Habari Kali
Loading...

Wema Sepetu na Mpenzi wa Linah Kunani?? Picha yao ya Kimahaba yanaswa Mtandaoni

Wema na Mpenzi wa Linah
Nadhani hatuna haja ya kueleza zaidi ni maeneo gani hiyo picha itakuwa imepigwa. Wewe mwenyewe unaweza kuwa shahidi wetu. Pichani ni mwanadada wetu Wema Sepetu na kijana aliyetajwa kuwa ni mpenzi wa mwanamuziki linah sana.  Hatujui kinachoendelea mpaka sasa, yawezejana ni video mpya inafanyiwa promo, yawezekana ni tangazo la TV au bidhaa mpya mtaani na wala haituhusu,  Ila tumeona si vyema tusipowaletea kinachojiri hivi sasa kati ya hao wawili.

Sisi yetu macho.

WEMA AONESHA MAHABA NIUE LIVE

Musa Mateja LIVE! The Big Boss wa Kampuni ya Endless Fame Productions, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amejikuta akionesha mahaba niue kwa ‘kujibebisha’ kwa Mshiriki wa Big Brother Africa ‘Hotshots’ 2014 kutoka nchini Namibia, Luis Manana huku akimmwagia sifa nyingi na kudai ndiye laazizi wa moyo wake kwa sasa baada ya kuachana na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’.
The Big Boss wa Kampuni ya Endless Fame Productions, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ akiwa na Mshiriki wa Big Brother Africa ‘Hotshots’ 2014 kutoka nchini Namibia, Luis Manana.
TUJIUNGE VIWANJA VYA POSTA
Tukio hilo lililoshuhudiwa na gazeti hili lilijiri ndani ya Viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar, wikiendi iliyopita kwenye Shoo ya Instagram Party ambapo Wema alikuwa mmoja wa washiriki wa tamasha hilo lililohudhuriwa na mamia ya mashabiki hivyo walipata mshtuko waliposikia habari hizo njema kutoka kwa Madam.

AMMWAGIA SIFA KEDEKEDE
Akiwa kwenye pati hiyo, Wema alipanda stejini kwa ajili ya kuongea na mashabiki wake na baadaye alipanda Luis ndipo Madam akaanza kummwagia sifa kedekede na kabla ya kumtambulisha rasmi kuwa ndiye ubavu wake.
Kwa kinywa chake bila kumung’unya maneno, Wema alidai kwamba Luis ndiye mwanaume ampendaye kwa sasa hasa akivua shati lake kwani ana vitu adimu ambavyo vinamfanya asimruhusu kuwa mbali naye.

LUIS NAYE
Baada ya sifa hizo, Luis naye alisema kuwa alipanda ndege kutoka Namibia hadi Dar kwa ajili ya kuja kujumuika na mwanamke ampendaye ambaye ni Wema.

Wema na Luis Manana wakifuatilia jambo.
TEAM WEMA FULL SHANGWE
Utambulisho huo ulizua shangwe nyingi kutoka kwa mashabiki hasa Team Wema ambao kwa pamoja walionesha kusapoti uhusiano huo na hata baada ya kushuka walionekana kuwazonga huku wakipigana vikumbo kwa ajili ya kutaka kila mmoja kupiga nao picha. “Sisi Team Wema tumepitisha ile Team Haters (timu ya wenye chuki) wakale malimao kama alivyosema Gwajima (Askofu Josephat) kwamba kama kuna watu hawampendi Lowassa (Edward) basi wakale malimao,” alisikika mmoja wa Team Wema.

NI KWA MARA YA KWANZA BAADA YA DIAMOND
Usiku huo ulikuwa wa kwanza kwa mwaka huu kumuona Wema akimtambulisha mwanaume kwa mara ya kwanza kwenye tamasha kubwa kama hilo tangu alipoachana na Diamond ambaye kwa sasa anajivinjari na mwanamama Zarinah Hassani ‘Zari The Boss Lady’.Kuna madai kwamba baada ya wawili hao kuwa beneti tangu waliposhuka jukwaani walikwenda kulala hoteli moja kwa mujibu wa wafuatiliaji.

WALILALA WOTE HOTELINI
Chanzo chetu cha habari kilichokuwa ndani ya hoteli hiyo (jina linahifadhiwa) kilidai kwamba siku hiyo Wema na Luis waliingia hotelini hapo na kulala hadi kesho yake, jambo ambalo lilikuwa siyo kificho tena hasa kwa wahudumu na watu wote walioongozana na msafara wa wawili hao. “Kweli kabisa Luis anatoka kimapenzi na dada yetu Wema maana nimeshuhudia tangu jana, Wema alikuja hotelini na baadaye wakaondoka wote.

...Wakikumbatiana kimahaba.
“Hata usiku wakati wanatoka Viwanja vya Posta pale Kitonyama walirudi na kulala pamoja, achilia mbali hiyo, Wema na Luis ni watu ambao wanaonekana kuwa katika mapenzi kwa muda sema tu Luis alikuwa hajapata nafasi ya kuja Dar,” kilisema chanzo hicho.
KUMBE LUIS ANAJUA KISWAHILI!
Baada ya kujiridhisha na uwepo wa uhusiano wa wawili hao, mwanahabari wetu alifuatilia kwa makini baadhi ya akaunti zinazotumiwa na Luis kwenye mitandao ya kijamii ambapo aligundua kuwa jamaa huyo amekuwa akimuweka Wema kwenye peji zake huku akimmwagia sifa na maneno ya kimahaba tena kwa Lugha ya Kiswahili.

Baadhi ya maneno aliyokuwa ameandika Luis katika peji yake ya Instagram akiambatanisha na picha zao yalisomeka: “Najaribu kumtuliza... Mtoto mzuri.“Huyu msichana anaweka tabasamu usoni mwangu.”

AUNT: SITAMZIKA WEMA SIKU AKIFA! WEMA NAYE AJIBU MAPIGO

Musa mteja
‘Nikifa usije kunizika, ukifa sitakuzika’! Ni maneno makali sana kuyatamka kiasi kwamba, enzi za wahenga ilipotokea ndugu, marafiki au majirani wakaapishana kwa maneno hayo, walitafutwa wazee wenye hekima ili kuondoa laana hiyo.
Msanii wa sinema Bongo movie Aunt Ezekiel Grayson.
Sasa, hivi karibuni, baada ya kuvunjika kwa urafiki wa ‘kupika na kupakua’ kati ya mashostito wawili walio katika tasnia ya Bongo Movies, Aunt Ezekiel Grayson na Wema Isaac Sepetu maneno hayo yametumika pasipo sababu, Ijumaa Wikienda lina kila kitu!
Wasanii wa sinema Bongo movie Wema Sepetu na Aunt Ezekiel.
AUNT BILA KUUMA MANENO
Juzi, Aunt ameibuka na kutoa kauli kali bila kuuma maneno kwamba, Wema akitangulia kuaga dunia, yeye hatakwenda kumzika kwa maana ya kuuaga mwili wake sanjari na kuomboleza.
Msanii wa Bongo movie Wema Sepetu akiwa na ndugu zake.
KIASA CHA KAULI
Kauli hiyo ya Aunt imekuja siku chache baada ya Wema naye kudaiwa kutoa kauli kama hiyo akisema kwamba, kutokana na urafiki wake na Aunt kufa na kuwa maadui, basi hata akifa, Aunt asiende kumzika.
 MSIKIE AUNT ‘LAIVU’
Ijumaa wikienda: Aunt pole kwa kulea mimba! Nina machache sana. Wema amedaiwa kuanika hatima ya ugomvi wenu kwamba, hali ilipofikia hata akifa wewe usiende kumzika. Wewe unasemaje?
Aunt: Kwanza nashangaa taarifa za kwamba nina ugomvi na Wema maana hata hao ndugu zake nimesikia wanaongea mambo kibao.
“Ila mimi sioni kama kuweka picha ya tangazo la shoo ya Zari (Zarinah Hassan) kwenye peji yangu ya Instagram ni kosa. Kwa hiyo kama yeye hataki kuzikwa na mimi, hata mimi nasema sitamzika Wema.
 AANZA KUFUNGUKA
”Halafu sidhani kama kuna mtu anaweza kunipangia kitu kwenye peji yangu mwenyewe ambayo nina uamuzi wa kufanya chochote ninachojisikia.
 ILIKUWA UTANI, IYOBO ATAJWA
“Mimi sidhani kama hapo kuna ugomvi, maana nilichoandika na kuweka siku hiyo ilikuwa ni utani lakini hata kama yeye na ndugu zake walichukulia ‘siriasi’ basi bado walitakiwa kutambua kuwa, mchumba wangu Iyobo (Moses) ni mfanyakazi halali wa kundi la muziki la Diamond (Nasibu Abdul), hivyo nilikuwa na haki ya kumsapoti kwa asilimia zote maana fedha anazopata kupitia huko ndizo zinazonifanya mimi na familia yangu niishi,” alisema Aunt.
 FAMILIA YAWEKA KIKAO
Kufuatia vuguvugu hilo kushika kasi, hivi karibuni familia ya  Wema inadaiwa kuweka kikao na kusema kwamba walimuonya ndugu yao huyo siku nyingi kwa kumwambia kuwa, urafiki wake na Aunt ni sawa na ‘spea’ za ki-China kwani waliamini hautadumu kwa sababu ni unafiki tu bora hata alivyokuwa na Kajala Masanja.
Chanzo makini kutoka katika familia ya Wema kimelipenyezea ubuyu Ijumaa Wikienda ambapo kilitiririka:
“Mama Wema kama kawaida yake, alifikia hatua ya kusema kwa sasa hataki tena kumwona mwanaye akirudia urafiki wake na Aunt kwa sababu ni mnafiki.
 MAAZIMIO YA KIKAO YAFIKA KWA WEMA
“Maneno hayo ya mama na ndugu wengine, yalifikishwa kwa Wema, akawaelewa na kusema hana haja tena ya kuwa karibu na Aunt hata itokee nini maana hakuna anachomsaidia.”
 AUNT TENA, AMWANIKA WEMA SASA
Aunt alipoambiwa kuhusu maazimio ya kikao cha familia ya Wema na jinsi staa huyo alivyoyapokea, alisema:
 “Kama familia yake wamefikia hatua ya kuingilia hili, mimi nafikiri sina tatizo maana nina maisha yangu na yeye (Wema) ana maisha yake. Ila tu kama ni ishu ya wazazi, naomba wajue pia mimi sijajizaa wala sijazaliwa na miti, nina ndugu tena wanajitambua kwa kila hali.
“Nikiangalia sababu za ugomvi ni za kibinafsi sana hata hazifai kuingiliwa na mtu, maana haiwezekani kwenye maisha haya eti Wema akinuniana na mtu basi na mimi nimnunie, sijaumbwa hivyo wala sina unafiki huo.
“Kama staili ya maisha ikiwa kila atakayekwazana naye na mimi nimchukie siku wanapoelewana mimi si nitaonekana sifai kote? Wao wafahamu kuwa mimi najitambua wala si wa kuburuzwa hivyo.
“Kama wanasema hawawezi kushiriki lolote kwangu hata mimi sina sababu ya kujipendekeza kwao.
 WEMA AZIDI KUCHAMBULIWA
“Hakuna kitu kibaya katika maisha kama kuwa na rafiki ambaye siku zote yeye akikosana na mtu basi na wewe ukosane naye. Mbona mimi maadui zangu yeye ni marafiki zake na wala sijawahi kununa. Iweje sisi tukorofishane na watu yeye aongee nao ila yeye akikorofishana na watu basi hataki kabisa hata kutuona nao?”
 WEMA NAYE ATEMA NENO
Baada ya Ijumaa Wikienda kupata fukunyuku hizo lilimsaka Wema kwa maana ya kujiridhisha na kinachodaiwa kusemwa na yeye na familia yake, mambo yalikuwa hivi:
“Yaani hata sitamani kusikia jina la Aunt maana alichokifanya ni bora hata ya Kajala ambaye ishu yake ni ya moja kwa moja. Nashindwa kuliweka wazi sana lakini familia yangu haitaki hata kumsikia kwa jinsi ilivyochukizwa naye.
“Sifikirii kama kuna siku nitakuja kukaa naye tena au kuongea chochote mbele yake maana alichokifanya si cha kunifanyia mimi tuliyeshibana kama mapacha.”
Aunt  ‘mama kijacho’ na Wema walikuwa marafiki walioshibana kabla ya kutofautiana baada ya Aunt kutoa sapoti kwa mpenzi wa Diamond, Zari kwenye shoo yake ya Zari All White Party kwa kuposti picha kwenye mtandao iliyoonesha kupigia debe shughuli hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Mlimani City hivi karibuni jambo lililomkera Wema akiamini Aunt  ni mnafiki, yuko kwake na kwa mahasimu wake hao.

WEMA ALIA KUTOKUWA NA BAHATI NA MARAFIKI!


Beautiful Onyinye wa Bongo, Wema Sepetu amefunguka kuwa, anajua siku zote yeye hana bahati ya kuwa na marafiki kwa kuwa hata akiwa nao mwishowe kunatokea mgogoro na kuachana huku kila mmoja akimuona mbaya.

Beautiful Onyinye wa Bongo, Wema Sepetu.
Akizungumza na gazeti hili juzi, Wema alisema anaumia sana kwa kuwa mara nyingi anawapenda sana rafiki zake kwa moyo mmoja lakini mwisho wa urafiki wao huwa ni mbaya sana tena huvunjika kwa kugombana.
“Mimi nimeshajiona siku nyingi sina bahati kabisa, hata nikiwa na marafiki ambao nawapenda kutoka moyoni, mara nyingi wananigeuka na mama yangu amekuwa akinisihi mara nyingi sana, sasa naona bora nifuate ushauri ambao mama yangu ananishauri wa kuangalia watu wa kuanzisha urafiki nao,” alisema Wema.

"ILI AZAE, WEMA ALALE JUU YA KABURI LA MAREHEMU MWANANGU KANUMBA..."...BABA KANUMBA


Staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu.
Waandishi wetu
Mshangao! Baba mzazi wa aliyekuwa mwigizaji mkubwa Bongo, marehemu Steven Kanumba ‘The Great’, Charles Kusekwa Kanumba amefunguka kuwa ili azae, staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu anatakiwa alale juu ya kaburi.
Hayo yanakuja siku chache baada ya Wema aliyewahi kuwa mchumba wa Kanumba kudai kusumbuliwa na tatizo la kukosa uwezo wa kuzaa hivyo mzee huyo kujiongeza na kusema ni kwa sababu alitoa mimba ya mwanaye huyo.
Baba mzazi wa aliyekuwa mwigizaji mkubwa Bongo, marehemu Steven Kanumba ‘The Great’, Charles Kusekwa Kanumba.
Akizungumza na waandishi wetu, baba huyo alisema kama kweli Wema alitoa mimba ya Kanumba basi atakuwa alijilaani kwa sababu ukoo wao ukitoa mimba unaweza kufa au kujilaani (kutokupata mtoto) hivyo anatakiwa kutambika kwa kulala juu ya kaburi la mama mkubwa wa Kanumba ambaye ni bibi wa babu wa mzee Kanumba.
Alisema sambamba na hilo, Wema atatakiwa kurithiwa na ndugu wa Kanumba (kati ya kaka au mdogo wake).
“Kwenye ukoo wetu ukitoa mimba kuna mambo mawili, moja ni kufariki dunia au ‘kujikila’ (kujilaani) kwa kutokuzaa, pengine ndicho kilichomtokea Wema,’’ alisema baba Kanumba.

KUTAMBIKA KABURINI
Mzee huyo alisema kuwa mama mkubwa huyo alishafariki dunia kwa hiyo yeye na marehemu Kanumba walipaswa kwenda kaburini kwake kufanya tambiko zito, wakiwa wamevaa mavazi maalumu ya kiasili na mikononi wameshika vibuyu, jambo ambalo lingempasa Wema kukaza moyo.Alisema kuwa wakiwa kaburini hapo, Wema alitakiwa achotewe mchanga na kushikishwa kisha kusemewa maneno ya kuomba msamaha kwa kilichotokea.

VITU VYA TAMBIKO
Alisema walitakiwa waende na maziwa, unga wa mtama na hayo mavazi maalumu kwa ajili ya tambiko hilo.

KURITHIWA NA NDUGU
Aliendelea kudadavua kwamba, kwa sasa Kanumba hayupo duniani hivyo Wema anapaswa kuchukuliwa na kaka au mdogo wake wa damu kwenda kutambika, ikiwa ni pamoja na kuzaa naye ili kufungua mlango wa kizazi, hata kama ataachika basi ataendelea kupata watoto.

MAMA MKUBWA NI NANI?
Baba Kanumba alisema mama mkubwa huyo ni bibi yake mzee Charles Kanumba ambaye katika ukoo wao alikuwa mganga wa wanawake walioshindwa kupata watoto au wenye tatizo la kizazi.

Hata hivyo, baba Kanumba alimalizia kwa kusema kuwa, ingekuwa zamani ilikuwa ni kurithiwa tu lakini kwa sasa mila hizo zinapingwa vikali.Gazeti hili lilipomtafuta Wema ili kumfikishia taarifa hizo hakupatikana hivyo jitihada zinaendelea.

WEMA, KAJALA TENA! WAKUTANA CLUB WAKWEPESHWA WASIPIGANE

Brighton Masalu MAJANGA! Wasanii wawili mahasimu katika tasnia ya filamu, Kajala Masanja na Wema Sepetu ‘Madam’ wametengeneza tena vichwa vya habari baada ya kukutana ndani ya klabu ya usiku ya Maisha iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita na kuzua minong’ono miongoni mwa wadau wengi wa burudani, Risasi Mchanganyiko linakupa hatua kwa hatua.
Msanii wa filamu Bongo,Kajala Masanja akifurahia jambo.
Matukio hayo tofauti kwa wasanii hayo yalitokea ndani na nje ya ukumbi huo katika shoo maalum ya kumchangia mke wa msanii Mabeste  Venus, Lisa Karl Fickenscher  iliyowakutanisha mastaa wengi wa ‘category’ mbalimbali.
SHUNGULI YAANZA VIZURI
Shughuli nzima ilionekana kwenda vizuri, isipokuwa mara chache ambako kulitokea vituo vya hapa na pale, ingawa vingi kati ya hivyo vilisababishwa na baadhi ya wahudhuriaji kuzidiwa na kilevi.

WATENGANISHWA
Wakati flani ‘usiku mnene’, Kajala alijongea kwenye jukwaa maalum la waalikwa (V.I.P) kutoka kujichanganya kwa wadau, ambako pia alikuwa amekaa Madam aliyeonekana kuzidiwa na ‘kiburudisho’.

Akitambua wazi kuwa lolote lingeweza kutokea, Petit Man, mtu wa karibu wa Wema, alimshika mkono na kumtoa eneo hilo, lakini muigizaji huyo alipohoji sababu za kuondolewa ‘V.I.P’, aliambiwa kuwa hapakuwa sehemu salama kwa wakati huo. 
KAJALA NDANI YA NYUMBA
Kajala alionekana akijiachia kwa mapozi na ‘mihangaiko’ ya hapa na pale ikiwemo kucheza na kubadili vinywaji akiwa sanjari na marafiki zake.Wakati wote, msanii huyo alionekana mwenye furaha iliyoambatana  na tabasamu na vicheko vya mara kwa mara jambo lililotafsiriwa kama tayari alikuwa amepata kiburudisho cha kutosha.

AKUTWA NA MKASA
Mapambazuko yalipoanza kulivamia anga, Kajala na ‘kampani’ yake walitawanyika lakini wakati wakiwa nje ghafla jamaa mmoja ambaye hakufahamika ‘aliwa-join’ na kuwachangamkia kusiko kwa kawaida huku wao wakionekana kutompa ushirikiano aliouhitaji.


Wema Sepetu akiwa kwenye gari.
AMSHIKA MAKALIO
Hata hivyo, jamaa huyo ‘alifika mbele’ zaidi kwa kumshika makalio Kajala ambaye alimnasa kibao. Katika kujibu mapigo, jamaa huyo alimpiga na chupa ya bia kichwani na kusababisha jeraha usoni.
Baada ya tukio hilo, marafiki wa pande zote mbili walijitahidi kutuliza hali ya hewa iliyochafuka na kila mmoja akaendelea na hamsini zake.

WEMA SASA
Kwa upande wake, Wema ambaye alipaswa kuwa Msema Chochote (MC) wa hafla hiyo, alipanda jukwaani kwa kusaidiwa na watu kutokana na kuzidiwa na kinywaji kisichojulikana.Baada ya kupanda, muigizaji huyo nyota alishindwa kumudu kuendelea na ratiba, kwani alizungumza maneno yasiyoeleweka na hatimaye kuishia kuwasalimu mashabiki, kitu kilichoharibu shughuli hiyo kwa jumla.

ATOKA UKUMBINI NA GLASI
Baada ya kushuka jukwaani, mmoja wa wapambe wake wa muda mrefu, Petty Man alimshika mkono na kumsindikiza hadi nje, ambako akiwa ameshikilia glasi yake ya kinywaji, Wema aliingia nayo kwenye gari, kabla ya kumwaga kilichokuwemo ndani na kumpa mtu mmoja glasi hiyo ili airudishe ndani.

Mwandishi wetu alipotaka kujua sababu ya Wema kulewa na kushindwa kufanikisha jambo muhimu, alimtaka kumuacha kwani hakuwa na muda wa mahojiano.“Tafadhali sana (akilitaja jina la mwandishi), sihitaji mahojiano, hapa nimekuja kwenye starehe, naomba uniache,” alisema Wema huku akibamiza mlango wa gari kwa nguvu na kumtaka dereva wake (Petty Man) kuondoa gari.
KUTOKA KWA WADAU
Baadhi ya watu walioshuhudia matukio ya Wema na Kajala kwa nyakati tofauti, walisikika wakisema kuwa ni kama mkosi uliowakumba wawili hao marafiki wa zamani.“Hawa bwana wana matatizo sana, wote wamekutwa na majanga kwenye eneo moja, lakini nadhani hata matatizo yao yanachangiwa sana na bifu lisilokuwa na kichwa wala miguu, wajishushe na wasameheane,” alisikika akisema mdau mmoja.

Wema: Kumiliki Au Kutomiliki Bastola ni Siri Yangu

Staa wa Bongo Movie, Wema Sepetu, amedai kwamba itabaki kuwa siri yake kama ni kweli anamiliki bastola ama la kwa kuwa si sifa kutangaza umiliki wa silaha.

“Hii ni siri yangu kama namiliki bastola au la, lakini mimi sioni ajabu kumiliki bastola, mtu kama mimi mwenye maadui wengi inasaidia katika ulinzi wa maisha yangu,” alieleza Wema.
Wema aliendelea kuwataka wanaojiuliza kama anamiliki bastola ama la waendelee na mambo yao mengine kwa kuwa hawatajua jambo hilo ambalo ni siri katika kuimarisha ulinzi wake.

Gazeti la Mtanzania

Wema Sepetu na Aliyekuwa Mume wa Zarii Kunanii? Wapanga Kuwaumiza Diamond na Zari Kwa Kumsapoti Ali Kiba Kill Music Awards

Week end hii iliyopita Wema Sepetu na Aliyekuwa Mume wa Zari Ivan wamekuwa busy sana kumspoti Ali Kiba na Kumpromote kwenye page zao za Instagram kitu ambacho si cha kawaida na kimechukuliwa kuwa wawili hao wamepanga kufanya hivyo kumuumiza Diamond na Zari ...Wengi wamehoji iweje Mganda Huyo aliyekuwa mume wa Zari ghafla tu aanze kushabikia Bongo Flava na huku Wema nae Akiwa Busy kuposti Promotion za Kuwaambia watu wampigie kura Ali Kiba asimu wa Diamond?...Je Wameambizana? Je nini Kina endelea Kati yao Kwa Siri??

Angalia Picha Hizi kutoka katika Page zao za Instagram :
Posts za Mume wa Zari 
Post za Wema Sepetu

"‘RAY, STEVE NYERERE WANAFIKI WAKUBWA'..."...WEMA SEPETU

Staa wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’.
Musa Mateja STAA wa filamu Bongo, Wema Sepetu juzikati alijikuta akivunja ukimya kwa kusema kwamba, wasanii wenzake Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na Vincent Kigosi ‘Ray’ ni wanafiki wakubwa baada ya kumtosa kwenye Pati ya Instagram iliyofanyika hivi karibuni jijini Mwanza.
Staa wa filamu Bongo,Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.
Akizungumza na paparazi wetu, Wema alisema alikubaliana na mastaa hao kutoenda kwenye Shoo ya Zari All White Party iliyofanyika Mlimani City jijini Dar badala yake waongozane naye jijini Mwanza lakini wakamgeuka.
“Sitaki kabisa nisikie mtu ananiambia habari ya Steve Nyerere au Ray maana ni wanafiki wakubwa, hawawezi kuniahidi kutokwenda pati ya Zari lakini wakaenda na wasije Mwanza kama walivyoniahidi,” alisema Wema.Paparazi wetu baada ya kupata malalamiko ya Wema, alimsaka Steve ili aweze kuzungumzia unafiki wao, akafunguka:
“Kweli mimi na Ray tuliahidi kuungana na Wema kwenye shoo yake ya Mwanza ila siku ya mwisho tulikwama baada ya kupungukiwa fedha ya nauli, hivyo tukashindwa kabisa na tusingeweza sisi kwenda huko kwa kumtegemea yeye atulipie kila kitu.Tukaona twende kwa Diamond ambaye naye alitualika.” Ray hakuweza kupatikana mara moja kuzungumzia tuhuma hizo.

Pamoja na Kukanusha Mara Nyingi ..Watu Wadai Wema Sepetu Anatumia Madawa ya Kulevya Pamoja na Kukanusha Mara Nyingi ..Watu Wadai Wema Sepetu Anatumia Madawa ya Kulevya "Unga"


Musa Mateja PAMOJA na mwenyewe kukanusha kuwa si mtumiaji wa madawa ya kulevya (unga), watu wanazidi kusema eti supastaa wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu ‘Madam’ anatumia unga, Risasi Jumamosi limesheheni data.
Supastaa wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu ‘Madam’.
UBUYU WAVUJISHWA
Kwa mujibu wa chanzo makini, Wema amekuwa akitumia kilevi hicho kwa muda mrefu huku akifanya jambo hilo kwa siri kubwa.“Hivi hamna habari ya Wema kubwia unga? Mbona kila mtu anajua, watu wengi tu wanafahamu lakini wanashindwa namna tu ya kumueleza mwenyewe ili aache maana kila mtu anamhofia si unamjua naye Madam mtu wa kumaindimaindi,” kilisema chanzo hicho.

MITANDAO YAKAZIA MADAI
Kama hiyo haitoshi, kwa nyakati tofauti, watumiaji mbalimbali wa mitandao ya kijamii wamekuwa wakidai kuwa staa huyo anabwia unga licha ya kuwa hawana ushahidi wa moja kwa moja.“Mimi sijawahi kumuona lakini kuna watu wake wa karibu tu wananihakikishia kwamba Wema anatumia madawa ya kulevya, ila naamini mwenyewe anaujua ukweli wote wa haya yanayosemwa,” ilisomeka sehemu ya maoni mtandaoni.

RISASI LAMFUNGIA KAZI
Baada ya kupata madai hayo, Risasi Jumamosi lilimfungia kazi Madam ili kuweza kumsikia anazungumziaje tuhuma hizo nzito.

Jumatano iliyopita, mwanahabari wetu alikwenda nyumbani kwa mwigizaji huyo mwenye mvuto wa kipekee, Mtaa wa Bwawani-Kijitonyama lakini bahati mbaya alikuwa ametoka kwenda kurekodi na hata alipofanya subira hadi jioni, bado hakurejea huku simu yake ikiita bila kupokelewa.
JITIHADA ZAIDI
Siku iliyofuata, mwanahabari wetu aliyeambatana na mmoja wa wahariri wa Global Publishers, walitia timu kwa mara nyingine nyumbani kwa Madam lakini pia mwigizaji huyo alikuwa ametoka lakini bahati nzuri alipopigiwa simu alipokea, mambo yalikuwa hivi:Risasi: Wema tumekutafuta sana hapa nyumbani kwako bila mafanikio tuna ishu ya msingi kweli tunataka kujua kutoka kwako?

Wema: Poleni, ishu gani?
Risasi: Tumepokea habari kuwa wewe unatumia madawa ya kulevya,  umewahi kusikia hizi habari?
Wema: Ndiyo hizo habari nimewahi kuzisikia. Nakumbuka nilianza kuzisikia tangu kipindi kile mimi natembea na CK (yule kigogo wake), walivumisha sana lakini hakuna ukweli wowote.

ADAI WAMEMPONZA
“Tena imefika wakati wananikosesha hadi amani, imenifanya hadi niwe nakaguliwa kupindukia bila sababu za msingi, juzi hapa wakati naenda Mwanza (kwenye shoo ya Instagram), walinibana sana pale Air Port hadi nikataka kuachwa na ndege.

Wema Sepetu ‘Madam’.
AISHI KWA TAHADHARI
“Yaani kwa sasa nimelazimika kuweka hadi ulinzi mkali pale nyumbani, maana huwezi jua watu wasionipenda wanaweza kuja wakanibambikia nikaonekana natumia kumbe sijui hata ukoje. Sasa hivi kila atakayeingia lazima akaguliwe, ahojiwe ndipo aingie.

ATAJA KUHUSISHWA NA ROMMY
“Kuna wakati walinitaja kuwa natumia kwa kuwa nina ukaribu na Rommy Johnson (binamu yake msanii Diamond) kitu ambacho nilikikanusha na ninaendelea kusema hakuna ukweli wowote.

MAMA’KE ARIPOTI POLISI
“Ili kuwataka watu wasinihusishe kwa namna yoyote na kujihadhari, tuliongea na mama, akaenda kutoa taarifa polisi Mabatini ili nisije kupata tatizo lolote linalohusishwa na madawa ya kulevya.”

RAFIKI ZAKE WANENA
Mwanahabari wetu aliwavutia waya marafiki wa Wema, Aunt Ezekiel na Martin Kadinda ambaye ni meneja wa mwigizaji huyo ambao kwa pamoja walidai hawajawahi kumuona Madam hata siku moja akibwia unga achilia mbali kukaa karibu na wabwiaji.

“Sijawahi kumuona Wema hata siku moja anatumia hivyo vitu (unga), watakuwa wanamzushia ili watimize azma yao ya kumchafua si unajua si wote wanampenda?,” alisema Aunt huku Martin akikazia:“Hakuna kitu kama hicho, Madam hatumii bwana, sisi tupo naye, tunafanya naye kazi siku zote, hatujawahi kumuona, huo ni uzushi tu.”

Andiko la Wema Kuhusu Sheria ya Makosa ya Mtandao...Anasema Yupo Tayari ATUKANWE Kuliko Kukubali Serikali Iwafunge Midomo Watanzania


Naomba mimi kama Wema Sepetu, nitoe tamko langu rasmi kuhusu hii Sheria mpya iliyopitishwa bungeni. Naongelea Sheria ya cybercrime au cyberbulling. 
 
Ukweli ni Kwamba watanzania tunatumia vibaya mitandao ya kijamii. Matusi yamekuwa ni mengi na sometimes hawavumiliki. Kwa kweli kunahitahija Kuwa na laws in place za kupunguza unyanyasaji kupititia mitandao ya kijamii. That said, yes nai support hii bill ya cyber crime to an extend.

Kama jinsi ambavyo watanzania tunatumia vibaya mitandao kwa kuumizana kwa njia ya matusi na kuchafuana, wana siasa wetu waliopitisha hii Sheria ya cybercrime pia wameitumia vibaya hii Sheria na kuitumia kama silaha ya kumfunga mdomo mtanzania.

Kusema ukweli mimi kama Wema Sepetu nimechoka kutukanwa, mpaka mama yangu mzazi anadhalilishwa humu Kwenye mitandao.
 
 Kuna kipindi nilifikia hatua ya kuwaza bora nife tu ili kuepukana na matusi na kuandikwa na magazeti kwa habari za uongo.

 Lakini as much as ningependa Kuwe kuna Sheria kama hii ya kunisaidia mimi Wema niepukane na matusi Naona ni bora niendelee kutukanwa mpaka Siku nitakayokufa kuliko kuona fans wangu mimi, fans wa Wolper, fans wa Jokate, fans wa Ali Kiba, fans wa Diamond Platinumz na Wengine wengi wakinyang'anywa haki yao ya msingi kabisa ambayo ni haki ya kuweza kufungua mdomo na kuongea hata yale ambayo sisi mastar na wanasiasi hatukubaliano.....
 
Je mimi kama Wema nitasemaje nawadhamini fans wangu ambao wao ndo wamenipa umaarufu huu na kunifikisha hapa nilipo kama hapo hapo nitawanyanyasa kwa kuwapokonya haki yao ya freedom of speech.

Mimi Wema sijakamilika , wote mnajua ninamapungufu yangu , je mimi Wema nitawezaje kujua makosa yangu ili niweze kubadilika na kufanyA vizuri kama sitokubali kusikiliza maoni ya watu wote yawe mabaya au mazuri?Nafikir wore mnajua hakuna page ya Mtanzania hapa instagram yenye matusi na malumbano kama page yangu mimi ....

Nimeshauriwa sana Kuwa nianze kublock wote wanaoniwekea comment za matusi na kufuta comments zao kama wanavyofanya mastaa wengine lakini nimegoma. Je mnadhani mimi nafurahia hizo comment za matusi? Tena Kwenye page yangu mwenyewe? Hapana zinaniumiza ila pia nakumbuka Kuwa mimi ni kioo cha Jamii nakumbuka Kuwa kabla ya Wema sepetu first comes nchi yangu .....

Niko tayari nitukanwe lakini haki za fans wangu, haters wangu na watanzania wote kwa ujumla ziwe po pale pale. Watanzania naomba tuungane katika kumsupport my dada Kwenye hili @iworeadress @iworeadress. 
 
Mimi nimemwelewa sana anachokisema. Tunaelekea pabaya Sasa....Tupiganie haki zetu za uhuru wa kuongea. Tusipojipigania hakuna wa kutupigania. Naamini Chama changu nachokipenda cha CCM kitatusikukiza wananchi wake na kufanyia hilo kazi.Tafadhali follow hii page ili tuweze kuchangia na kabadilishana mawazo . @ccmchangeorquit

By Wema Sepetu on Instagram

Barua Nzito Wema Kuna Kitu cha Kujifunza kwa‭ ‬Zari‭!

KWAKO mtoto mzuri, Beutiful Onyinye, Wema Sepetu !'Madam'. Vipi uko poa? Ukitaka kujua afya yangu, mimi ni mzima namshukuru Mungu, hofu na mashaka ni kwako wewe uliye mbali na upeo wa maisha yangu.

Kitambo kidogo hatujaonana, nimeona si mbaya kama nitakukumbuka kwa barua maana najua kutokana na majukumu yako na yangu kuwa mengi, wakati mwingine tunaweza tukafikisha hata miezi sita hatujaonana.

Dhumuni la barua hii ni kutaka kukushauri kwamba unaweza kujifunza kitu kutoka kwa mpenzi wa sasa wa aliyekuwa mpenzi wako, Nasibu Abdul !'Diamond, Zarinah Hassan !'Zari!

Naomba usinielewe vibaya. Sina nia ya kukupambanisha wala kutaka kukukejeli kwa namna yoyote. Kuna kitu kidogo tu cha kujifunza kutoka kwa binti huyo wa Kiganda.
Achana na maneno yanayosemwa mtaani, kila mmoja ana upungufu wake lakini binadamu tunashauriwa kuiga yale mazuri kutoka kwa wenzetu.

Iko hivi Wema, wewe na yeye mna nafasi moja nzuri katika jamii. Nyinyi ni maarufu. Mnapendwa na watu kupita maelezo. Mna ushawishi mkubwa sana katika jamii hivyo mnaweza kufanya jambo na likapata mafanikio makubwa sana.

Umaarufu wenu ni biashara. Kwa nini uendelee kubaki chini wakati umezungukwa na fursa kibao? Umaarufu wako ni biashara kama utaamua kuwa !٪serious!& na kila hatua unayoipiga.
Nikwambie ukweli bila unafiki, unapaswa kuiga jambo moja tu la msingi kutoka kwa Zari, kuwekeza na kuheshimu fedha.

Mwenzako anaijua fedha. Anajua namna ya kuitafuta na namna ya kuiwekeza katika maeneo ambayo yatazidi kuzizalisha. Akili yake inawaza pesa na si starehe zisizokuwa na msingi.
Mfano mdogo tu ni !٪idea!& kama ya All White Party aliyofanya Zari kule Uganda. Alifanikiwa, anaendelea kufanya na wiki iliyopita aliifanya pale Mlimani City jijini Dar na kupata mafanikio makubwa.

Kwangu mimi kile ni kitu kikubwa sana ambacho kinaingiza fedha nyingi kwa wakati mmoja. Si vibaya kama utaiga vitu vya namna hiyo. Nisikufiche, nafasi ya umaarufu uliyonayo Kibongobongo, unaweza kufanya zaidi ya shoo ile kama utaamua na kupata watu wazuri wa kufanya nao kazi.

Na unapofanya mambo makubwa kama hayo, lazima pia udhibiti matumizi yako. Starehe zipo lakini wakati mwingine unapaswa kuheshimu fedha. Yale mambo ya kwenda kuzimwaga ukumbini eti kuwa kama kina pedeshee !٪nanilii!&, si mazuri.

Jeuri ya fedha ifanye kwa kufungua miradi mikubwa ambayo hata utakapozeeka utainjoi matunda yake. Kuigiza kuna mwisho, huwezi kuwa mwigizaji milele, kuna wakati utatakiwa kuwa msimamizi wa miradi yako tu binafsi na mkono uende kinywani kiulani tu.

Usikubali kushikiwa akili na wapambe, unayoshauriwa na wapambe yachuje maana si yote yanakuwa na manufaa. Tumia kipaji na jina lako vizuri, una nyota ya kupendwa basi kupendwa huko kuwe na faida.
Natambua una idea zako ambazo tayari umeanzisha kama kipindi chako cha In My Shoes, usiishie hapo fanya makubwa zaidi.
Kwa leo acha niishie hapo. Ni matumaini umenielewa.
Wasalaam

BY: Eric Evarist/ GPL

SHABIKI WA WEMA SEPETU AFUNGUKA YA MOYONI KUHUSU MAPENZI YA WEMA NA DIAMOND PLATNUMZ YALIVYOKUWA


nanukuu kutoka kwa shabiki mtaa wa pili unajuwa watu mnaongea mengi bila ya kufikiria vizuri kama kila mtu na bahati yake.ktk mapenzi kuna mambo mengi sana alikuwa ndani ya mahusino ndio anaelewa VIZURI ninawezakana wema alijaribu sana tumia hiyo fursa lk aikwezekana jamani sio kama ameshindwa MBONA MADAME RITA ALIKUWA NA MENGI LK AKUOLEWA KWANI ALIKUWA ATAKI LK SIO BAHATI yake.tuseme jambo moja diamond ajampenda wema 100% labda 50% (ssa zari alikuwa na nguvu moja nitakupa mtoto lk fata mashariti yang) lk wema ameona kila anachojaribu kwa mwenzie akifanyia kazi ssa sio fursa wajemeni ni bahati tu.na zari kama ngekuwa mke bora mbona ameondoka kwa ivan? mke bora anavumilia kila kitu kwa mume wake kama dini zinavyosema.mara gani wema amejaribu kwa diamondo lk hakuna kitu.ok wema kashindwa peny je na jojo nae wote hakuna ata mwenye akili sio hivi kwenye mapenzi kuna siri nyingi na huyo zari ana yake kibao subiri tu

LICHA YA KUWA MGUMBA...WEMA SEPETU AOLEWA, MWENYEWE AFUNGUKA NA KUSEMA HAYA!

WSepetu
Pichaz ziko mitandaoni.. Wema Sepetu nae kapost kwenye ukurasa wake wa Instagram, amevaa gauni la harusi.. Wema Sepetu ameolewa kweli au movie????
Soudy Brown kamtafuta Wema.. alichokijibu ni kwamba ni kweli ameolewa ila hayuko tayari kumtaja mume wake.. amesema kuwa kaamua kufunga ndoa ya siri kwa kuogopa kupigwa ‘juju’.
Sepetuur
Wema amesema ndoa yao ilifungwa bomani kwa sababu mume wake ni mkristo.. kingine ni kwamba harusi ilihudhuriwa na watu watano pamoja na familia yake ila mwishoni mwa mwezi huu watafanya sherehe rasmi.
Kuhusu ishu ya kutopata mtoto Wema amesema mwanaume huyo anajua na amekubaliana na hiyo hali lakini inawezekana kwake wakapata mtoto.

Tetesi za Ndoa ya Wema Sepetu zazua Gumzo Mjini!

Ubuyu Mpya unaoenea kwa siri kwenye mitandao ya kijamii kwa sasa, ni kuhusu ndoa ya super star wema sepetu inayotarajiwa kufungwa ivi karibuni. Chanzo cha ubuyu kinaeleza kuwa hatua zote muhimu zimeshachukuliwa, kinachosubiriwa tu ni bwaba harusi huyo mtarajiwa kuchukua jiko lake bila kipingamizi chochote. Mpaka sasa ivi bado mume huyo mtarajiwa wa staa huyo hajawekwa wazi kwa kuogopa watu wabaya kumfanyia fitna.

Mpaka sasa management yake inafanya siri kubwa kuhusu tukio hilo muhimu litakalobadilisha title na heshima ya msanii huyo.

WEMA: MAMA’NGU AMEPOTEZA UWEZO WA KUONA KWA 75%!

Mwandishi Wetu
Pole sana mama! Staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amefunguka kuwa mama yake mzazi, Miriam Sepetu anasumbuliwa na macho ambapo madaktari wamegundua kwamba amepoteza uwezo wa kuona kwa asilimia sabini na tano (75%).
Kwa mujibu wa Wema, aliamua kumpeleka mzazi wake huyo hospitalini (hakuitaja) ndipo alipohakikishiwa tatizo hilo ambalo limekuwa likimsumbua kwa muda mrefu.
“Kumnusuru mama yangu asipate upofu wa moja kwa moja inabidi afanyiwe operesheni ya macho,” alisema Wema kwa huzuni kwa kuwa hakuna kama mama.

WEMA ADAIWA KUTIBUA NDOA YA PETIT MAN


MUSA MATEJA NA IMELDA MTEMA
Hatimaye lile sekeseke la ndoa ya meneja wa wasanii wa Bongo Fleva wanaosimamiwa na Kampuni ya Endless Fame, Petit Man na mdogo wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Esma Platnumz limemdondokea Wema Isaac Sepetu anayedaiwa kuitibua kiasi cha kuwatenganisha na kila mmoja kuchukua hamsini zake.
Habari kutoka chanzo chetu zilidai kwamba, Wema amehusika kwa asilimia kubwa kutibua ndoa hiyo kwani amekuwa akimtafutia mademu Petit Man, jambo ambalo Esma alilishtukia na kuamua kumbwatukia Wema kwa kuandika maneno makali kwenye mitandao ya kijamii.
“Kwa taarifa yenu Esma anamlalamikia Wema kuwa anamfanya mumewe kuwa mhuni kiasi kwamba anachukua mademu, tena marafiki zake na hata akimuuliza Petit Man anajifanya hao ni mashoga wa Wema.“Anapomkomalia, mara kadhaa umekuwa ukizuka ugomvi mkubwa na Petit Man anahama nyumbani kwake na kukimbilia kwa Wema,” kilisema chanzo chetu.Baada ya kunyetishiwa ‘infomesheni’ hizo, gazeti hili liliingia kazini kusaka ukweli wa mambo yanayodaiwa juu ya
lilianzia kwa Esma, alipopatikana alisema ni kweli hivi karibuni aliandika ujumbe kwenye Mtandao wa Instagram, ingawa kwenye maelezo yake hakumtaja mtu bali aliandika kwa hisia kama binadamu mwingine anavyoweza kuandika.
“Nani anasema nimemtukana mtu? Niliandika mambo ambayo nilijisikia mwenyewe lakini sikumtaja wala kumlenga mtu yeyote, kama kuna mtu alikwazika basi atakuwa anajichanganya mwenyewe.“Mimi sina tatizo na Wema na mambo ya familia yangu siwezi kumwambia kila mtu hivyo kama kuna ugomvi kati yangu na mume wangu hayo ni mambo ya familia yetu,” alisema Esma.
Kwa upande wake Wema alifunguka kwamba hajawahi kuongea jambo na Esma na kama kuna kitu aliandika kwenye ‘peji’ yake yeye hakuona.Alisema anachokumbuka ni kwamba aliongea naye (Esma) akiwa Hospitali ya Aga Khan Aghakan, Dar.
“Huwa siongei na Esma mara kwa mara kwani sina sababu sana ya kuwa naye kwa kuwa si mume wala bwana’ngu.
“Pia sijawahi kukwaruzana naye, sasa kama kuna kitu alisema, mimi namtafutia wanawake mumewe basi atakuwa anakosea kabisa,” alisema Wema.

Tatizo la Kushindwa Kuzaa Kwa Wema Sepetu Waganga wa Kienyeji na Madaktari Kila Kona Wajitokeza Kumsaidia, Wema Adai Yupo Tayari

Kufuatia  tatizo la kushindwa kupata ujauzito alilonalo msanii maarufu Bongo, Wema Sepetu, hivi karibuni waganga wapatao 26 kutoka sehemu mbalimbali nchini walijitokeza na kuomba kuunganishwa na staa huyo ili wamtibu.

Waganga hao wa tiba asilia pamoja na madaktari kutoka hospitali mbalimbali kwa nyakati tofauti walipigia simu  na kueleza kuwa, wanashangaa kuona Wema anakosa amani wakati wao wanaweza kumtibu na kuweza kuitwa mama kama wenzake.

Unajua wapo wanawake ambao wanakosa amani kwa mambo ambayo hawastahili, hili la Wema kutopata mtoto linatibika, mpeni namba yangu kisha anitafute,” alisema mmoja wa wataalam hao aliyeomba jina lake lisiandikwe.

Katika kujua Wema anapokeaje ofa aliyopewa na waganga hao, alitafutwa na alipopatikana alikubali mara moja kutibiwa tatizo alilonalo lakini akatoa angalizo.

Kuna watu wengi sana ukiacha ambao wamejitokeza kwenu, mimi nina meseji zaidi ya 400 ambazo nimetumiwa kwenye namba yangu ya WhatsApp na simu kibao nimepigiwa watu wakijitolea kuja kushughulikia tatizo langu, kiukweli kabisa nipo tayari.

Lakini ni vizuri wakati naanza kutibiwa tayari nikawa na mwenza wangu ambaye tutakuwa tumekubaliana na pale tatizo litakapoisha, iwe rahisi kuzaa mara moja,” alisema Wema.
Older Posts
© Copyright ZEE LA UDAKU | Designed By Code Nirvana
Back To Top