Habari Kali
Loading...

UKATILI..!! MAMA AMLA MTOTO WAKE AKIWA HAI!

indiaaaa
Kumekuwepo na matukio ya baadhi ya wazazi kuwanyanyasa na hata wengine kuripotiwa kuwaua watoto wao wa kuwazaa wenyewe kutokana na sababu mbalimbali.
Headlines nyingine leo zinatokea kule India ambapo mama mmoja amefunguliwa mashtaka baada ya kuripotiwa kumla mtoto wake wa miaka minne huku akiwa  hai.
Pramila Mondal ambaye anadaiwa  kuwa na matatizo ya akili alifanya kitendo hicho akiwa nyumbani kwake na kukutwa na shemeji yake akiendelea kumla mtoto huyo sehemu mbalimbali za mwili wa mtoto wake huyo ambaye alikuwa wa kike.
Baada ya Polisi kufika na kumshilika mama huyo, mtoto huyo alikimbizwa katika hospitali ya Malda Medical center huku akiwekwa katika chumba cha uangalizi maalum kutokana na kuwa na majeraha makubwa.
Polisi walisema pamoja na mama huyo kudaiwa kuwa na matatizo ya akili pia pombe pamoja na madawa vimechangia yeye kufanya tukio hilo.

UKATILI..!! MAMA AMCHOMA MOTO MTOTO MIAKA 7


Saimeni Mgalula, Mbeya
Ukatili kila kona! Mwanamke aliyetajwa kwa jina la mama Joy amechezea kipigo ‘hevi’ kutoka kwa wananchi wenye hasira kali akidaiwa kumchoma moto mikononi mtoto anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka saba ambaye jina halikupatikana kwa madai ya kumuibia shilingi elfu ishirini.

Mtoto huyo akiugulia maumivu baada ya kuchomwa moto na mamaa'ke.
Tukio hilo la kinyama ambalo ni sehemu ya matukio ya mateso kwa watoto yanayotokea kila kukicha maeneo mbalimbali nchini, lilijiri juzikati katika Mtaa wa Nello Kata ya Kaloleni wilayani Momba mkoani hapa majira ya saa 11:20 jioni.
Wakizungumzia tukio hilo, baadhi ya mashuhuda walisema kuwa mtoto huyo alikuwa akiishi katika mazingira magumu almaarufu kwa jina la chokoraa hivyo hana makazi maalum.
Walifunguka kuwa mara baada ya kuwa na maisha hayo, ilibidi mama Joy amuombe aishi naye ambapo mtoto huyo alikubali na kuacha kulala nje ya nyumba na udokozi kwa kuwa alikuwa anapata chakula.
Kwa mujibu wa mashuhuda hao, walisikia kelele za mtoto huyo akilia kwa sauti na walipotoka kumwangalia ndipo wakakuta ameungua mikono na alipoulizwa kulikoni alisema kuwa mama Joy ndiye aliyemchoma akimsingizia kuwa ameiba kiasi hicho cha fedha.
Walidai kwamba, baada ya kusikia hivyo, baadhi ya wananchi wenye hasira kali walianza kumbonda mama Joy huku wakimkokota kuelekea Kituo cha Polisi Tunduma ili sheria ichukue mkondo wake.
Hadi gazeti hili ‘linaanua matanga’ eneo la tukio mama huyo alikuwa ameshikiliwa polisi huku mtoto huyo akipelekwa hospitalini kwa matibabu.

IMAMU: NIMEMWAGIWA TINDIKALI KUTETEA MALI ZA MSIKITI


Na Musa Mateja UNYAMA wa kutisha! Bwana mmoja ambaye ni imamu, aliyefahamika kwa jina la Mustafa Omar Mustafa, mkazi wa Ghana, Kata ya Nyamanoro jijini Mwanza, amefanyiwa unyama wa hali ya juu kwa kumwagiwa tindikili na watu wanaosadikiwa kuwa ni waumini wenzake, kisa kulinda mali za msikiti wao uliopo katika mtaa huo wa Ghana. Uwazi linakupa habari kamili.
Mustafa Omar Mustafa, anayedaiwa kumwagiwa tindikali.
ILIKUAJE?
Akizungumza na mwandishi wetu kwa masikitiko Mustafa alisema kuwa, tukio hilo la kinyama alifanyiwa majira ya saa mbili kasorobo usiku, Jumapili ya Agosti 31, mwaka jana akiwa nyumbani kwake Ghana.

“Nilikuwa katika hali ya furaha na familia yangu, sikuhisi kabisa hatari ambayo ilikuwa inakuja kutokea katika maisha yangu. Tukiwa hatuna hili wala lile, tulishitukia kundi la watu likivamia nyumba yangu ndipo waliponitendea unyama huu na kutoweka,” alisema.
AKIMBIZWA HOSPITALI YA MKOA SEKOU-TOURE
 “Baada ya unyama huo familia yangu na jamaa wa karibu kwa haraka walinikimbiza katika kituo kidogo cha polisi cha kata hiyo ambapo nilipata kibali cha matibabu (PF3) na kukimbizwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mwanza, Sekou-toure, ambapo nilipokelewa na kuingizwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.“Katika chumba hicho nilikaa kwa muda wa siku sita nikahamishiwa katika chumba cha wodi za kawaida.”

Mustafa akionyesha jeraha alilolipata mkononi.
MATIBABU YASHINDIKANA AHAMISHIWA CCBRT
“Baada ya hali yangu kuzidi kuwa mbaya, madaktari wa hospitali hiyo walinishauri kufanya utaratibu wa kwenda kupata matibabu zaidi katika Hospitali ya CCBRT Dar ambayo inasifika kwa kutoa huduma nzuri ya matibabu ya macho.

“Kama unavyoona sehemu kubwa niliyoathirika na tindikali ni usoni, kifuani na mgongoni! Mwanzoni kabisa macho yote hayakuwa yanaona ndipo nilipohamia CCBRT, ambapo angalau nimeweza kupata matibabu, namshukuru Mungu sasa jicho moja la kulia linaweza kuona kwa mbali.
KISA CHA KUMWAGIWA TINDIKALI
 “Kabla ya tukio hilo katika msikiti wetu kulikuwa na mgogoro kati ya waumini na viongozi wa msikiti.
Hatukuwa tunawataka ambapo baada ya mvutano wa muda mrefu uliosababisha kufikishwa  mahakamani baadhi ya watu, uchaguzi wa viongozi wengine ulifanyika chini ya uangalizi maalumu wa mahakama, baada ya kupatikana viongozi wapya nilipendekezwa kuwa imamu na nikawa naongoza sala za asubuhi.

Jeraha la kifuani.
“Kadiri siku zilivyozidi kusonga mbele, nilianza kujihusisha na shughuli mbalimbali za msikiti ikiwemo kufanya usafi wa mazingira  na kutunza baadhi ya rasilimali jambo ambalo lilionekana kutolifurahisha kundi la baadhi ya watu ambao hawakuwa wanaupenda huo uongozi mpya, ambapo kwa kile walichokiita kunikomesha ndipo walipoamua kunimwagia tindikali.
MSAADA
“Kutokana na hali mbaya ya kiuchumi niliyonayo, nawaomba Watanzania watakaoguswa na matatizo yangu kunisaidia ili niweze kupata huduma ya matibabu zaidi kwani hali yangu kiuchumi kwa sasa ni mbaya sana.

“Nawashukuru sana wote ambao wamenisaidia mpaka angalau nimekuwa katika hali hii, japo hali yangu bado haijawa vizuri sana hasa kimaisha, maana nimeshatumia fedha zangu zote kwa ajili ya matibabu na leo hii nafikia hatua ya kuomba kwa kuwa familia inanitegemea na haina namna tena, mtaji wangu wote umeishia katika matibabu.
“Kabla ya kufanyiwa unyama huu nilikuwa wakala wa mitandao ya simu na sasa changamoto yangu kubwa ni hali ya hewa ya jijini Dar es Salaam kuwa ya joto sana, hivyo napata maumivu sana kwenye majeraha yangu.
Jeraha la mgongoni.
MACHO
 “Hivi sasa matibabu ya macho bado yanaendelea ingawa nimeambiwa nirudi tena mwezi ujao (Juni) ambapo nimepewa uhamisho kwenda katika Hospitali ya Ocean Road kwa ajili ya kushughulikia tatizo la ngozi ambayo nayo imeharibika vibaya.

“Nilikwenda katika hospitali hiyo nikaambiwa kumuona daktari tu, natakiwa kutoa shilingi elfu hamsini, kiasi ambacho kwa sasa ni kikubwa sana kwangu maana nakosa hata shilingi mia mfukoni.“Ninayoyasema hapa ni rahisi kwa asiye jua hali yangu kuona kama natania ila ukweli ni kwamba hata fedha ya kwenda hospitali kumuona huyo daktari sina.
“Nawaomba Watanzania wanisaidie ili niweze kumuona daktari kisha nipate nauli ya kurudi Mwanza kukaa na familia yangu japokuwa siwezi kuihudumia. Changamoto ni kwamba baada ya mwezi natakiwa kurudi Dar kwa matibabu ya macho na ngozi.
“Nampongeza sana Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, Eric Shigongo kwa kuwa nami bega kwa bega tangu nipate tatizo hili na hakika yeye ni mtu mwenye upendo wa dhati, pia nawashukuru wote ambao wanaendelea kunijulia hali,” alisema Mustafa huku akilengwalengwa na machozi.
 Aliyeguswa na habari hii awasiliane naye kwa namba 0752 362 221, kutoa ni moyo.

UKATILI..!! MUME AMNYONGA MKEWE, KISA WIVU WA MAPENZI!

Stori: Waandishi Wetu INAUMA sana! Katika kinachoonekana kama ni wivu wa kimapenzi, dada mmoja aliyefahamika kwa jina la Magdalena Lucas ( 23) ameuawa kikatili na ‘mumewe’ aliyetajwa kwa jina la Stephano Lucas (28) nyumbani kwao maeneo ya Mbezi Luis jijini Dar es Salaam wiki iliyopita baada ya kupigwa na kitu kizito kichwani na mwili wake kufungiwa chumbani kwa siku tatu.
Magdalena Lucas enzi za uhai wake.
Akizungumza na gazeti hili, mmoja wa majirani wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Benson Boaz alisema, imekuwa vigumu kwao kujua chanzo hasa cha kifo cha msichana huyo aliyekuwa mfanyabiashara ndogondogo, ingawa alikiri kuwa mara kwa mara wanandoa hao walikuwa wakizozana kutokana na wivu uliokithiri wa mwanaume.
MUME ALIKUWA NA WIVU
“Mwanaume ambaye alikuwa fundi ujenzi, alikuwa na wivu uliovuka kiwango kwa Magdalena, alikuwa akimuwekea mipaka kuzoeana hata na majirani, huyu kijana hakutaka na alipomuona mkewe anajichanganya na watu hakupendezwa kabisa,” alisema.

Jeneza lililobeba mwili wa Magdalena Lucas likiandaliwa kwa ajili ya mazishi.
Aliongeza kuwa mara ya mwisho walimuona marehemu Ijumaa ya Mei 8 mwaka huu akiwa na mumewe lakini hawakuwaona tena na hawakuwa na shaka kwa kuwa mlango wao ulikuwa umefungwa kwa nje.
CHUMBA KUTOA HARUFU
“Jumapili jioni tukasikia chumba chao kikitoa harufu kali, ndipo tukapata hofu na kutoa taarifa polisi, walipofika na kuuvunja mlango, wakamkuta dada huyo ameuawa, akionekana kupigwa na kitu kizito kichwani maeneo ya usoni kiasi cha jicho lake kunyofoka. Hatujui kilichotokea maana hatukusikia kelele huenda kwa vile mvua nyingi ilikuwa inanyesha na mwanaume hajaonekana hadi leo,” alisema jirani huyo.

DADA HAMJUI SHEMEJIYE
Dada wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina moja la Asteria alisema kifo hicho ni pigo kubwa kwenye familia yao kwa kuwa tangu mdogo wake aanze kuishi na Stephano, hakuwahi kuwaonesha ndugu zake.

Mwili ukiagwa kwa ajili ya mazishi.
“Tangu mdogo wangu aanze kukaa na huyo shemeji,  sisi ndugu hatukuwahi kutuoneshwa tukamjua hata kwa sura, lakini majirani walijua kuwa ni mke wake, naumia sana, ni bora asingeamua kuishi naye kwani hakuwa na upendo wa kweli ndiyo maana kaweza kumfanyia ukatili wa aina hiyo,” alisema.
Marehemu ambaye hakubahatika kupata mtoto, alizikwa katika Makaburi ya Tandale kwa Ali Maua lakini ndugu na jamaa hawakupata nafasi ya kuuaga mwili wake kutokana na kuharibika.Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, ACP Camillius Wambura alisema habari hizo hazijamfikia lakini atafuatilia kwa kina tukio hilo ili hatua za kisheria ziweze kuchukua mkondo wake.

UKATILI WA KUTISHA..!! BABA MZAZI AKESHA AKIBAKA WANAYE!


Stori: Joseph Ngilisho, Arusha USHETANI! Watoto wa kike wawili wenye umri wa miaka 8 na 14, wakazi wa Unga Limited jijini hapa, wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa Mount Meru baada ya kuharibiwa vibaya sehemu zao za siri kwa madai ya kulawitiwa na kubakwa na baba yao mzazi waliyemtaja kwa jina moja la Ezekiel, Uwazi linakupa zaidi.
Watoto wanaodaiwa kubakwa na baba yao.
Akizungumza na gazeti hili kwa tabu hospitalini hapo, mtoto mwenye miaka 14 anayesoma darasa la nne, Shule ya Msingi Mkombozi (jina limehifadhiwa) alisema alianza kubakwa siku nyingi na baba yake huyo huku siku zingine akifanyiwa ukatili huo kwa usiku kucha huku akipata maumivu makali.
MSIKIE MWENYEWE
“Mimi na ndugu yangu tulikuwa tukiishi na baba na wadogo zangu wengine lakini baba alinihamishia mimi kwenye kitanda chake chumbani kwake nikawa nalala naye na akawa ananibaka usiku na asubuhi. Jua linapochomoza nilikuwa natoka,’’ alidai mtoto huyo.

“Nilikuwa naumia sana. Kila nilipoona usiku unaingia moyoni nilikuwa nikisema muda wa mateso umefika. Nilikuwa napenda kulala ili niamke kwenda shule, lakini baba alikuwa haniachii! Hali hiyo ilinifanya kesho yake nishinde nasinzia.”
ALIKUWA AKITUMIA VITISHO
Binti huyo aliongeza kuwa, pamoja na kuingiwa na akili ya kutaka kuwaambia majirani, lakini baba yake alimwendea  mbele kama alijua kwani kila alipomaliza unyama huo alimwambia angemchoma kisu kama angetoboa siri hiyo kwa watu au kwa mama yake mzazi.

KUMBE MAMA ALIFUKUZWA
“Mtu wa kumwambia matatizo hayo ni mama yangu mzazi ambaye baba alimfukuza nyumbani na alikuwa akiishi sehemu nyingine. Hata hivyo, nilipomwambia mama kwamba baba anatubaka, hasa mimi usiku kucha mpaka naamka nimechoka na siwezi kutembea, aliniambia nisijaribu kumwambia mambo hayo ya kijinga.”

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, SACP Leberatus Sabas.
KUBAKWA KUNAENDELEA!!
Binti huyo alitoa ya moyoni kuhusu kisa chake hicho cha kubakwa na kulawitia kwa kusema:
“Sijui ni nini?! Siku nyingine nikiwa na mdogo wangu tunayesoma naye shule, tuliitwa na babu mmoja anaitwa Elias. Tulikwenda hadi nyumbani kwake.

“Tulipofika, babu alitupa chipsi na kula. Halafu alimwambia mwenzangu atoke nje na kuanza kunibaka mimi. Alipomaliza, alimuita mwenzangu, naye akambaka. Alikuwa akitupatia chipsi kisha wakati wa kuondoka alitupa shilingi elfu mbili (2,000).
MARA TATU ZATAJWA
Uwazi lilipomuuliza binti mwingine wa miaka nane kuhusu kufanyiwa unyama huo, alisema: “Mimi babu Elias alinibaka mara tatu sehemu za mbele na sehemu za nyuma, akanipa shilingi elfu mbili na chipsi.”

MJUMBE WA MTAA AZUNGUMZA
Kwa upande wa balozi wa eneo hilo, Janet Tirisho alipoulizwa kuhusu ukatili huo, alisema kuwa alifanikiwa kuwaokoa watoto hao ambao walizoea kufanyiwa mchezo huo mchafu wa kubakwa kwa muda mrefu huku mama yao akidaiwa kupokea fedha kutoka kwa wanaye hao.Alisema sakata hilo walilifikisha Kituo Kikuu cha Polisi Arusha na watuhumiwa wakafunguliwa jalada lenye namba AR/RB/6252/2015- KOSA LA KUBAKA.

UCHUNGUZI WA KIDAKTARI
Daktari mmoja ambaye hakupenda jina lake kuandikwa gazetini alisema watoto hao wamefanyiwa uchunguzi na wamegundilika kuwa wameharibika vibaya sehemu zao za siri.

Naye Katibu wa Afya, Hospitali ya Mount Meru, Enjo Kimati, aliyezungumza kama msemaji wa hospitali hiyo alisema kuwa matukio ya ubakaji yameongezeka maradufu  kwani watoto wenye umri wa miaka mitano hadi 15 wamekuwa wakifikishwa hosptalini hapo na kugundulika wamebakwa na kulawitiwa.
KAMANDA WA POLISI
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, SACP Leberatus Sabas (pichani) amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema: “Tumefanikiwa kumtia mbaroni babu Elias lakini baba mzazi, Emmanuel Ezekiel alitoroka. Jeshi la polisi linamsaka ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria kujibu shitaka la kubaka linalomkabili.”

UKATILI..!! Watu 15 Wauawa Kwa Mapanga Geita !


WATU 15 wameuawa kwa kukatwa mapanga katika matukio tofauti mkoani Geita kwa imani za ushirikina.
 
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Joseph Konyo alisema matukio hayo ya mauaji yametokea katika  miezi mine kuanzia Januari hadi Aprili mwaka huu.
 
Konyo alisema  mauaji hayo yametokana na imani potofu za ushirikina na wahusika wakubwa wa matukio hayo ni waganga wa kienyeji wanaopiga ramli chonganishi.
 
“Kwa mwaka huu mpaka hivi sasa  tulikumbwa na matukio 15 ya mauji yaliyotokana na imani za ushirikina ambako katika wilaya tano kulikuwa na wastani wa watu watatu ambao waliuawa, lakini tunashukuru matukio haya tumepungua kwa sababu ya operesheni ya kuwasaka waganga,” alisema Konyo.
 
Wakati huohuo, Kamanda Konyo amethibitisha kuwa mtu mmoja, Lyoba Juma (23), mkazi wa Kijiji cha Milwa Butiama amefariki dunia kwa kugongwa na gari ya Land Cruiser mali ya Mgodi wa GGM iliyokuwa likiendeshwa na Yusuph Hashibeli.
 
Alisema tukio hilo lilitokea  ndani ya mgodi wa dhahabu wa GGM eneo la WD1 wakati  Juma  na vijana wenzake walipokwenda kupora mawe yanayodhaniwa kuwa na dhahabu.

Kamanda alisema  walinzi waliokuwa katika doria waliwafukuza na yeye aliteleza katika kifusi na kubiringika mpaka barabarani ndipo tairi za nyuma ya  gari hiyo ilipomkanyaga  kichwani.

Ukatili...!! Mwanafunzi auawa na BABA yake mzazi baada ya kukutwa na barua ya Mapenzi!

MWANAFUNZI wa Kidato cha Pili, Jofrey Robert Mwakatenya (15) Ameuawa kikatili na baba yake mzazi, Robert Mwakatenya (35) baada ya kumkuta akiwa na barua ya mapenzi, inayodaiwa aliandikiwa na rafiki wake wa kike.

Mzazi huyo ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa eneo la Majengo ‘D’ Manispaa ya Sumbawanga, anadaiwa kumwadhibu mwanafunzi huyo, ambaye ni mtoto wake wa kwanza kwa kupiga ngumi na mateke mfululizo kwa zaidi ya saa tatu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa , Jacob Mwaruanda alithibitisha tukio hilo, lilitokea usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita. Alisema bado wanamtafuta mtuhumiwa huyo kwani baada ya kufanya kitendo hicho alitokomea.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mwenyekiti wa Serikali Majengo D, Antony Nyambo alidai kuwa mzazi huyo alikuwa na tabia ya kumwadhibu mwanawe huyo, akimtuhumu kuwa ni mtoro wa shule .

“Nilitaarifiwa juu ya kisa hiki Jumapili saa mbili asubuhi baada ya kutoka katika ibada na raia mwema, ndipo niliamua kufika nyumbani kwa marehemu, nilimkuta akiwa amelazwa chumbani, nilipomfunua niliona akiwa ametapakaa vumbi mwili mzima huku akiwa amevaa nguo ya ndani tu,” alidai mwenyekiti huyo wa mtaa.

Inadaiwa kuwa usiku huo wa tukio, mtuhumiwa alianza kumwadhibu kumpiga ngumi na mateke kuanzia saa mbili usiku hadi usiku wa manane.

Mtoto huyo baada ya kupata kipigo hicho, alizimia ambapo baba yake alimwagia maji mwilini hadi akazinduka, kisha akamwamuru alale chumbani humo pamoja na mdogo wake.

Mzazi wa mtoto huyo alidamka alfajiri na kwenda kwenye chumba walicholala watoto hao na kugundua kuwa Jofrey alikuwa mfu.

“Ndipo baba huyo alipoaga nyumbani hapo, akidai kuwa anaenda kutafuta gari ili Jofrey aweze kupelekwa hospitalini kwa matibabu. Mzazi huyo hakurudi tena nyumbani kwake hadi sasa,” alibainisha.

UKATILI...!! BINTI NUSURA ABAKWE, AKATWA MAPANGA


SHANI RAMADHANI
KHAA! Binti aliyejitambulisha kwa jina la Elizabeth Sombe (13), mkazi wa Mafinga mkoani Iringa ambaye alikuja jijini Dar kwa ajili ya kufanya kazi za ndani, amelazwa katika Hospitali ya Taifa  Muhimbili (MNH) wodi ya Mwaisela namba mbili, Dar baada ya kucharangwa mapanga na kundi la vijana kufuatia kukataa kubakwa.
Elizabeth Sombe anayedaiwa kunusurika kubakwa.
Akizungumza na Amani juzi, Elizabeth alisema aliamua kuja Dar kufanya kazi baada ya kukatisha masomo yake akiwa darasa la sita kutokana na ugonjwa wa kifafa na hali duni waliyonayo nyumbani kwao.“Siku moja nyumbani alikuja rafiki yangu na kumwambia mama yangu kuwa amenitafutia kazi Dar hivyo nijiandae kuondoka naye. Nilijiandaa, nikaja Dar.
“Nilipokelewa na rafiki wa yule mama Neema ambaye anaishi huku, akanipeleka kwa mtoto wake anaitwa mama Junior. Ni Mbagala Rangi Tatu lakini naye anaishi maeneo hayohayo.“Nilianza kufanya kazi ikiwemo kumlea mtoto, kufua, kufanya usafi wa ndani na kupika lakini siku nyingine chakula cha mchana alikuwa akimtuma mtu atuletee nyumbani,” alisema Elizabeth.
Jeraha alilolipata baada ya kujeruhiwa na panga.
“Siku ya tukio, ilikuwa Jumatatu ya wiki iliyopita usiku nakumbuka, bosi wangu alinituma dukani kununua vocha usiku kama saa tatu hivi ndiyo nikavamiwa na vijana wanne, wakanifunga kitambaa usoni na kuanza kunivua nguo, nilijitahidi sana kupiga mayowe kuomba msaada kwa watu wa jirani na wao walipoona napiga mayowe wakaanza kunicharanga mapanga mpaka nikapoteza fahamu. Nilipokuja kuzinduka nilijikuta niko hapa hospitali asubuhi, sikujua nilifikaje,” alisema Elizabeth.
Aliendelea: “Sina msaada wowote ule kwani hata kurudi Mbagala naogopa na sitaki kumuona yule mama machoni mwangu maana sijamuona, naomba wasamaria wema wanisaidie kwani mpaka sasa sijui nikitoka nitakwenda wapi kwani tangu nimekuja Dar ni miezi miwili tu hata mshahara sijawahi kulipwa. 
Jeraha la mguuni.
“Nahitaji msaada wa nauli na mavazi kwa kuwa sina nguo na hata zile nilizokuwa nimezivaa siku ile zilikuwa zimechanika zote, bora nirudi nyumbani nikamsaidie mama kwani nilimuacha akiwa mgonjwa na sijui anaendeleaje maana ana ujauzito uliopilitiza miezi na alikuwa mbioni kufanyiwa operesheni.”

Kwa yeyote aliyeguswa kumsaidia binti huyo ili aweze kurejea kwao Iringa, anaweza kutuma pesa kwa namba 0712 121330.

UNYAMA...!! MUUGUZI AMCHAPA MJAMZITO VIBOKO..NI WAKATI WA UCHUNGU WA KUJIFUNGUA, MTOTO AFIA TUMBONI.

Muuguzi mmoja wa zahanati ya Muungano, Chamwino, mkoani Dodoma, amekumbwa na kashfa nzito baada ya kudaiwa kumchapa viboko mama mjamzito, wakati akiwa katika hali ya uchungu wa kujifungua na kusababisha mtoto aliyetaka kujifungua kufariki akiwa tumboni.

Aidha, mama huyo ambaye kwa sasa amelazwa katika chumba cha uangalizi maalumu (ICU) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, hali yake inaelezwa kuwa mbaya.

Mwanamke huyo, Mariamu Maroda, anadaiwa kulazwa kwenye chumba hicho kwa zaidi ya wiki moja, ambapo pamoja na kufanyiwa upasuaji, hakufanikiwa kupata mtoto wake akiwa hai.

Akisimulia mkasa huo, mama mdogo wa Maroda, Joyce Charles, alisema Aprili 3, mwaka huu Saa 12:00 jioni, walimpeleka zahanati ya Muungano akiwa na dalili za kujifungua na kupokelewa na muuguzi aliyemfahamu kwa jina la Lucy.

“Nilishuhudia Lucy akimchapa Maroda viboko kwenye mapaja na mgongoni, akisema ana uwezo wa kujifungua lakini anadeka tu, nilishindwa kuingilia nikihofia asimdhuru zaidi mwanangu, ila nilihuzunika sana,” alisema.

Alisema muuguzi huyo alitumia fimbo tatu kumchapa mgonjwa wake, ambazo alikuwa akizitumia kila moja inapovunjika. Alisema fimbo hizo zilipomalizika, alianza kumfinya kwenye mapaja kwa kutumia rula.

“Kesho yake saa 12:00 alfajiri, huku hali ya mgonjwa ikiwa mbaya, walitupatia gari likatupeleka hospitali ya Mvumi Misheni, ambako walisema hali aliyokuwa nayo mgonjwa wasingeiweza na kutuelekeza tumpeleke hospitali ya rufaa, lakini walimpa mgonjwa chupa mbili za damu,” alisema.

Alisema Maroda alifikishiwa chumba cha upasuaji na kisha alilazwa wodi namba 17, lakini miguu na tumbo vilianza kuvimba na alipochunguzwa ikabainika ana usaha tumboni, hivyo aliamriwa arudishwe kwenye chumba cha upasuaji.

 “Yaani ukimuona, mwilini ana alama za fimbo na kufinywa. Sasa walipomfanyia upasuaji kwa awamu ya pili, alipelekwa ICU mpaka hivi tunavyozungumza ni zaidi ya wiki moja,” alieleza Charles.

Viongozi wa Hospitali ya Rufaa, wenye mamlaka ya kuzungumzia suala hilo walionekana ‘kurushiana mpira’ walipotakiwa kuelezea suala hilo. Hata hivyo, Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anatoria Mkindo, alikiri kuwepo kwa mgonjwa huyo.

Awali Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Zainab Chaula, alisema hakuwa na taarifa za kina kuhusu Maroda.

Mkindo alisema walikuwa wameagiza Ofisi ya Mganga wa Wilaya wa Chamwino, kuwapelekea taarifa kuhusu suala hilo.

Alisema pia wametaka Ofisi ya Mganga Mkuu wa mkoa, ifahamishwe hatua zilizochukuliwa dhidi ya mtumishi aliyedaiwa kumchapa viboko mjamzito huyo.

“Mimi sio msemaji, anayetakiwa kuwapa taarifa kamili ni RMO (Chaula) kwanini awalete kwangu, nilichowaeleza ni ambacho nafahamu lakini siyo msemaji, nashauri muende ofisini kwa matroni wa hospitali mtapata taarifa kamili,” alisema.

Afisa Muuguzi wa ICU, Christina Mlumba, alisema, Maroda alipelekwa ICU baada ya kufanyiwa upasuaji na kwamba hali yake inaendelea vizuri.

Mdogo wa Maroda, Silika Mkwawi alivieleza vyombo vya habari kuwa ingawa hakuingia kwenye chumba cha kujifungulia katika zahanati ya muungano, dada yake alipotolewa nje, muuguzi alimueleza kuwa alimchapa fimbo mbili tu, kwa sababu ya kudeka kwake.

KIJANA AMCHINJA MAMA YAKE MZAZI NA KUTOA TAARIFA UONGOZI WA KIJIJI..!!


Jeshi la Polisi mkoani Singida, linamshikilia Jumanne Yusuph (33), Mkazi wa Kijiji cha Mtamaa ‘A’ Manispaa ya Singida kwa kumuua mama yake mzazi, Tausi Abdalah (56) kwa kumchinja na kisu shingoni, juzi alfajiri katika kijiji hicho.
Baada ya kumchinja mama yake, kijana huyu alikwenda kwa mama yake mkubwa kutoa tarifa, kisha tena akaenda kwa mwenyekiti wa kijiji kumjulisha kuwa amefanya mauaji ya mama yake.
Kabla ya mauaji hayo, mtuhumiwa huyo aliwaua ng’ombe watatu wa mama yake kwa kuwacharanga na mapanga.
Pia inadaiwa kuwa aprili 16 mwaka huu, mtuhumiwa huyo alifika kwa mama yake na kubomoa sehemu ya nyumba yake kisha akatokomea kusikojulikan

KAMA UNA ROHO NDOGO HUWEZI KUTAZAMA HIZI PICHA.LAKINI HIVI NDIVYO UHAI WA MWANAMKE HUYU ULIVOKATISHWA KINYAMA.

 
Wiki iliyopita tuliongea katika leo tena juu ya kisa cha Marehemu Nasra pichani.Mama huyu alikuwa mkazi wa Bunda mkoani Mara lakini Dar es salaam alifika kufanya matibabu katika hospital ya Muimbili.Kwa miaka takribani 23 alikuwa mke wa bwana Elia Makumbati na kujaaliwa kupata watoto wanne mkubwa kabisa yupo chuo kikuu cha UDOM.Kwa miaka yote wamekuwa na misuko suko sana kwenye ndoa mama akiwa anapigwa sana hata kuchanwa na viwembe.
 
Mwezi wa pili walitofautiana baada ya bwana kuoa mke mwingine.Wakiwa wametofautiana na Nasra kuendelea na maisha siku hiyo bwana akamfata akamkuta barabarani anatoka kazini.Akiwa na rafiki yake wanatembea akamfungia breki mguuni akamwambia anataka kuongea nae.Nasra akakataa akamwambia kama kuna maongezi hawezi kuongea nae kama vipi amfate nyumbani huku anaendelea kutembea.Bwana yule akamfata kwa nyuma akamgonga na gari na baada ya Nasra kuanguka akanasa chini hivyo kuendelea kumburuza umali wa kama mita 150 hivi.Alipofika kwenye tuta akanasuka bwana ndio kushuka kwenye gari kukimbia.
 
Kiukweli aliumia sana sana ngozi yote ya mgongoni,mbavuni,makalio,ikavuka na kubaki kwenye lami.Sikio lake la kushoto lote likaliwa na lami,mbavu 7 zilivunjika pamoja na mguu.Akapelekwa hospitali na baadae kulazwa Bugando Mwanza lakini ikawa anahitajika kuhamishiwa hospital ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.Akiwa muhimbili alikuwa na hali mbaya sana baadae ikathibitika kuwa ameumia ndani kwa ndani kwani alibadilika sana akavimba  na kuwa mweusi.Kwamuda wote wa miezi takribani sita alikuwa katika maumivu makali na bahati mbaya hakuweza kupambana tena kupigania maisha yake.
Nasra pichani kulia mwenye kilemba chekundu akiwa na ndugu zake wakati akiwa mzima.
Usiku wa kuamkia jumanne ya tarehe 10 Nasra akaaga dunia.Ilikuwa ni huzuni sana jinsi alivyoteseka na namna mazingira ya kifo chake kilivyotokea.Tulikuwa na matumaini kuwa angeweza kupona maana dakika za mwisho alikuwa anaongea japo kwa shida.
Tunaomba mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Nasra mahala pema peponi,Amina.
Hii ni picha ya muwewe Elia Makumbati ambae mpaka sasa anatafutwa na jeshi la polisi kwa kitendo cha kinyama alichokifanya.Jeshi la polisi mkoani Mara wanafanya juhudi za kila namna kumkamata lakini amekuwa akikimbia mara aonekane Kenya,Botswana na kwengineko lakini bado hajakamatwa.Kwa utakae muona usisite kutoa ripoti zake.Mpaka askari wa upelelezi wa kimataifa interpol ina taarifa zake.

Baba Ahukumiwa Kifungo cha Maisha Jela Kwa Kosa la Kumbaka Mtoto wake Wa Miaka 9 na Kumsababishia Ujauzito !


Mahakama ya Hakimu Mkazi wilaya ya Shinyanga imemhukumu kifungo cha maisha jela mkazi wa mtaa wa Kitangili katika manispaa ya Shinyanga baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka na kumpa ujauzito mtoto wake wa kambo, mwanafunzi wa darasa la tatu.
 
Alimbaka mtoto huyo kutimiza masharti ya mganga ili kutoa tiba kwa mkewe.
 
Akisoma hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi mwandamizi wa wilaya, Thomson Mtani alisema mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka ukiongozwa na wakili wa serikali, Judith Tuka.
 
Mtuhumiwa Osward Charles (45) mkazi wa Kitangili alifikishwa mahakamani kwa tuhuma mbili. Kosa la kwanza likiwa ni kumbaka mtoto wake mwenye umri chini ya miaka kumi ambaye ni mwanafunzi kinyume na kifungu namba 130, kifungu kidogo cha kwanza na cha pili na kifungu namba 131 kifungu kidogo cha pili cha sura ya 16 cha kanuni ya adhabu.
 
Kosa la pili ni kumwingilia kimwili mtoto wake ambaye ni mwanafunzi wa shule na kumpa ujauzito kinyume na kanuni ya tano ya sheria ya elimu ya mwaka 2003 inayotoa adhabu kwa watu wanaowaoa na kuwapa mimba wanafunzi wa shule kama ilivyo katika kifungu cha 35 kifungu kidogo cha tatu cha sheria ya elimu ya 353.
 
Ilidaiwa na mwendesha mashtaka mwanasheria wa serikali Judith Tukakuwa, kati ya Novemba 12 mwaka 2012 na Septemba katika eneo la mtaa wa Kitangili manispaa ya Shinyanga mshitakiwa alimbaka mtoto wake wa kambo ambaye ni mwanafunzi mwenye umri wa miaka tisa na kumsababishia ujauzito.
 
Awali mshitakiwa katika mwenendo wa kesi alikana kutenda makosa hayo lakini katika utetezi wake mbele ya mahakama kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo ili mahakama impunguzie adhabu alikiri kumbaka mtoto wake mbele ya mama yake mzazi kwenye kitanda kimoja baada ya kupewa maagizo ya mganga wa jadi kama sehemu ya tiba ya mke wake aliyekuwa akisumbuliwa na maradhi.

UKATILI! AMUUA MTOTO WAKE KWA KUSHAURIANA NA MUMEWE MPYA BAADA YA NDOA YAKE YA KWANZA KUVUNJIKA!

Ice Axe, aina ya shoka ambalo Gonzalo alimpigia mtoto huyo. 
Tunaona ndoa nyingi zinavunjika, kila mtu anaenda upande wake alafu maisha yanandelea.. Mara nyingi waathirika wa matukio ya aina hii ni watoto, hii ishu imetajwa mara nyingi pia kwamba inasababisha sana kuwepo kwa ongezeko la watoto wa mitaani kila siku.

Hii ni ya kusikitisha kidogo, mwanamke mmoja Mexico ambaye jina lake ni Karina Luna Sandoval hakuna na raha kwa kitendo cha kutelekezwa na mzazi mwenzake ambaye walizaa nae mtoto mmoja ambaye alikuwa tayari ana umri wa miaka 7.

Akampata mpenzi mwingine, Gonzalo del Rio Hernandez wakashauriana eti waandae zawadi ambayo watampa jamaa ambaye alimzalisha mwanamke huyo na kumtelekeza.. walivyoshauriana wakaona zawadi ambayo jamaa hatoisahau ni kumuua mtoto huyo.

Akampeleka mtoto huyo kwenye bustani akamwambia amsubiri baba yake anakuja, hiyo ilikuwa December 20 2015, akatokea Gonzalo na shoka dogo akaanza kumpiga mtoto huyo kwa lengo la kumuua.

Watu walisikia kelele za mtoto huyo akiwa analia, wakafanikiwa kuwakamata mwanamke huyo pamoja na mpenzi wake huyo ‘mpya’, Ambulance ikamchukua mtoto kumpeleka Hospitali, lakini kwa bahati mbaya wiki mbili baadae akafariki.
Karina na Gonzalo walikiri kufanya kosa hilo, hukumu iliyotolewa na Mahakama ni kifungo cha miaka 42 jela kwa Karina na mpenzi wake huyo amefungwa kifungo cha miaka 40.

Mwanamke Afanyiwa Ukatili Wa Kutisha Na Mume Wake...Achomwa Moto Kwa Petrol, Mtoto Wa Mwezi Mmoja Afariki Dunia


Machi 31 mwaka huu, mwanamke mmoja mkazi wa Bwai wilayani Butiama, Kudra Nanja alifanyiwa ukatili na mumewe wa kuchomewa ndani ya nyumba kwa petroli, tukio lililosababisha mtoto wake Tatu Simioni aliyekuwa na umri wa mwezi mmoja u nusu kufariki dunia.

UKATILI...!! MUME AMWAGIA MKEWE UJI WA MOTO KIFUANI, AMUACHA AKIOZA NDANI NA YEYE KUTOKOMEA


HUU ni ukatili uliopitiliza! Mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Neema Mwita, anateseka katika Hospitali ya Mkoa wa Mara kufuatia jereha kubwa alilopata baada ya mumewe aliyemtaja kwa jina la Juma Mwita kummwagia uji wa moto kisa kikiwa ni kuchuma mahindi shambani bila ridhaa ya mumewe huyo.Akizungumza na Uwazi huku akimwaga machozi kila wakati, mwanamke huyo alisema siku ya tukio, yeye na mumewe walikuwa kazini na mwanaume huyo ambaye alipata tenda kubwa ya kufyatua matofali.

 
Neema Mwita akihojiwa.
MSIKIE MWENYEWE
“Nilikuwa nakusanya majani. Baada ya kukusanya kwa muda mrefu ambapo niliagizwa na mume wangu, niliamua kwenda shambani kuchuma mahindi kisha nikarudi nyumbani kupika chakula cha mchana ili akitoka kazini ale.

“Nikiwa jikoni nasubiri uji uchemke ili nisonge ugali, mume wangu alirudi ghafla na kuanza kunigombeza eti kwa nini nilichuma mahindi shambani na nilirudi nyumbani bila ridhaa yake?” alisema na kuanza kulia.
MUME ACHUKUA UJI WA UGALI
Mwanamke huyo aliendelea kusema: “Alinihoji ni kazi gani kubwa niliyoifanya kule kwenye matofali mpaka nikaamua kurudi nyumbani. Kabla sijajibu aliifuata sufuria yenye uji unaochemka jikoni na kunimwagia ambapo ulitua kifuani kwangu na kuniunguza vibaya, kama unavyoona. Sijajua mume wangu alikusudia nini kunifanya hivi!”

JIRANI AMWOKOA
Mwanamke huyo aliendelea kusema kuwa, baada ya kumwagiwa uji huo na kuungua, alianguka chini na kulia kwa maumivu, ndipo jirani yake mmoja alimwona akihangaika na kumchukua hadi ndani.

AKAA NYUMBANI SIKU SABA
“Ndani nilikaa kwa wiki nzima, maumivu yalikuwa makali sana. Ndipo wazazi wangu walipopata taarifa wakaja kunichukua. Hata hivyo, wazazi wangu nao hawakunipeleka hospitali, waliniweka nyumbani na kuniletea mganga wa kienyeji.”

 
Mwandishi akizidi kumuhoji Neema Mwita.
MUME AKIMBILIA KUSIKOJULIKANA
Neema alisema mumewe aliyeoana naye kwa upendo na kiapo cha kuishi katika shida na raha mpaka kufa, alikimbia baada ya tukio hilo na hajawahi kuonekana mpaka sasa ambapo polisi wanaendelea kumsaka usiku na mchana.

TAARIFA ZINAFIKA SERIKALINI
Mwanamke huyo ambaye kutokana na kuungua huko mishipa yake ya sehemu ya kidevuni imeshikana na ya shingo, alisema baada ya wiki moja, taarifa zilimfikia Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyamisanga, Boke Chacha ambaye alimchukua mikononi mwa wazazi hao na kumpeleka hospitali kwa matibabu.

LICHA YA KUUNGUA, AMETELEKEZWA
Neema, anasikitisha sana kwani licha ya kupitia kipindi hicho kigumu, anadai ametelekezwa na wazazi wake  na mtu anayemsaidia ni mwanaye wa kiume anayeitwa Wambura Juma aliyekuwa akisoma kidato cha tano.
“Mtoto wangu huyu kwa sasa hasomi kwa sababu ya kunisaidia mimi, alilazimika kuacha masomo toka tukio hili liliponitokea,” alisema Neema.

ANA MIEZI NANE HOSPITALINI
Neema anasema tangu alazwe hospitalini hapo, sasa ni mwezi wa nane lakini anamshukuru Mungu ameanza kujikongoja kutembea japo kwa taabu sana.


Muonekano wa jeraha alolipata Neema baada ya kuunguzwa na mumewe kwa uji wamoto.
MADHARA ALIYOYAPATA
Neema amepata madhara makubwa kufuatia tukio hilo kwani kwa sasa mkono wa kulia haukunjuki sawasawa kama zamani, hawezi kunyoosha shingo kutokana na nyama za shingo kuungana na kidevu, mdomo wake umepinda kidogo huku titi la upande wa kulia likiwa halipo tena!

APATIWA SIMU YA MKONONI
Joyce Kiria ni Mtangazaji wa Kipindi cha Wanawake Live kinachorushwa hewani na Runinga ya EATV, alimtembelea Neema hospitalini na kumpa msaada wa simu ya mkononi ili iwe rahisi kwa wale watakaojitokeza kutaka kumsaidia kwa ajili ya pesa za matibabu kutumia simu hiyo.

ANAHITAJI MSAADA
Ndugu msomaji, Neema anahitaji msaada wako wa hali na mali. Kama utakuwa na chochote na umeguswa na maumivu yake, unaombwa kutumia mawasiliano yake  0656 151 072 au 0756 768 305.

Ukatili aliofanyiwa mwanamke mwenye ujauzito wa miezi saba..!! Soma hapa

26C9C97600000578-3001792-image-m-34_1426741619536Mwanamke mmoja Michelle katika jimbo la Corolado Marekani amepoteza kichanga chake baada ya mwanamke mmoja kumchoma kisu tumboni na kuchukua kichanga chake kilichokuwa na miezi saba.
Dynel Catrece Lane ndie mwanamke ambaye ametajwa kuhusika na kosa hilo, alimchoma mwanamke huyo kisu tumboni na kumtoa kichanga hicho halafu akakimbia kwenda Hospitali akidai kwamba ametokwa ujauzito, wakati huo alikuwa amekishika kichanga hicho mkononi kikiwa kimefariki.
Dynel-Catrece-Lane-
Dynel Catrece Lane
Baada ya Lane kufanya tukio hilo na kukimbia, Michelle alipiga simu ya dharura 911 kuomba msaada; “amenichoma tumboni.. nina ujauzito..
26C9C9E800000578-3001792-Police_hoped_to_gain_access_to_the_home_on_Wednesday_night_using-m-3_1426791815762
Polisi wakiwa eneo la tukio
Michelle alifikishwa Hospitali na kuendelea kupatiwa matibabu ya majeraha aliyochomwa kisu na mwanamke huyo.
Lane amefunguliwa mashtaka matatu, kosa la kuua, kutesa na kosa la kukiuka haki za watoto.

UKATILI! MTOTO MIAKA 16 AMBAKA MTOTO WA DADA YAKE MWENYE MIAKA 3

JESHI la Polisi mkoa ni Kilima njaro, linamshikilia kijana mwenye umri wa miaka 16,mkazi wa Sabuko, Wilaya ya Siha ,mkoani humo kwa tuhuma za kumbaka mtoto wa dada yake mwenye umri wa miaka mitatu(wote majina yanahifadhiwa).

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo, Koka Moita, alisema mtuhumiwa anadaiwa kumbaka mtoto huyo nyumbani kwao na kumsababishia maumivu makali sehemu zake za siri.

"Tukio hili limetokea saa 10:45 alasiri,wakati mama wa mtoto huyo akiwa ametoka nyumbani kwenda kwenye shughuli zake za kujitafutia riziki na kumuacha mtoto na mjomba wake ndipo mtuhumiwa alitumia muda huo kufanya kitendo hicho cha kikatil i na kinyama," alisema Kamanda Moita.

Aliongeza kuwa,mama wa mtoto huyo aliporudi nyumbani jioni,alimkuta mtoto wake akilia kutokana na maumivu makali na alipomchunguza akabaini alibakwa.

"Baada ya kubaini mtoto wake amebakwa, alitoa taarifa polisi ambao walimkamata mtuhumiwa na kufikishwa Kituo cha Polisi kwa mahojiano kabla yakufikishwa mahakamani," alisema.

Kamanda Moita alisema kwa sasa mtoto huyo anaendelea na matibabu katika Hospitali ya KibongĂ­to, iliyoko wilayani humo ambapo jeshi hilo linaendelea na uchunguzi.

Alitoa wito kwa wazazi na walezi kuwa waangalifu na watoto wao kutokana na matukio ya ubakaji hususani kwa watoto kuongezeka siku hadi siku.

"Awali matukio ya ubakaji hayakuwepo hapa Kilimanjaro tofauti na sasa...tatizo hili linachangiwa na ukosefu wa maadili kwenye jamii, tabia hii inapaswa kukoma mara moja," alisema.

UKATILI...!! Mama amkata mwanaye nyama ya paja, achoma kama mshikaki huko mkoani Kilimanjaro!!

Mwanamke mmoja Kilimanjaro amekamatwa na polisi akidaiwa kumkata mtoto wake mwenye umri wa miaka nane nyama ya paja na kuichoma mithili ya mshikaki.
Mwananmke huyo aliyetajwa kwa jina la Dafrosa Massawe anadaiwa kufanya unyama huo mwishoni mwa wiki na majirani wanasema mama huyo alifanya hivyo akiwa amelewa.
Kamanda wa Polisi Kilimanjaro Koka Moita alisema mwanamke huyo ataendelea kushikiliwa hadi uchunguzi wa tuhuma hizo utakapokamilika kabla ya kupelekwa mahakamani.
Akizungumza na Gazeti la MWANANCHI katika hospitali ya Kibosho mtoto huyo alisema hafahamu kosa alilofanya hadi mama yake ambaye ni mtengenezaji wa pombe za kienyeji kumfanyia kitendo hicho.
Alisema mama yake alirudi nyumbani usiku na kumkuta amekaa na kumsalimia kisha akamwomba chakula wakati akijua hakuna na baadae aliingia jikoni na kuchukua kisu kisha kumkata nyama kwenye paja lake baada ya kumwambia alishinda na njaa siku nzima.
Alisema baada ya kuikata aliichoma kama mshikaki na ilipoanza kufuka moshi na kutoa harufu aliitoa jikoni na kumwekea mtoto huyo puani ili avute harufu yake.

UKATILI! Mwanamke Apigwa Mawe Hadi Kufa Huko Somalia Baada ya Kufanya Mapenzi Nje ya Ndoa

Mwanamke mmoja ameuawa kwa kupigwa mawe nchini Somalia na kundi la wanamgambo wa Al Shabaab.
Ripoti zinasema kuwa takriban watu 200 akiwemo gavana wa eneo hilo walishuhudia watu wakimpiga mawe mwanamke huyo kwenye mji wa Barowe.
Mwanamke huyo wa umri wa miaka 30 alikuwa ameshutumiwa kwa kufanya mapenzi nje ya ndoa.
Wadadisi wanasema kuwa mauaji hayo ini ishara ya ushawishi wa kundi la Al shabaab hata baada ya kushambuliwa na serikali ya Somalia pamoja na vikosi vya muungano wa Afrika.
MAWE
Mji wa Barowe ambao uko umbali wa kiomita 200 kutoka mji mkuu Mogadishu umekuwa ngome ya Al Shabaab.

UKATILI! Mvuta Bangi Aua Watu watatu na kumjeruhi mmoja kwa panga na mkuki huko Geita

Matukio ya mauaji ya watu wasio na hatia, yameendelea kuuandama Mkoa wa Geita, kufuatia watu watatu kuuawa kwa kukatwa mapanga na kuchomwa mkuki huku mmoja akijeruhiwa baada ya mtu mmoja anayesadikiwa ni mgonjwa wa akili kutekeleza unyama wake.
Tukio hilo lililotokea jana asubuhi katika kijiji cha Nyamilyango wilayani Geita, na  aliyejeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Geita ni Mathayo Sindamsanga, na hali yake imeelezwa ni mbaya. Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Adam Sijaona, alithitibisha kupokea miili mitatu iliyohifadhiwa hospitalini hapo pamoja na majeruhi mmoja.
kisu
Dk. Sijaona aliwataja waliouawa kuwa ni Pindo Makono, Ndakazi Bertha Masabile na Jacob Bukulu, ambao ni wakazi wa kijiji hicho.
Hata hivyo, mtu huyo aliyesababisha mauaji hayo, alikamatwa na wananchi wenye hasira na kisha kumfikisha kituo cha polisi.
Dk. Sijaona alisema marehemu hao walifariki dunia kutokana na kuvuja damu nyingi mwilini kufuatia muuaji kutumia panga na kuwacharanga na kisha mkuki kuwatoboa miili.
Akizungumzia tukio hilo, Diwani wa Kata ya Bugulula, Elisha Lupuga, alisema lililotokea juzi saa 1:00 jioni katika kitongoji cha Misheni katika kijiji cha Nyamilyango baada ya mtuhumiwa, Rashid Ramadhani, mkazi wa kijiji hicho kutumia mkuki na panga kuwaua watu hao.
“Dhamira yake mpaka sasa haijafahamika ilikuwa nini, lakini amekuwa na tabia ya kuvuta bangi  kwa muda mrefu, hivyo tunahisi amevurugukiwa akili yake,” alisema Lupuga.
Hata hivyo, Lupuga alisema baadhi ya waliouawa walikuwa na mahusiano na mtuhumiwa, lakini hakufafanua ni mahusiano ya namna gani waliyokuwa nayo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Geita, Joseph Konyo, alithibitisha kutokea tukio hilo na kwamba mtuhumiwa anashikiliwa katika kituo cha polisi akisubiri hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi yake.
Tukio hilo limeibua upya simanzi na vilio kwa wananchi wa mkoa huo ambao mara kwa mara wamekuwa wakikumbwa na matukio ya mauaji ya aina mbalimbali.

Hilo ni tukio la pili ndani ya wiki moja baada ya usiku wa kuamkia Septemba 7, mwaka huu, watoto wanne wa familia moja kuuawa kufuatia nyumba yao kuteketezwa na moto katika kitongoji cha Elimu kata ya Kiangalala wilayani Geita.
Watoto walioteketea na moto huo ni Reginald Robert (9) mwanafunzi wa darasa la nne na Sofia (6) wa Shule ya Msingi Ukombozi na Remijius (4) wa chekechea pamoja na Scolastika (15) aliyekuwa akisoma shule ya sekondari Mwatulole.
Katika tukio hilo, baba wa familia, Robert Reginald (49), mkewe Angelina Reginald na watoto Robert mwenye umri wa miaka miwili na miezi mitatu na Yohana (1), walinusurika katika janga hilo.
Older Posts
© Copyright ZEE LA UDAKU | Designed By Code Nirvana
Back To Top