwa na wanamuziki wenzake wa labe hiyo kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na CEO, Joe Kariuki.
 
Uvumi huo ulianzishwa na baadhi ya wasanii wengine, wa label hiyo wanaodai kuwa tangu Baby Madaha asainishwe Candy n Candy maisha yake yamebadilika na kwamba amekuwa akipendelewa zaidi.
 
Akizungumza   Bongo5  jana , Baby amesema CEO wa Candy N Candy, Joe Kariuki alishauriwa na wadau kwamba amwendeleze yeye na akifanikiwa awasaidie na wenzake.
 
“Joe amesikia na hajapenda hili swala kwasababu sisi tupo kizazi zaidi kwasababu mimi najituma kufanya kazi ya muziki ambayo imenipeleka Candy n Candy na sio mambo mengine kama wanayosema wao. 

"Huu ni wivu ni kwasababu mimi ni msanii mkubwa tayari nimeshatengeneza jina kwenye muziki sema kuna kipindi nilijikita kwenye filamu sana, kwahiyo siwezi lingana nao hata kidogo,” amesema.
 
“Candy n Candy walihitaji mwanadada ambaye ataweza kuongea zaidi ya lugha mmoja kwasasababu ya kufanya muziki kimataifa na kigezo kingine walichokitaka ni huyo mwanamuziki mwanadada kuwa na mwenekano mzuri. 

" Wasanii wote wa Candy n Candy tulipelekwa studio, tukarekodi kila msanii.Wale Four – D ndio walianza kurekodi sasa kukawa na msichana mmoja anatoka kimapenzi na msanii mwezake wakawa wanatukanana na kushikanashikana pamoja na kumsema bosi wao. 

"Baada ya kurekodi bosi akapokea ushauri kutoka kwa wadau kwamba ‘hii kazi ya Four – D ni mbaya kwanini usimwendeleze Baby Madaha halafu baadaye Baby Madaha akawainua wenzake’. 

"Bosi akatuambia ‘sasa ngoja nianze na Baby Madaha nyie wengine mtafuata’ wale Four – D hawakuwa wavumilivu ndio wakaanza kusema maneno mengi,” amefafanua Baby  na  kuongeza
 
“Kiukweli mimi najituma katika kazi, Top C wanataka wafanyiwe kila kitu watafutiwe kila kitu. 

"Kwahiyo mimi naona kama wangenisikiliza mimi kama mimi kwasababu nimepitia kwenye academy ya muziki kwahiyo naulewa muziki, haikuwa na sababu ya kuongeaongea maneno mtaani.

"Mpaka leo Top C anapigiwa simu akafanye video hawajaenda wanasema ana matatizo ya kifamilia, sasa ni bosi gani aache kufanya kazi na watu ambao wako serious amfuate yule aliye bize?"
 
Hata hivyo Baby amesema kwa kuwa Joe ni mwanaume na yeye ni mwanamke endapo wakiwa wapenzi si japo la kushangaza wakikubaliana kufanya hivyo.
 
“Haya ni mafanikio yangu ndio maana wanaongea,leo nimezindua bag na perfumes wana wivu, kwani Joe si yupo single na mimi nipo hivyo hivyo!! Kwahiyo kama tukikubalina personal ni sisi,muziki ni muziki na mapenzi ni mapenzi. Kwahiyo yote yanawezekana.”

PICHA: "RAY C" NA "RECHO" NI MAPACHA WA MATUMBO TOFAUTI, HAWAFANANI SAUTI TU...WANAFANANA SURA PIA..!! WATAZAME HAPA..


Mara ya kwanza tu Recho alipoanza kusikika, sauti yake ilianza kufananishwa na ya Ray C. Kuanzia kwenye Kizunguzungu, Upepo na Nashukuru Umerudi, Recho alikuwa Ray C mtupu.
Hata hivyo hiyo haikumsumbua, Ray C ambaye alisema kuwa ni faraja kumsikia Recho akiimba kama yeye na tangu hapo wamekuwa marafiki.
Lakini wawili hawa, hawafanani sauti tu. Picha hii (hapo juu) iliwekwa na Ray C kwenye Instagram na wengi walidai kuwa, warembo hao wanafanana kama mapacha vile.

"SIKUWA NAJUA MAPENZI NI NINI MPAKA NILIPOPATA MTOTO"....MWANA FA

Rapper Hamis Mwinjuma aka Mwana FA amesema alikuwa hajui mapenzi ni kitu gani mpaka pale binti yake aliyetimizia miaka miwili hivi karibuni, Maleeka kuzaliwa.

page

Mwana FA amesema tangu awe na mtoto, maisha yake yamebadilika kwa kiasi kikubwa na kumfanya aishi maisha ya kujilinda zaidi kuliko zamani.
Nimekuwa very careful, I am worried, siko reckless kama nilivyokuwa. Naogopa nina mtu ananitazama na sitaki kumwangusha. Watu wengine tumekua kidogo juu juu sana, sitaki maisha yangu ambayo mimi nimekua impitie mwanangu hata kidogo,” alisema FA.
“Amenibadilisha, nawaza, nina wasiwasi kuhusu maisha yangu ya mbele. Kiukweli maisha yangu ya kufikiri kuhusiana na maisha na vitu vingine vinavyonizunguka vimebadilika sana kwaajili ya binti.”
Older Posts
© Copyright ZEE LA UDAKU | Designed By Code Nirvana
Back To Top