Habari Kali
Loading...

'Mimba' Ya Lulu Michael Yapotea..!! Mwenyewe afunguka


Miezi miwili iliyopita kuliibuka madai mazito kwamba staa bei mbaya wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameongezeka tumbo hivyo mashabiki wake wakapiga vigelegele kwamba huenda ana mimba lakini sasa tumbo hilo limeyeyuka.

Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika, Lulu kwa sasa anakatiza viunga vya chuo anachosoma cha Magogoni jijini Dar akichukua masomo ya Uhusiano wa Umma, akiwa hana lile tumbo la Aprili.
 
Mwandishi alizungumza na baadhi ya wanafunzi wenzake ambao walidai msanii huyo alikuwa hafiki chuoni hapo kwa muda mrefu lakini sasa amejaa tele ‘mwepesii’.
 
“Hakuwa akija chuoni kwa muda, baadaye akawa anahudhuria kwa ‘kupibu’ kisha kuacha tena ila ameanza juzi tu kutokana na kuwepo kwa mitihani,” alisema mmoja wa wanachuo hao.
 
Kama taaluma inavyoelekeza, mwandishi wetu alimtafuta Lulu kupitia simu yake ya mkononi huku ikiita bila majibu.
 
Baadaye alitumiwa ujumbe wa  kuulizwa  kuhusu  sakata  hilo  ambapo   alijibu: “Hao wanaodai nina mimba walinipa wao? Sina nafasi ya kufafanua.” 
 
Hivi karibuni Lulu aliripotiwa na mitandao ya kijamii kuwa huenda ana mimba.

Chanzo: Gpl/Gazeti  la  Amani

Joketi Kidoti kaachia picha mpya akionyesha umbo lake lilivyobomba


Instagram umekuwa ni mtandao ambao hakika umeleta upinzani mkubwa kwenye mitandao mingine ya kijamii diniani kwa sasa mastar na wasio mastar wamekuwa wateja wa mtandao huu sasa tukutane na picha hizi toka kwa Joket
Tanzania singer and model Jokate "Kidoti" Mwagelo shared this images today oops!! OMG men will flaunts after see this.






           

BAADA YA MAUZAUZA KUZIDI: LULU ATAMANI KUIMBA INJILI!

Lulu Atamani Kuimba Injili
Staa wa bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema anatamani sana siku moja  kuimba muziki wa injili kwa vile anacho kipaji cha uimbaji.
Staa huyo aliyasema hayo wakati akihojiwa  kwenye kipindi cha  televisheni cha The Sporah Show wiki hii.
“Napenda kuimba...nadhani naweza kuimba, napenda kama siku ikitokea nimekuwa muimbaji  niimbe gospel, napenda sana gospel" alisema Lulu.
Pia Lulu alisistiza kuwa yeye ni mtu mwenye hofu ya Mungu.
“I’m  God fearing  yaani namuogopa sana na namuheshimu sana Mungu sio kumuogopa peke yake. Kwahiyo pamoja na yote ninayoyafanya  imani yangu ipo palepale hata mungu anajua.
Mnanijua kwa nje , huo ndio upande mnaoujua, kuna upande wangu wa ndani na hauwezi kuujua lazimu muwe watu wa ndani sio kila mmoja anaweza kuujua”-Lulu alisisitiza.

WEMA, KAJALA TENA! WAKUTANA CLUB WAKWEPESHWA WASIPIGANE

Brighton Masalu MAJANGA! Wasanii wawili mahasimu katika tasnia ya filamu, Kajala Masanja na Wema Sepetu ‘Madam’ wametengeneza tena vichwa vya habari baada ya kukutana ndani ya klabu ya usiku ya Maisha iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita na kuzua minong’ono miongoni mwa wadau wengi wa burudani, Risasi Mchanganyiko linakupa hatua kwa hatua.
Msanii wa filamu Bongo,Kajala Masanja akifurahia jambo.
Matukio hayo tofauti kwa wasanii hayo yalitokea ndani na nje ya ukumbi huo katika shoo maalum ya kumchangia mke wa msanii Mabeste  Venus, Lisa Karl Fickenscher  iliyowakutanisha mastaa wengi wa ‘category’ mbalimbali.
SHUNGULI YAANZA VIZURI
Shughuli nzima ilionekana kwenda vizuri, isipokuwa mara chache ambako kulitokea vituo vya hapa na pale, ingawa vingi kati ya hivyo vilisababishwa na baadhi ya wahudhuriaji kuzidiwa na kilevi.

WATENGANISHWA
Wakati flani ‘usiku mnene’, Kajala alijongea kwenye jukwaa maalum la waalikwa (V.I.P) kutoka kujichanganya kwa wadau, ambako pia alikuwa amekaa Madam aliyeonekana kuzidiwa na ‘kiburudisho’.

Akitambua wazi kuwa lolote lingeweza kutokea, Petit Man, mtu wa karibu wa Wema, alimshika mkono na kumtoa eneo hilo, lakini muigizaji huyo alipohoji sababu za kuondolewa ‘V.I.P’, aliambiwa kuwa hapakuwa sehemu salama kwa wakati huo. 
KAJALA NDANI YA NYUMBA
Kajala alionekana akijiachia kwa mapozi na ‘mihangaiko’ ya hapa na pale ikiwemo kucheza na kubadili vinywaji akiwa sanjari na marafiki zake.Wakati wote, msanii huyo alionekana mwenye furaha iliyoambatana  na tabasamu na vicheko vya mara kwa mara jambo lililotafsiriwa kama tayari alikuwa amepata kiburudisho cha kutosha.

AKUTWA NA MKASA
Mapambazuko yalipoanza kulivamia anga, Kajala na ‘kampani’ yake walitawanyika lakini wakati wakiwa nje ghafla jamaa mmoja ambaye hakufahamika ‘aliwa-join’ na kuwachangamkia kusiko kwa kawaida huku wao wakionekana kutompa ushirikiano aliouhitaji.


Wema Sepetu akiwa kwenye gari.
AMSHIKA MAKALIO
Hata hivyo, jamaa huyo ‘alifika mbele’ zaidi kwa kumshika makalio Kajala ambaye alimnasa kibao. Katika kujibu mapigo, jamaa huyo alimpiga na chupa ya bia kichwani na kusababisha jeraha usoni.
Baada ya tukio hilo, marafiki wa pande zote mbili walijitahidi kutuliza hali ya hewa iliyochafuka na kila mmoja akaendelea na hamsini zake.

WEMA SASA
Kwa upande wake, Wema ambaye alipaswa kuwa Msema Chochote (MC) wa hafla hiyo, alipanda jukwaani kwa kusaidiwa na watu kutokana na kuzidiwa na kinywaji kisichojulikana.Baada ya kupanda, muigizaji huyo nyota alishindwa kumudu kuendelea na ratiba, kwani alizungumza maneno yasiyoeleweka na hatimaye kuishia kuwasalimu mashabiki, kitu kilichoharibu shughuli hiyo kwa jumla.

ATOKA UKUMBINI NA GLASI
Baada ya kushuka jukwaani, mmoja wa wapambe wake wa muda mrefu, Petty Man alimshika mkono na kumsindikiza hadi nje, ambako akiwa ameshikilia glasi yake ya kinywaji, Wema aliingia nayo kwenye gari, kabla ya kumwaga kilichokuwemo ndani na kumpa mtu mmoja glasi hiyo ili airudishe ndani.

Mwandishi wetu alipotaka kujua sababu ya Wema kulewa na kushindwa kufanikisha jambo muhimu, alimtaka kumuacha kwani hakuwa na muda wa mahojiano.“Tafadhali sana (akilitaja jina la mwandishi), sihitaji mahojiano, hapa nimekuja kwenye starehe, naomba uniache,” alisema Wema huku akibamiza mlango wa gari kwa nguvu na kumtaka dereva wake (Petty Man) kuondoa gari.
KUTOKA KWA WADAU
Baadhi ya watu walioshuhudia matukio ya Wema na Kajala kwa nyakati tofauti, walisikika wakisema kuwa ni kama mkosi uliowakumba wawili hao marafiki wa zamani.“Hawa bwana wana matatizo sana, wote wamekutwa na majanga kwenye eneo moja, lakini nadhani hata matatizo yao yanachangiwa sana na bifu lisilokuwa na kichwa wala miguu, wajishushe na wasameheane,” alisikika akisema mdau mmoja.

LULU AANIKA SIRI YA KUWAPA URODA WANAUME WALIOMZIDI UMRI!


Gladness Mallya
 Funguka! Sexy lady kunako sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunguka kuwa anapenda kuminya ‘ku-date’      na wanaume wanaomzidi umri kwa sababu wanakuwa na nafasi nyingi katika maisha yake.
Elizabeth Michael ‘Lulu’
Akizungumza runingani juzikati, Lulu alisema anapenda kuwa na wanaume wanaomzidi kwa sababu wana nafasi tatu katika maisha yake ya kawaida, wanakuwa kama kaka, baba na mpenzi.
“Siwezi kuwa na mwanaume ambaye tunalingana kwa sababu atakuwa hana sifa hizo,” alisema Lulu.

KAJALA: NIACHENI NA MAISHA YANGU

Staa mkali wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja.
Imelda Mtema
KUFUATIA mashabiki kumlaumu kwa kitendo chake cha kuhudhuria shoo ya Zari All White Party, staa wa filamu Bongo, Kajala Masanja amefunguka kwa ukali kuwataka watu kumuacha na maisha yake kwa sababu hayawahusu.

Akipiga stori na gazeti hili, Kajala  alisema  amekuwa mvumilivu kwa muda mrefu lakini kitendo cha watu kutaka kumpangia nini cha kufanya au wapi pa kwenda, kimevuka mipaka maana hawajui alipotoka wala anakokwenda.
“Watu wanazidi sasa, wanataka kunipangia wapi pa kwenda na wapi siyo pa kwenda, kwani kwenda kwa Zari kuna tatizo gani,  kwa hiyo mtu akiwa na tofauti na Wema, kila mmoja lazima atofautiane na huyo mtu? hayo mambo ya  wapi jamani, watu wasinipangie  maisha ya kuishi,” alisema Kajala.

WEMA, AUNT KIMENUKA KISA ZARI!


Imelda Mtema na Hamida Hassan
KIMENUKA! Mashosti wa kufa na kuzikana, Wema Isaac Sepetu na Aunt Ezekiel Grayson wanadaiwa kugombana baada ya Aunt ‘kuposti’ kwenye ukurasa wake wa Instagram tangazo lililohusiana na pati ya mwandani wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ iliyofanyika Mlimani City jijini Dar wikiendi iliyopita.
Mashosti wa kufa na kuzikana, Wema Isaac Sepetu na Aunt Ezekiel Grayson.
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa mastaa hao wa sinema za Kibongo, baada ya Aunt kuposti tangazo hilo akiwalaumu watu wa mtandao wa huduma za simu waliomtumia ndipo Wema akaona na kuja juu.
Ilielezwa kwamba baada ya Aunt kutupia picha ya tangazo hilo, Wema alichukizwa na kitendo hicho huku akimuona Aunt kuwa amemsaliti.

Aunt Ezekiel Grayson.
Ilisemekana kwamba katika utetezi wake, Aunt hakupendezwa na tangazo hilo alilotumiwa na mtandao huo wa simu.
“Wema alivyoona alichukia na kusema Aunt alikuwa akimsaliti na alitumia tangazo lile kijanja kwa ajili ya kuwatangazia watu kuhusu pati ya Zari wakati anajua kabisa kuwa Wema hazipandi na Zari kwa sababu anatoka na aliyekuwa mchumba’ke (Diamond),” kilisema chanzo hicho.

 
Wema Isaac Sepetu.
Katika sakata hilo, kuna watu ambao waliona Aunt hakuwa na kosa lakini wapo walioona hakuwa sahihi, jambo ambalo lilichochea ugomvi wao huku wakidaiwa kukesha wakitukanana.
Gazeti hili lilipozungumza na Aunt kuhusiana na sakata hilo, alikiri kutokea akisema kuwa hakuwa na maana mbaya kuposti tangazo hilo lakini kila mtu ana mtazamo wake.
“Mimi sikumaanisha chochote kibaya kuhusu hilo tangazo na wala sikujua kama kuna mtu anaweza akalichukulia tofauti kabisa na hapo na mimi ndiyo nashindwa cha kuzungumza,” alisema Aunt.
Alipopigiwa Wema simu yake iliita bila kupokelewa hadi gazeti hili linakwenda mitamboni.

YABAINIKA CHANZO CHA ZARI KUMPENDA DIAMOND HIKI HAPA! SOMA HAPA

Kumbe! Imebainika kuwa maneno ‘gold digger’ katika ulimwengu wa fursa yanamaanisha kuwa ni mtu anayeona fursa na kuzitumia katika ‘kufaiti’ kupata mafanikio (utajiri) kwenye maisha.
Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’
Ndivyo alivyo mwandani wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ambaye humwambii kitu linapokuja suala la kuona fursa na kuzifanyia kazi.
Wema Isaac Sepetu
PAMOJA NA HAYO, WEMA MREMBO ZAIDI
Pamoja na sifa hiyo iliyomfanya Zari kuwa mmoja wa mastaa matajiri Afrika Mashariki lakini kwa mujibu wa mashabiki waliomuona ‘laivu’ usiku wa Ijumaa iliyopita kwenye shoo yake ya Zari All White Party katika Ukumbi wa Mlimani City walisema aliyekuwa mpenzi wa Diamond kabla yake, Wema Isaac Sepetu ni mrembo zaidi kuliko yeye.
Wema Sepetu na Zari The Boss Lady
Likiwa ndani ya mjengo, Ijumaa Wikienda liliwashuhudia wadau wengi ambao walimuona Zari kwa mara ya kwanza wakimshangaa na kudai kuwa yupo tofauti na anavyoonekana.
Kwa mujibu wa mashabiki hao, picha ambazo wamekuwa wakiziona kwenye mitandao ya kijamii zinakuwa zimeeditiwa (kuhaririwa) na kwamba ukimuona ‘live’ huwezi kuamini.
YUPO TOFAUTI NA KWENYE PICHA
“Jamani siamini kama huyu ndiye Zari tunayemuona kila siku kwenye Instagramu maana yupo tofauti sana.
“Kwa waliokuwa wanasema anamzidi Wema wamenoa. Wema ni habari nyingine,” alisema mmoja wa warembo waliokuwa wakisukumana kumuona Zari.
“Mimi nadhani ni kwa sababu labda amezaa watoto watatu na sasa ana ujauzito wa Diamond wa mtoto wa nne so hawezi kumfikia Wema ambaye bado hajazaa,” alisema mrembo mwingine akimtetea Zari.
MAKE-UP 100%
“Hamna bwana, kinachombeba Zari ni make-up (vipodozi) ambavyo anatumia kwa asilimia mia moja lakini Madam (Wema) hata asipotumia make-up lazima utampenda tu,” alisema mwingine aliyedaiwa ni Team Wema.
Kuhusu make-up, Ijumaa Wikienda lilizungumza na mmoja wa watu wa Timu ya Diamond ya Wasafi Classic Baby (WCB) ambaye yupo kitengo cha mapambo ambaye alithibitisha kuwa Zari hufanyiwa make-up kwa muda mrefu hadi mwenyewe akubali kuwa yupo sawa.
Mdau mwingine aliliambia gazeti hili kuwa Zari ni mjasiriamali na ameona kwa Diamond kuna fursa ndiyo maana akakubali kumbebea ujauzito lakini si kweli kwamba ni mrembo kuliko Wema.
“Ameona fursa kwa Diamond. Kwa mfano shoo kama hii (Zari All White Party) asingeweza kuifanya bila kuwa na ‘koneksheni’ na Diamond,” alidai mdau mwingine.
 ZARI AMEONA FURSA
Habari zinasema kuwa Zari ameona kuna fursa nyingi Bongo ndiyo maana amekubali kufunga ndoa na Diamond bila kujali kigezo cha umri. Ana umri wa miaka 34 wakati Diamond ni 26.
Akijibu swali juu ya uraia wake wa Uganda na Afrika Kusini na kwamba yeye na Diamond wanatarajia kuishi nchi gani mwanamama huyo alifunguka:
“Tutaishi hapahapa (Bongo). Kwa utamaduni wetu (Waafrika) inabidi mwanamke uondoke nyumbani kwenu umfuate mpenzi wako mkaishi wote.
“Watanzania ni watu poa sana, siwezi hata kuwalinganisha ni wakarimu sana.”
HISTORIA INASEMAJE?
Kuna madai mazito kuwa Zari si mtu wa kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na mtu ambaye hana fursa ya kimaendeleo kwani historia inaonesha kwamba wanaume wengi aliowahi kuwa nao walikuwa ni watu wenye nazo.
 HAJAWAHI KUWA NA MWANAUME HOEHAE
Baadhi ya wanaume waliowahi kuwa naye wanaosemekana kwamba hawakuwa watu hoehae ni pamoja na aliyekuwa mumewe, Ivan Semwanga ambaye alizaa naye watoto watatu akiwa ni mmoja wa mabilionea nchini Uganda.
Wengine ni Isaac Lugudde ambaye ni staa wa mpira wa kikapu nchini Uganda, mtoto wa mjini nchini Uganda, Farouk Sempala, Jenerali Jeje Odong, wasanii wa muziki, Moze Radio na  Weasel, Aziz Azion, Isaiah, Robert Ogwal a.k.a Rasta Rob, Exodus, DJ Shiru, mfanyabiashara mkubwa wa Nigeria na sasa ni zamu ya Diamond.

Le Mutuz: Zari all white party imeingiza 1.8 Billion jamani kina dada zetu bongo amkeni usingizini jiulize Who is Zari?

LEMUTUZ LIVE STRAIGHT TALK:- The "Zari White Party" hesabu za haraka haraka matokeo ni 1.8 Billion ndio maana ya AKILI KUBWA mkiwa mmelala usingizi sana na Mungu anawapenda basi atawaletea AKILI KUBWA ya kuwamsha..jamani kina dada zetu bongo amkeni usingizini jiulize Who is Zari? Kama una AKILI KUBWA utagundua ni Super Star made by Social Media especially Instagram

"NAHITAJI MWANAUME WA KUNIPA PENZI, NIMECHOKA KUWA MPWEKE"...MARIAH CAREY AFUNGUKA

Staa wa muziki wa Pop, Mariah Carey
STAA wa muziki wa Pop, Mariah Carey ameweka bayana kuwa sasa anaweza kupenda tena baada ya kuachana na mzazi mwenzake, Nick Cannon.
Mariah Carey akiwa na aliyekuwa mumewe Nick Cannon.
Staa huyo alisema kuwa lolote linawezekana chini ya jua na kwamba akipata anayempenda, hatajizuia kuwa naye hadharani.Akizungumza na  tovuti ya people.com, staa huyo alisema kwamba hatasita kujiachia na mtu atakayempenda kwani sasa hana kizuizi.
“Nikiwa kama binadamu nina haki ya kupenda na nikimpata ninayempenda, kila mtu atamjua kwa kuwa sitamficha. Hata akitaka kunioa pia nipo tayari,” alisema Mariah Carey mama wa watoto wawili, Oacha Monroe na Morocana aliowapata alipokuwa na mumewe Cannon.

WEMA NA ZARI WAINGIA KWENYE BIFU ZITO SANA..!! SOMA HAPA KUJUA CHANZO


Musa mateja na Imelda Mtema
Nisheedah! Gumzo la mjini wiki hii ilikuwa ni shoo ya mchumba wa Nasibu Abdul ‘Diamond’ Zarinah Hassan ‘Zari’ iitwayo Zari All White Party iliyofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar na ile ya Instagram Party ambayo ilimhusu mrembo Wema Sepetu iliyofanyika jijini Mwanza ambapo nyuma ya pazia, warembo hao walitoana jasho kuhakikisha wanafunikana, Risasi Jumamosi lina stori kamili.

Staa wa Bongo movie,Wema Sepetu.
MVUTANO WAANZA
Kwa mujibu wa chanzo, mvutano wa Wema aliyewahi kuwa mchumba wa Diamond na Zari ambaye anammiliki Diamond kwa sasa, uliibuka Alhamisi iliyopita wakati kila mmoja akijiandaa kwenda kwenye shoo inayomhusu.
“Wema na Zari leo ni full kutoana jasho, kila mmoja anataka kuwavuta mashabiki wengi upande wake.

ZARI APEWA SAPOTI
“Zari amepata sapoti kubwa kutoka kwa mpenzi wake wa sasa Diamond kwani walikuwa wanafanya shoo pamoja hivyo alikuwa na kibarua cha kuwakusanya mashabiki wote wa Diamond waende kwenye shoo yake ili Wema asipate watu,” kilisema chanzo hicho.

UPANDE WA WEMA
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, kwa upande wa Wema, yeye alikuwa na kibarua kizito cha kuwakusanya marafiki zake hususan mastaa wa Bongo Movies wasiende kwa Zari na badala yake waende Mwanza kwenye Instagram Party.

Zarinah Hassan ‘Zari’.
“Ni mnyukano wa aina yake, Wema alikuwa na kibarua kizito kuwashawishi Bongo Movies waikache shoo ya Zari waende Mwanza kwenye Instagram, bahati nzuri alifanikiwa kwani wasanii wengi walimuunga mkono,” kilisema chanzo hicho.
MATUSI
Hadi jana jioni, kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, Timu ya Zari (Team Zari) na ile ya Wema (Team Wema) zilikuwa zikirushiana matusi huku kila mmoja akionesha hisia zake.“Hakuna kwenda kwa Zari, twendeni kwa Wema Mwanza, watakaokwenda kwa Zari ni wapuuzi kabisa,” ilisomeka moja ya komenti ya mdau wa timu Wema huku timu Zari ikijibu:“Wajinga wakubwa watakaokwenda kwa Wema, mpango mzima ni kwa Zari na Diamond pale Mlimani City.”

Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa na mpenzi wake Zarinah Hassan ‘Zari’.
STEVE AFUNGUKA
Ili kuzidi kupata data zaidi, wanahabari wetu walimtafuta mdau mkubwa wa kuwashawishi watu, mwigizaji Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ambaye aliweka bayana kuwa wao kama Bongo Movies, wanamuunga mkono Wema.
“Niweke wazi tu kwamba sisi tutakwenda kwa Wema, hii shoo ya Zari na Diamond itatupitia kushoto kwa kweli,” alisema Steve.

KAJALA KWA ZARI
Kwa upande wake Kajala Masanja alikuwa tofauti na waigizaji wenzake ambapo alipokea kwa mikono miwili mwaliko wa Zari na kuanza kuihamasisha Team Kajala kwenda kwenye shoo  hiyo. 

WEMA AFUNGUKA
Jitihada za kumpata Zari aweze kufungukia mvutano huo hazikuzaa matunda kufuatia simu yake kuita bila majibu lakini bahati nzuri Wema alipatikana na kufunguka:“Mimi kama mimi nakwenda katika shoo inayonihusu ya Instagram, hiyo ya Zari siijui. Sijashawishi mtu ila watu wameamua kuniunga mkono, siwezi kuwazuia na hao wanaofikia hatua ya kutukana pia siwezi kuwazuia,” alisema Wema.

Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa na aliyekuwa mpenzi wake Wema Sepetu.
MWISHO UKOJE?
Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, shoo ya Zari ilitarajiwa kurindima na mashabiki wake huku Wema akiwa na mashabiki wake waliomuunga mkono hivyo kusababisha mtikisiko wa aina yake mjini.

KWA MARA YA KWANZA ZARI AFUNGUKA KWANINI ALIMKUBALI DIAMOND ALIPOMTONGOZA! SOMA HAPA


IMG_4056 
<<Mara ya kwanza ilikuwa kwenye social network tu.. nilikuwa namuonaona tu napita kwenye page yake na-like.. nilitoka kushoot video ya ‘Coco Baby’ South Africa tukakutana kwenye ndege..>>Diamond Platnumz anasimulia walivyokutana na mpenzi wake Zari kwa mara ya kwanza.

Kumbe hiki ndicho kilimvutia sana Zari kwa Diamond Platnumz>>Ni mchangamfu.. anajali.. Diamond ana akili sana, nilivutiwa nae kwa sababu ana akili sana.. anajituma sana, ni mtu mwenye malengo makubwa..>>Zari.
Kwani Diamond amewahi kuonana na watoto wa Zari?? Wanamchukuliaje? >>Bado hawajawahi kuonana.. ila watoto wanamjua.. kama mama yao nina furaha wao wana furaha pia>>—Zari.

HII NDIO KAULI YA MPENZI WA DIAMOND "ZARI" KWA WATANZANIA WOTE..!! SOMA HAPA

Zari Tlale aka The Bosslady amesema upendo anaoupata baada ya kuanzisha uhusiano na Diamond Platnumz, umemfanya agundue kuwa watanzania wamemkubali kama mtu wao.

Akiongea na Clouds FM/TV asubuhi hii, Zari amesema tangu ameanza kuja Tanzania amekuwa akipokea upendo zaidi kutoka kwa watanzania kiasi ambacho kimemfanya ajisikie kama yupo kwao.

“Siwezi hata kulalamika, watu wa Tanzania ni wakarimu sana ni watu wazuri sana, kwangu mimi sijapata hata tatizo, siwezi hata kusema kitu chochote kibaya kuhusu watu wa Tanzania,” alisema.

“Wamenikaribisha kama ni mtu wao na sasa mimi ni wao hivyo ni yote ni heri kabisa,” aliongeza.

Katika hatua nyingine Zari amesema Tanzania itageuka kuwa makazi yake ya mara kwa mara na mipango iliyopo ni kuanzisha mradi wa kibiashara nchini lakini baada ya kufanya utafiti na kubaini fursa za uhakika.

“Siwezi tu nikafungua biashara hapa eti kwasababu mimi ni maarufu nikafungua tu biashara ya kijinga na nikidhani ninaweza nikauza wazo langu la kijinga kwa watu hapa, wao sio wajinga wanatumia hela zao hivyo nahitaji kubaini wapi kuna hitaji, kipi naweza kufanya na hapo ndipo ntaenda na kuwekeza fedha zangu.”

HATIMAYE ZARI AJUA KUONGEA KISWAHILI, MSIKIE HAPA AKIONGEA

Zari Hassan is not only in love with her husband Diamond, but his national language too. Mr. Platnumz seems to have done some good work in making sure that his pregnant wife gets to learn how to effectively and eloquently communicate in Swahili.

Though she was born in Uganda where English is the national language, the Boss Lady has learnt how to fluently speak in the new foreign language. If you doubt it, below is the video promo she did in Swahili for her upcoming All White Party that will be held in Dar es Salaam.

Zari Hassan is not only in love with her husband Diamond, but his national language too. Mr. Platnumz seems to have done some good work in making sure that his pregnant wife gets to learn how to effectively and eloquently communicate in Swahili. Though she was born in Uganda where English is the national language, the Boss Lady has learnt how to fluently speak in the new foreign language. If you doubt it, below is the video promo she did in Swahili for her upcoming All White Party that will be held in Dar es Salaam.

HAWA NDIO WASANII AMBAO USTAA UMEWASHINDA,WAPO KAMA HAWAPO!!!

Na Hamida Hassan
Wapo mabinti ambao waliingia kwenye fani ya uigizaji kwa mbwembwe, wakawika sana kwenye vyombo vya habari na kuunyemelea ustaa lakini ghafla wakayeyuka.Walipoibukia kwenye fani walionekana watakuwa tishio na kuwafunika wale wakongwe waliokuwa wakionekana wao ndiyo wao. Sasa hivi hawajulikani wako wapi na wanafanya nini.

Skaina Ally
Skaina Ally
Huyu alikuwa tishio sana miaka ya nyuma. Umbo lake tata, uzuri wake vilimbeba, akawavutia baadhi ya wanamuziki ambao walimfanya kuwa Video Queen kwenye nyimbo zao kama vile Bob Junior aliyemtumia kwenye ‘kichupa’ chake cha Wimbo wa Kimbiji.

Aliigiza kwenye filamu mbalimbali kupitia Kampuni ya RJ. Hata hivyo, baadaye aliolewa kisha akaachika, mara akabeba ujauzito uliodaiwa ni wa mwanamuziki Nay wa Mitego. Baada ya kujifungua akawa kimya, mwanaye ni mkubwa lakini haijulikani sasa anafanya nini.
Zamda Salim
Huyu naye aliibuka miaka 2010 kwenye soko la filamu. Ana umbo zuri lililomfanya atumike kwenye filamu kadhaa.
 Naye alionekana kuja kuwafunika mastaa lakini cha kushangaza akaanza kufifia na mpaka sasa hata wewe msomaji unayefuatilia masuala ya burudani ukiulizwa yuko wapi na anafanya nini huwezi kuwa na jibu.Mara ya mwisho zilivuja picha akiwa amevaa shela, watu wakasema ameolewa lakini wengine wakadai ni filamu.

Zamda Salim
Ester Flaviana
Huyu ni mmoja wa maandagraundi walioibuka kwa kasi ya ajabu. Aling’ara kwenye magazeti, akaonekana kwenye filamu mbalimbali lakini naye mara ya mwisho zilivuja picha zake za utupu na mpaka leo hii haijulikani kajichimbia wapi.

Diana Kimaro
Diana Kimaro ni binti f’lani mcharuko. Mcharuko wake umeonekana kwenye filamu mbalimbali alizocheza kama vile Family Disaster. Aling’ara sana alipokuwa akiigiza kwenye filamu kama Pacha wa Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Mara ya mwisho alikuwa akisoma Moshi kisha baadaye akaonekana kwenye filamu ya Msuto Daily na Kigodoro lakini hawiki kama anavyowika shoga yake Lulu.

Rehema Fabian
Aliibukia kwenye Shindano la Miss Kiswahili 2008, akapaa zaidi pale alipokuwa akitoka kwenye magazeti na skendo tofauti huku akionekana kwenye filamu mbalimbali.Mara ya mwisho alikimbilia nchini China ambapo alidai kuchumbiwa na mtoto wa kigogo wa Nigeria. Juzikati ilisemekana ni mjamzito, amekaa kimya haijajulikana anafanya nini.

Neema Chande
Huyu alitokea kwenye umiss, alivuma sana alipojiingiza kwenye masuala ya filamu na kufikia hatua ya kutoa filamu yake aliyoipa jina la Time Goes Around. Alipamba kurasa mbalimbali za magazeti kwa habari zake tofauti.
Staa huyu kwa sasa yupo nchini India, anaonekana kwenye mitandao tu ya kijamii, haijulikani anafanya nini huko lakini kwenye anga za mastaa amepotea kabisa.

Pendo wa Maisha Plus
Jina lake kamili ni Upendo Mushi. Staa huyu aliibukia kwenye Shindano la Maisha Plus. Baada ya hapo alicheza kwenye filamu mbalimbali. Kuna kipindi ilidaiwa kutoka na marehemu Kanumba na Diamond Platnumz.
Lakini naye sasa hivi haijulikani anafanya nini. Wapo wanaosema anaigiza lakini habari zake zimekuwa ngumu kuzipata tofauti na ilivyokuwa zamani ambapo alikuwa hakauki kwenye vyombo vya habari.

Amisuu Malick
Huyu naye alipamba kurasa za magazeti baada ya kuibukia kwenye umiss. Wapo wanaodai alichumbiwa ndiyo sababu ya kuwa kimya.Marafiki zake wa karibu wanasema kuwa ameamua kutulia na kufanya mambo yake ambayo si lazima yaanikwe hadharani.

Sharzy Sadry
Huyu naye ni staa ambaye alitoka na marehemu Steven Kanumba kwenye filamu ya ‘The Shock’. Alionekana kuwashtua mastaa wa Bongo kwani filamu hiyo aliicheza kwa umahiri.Wapo waliosema kuwa Kanumba alimchukua ili kuziba pengo la Wema kwani kwa wakati huo Wema na Kanumba walikuwa wameachana.

Halima Madiwa
Aliibukia kwenye uigizaji wa filamu. Waliomchezesha kwenye filamu waliamini kuwa angekuja kuwa tishio. Akawa hakauki kwenye magazeti lakini naye cha ajabu kapotea.

HAMISA MABETO KAMA KIM, AMBER ROSE! UNAJUA KAFANYAJE?? SOMA HAPA


Na Hamida Hassan
Tabia ya mastaa kujipiga picha za nusu utupu wakiwa na mimba haikuwepo Bongo, wamekuwa wakifanya hivyo mastaa wa nje kama vile Kim Kardashian, Amber Rose na wengineo lakini mwanamitindo, Hamisa Mabeto amefanya hivyo kisha kuzitupia picha zake mtandaoni.

Hamisa Mabeto.
Hamisa alijifungua hivi karibu baada ya kufanikiwa kuificha mimba yake lakini kumbe alijipiga picha hizo za kihasara kisha kuzihifadhi.
Hata hivyo, baada ya mwanadada huyo kuziachia picha hizo, wapo walioonekana kumpongeza kwa namna mimba ilivyokuwa imempendeza lakini wapo waliomponda kwa kusema kuwa, hayo siyo maadili ya Kitanzania.
 Mabeto hakuweza kupatikana mara moja kuzungumzia sababu ya yeye kupiga picha hizo na kuziachia kwenye mitandao.


"KAMWE SIWEZI KUMLILIA MWANAUME...UZURI WANGU UNATOSHA KUPATA MABWANA WENGI NIWATAKAO!...''LULU

Wakati wanawake wengine wakionekana kubembeleza penzi na kujinyenyekeza kwa wapenzi wao ili wasiachike, Lulu Michael anasema hana muda huo kwani uzuri wake unatosha kuwavuta wanaume wa kila aina kutoka katika kila kona ya Tanzania.....

Lulu amedai kuwa inawezekana mwanaume wa kwanza kwake ndo chaguo lake namba moja, lakini suala la kuanza kulilia mapenzi au kuumia halipo na kamwe hawezi kufanya hivyo.

LULU NA KISA CHA MAISHA YA MVUNJA KIKOMBE!

SIKU za hivi karibuni imekuwa ikiripotiwa mtafaruku uliopo kati ya staa wa Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na mama wa aliyekuwa nyota wa tasnia hiyo, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa.Miongoni mwa mambo yanayozua hali hiyo, kwa mujibu wa mama Kanumba, ni kitendo cha Lulu kumsahau kama ‘mama’ yake na hivyo kukiuka ‘kiapo’ cha awali cha Lulu kumchukulia mama Kanumba katika udugu wa umama.
Staa wa Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Kiapo hiki kiliwekwa siku chache baada ya Lulu kuachiwa kwa dhamana akitoka kwenye Gereza la Segerea jijini Dar es Salaam alipokuwa akishikiliwa kwa madai ya kumuua Kanumba pasipo kukusudia.Siwezi kurudia hatua kwa hatua ya tukio hilo, wengi wanalifahamu lakini kwa ufupi tu, kifo cha Kanumba kilichotokea Aprili 7, mwaka 2012, nyumbani kwa marehemu huyo, Sinza ya Vatcan, Dar kilidaiwa kusababishwa na ugomvi mkubwa kati yake na Lulu chanzo kikisemekana kuwa ni wivu wa kimapenzi.
Lulu alikamatwa, akapelekewa Segerea huku akihudhuria kesi kwenye Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Dar es Salaam hadi alipoachiwa kwa dhamana Desemba 12, 2012.
MAISHA YAKE NA
MAMA KANUMBA
Ilikuwa baada ya kutoka jela, Lulu na mama yake, Lucresia Karugila ilisemekana walikwenda nyumbani kwa mama wa marehemu Kanumba, Mbezi ya Temboni, Dar kwa lengo la kumuomba radhi mwanamke huyo kwa yote yaliyotokea (ndiyo ubinadamu).Mama Kanumba aliwapokea vizuri, akawasikiliza, akamkubalia Lulu na ombi lake huku akisema yeye anaamini yaliyojiri ni mipango ya Mungu, akatoa la moyoni kwamba, atamchukulia Lulu kama mtoto wake kuanzia siku hiyo. Kwa maana hiyo, Lulu alichukua nafasi ya marehemu Kanumba.

MAISHA YALIENDELEA,
AMANI KILA KUKICHA
Tofauti na baadhi ya watu kuamini kwamba, mama Kanumba (kwa namna yoyote ile) asingekubali kumwona Lulu machoni pake maana akimwona anakumbushwa ‘machungu’ ya kifo cha mwanaye lakini ikawa kinyume, Lulu, mama Lulu na mama Kanumba wakawa kitu kimoja. Wakatangaza udugu.

Hata Lulu mwenyewe alibadili staili yake ya maisha, kujirusha kwa sana kwenye klabu za starehe za usiku kukaisha, sasa akawa mtu wa karibu sana na mama Kanumba kama mama yake.Magazeti Pendwa ya Global Publishers yaliripoti ukaribu wa watatu hao kiasi kwamba, ilikuwa raha tupu! Hapa mama Lulu, pale mama Kanumba, kule Lulu mwenyewe.
Ilifika mahali kila mwaka (tangu 2013), kwenye kumbukumbu ya kifo cha Kanumba, Lulu, mama yake na mama Kanumba walikuwa wakishirikiana kwa karibu sana. Walifika kanisani wote, makaburini wote na kuishia kwa shughuli nyingine.
Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiwa na mama Kanumba.
MABADILIKO KWA LULU
Hakuna aliyekuwa akijua kwamba Lulu kumbe ameanza kubadilika. Kwamba, hamtafuti mama Kanumba kama zamani kumjulia hali, hamsaidii kama ilivyokuwa awali.Hali hiyo ilitokea kumkera sana mama Kanumba kiasi kwamba, akizungumza na Magazeti Pendwa ya Global Publishers, siku ya kumbukumbu ya kifo cha Kanumba Aprili 7, mwaka huu kwenye Makaburi ya Kinondoni, Dar ambako ndiko alikozikwa marehemu huyo (Lulu hakufika), mama huyo alisema:

“Nasikitika sana namna ambavyo Lulu amekuwa tofauti na maneno yake ya zamani kwamba atakuwa sambamba na mimi katika kuadhimisha kumbukumbu ya Kanumba. Lakini leo kama hivi, hajatokea.
“Pia nasikitishwa kitendo cha kufanya bethidei ya mdogo wake jana (Jumatatu usiku) kule Posta wakati anajua ndiyo usiku ambao Kanumba alifariki dunia.

“Mbaya zaidi, akiulizwa na watu kwa nini sasa hivi hayupo sambamba na mimi kama zamani, anajibu majibu ambayo hayaeleweki. Kumbe maneno yake ya zamani kwamba atakuwa sambamba na mimi yalikuwa ya usaliti.
“Kwa hiyo na mimi sasa nimeamua kubaki peke yangu kama nilivyo, nitaendelea kumuenzi Kanumba mwanangu kwa sababu mimi ndiyo mama yake.”
Lulu alipoulizwa alijibu kuwa kwa sasa anaendelea na maisha yake na mtazamo mpya, alilia kifo cha Kanumba na hawezi kulia tena.

KWA MAANA HIYO SASA
Mtafaruku wa wawili hao unafanana sana na kisa kimoja nilichowahi kusimuliwa na mke wangu, kwamba kuna familia moja ilikuwa ikiishi na baba na mabinti wawili.Baba wa familia alikuwa mkali kupita kawaida. Mara zote kulipotokea kosa kwa watoto hao, mhusika alichapwa sana ili kukanywa. Hali hiyo ilisababisha kuzua hofu miongoni mwao na kumwogopa baba yao katika hali ya uadui.

Siku moja, binti mdogo alivunja kikombe, kwa kujua baba yake ni mkali sana atakuja kupigwa, alianza kulia mwenyewe huku akimsihi dada yake kuliweka moyoni hilo la kikombe kuvunjika.Dada mtu alimwambia ili asije kumsemea kwa baba yake na kuchapwa, afanye kazi mbalimbali ambazo alimpa. Binti hakuwa na jinsi, alifanya kazi hizo kwa moyo mweupe na kweli hakusemewe.
Lakini ikawa kila siku baba yao akiondoka akiacha maagizo ya kazi za kufanya zikiwemo ngumungumu kama kuchota maji, dada mtu alimwamuru mdogo wake kuzifanya huku akimtishia kwamba akigoma atamwambia baba yake kuhusu kikombe.
Binti alianza kubadilika mwonekano kwa sababu ya kufanya kazi ngumu na nyingi peke yake. Lakini mambo yalipomzidia, siku moja alimwambia baba yake ana shida. Baba alimsikiliza, akafunguka mambo yote kuanzia kwenye kuvunja kikombe hadi kufanya kazi zote peke yake. Huwezi amini, baba huyo alimkumbatia binti yake na kumwambia: “Nimekusamehe kuhusu kuvunja kikombe, adhabu uliyopata ni kubwa mwanangu.” Ukawa ndiyo mwisho wa utumwa!
KWA MAMA
KANUMBA NA LULU
Nimekuwa nikiyapima maneno ya mama Kanumba kwa Lulu na kubaini kwamba, kumbe mama huyo alitaka Lulu aishi maisha ya binti aliyevunja kikombe!Kwamba, kwa vile Lulu alikwenda nyumbani kwake na ‘kuungama’ kuhusu yaliyotokea nyuma na yeye kumsamehe na kuchukuliana kama mama na mtoto wake, alitakiwa kuishi hivyo maisha yake yote hadi kifo.

Mama Kanumba alitaka akikohoa, Lulu kafika. Akiwa na kiu ya maji, Lulu huyu hapa! Akihisi maumivu ya kichwa, Lulu katia timu. Kitendo cha Lulu kuamua kufanya mambo yake na kumsahau yeye, imebidi mama huyo apaze sauti kusema! (kama alivyofanya makaburini).
Naamini Lulu aliliona hilo mapema sana na akavumilia kuhakikisha hafanyi kosa ili mama Kanumba asipaze sauti kwa jamii kumsemea, yeye angewahi kujisemea mwenyewe ili asamehewe na kuwa huru!   

Agness Masogange Ajibu Maswali Kuhusu Tuhuma za Kufukuzwa South Africa, Kazi Anayoifanya South Africa, Kuhusu Mtoto Wake na Kuhusu Boifriend

Q1. Tulisikiaga umepata uraia wa south na ulisema hutorudi bongo ....mbona umerudi ghafla na kuna madai umetimuliwa ukweli ni upi?
.
AGGY:Hapa ni home hata iweje so ninapojiskia hamu ya kurudi narudi lkn sauz ndo sehemu ya kufanyia biashara zangu..
.
Q2: unafanya biashara gani ambayo watu hawaioni?.
.
AGGY:Sio lazima kila unachofanya lazima watu wajue, unachotakiwa kujua ni kwamba nafanya biashara zangu kule.
.
Q3: Tulisikia umepata mchumba huko south na ndo anayekupa jeuri ya kwenda na kuishi south.
.
AGGY:Ni kweli nina mchumba lakini hata nikienda kule siishi kwake nakaa kwangu na najilipia kodi mwenyewe
.
Q4: ulikuwa na mwanaume wako hapa bongo ambaye alikuwa anakupenda sana anaitwa Evance ilikuwaje ukammwaga??.
.
AGGY:Unajua kila mtu anapoamua kufanya jambo anakuwa ana sababu zakw mi naona Mungu tu akuamua tuwe pamoja hadi leo.
.
Q5: Hivi karibuni mtandao mmoja ulikuandika ww ndiye mwanamke mwenye shepu hatari africa mashariki je uliichukuliaje ile habari?
.
AGGY:Ahahahaaa nilijiskia vizuri na pia nilicheka sana nikajiuliza walinijuaje?
.
Q6: unasema sshv makazi yako ni south je ukipata mchumba bongo utakubali kurudi na kufunga nae ndoa?
.
AGGY: Hakuna mtu anayenizuia huko south km ntaridhika nae kwanini nisirudi?
.
Q7: wewe una mtoto lkn hujawahi kumpost hata siku moja km unavyopost zako na km mastar wenzio wanavyopoa watoto zao kwanini?
.
AGGY: Unajua unapozaa mtoto anakuwa sio mali yako pekeyako kuna babake pia ..siwezi kufanya hivyo kwa kuwa babake hapendi..
.
Q8: Hili suala la wewe kukamatwa na unga limewashitua wengi unawashauri nini wasichana wanaoifanya au wanaotaka kufanya hii deal?.
.
AGGY: Ni suala la kujitambua na kufikiri kabla ya kufanya ile sio kazi ya kufanya kwakuwa ukikamatwa majuto ni lazima
.
Q9: Tunajua ww hauna ttzo la kutozaa sbb tayari una mtoto je una mpango wa kupata mwingine?
.
AGGY: Kwa sasa sina mpango huo labda baadae sanaaa..
.
Q10: kwa sasa huonekani ktk video za muziki km zaman (video queen)vp au umeacha hii kazi
.
AGGY: Sijaacha na siwezi kuacha sema tu sijapata hilo deal kikubwa ni maslahi tu

ZARI AONYWA VIATU VIREFU NA UJAUZITO


MWANDISHI WETU
UBAVU wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari’ ameonywa kuacha viatu virefu kutokana na ujauzito alionao.
Kwa mujibu wa daktari mmoja ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini, alisema kama anataka kujifungua salama basi ahakikishe anaachana na suala la kuvaa viatu virefu kwa wakati huu ambao ni mjamzito.

Ubavu wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari’.
“Kama anajipenda na anampenda mwanaye ajaye, anapaswa kuachana na mambo ya viatu virefu kwa sasa hadi pale atakapojifungua,” alisema daktari huyo.Katika picha za hivi karibuni ambazo Zari amepigwa, tumbo lake linaonesha kwamba tayari mimba yake ni kubwa na yuko mbioni kuelekea kujifungua.
Older Posts
© Copyright ZEE LA UDAKU | Designed By Code Nirvana
Back To Top