Habari Kali
Loading...

Pichaz za mastaa 10 wa soka wenye mvuto zaidi duniani !!

C Ronaldo
Mastaa wa soka wanavutia wengi kwa ufundi wao uwanjani, lakini hata nje ya uwanja ni kawaida kuwaona wakiingia kwenye dili za ishu kama matangazo ya biashara, au fashion.. yes mvuto unazingatiwa pia upande huo !!
Nimekutana na hii mtandaoni na nimeichukua kuisogeza kwako mtu wa nguvu, list ya mastaa 10 wa soka wanaoongoza kwa mvuto zaidi duniani.
casu
1. Cristiano Ronaldo amekuwa na mafanikio makubwa kupitia soka, mwonekano wake wa kuvutia umemfanya aingize kiasi kikubwa cha pesa kupitia matangazo ya biashara na fashion.
kaka
2. Kiungo Ricardo Kaka anatokea Brazil..kwa sasa anaichezea klabu ya Sao Paulo kwa mkopo akitokea Orlando City
villa
3. David Villa kitu kingine kinachovutia wengi ni style yake ya nywele ambayo huwa anaibadilisha mara kwa mara.. pamoja na kuwa mmoja wa wachezaji wenye umri mkubwa lakini bado amekuwa na muonekano mzuri
4. Iker Cassilas ni mmoja wa makipa wenye mafanikio makubwa sana kutokana na uwezo wake.. Tegemezi la nguvu kwa Klabu ya Real Madrid, amekuwa ni mmoja wa wachezaji wenye muonekano mzuri
van
5. Robin Van Persie ni Mshambuliaji wa timu ya Manchester United
nando
6. Fernando Torres Ni mshambuliaji wa klabu ya Atletico Madrid na timu ya Taifa ya Hispania
gotz
7. Mario Gotze ni kiungo mwenye umri mdogo kutoka klabu ya Taifa ya Bayern Munich ya Ujerumani, amezaliwa mwaka 1992
mes
8. Ana ufundi wake wa nguvu uwanjani akiwa ndani ya jezi ya Klabu yake ya Barcelona, Lionel Messi ameingia kwenye orodha ya wachezaji wenye mwonekeano mzuri pia
pque
9. Gerard Pique ni mlinzi wa timu ya Taifa ya Hispania na Barcelona, amezaliwa mwaka 1987 na ni mume wa staa wa muziki duniani, Shakira.
faaa
10. Cesc Fabregas ni kiungo wa timu ya Taifa ya Hispania na klabu ya Chelsea, Ni baba wa mtoto mmoja wa kike.. staa huyu amezaliwa mwaka 1987

Floyd Mayweather VS Manny Pacquiao kazi imeisha !! Huyu ndiye mshindi

fight-8a_rnd_5_3289903b
Najua watu wengi waliisubiri hii kwa hamu.. wengine hata sio mashabiki wa boxing lakini walijikuta wakivutiwa na hii.. Promo ilikuwa kubwa sana, pambano la kihistoria ambalo dunia nzima ililisubri ni hili kati ya Floyd ‘Money’ Mayweather na Manny Pacquiao.
Points tayari zimeamua, pambano limeenda kwa round 12, Floyd Mayweather kamshinda Pacquiao kwa points sita tu.. Floyd ana points 117 na Pacquiao ana points 111.
wattt_3289915b
Kwa matokeo hayo Mayweather kaendeleza kuweka rekodi yake kubwa ya kutoshindwa pambano hata moja tangu amekuwa professional boxer.
fight-6-a_rnd_2_3289901b
fight-end-manny_3289916b
fight-floyd-manny-_3289909b
fight-floyd-win-be_3289919b
fight-manny-floyd-_3289911b
fight-manny-floyd-_3289914b
Shilingi yako uliweka upande upi mtu wangu ?? Nitafurahi kuona utakachoniandikia kuhusu hii..

Hofu ya kocha wa Manny Pacquiao ipo kwa Floyd Mayweather…unajua kasemaje? SOMA HAPA

city

Pambano la kimataifa kati ya mafahali wawili Floyd Mayweather na Manny Pacquiao sasa wanahesabu masaa tu kuweza kupanda jukwaani kwa ajili ya kumaliza utata wa nani mbabe kwa mwenzake.
Ikiwa ni siku moja tu kabla ya pambano hilo kufamyika, kocha wa Pacquiao, Freddie Roach ametamka kuwa huenda Maywether akagoma kupanda ulingoni siku ya pambano hilo.
flooRoach amesema hadhani kama Mayweather alitaka kupigana na alilazimishwa kupigana katika pambano hili ambalo mwenyewe hakulitaka.
pac
Mabondia hao usiku wa jana walikutana na waandishi wa habari na kuonyesha mkanda ambao mshindi atakabidhiwa baada ya mchezo huo.
etiii
Kwa pamoja wamekutana na kila mtu ametoa ya moyoni, lakini kila mmoja kajigamba kushinda pambano hilo.

HII NDIO BEI ZA KIINGILIO ZA PAMBANO LA MANNY PACQUIAO NA FLOYD MAYWEATHER!

Manny-Pacquiao-vs-Floyd-Mayweather-Pacquiao-vs
Zimebaki siku 9 kabla ya pambano lilopewa jina la ‘Fight of the Century‘ kati ya mwanasumbwi tajiri zaidi duniani Floyd Mayweathe Jr ambaye ana rekodi ya kutopoteza pambano hata moja tangu aanze kucheza mchezo huo, dhidi ya mfilipino mwenye rekodi nzuri kabisa Manny Pacquiao kufanyika, leo hii bei ya viingilio vya kutazama mchezo huo imetangazwa.
Unaambiwa tiketi ya bei ya chini kabisa itakayokuwezesha kuingia MGM Grand Garden Arena itakuwa ikiuzwa kwa dola 1500 ambayo ni zaidi ya millioni 2.5 kwa hela yetu TZ.
Kwa wale vibopa ambao wa kati tiketi zao zitauzwa kwa dola 7500.
Tiketi hizi zitaanza kuuzwa leo usiku saa 2 kwa saa za Marekani ambapo jumla ya ticket zitakazouzwa ni ticket 1000.
Wakati huo huo zimetengwa tiketi za bei ya juu zaidi ambazo zitakuwa kwa ni dola 10,000 huku nyingine zikiuzwa kwa dola 200,000 kwa watu mashuhuri wenye uwezo wao yani.
Pia kwa wale watakaoshindwa kulipa viingilio hivyo, umeandaliwa mpango kuandaa sehemu itakayoingiza watu 50,000 ambao watalipa viingilio dola 150.

MASKINI..!! BALOTELLI NDIYE MCHEZAJI ANAYEONGOZA KWA KUBAGULIWA EPL!

Mshambuliaji wa Liverpool Mario Balotelli.
Mshambuliaji wa Arsenal Danny Welbeck.
Takwimu zimeripotiwa  hivi karibuni na Kick it Out, zinaonesha kuwa Mario Balotelli ndiye mchezaji aliyebaguliwa sana katika ligi ya Uingereza, huku mchezaji huyo akipokea zaidi ya ujumbe 8000, asilimia 50 kati ya hizo zikiwa ni za kibaguzi.
Kick it Out wameripoti takwimu hizo za kushtua, ambao walibaini kwamba raia huyo wa Itali (Mario Balotelli) alilengwa sana katika mitandao ya Twitter huku mshambuliaji wa Arsenal Danny Welbeck akipokea ujumbe 1700 asilimia hamsini kati ya hizo zikiwa za kibaguzi.
Mshambuliaji mwenza wa Balotelli katika kilabu ya Liverpool Daniel Sturridge pia alionekana kulengwa katika mitandao ya kijamii baada ya kupokea ujumbe wa 1600 asilimia 60 ikiwa ni ujumbe wenye mwelekeo wa kijinsia.
Utafiti huo pia umebaini kwamba kilabu ya Chelsea ndio kilabu iliobaguliwa zaidi kwa ujumbe 20,000 huku liverpool ikiwa ya pili na ujumbe 19,000 Arsenal ikiwa ya tatu kwa ujumbe 12,000 huku Manchester City na Manchester United zikipokea ujumbe 11,000.
 NA BBC

Eti Ronaldo na Messi ndio wakali kwenye soka?? Eric CANTONA kasema hao wote sio, kataja jina la mkali wake !!

article-2455213-18B00C9F00000578-331_634x409
Hii story imesikika pia kwenye AMPLIFAYA jana April 15 2015, labda wewe hukusikia kile alichokisema staa wa soka wa zamani ambaye yuko kwenye vitabu vya kumbukumbu vya mastaa wa soka ambao dunia inawakumbuka kwa uzuri wao kwenye mchezo huo.
Ni kweli Cristiano Ronaldo amechukua tuzo ya mchezaji bora wa soka duniani kwa mwaka wa tatu mfululizo.. anaemfuatia kwa ukaribu zaidi ni Lionel Messi.. vijiweni kuna story bado kwamba nani bora kati yao.
Eric Cantona kataja jina tofauti.. YES.. ndio mawazo yake na yeye kwa hiyo usishangae akakutajia jina la staa wake.. amemtaja Javier Pastore staa mwingine wa soka raia wa Argentina, anachezea klabu ya Paris Saint-Germain.
.
Javier Pastore
Nimeangalia mechi mbili za PSG nikaona amavyocheza.. kwangu mimi yeye ni mchezaji mbunifu zaidi kwa sasa. Napenda jinsi Pastore anavyocheza“– Eric Cantona.
Nitafurahi kuona comment yako, unadhani ni sawa Cantona kumtaja Pastore kuwa ndio mchezaji kwa kumuangalia kwenye mechi mbili tu?
Tunaona mastaa kama akina Beckham wamestaafu wameamua kuwa wafanyabishara na wanamitindo, Cantona kwa sasa ni staa wa movie.
Cnatona FRONTT

PACQUIAO AJICHUA VIKALI KUELEKEA PAMBANO LAKE LA KARNE DHIDI YA MAYWEATHER

Manny Pacquiao akijiandaa na pambano lake dhidi ya Floyd Mayweather.
Maandalizi yakiwa yamepamba moto kwenye gym ya masumbwi ya Wild Card iliyopo Los Angeles nchini Marekani.
BONDIA mahiri kutoka Ufilipino, Manny Pacquiao ameendelea kujichua vikali katika gym ya masumbwi ya Wild Card iliyopo Los Angeles nchini Marekani.
Pacquiao anajiandaa na pambano lake kali dhidi ya Floyd Mayweather litakalopigwa Mei 2, mwaka huu katika Ukumbi wa MGM Grand Garden jijini Las Vegas, Marekani.
Pambano hilo linatazamiwa na wadau wa masumbwi kuwa la karne kutokana na umahiri wa mabondia hao wawili.
Pichani juu ni taswira mbalimbali za Manny Pacquiao akiwa mazoezini.

STEVE Ajutia Maamuzi Yake ya Kuhamia Kuishabikia AZAM Kutoka YANGA, Asema Maisha Yake Yamekuwa Mabovu..Abembeleza Kazi Azam

Aliyekuwa mshabiki maarufu wa Team ya Yanga Steve Amefunguka na kusema kitendo chake cha kuhamia kuwa mshabiki wa Azam kutoka Yanga kimefanya maisha yake yawe Mabovu kimaslahi na umaarufu kupungua sana

Amesema japo bado anaitamani Yanga lakini hawezi kurudi tena kuishabikia Yanga kwa kutoonekana Msaliti ...Hivyo anachofanya kwa sasa ni kumuomba Bosi wa Azam Ampe kazi ya Kuajiriwa katika Team hiyo kama Mshabiki wa Damu ..


Steve alipata umaarufu mkubwa baada ya Yanga kufungwa Tano na Simba miaka kadhaa iliyopita ambapo Steve alirekodiwa na Vituo mbali mbali vya TV akimwaga Kilio cha nguvu

Hii ndiyo List ya makocha 10 wa soka wanaopokea mshahara mkubwa zaidi…!

Mtandao wa Richest Lifestyle umetoa list mpya February 2 2015 ya makocha wa mpira wa miguu wanaoongoza kwa utajiri kupitia soka.
Ukitofautisha na kipato cha makocha wa hapa kwetu ambao bado wamekuwa hawapewi kipaumbele kama ilivyo kwa wenzetu, huku klabu kubwa kama za Simba na Yanga bado zimeendelea kuwaamini makocha wa kigeni
Hii ndiyo list kamili ya makocha wenye kupokea kiasi kikubwa cha fedha ndani ya klabu zao:-
1. Pep Guardiola
Pep Guardiola, Bayern Munich manager
Huyu ni kocha wa Buyern Munich, ameitumikia timu yake kwa mafanikio makubwa huki akiisaidia kupata mataji mbalimbali, ndiye kocha anayeongoza kwa kulipwa mshahara mkubwa kuliko wote kwa kupokea kiasi cha dola milioni 24
2. Jose Maourinho
mor
Huyu ni kocha wa Chelsea ambaye anajulikana kwa kuwa na maneno mengi,kwa sasa yupo mbioni kuwania ubingwa wa ligi kuu ya England,ni kocha anashika nafasi ya pili kwa kulipwa kiasi kikubwa cha pesa na hupokea kiasi cha dola milioni 17
3. Marcello Lippi
macelo
Ameifundisha kwa mafanikio makubwa timu ya Taifa ya Italy na kufanikiwa kutwaa kombe la dunia mwaka 2006,anapokea kiasi cha dola milioni 14
4. Fabio Capello
capelo
Huyu ni kocha wa timu ya Taifa ya Russia,anapokea kiasi cha dola milioni 13
5. Carlo Ancelotti
carlo
Huyu ni kocha mkuu wa Real Madrid, anapokea kiasi cha dola milioni 10.5
6. Arsene Wenger
Arsene Wenger, Manager of Arsenal
Amekuwa kocha wa Arsenal toka mwaka 1996, na anapokea kiasi cha dola milioni10
7. Gerardo Martino
gera
Huyu ni kocha wa Argentina,anapokea kiasi cha dola milioni 7.5
8. Jurgen Klopp
jurge
Huyu ni kocha wa Borrusia Dortmund, anapokea kiasi cha dola milioni 6
9. Manuel Pellegrini
pele
Huyu ni kocha wa Manchester City, anapokea kiasi cha dola milioni 5.75
10. Jorge Jesus
benfic
Huyu ni kocha wa klabu ya Benefica tangu mwaka 2009, anapokea kiasi cha dola milioni 5.5
Older Posts
© Copyright ZEE LA UDAKU | Designed By Code Nirvana
Back To Top