Habari Kali
Loading...

AJALI YA BASI NA TRENI YAUA 5 NA KUJERUHI 24 WILAYANI KILOSA


Maofisa wa usalama barabarani wakichukua taarifa eneo la ajali.
Coaster baada ya kuigonga treni.
Wananchi wakishuhudia ajali hiyo.
WATU watano wamepoteza maisha huku 24 wakijeruhiwa baada ya basi la abiria kuligonga treni lililokuwa linatoka Morogoro – Dodoma leo asubuhi katika eneo la Kibaoni, wilayani Kilosa mkoani Morogoro.
Basi lililohusika katika ajali hiyo ni aina ya Isuzu Coaster lenye namba za usajili T837 CTM linalomilikiwa na Feisal A. Khuwel wa wilayani Kilosa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa ajali hiyo imetokea leo majira ya saa 1 asubuhi na imetokana na uzembe wa dereva wa basi.
Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wiaya Kilosa, Dickson Masale amethibitisha kupokea miili ya watu watano akiwemo dereva wa basi pamoja na majeruhi 24.

MAFURIKO DAR YALIVYOACHA VILIO! TAZAMA PICHA HAPA


Stori: Haruni Sanchawa na Makongoro Oging’
Mvua kubwa iliyonyesha ambayo haijawahi kunyesha ndani ya Jiji la Dar es Salaam kwa kipindi cha miaka kumi,  imeacha vilio na umaskini mkubwa kwa wakazi  wake, imebainika.
Mwili ukiwa kwenye gari la polisi.
Timu ya Uwazi kipindi chote cha mvua ilikuwa mitaani na kubaini kuwa hadi juzi watu zaidi ya kumi walipoteza maisha kutokana na mvua hiyo na baadhi ya miili iliyopatikana haijatambulika na ndugu zao na waliotambuliwa wameshazikwa na kuacha vilio.
Aidha, waandishi wetu walishuhudia jeshi la polisi likitoa maiti moja katika Mto Msimbazi uliyoko Magomeni jijini Dar es Salaam, hata hivyo haikuweza kutambuliwa hivyo kuaminika kuwa ilisombwa na maji kutoka mbali.Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Kipolisi ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova aliliambia Uwazi kuwa maiti kadhaa zilikuwa zimehifadhiwa Hospitali ya Muhimbili na ndugu walikuwa hawafahamiki na kuwataka waliopotelewa na ndugu zao kwenda kuzitambua. 
Waandishi wetu katika mitaa mbalimbali jijini Dar es Salaam, walibaini athari kubwa za maji yaliyoingia katika majumba ya watu hasa maeneo ya Jangwani, Kigogo, Kinondoni na wakazi wake kuachwa wakiwa hawana makazi ya kuishi, hivyo familia kusambaratika.
Maeneo ya Jangwani ilionekana kama kisiwa kwani nyumba nyingi zilizingirwa na maji na kuhamwa na wakazi wake, huku wengine wakilalamika kuwa wamepoteza mali zao ambazo zimesombwa na maji na mbwa wa polisi walitumika kusaka maiti.
Mwili ulioopolewa kwenye maji.
Neema Laulence mkazi wa  Magomeni Makuti, alisema kuwa kutokana na mvua hiyo, watu  wamekosa makazi baada ya nyumba zao kujaa maji, hata hivyo alisema serikali haipaswi kulaumiwa kwa sababu viongozi wa mkoa wamejitahidi sana kuelimisha wanaoishi mabondeni ili wahame lakini wamekuwa wabishi.
Abdallah Hamis alisema: “Mvua hii ni kubwa na haijawahi kutokea na walioathirika wajilaumu wenyewe maana  serikali ilishatoa viwanja Mabwepande lakini baadhi yao waliviuza na kurudi mabondeni.”Naye Mwanaisha Hamisi maarufu kwa jina la mama Kabang, alisema  serikali itumie nguvu kuwahamisha watu wanaokaa mabondeni kwa sababu wanapofariki taifa linapata aibu.
“Ni aibu serikali kushindwa kuwadhibiti watu wanaong’ang’ania kuishi mabondeni. Iwahamishe kwa nguvu,” alisema Mwanaisha.Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Dk. Agnes Kijazi akizungumzia hali ya mvua nchini alisema: “Maeneo ambayo hali ya mvua inaweza kuyaathiri zaidi na kukumbwa na vimbunga ni pamoja na kanda ya kati, nyanda za juu kusini magharibi, magharibi mwa nchi na maeneo ya ukanda wa Pwani hivyo wananchi wachukue tahadhari.”
Nyumba ikizingilwa na maji.
Naye Mkuu  wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Said Meck Sadik alisema anasikitishwa na kitendo cha baadhi ya watu kuilaumu serikali wakati miaka mingi imekuwa ikiwahimiza wanaoishi mabondeni kuhama.
“Ukweli ni kwamba safari hii hatuwapi hifadhi kwa sababu wamekuwa jeuri na pia baadhi yao wameishitaki serikali mahakamani, sasa tufanye nini?” alihoji.

PICHA: ATHARI YA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA DAR NA PWANI

Eneo la Stendi Kuu ya Mabasi Bagamoyo lilivyokumbwa na mafuriko ya mvua zinazoendelea kunyesha.
Maji yakitapakaa eneo la Stendi Kuu ya Bagamoyo hivyo kusababisha usafiri na biashara ndogondogo kusitishwa kwa muda.
Gari likiwa limesombwa na mafuriko jijini Dar.
Waliokuwemo kwenye gari hilo ni dereva na bosi wake ambao hawakufahamika majina lakini walifanikiwa kujiokoa.

Bado tatizo la ajali TZ limeendelea kukaa kwenye headlines, hii imetokea leo Morogoro..

AJAStori za ajali Tanzania zimekuwa kwenye headlines nyingi.. cha kushtua zaidi ni kwamba ajali hizi zimetokea mfululizo sana, watu wengi wamefariki, wengine wengi majeruhi.. mara nyingi mwendokasi umehusshwa sana na hizi ajali.
Leo iko hii kutoka Morogoro, watu 15 kujeruhiwa na wengine zaidi ya 50 wamenusurika katika ajali ya basi la Takbir lililokuwa likitokea Geita kuligonga basi la kampuni ya Abood katika eneo la Lubungo Mikese.
Majeruhi wa ajali hiyo wamesema chanzo cha ajali ni  dereva wa basi la Takbir kutokuwa makini na kuendesha gari kwa mwendokasi.. baada ya ajali hiyo dereva huyo alikimbia.
Kamanda wa Polisi Morogoro, Leonard Paulo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

SAD NEWS: Zaidi ya Watu 900 Wadaiwa Kupoteza Maisha kwa Tetemeko la Ardhi Nchini Nepal !


TETEMEKO la ardhi limetokea nchini Nepal jana  na na kupoteza maisha ya watu  ya 900 na kuangusha Mnara wa Karne ya 19 Mjini, Kathmandu pamoja na kusababisha maporomoko ya theluji kutoka katika milima. 

Taarifa zinadai kuna uharibifu katika maeneo ya nje ya kitovu cha tetemeko hilo lenye ukubwa wa kipimo cha richter cha 7.9 maili 50 kutoka Pokhara mji wa pili kwa ukubwa nchini Nepal. 

Tetetemeko hilo la ardhi ni kubwa kabisa kuwahi kuikumba nchi hiyo katika kipindi cha miaka 81 na pia limesababisha athari katika majimbo ya nchi jirani kaskazini mwa India na Bangladesh. 

Kunauwezekano vifo hivyo vinaweza kuongezeka katika Bonde la Kathmandu ambalo lina watu milioni 2.5.

Naibu balozi wa Nepal mjini New Delhi Prasad Pandey amesema inahofiwa kuwa mamia ya watu wamekufa na kuna ripoti ya kuwepo kwa uharibifu mkubwa kila sehemu kubwa na kwamba sio tu katika baadhi ya maeneo ya Nepal bali ni nchi nzima imeathirika. 

Nepal ilikumbwa na tetemeko kubwa la ardhi kuwahi kurekodiwa nchini humo hapo mwaka 1934 likiwa na kipimo cha 8.0 ambapo watu 8,500 walipoteza maisha yao.
Baadhi ya Waokoaji wakiwa wamsaidia mmoja wa waathirika wa Tetemoko hilo aliekuwa amefukiwa kwenye kifusi ya moja ya majembo yaliyoporokoma kutokana na tetemeoko hilo.
Sehemu ya athari za tetemeko hilo.
Jitihada za kuokoa waliofunikwa na kifusi zikiendelea.
Wananchi wa Nepal wakishirikiana kwa pamoja kuvuta kamba. 

Ramani inayoonyesha sehemu iliyokumbwa na tetemeko hilo.
 
Picha zote kwa hisani ya Mtandao wa Daily Mail

BREAKING NEWS: AJALI MBAYA YATOKEA SHINYANGA NA KUUA WATU 10! TAZAMA PICHA HAPA

candles
Imekuwa ishu kubwa kwenye vyombo vya Habari sasa hivi.. mfululizo wa ajali za barabarani kila mtu anapata maswali mengi, nini chanzo cha ajali hizo? Njia ipi itumike ili kumaliza tatizo la ajali??
Wakati hayo yakiendelea naipokea ripoti nyingine toka Shinyanga, inahusu ajali ya basi la Unique ambalo limegongana na lori, kwenye ajali hiyo watu 10 wamefariki.. zimepita siku chache tu toka itokee ajali ya Toyota Hiace ambayo iliua watu 19 Mbeya pamoja na kuporomoka kwa mgodi ambao ulifukia watu 19 Kahama.
IMG-20150422-WA0031
IMG-20150422-WA0032
IMG-20150422-WA0034
IMG-20150422-WA0035
IMG-20150422-WA0037

AJALI TATU VIFO 40 NDANI YA SIKU SITA!

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Mohamed Msangi.
MSHITUKO wa matukio ya mfululizo ya ajali, umeendelea kugubika nchi, baada ya watu 20 kupoteza maisha katika ajali ya basi dogo aina ya Toyota Hiace, iliyotokea jana wilayani Rungwe mkoani Mbeya.
Ajali hiyo ambayo taarifa na picha zake zilisambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii, imesababisha taharuki kutokana na ukaribu wake na matukio mengine ya ajali yaliyotokea wiki hii.

Baadhi ya wakazi wa jirani na eneola tukio wakitazama gari lilivyopata ajali kando kando ya mto Kiwira.
Tangu Jumapili iliyopita mpaka jana, siku zisizozidi sita kumetokea ajali kubwa tatu zilizohusisha mabasi ya abiria na kuteketeza maisha ya watu 40.
Mbali na ajali hizo, wiki hii Kamanda wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga alitoa takwimu zilizosababisha huzuni kwa Watanzania, kwamba kati ya Januari mosi na Aprili 12 sawa na siku 102, watu 969 walipoteza maisha katika ajali za barabarani.

Wananchi wa Kiwira wakiangalia baadhi ya Miili ya Watu waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo.
Ajali za wiki
Jumatano wiki hii, basi la Air Jordan lililokuwa likitokea mkoani Mwanza kwenda Arusha, lilipata ajali na kusababisha kifo cha mtu mmoja na majeruhi 20.

Ajali hiyo ilitokea wakati Watanzania wakiwa na kumbukumbu ya ajali iliyotokea Jumapili ya wiki jana, ambapo watu 19 waliteketea kwa moto, baada ya basi la Kampuni ya Nganga Express na lori aina ya Fuso kugongana uso kwa uso na kuwaka moto katika eneo la Iyovi, Milima ya Udzungwa, mkoani Morogoro.
Ajali ya Mbeya
Akizungumza na gazeti hili jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Mohamed Msangi, alisema ajali hiyo mpya imetokea katika eneo la Ilongo ambalo limebatizwa jina la Uwanja wa Ndege karibu na Kiwira, ambapo watu 18 walipoteza maisha papo hapo.

“Watu wanne waliojeruhiwa, mmoja alikuwa katika hali mbaya na kwa bahati mbaya alifia njiani wakati akipelekwa Hospitali ya Wilaya ya Rungwe kwa matibabu,” alisema Kamanda Msangi.
Kamanda Msangi alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi na dereva kutokuwa makini katika uendeshaji wake. Taarifa zilizotufikia baadae, zilieleza kuwa abiria mwingine aliyekuwa akipatiwa matibabu, alifariki akiwa hospitalini.

Mashuhuda
Mashuhuda wa ajali hiyo walidai kuwa chanzo cha ajali ni mwendokasi uliosababisha dereva ashindwe kumudu gari hilo katika mteremko wenye kona, akajikuta gari likimshinda na kutumbukia katika Mto Kiwira.
Walidai kuna uwezekano dereva huyo alikuwa akikimbizwa na baadhi ya madereva wa mabasi aina ya Toyota Coaster, yanayofanya safari zake kati ya Mbeya, Tukuyu na Kyela.

(CHANZO:GAZETI LA HABARI LEO)

ANGALIA HAPA PICHA KUTOKA KWENYE AJALI YA GARI ILIYOUA 19 LEO JIJINI MBEYA.

Ajali za Tanzania kwenye vichwa vya habari zimezidi kuongezeka, leo April 17 2015 ajali nyingine imetokea Mbeya baada ya gari la abiria kupoteza mwelekeo na kuingia mtoni Mbeya. Taarifa zilizothibitishwa na kamanda wa Polisi Mbeya zinasema waliofariki mpaka sasa ni 19,

MAAJABU 5 AJALI YA BASI, FUSO! TAZAMA PICHA HAPA


Muonekano wa alama ya mnyama anayefanana na Chui akitembea akiwa na mtoto wakati wa magari hayo yakiwaka moto.
WAANDISHI WETU
MAAJABU matano yameibuka kufuatia ajali mbaya iliyohusisha lori aina ya Fuso na basi la abiria iliyotokea Jumapili iliyopita eneo la Iyovi, Ruaha, Kilosa mkoani Morogoro ambapo zaidi ya watu 19 walifariki dunia, 13 kati yao kuteketea kwa moto na kuzikwa kwenye kaburi moja katika Makaburi ya Msavu mwanzoni mwa wiki hii, Amani linakujuza.
Ajali hiyo ilitokea baada ya lori hilo lenye namba za usajili T 164 BKG kugongana na basi la abiria la Kampuni ya Nganga lenye namba za usajili T 373 DAH lililokuwa likisafiri kutoka Kilombero mkoani Morogoro kuelekea Mbeya eneo la Kijiji cha Msimba katika Tarafa ya Mikumi.
Picha ikionyesha mtu akiwa amevaa vazi la kanzu huku kiunoni kama  amejifunga mkanda, kama zilivyo picha za kuchorwa zinazowaonesha wanafunzi wa Yesu, Inasemwa na watu kuwa mtu huyo, huenda ni malaika wa amani.
Ajabu la kwanza linaloonekana kwenye picha zilizopigwa wakati magari hayo yakiungua moto, zinaonesha alama ya mnyama anayefanana na Chui akitembea akiwa na mtoto wake, kitu ambacho kimewafanya watu wengi kushindwa kutafsiri suala hilo.
Kana kwamba haitoshi, katika picha hiyo chini kidogo ya mnyama huyo, kuna ajabu lingine ambapo picha kama ya mtu akiwa amevaa vazi la kanzu huku kiunoni kama  amejifunga mkanda, kama zilivyo picha za kuchorwa zinazowaonesha wanafunzi wa Yesu. Inasemwa na watu kuwa mtu huyo, huenda ni malaika wa amani.
Ajabu la tatu katika tukio hilo la kusikitisha ni mpigapicha ambaye anahisiwa kuwa ndani ya gari dogo, umbali wa mita kadhaa kutoka eneo la tukio. Lakini wakati picha hiyo ikionesha mvua zilikuwa zikinyesha na barabara kuonekana kuloa kutokana na maji ya mvua, lakini katika eneo ambalo magari hayo yaligongana, kunaonekana kukavu jambo linalozua maswali mengi kuliko majibu.
Ajabu la nne ni kuwepo kwa taarifa kutoka kwa walionusurika katika ajali hiyo kuwa mmoja wa marehemu, aliweza kuzungumza kwa simu na wanaodhaniwa kuwa ndugu zake wakati akiteketea kwa moto. Inadaiwa kuwa walimsikia akiwaambia kuwa sauti wanayoisikia ni ya moto na kwamba atakata kauli wakati wowote na hakuelewa kama wangeitambua maiti yake.
Muonekano wa magari hayo baada ya kuwaka moto.
Na ajabu la mwisho kabisa katika ajali hiyo ni maelezo ya kuwa mmoja wa marehemu aliyefariki dunia baada ya kuungua moto, ni pale alipotambuliwa baada ya kuonekana mabaki ya mguu wake mmoja, uliokuwa na kiatu. Inadaiwa kuwa ndugu walimtambua kutokana na masalia ya kiatu hicho, ingawa mwili wake wote ulikuwa umeungua vibaya na asingeweza kutambuliwa.
Hata hivyo, akizungumza na gazeti hili kuhusu ajali hiyo, mtabiri maarufu Maalim Yahya Hussein, alisema ajali hiyo haikuwa ya kawaida, kwani siyo rahisi kwa moto kuanzia kwenye buti, tena kwa mlipuko wa ghafla. Aliihusisha ajali hiyo na harakati za kisiasa, akisema ni mwaka wa uchaguzi, ambao una mambo mengi.
Polisi wakiwa eneo la tukio.
Kuhusu picha ya mtu anayeonekana, ambaye katika mitandao kadhaa ya kijamii anatajwa kuwa ni malaika, alisema anayeonekana siyo malaika, kwani wao kazi yao ni kusaidia.
Mazishi ya watu hao yalifanyika Jumatatu iliyopita na kuhudhuriwa na viongozi wa dini zote, wa serikali na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa, tukio hilo la simanzi lililowatoa machozi mamia ya waombolezaji waliojitokeza.

BASI LA DAR EXPRESS LAPATA AJALI MBAYA: TAZAMA PICHA HAPA

ZAIDI ya abiria 60 wamenusurika kifo, baada ya basi la Dar Express lililokuwa linatoka Dar kwenda Nairobi kupasuka tairi la mbele kushoto kisha kupinduka katika eneo la Msata karibu na daraja la Wami mkoani Pwani leo.

TAHADHARI: KONA HIZI ZA IYOVI NI KALI, DEREVA KUWA MAKINI, EPUSHA MAISHA YA ABIRIA

Wewe ni  dereva  wa basi la abiria ama gari  binafsi ? hebu  chukua  hatua ya  kupunguza ajali  leo kwa kujihadhari na  kona  hizi na Iyovi na Kitonga na  kona  nyingine kali kama  hizi nchini kwani maisha  yako ni  dhamani  kubwa na uhai  wake bado tunautamani.
 Vema  kuheshimu alama  za barabarani na  kuacha mbwembwe  uwapo  barabarani katika kona kali kama hizi.
 Katika kona  kama  hizi  zingatia  alama  za usalama  barabarani  usiwe na haraka  ya  kulipita gari la mbele.
Kulipita gari la mbele katika kona kama hizi ni hatari.
Hapa  ni eneo ambalo  watu 19  walipoteza maisha kwa fuso kugongana na basi na Nganga na kisha  kuwaka  moto uzembe  ukiwa ni wa dereva wa basi aliyetaka  kulipita gari la  mbele  katika  kona kali.
 
 Usilipite gari katika  kona kama hili.
 Alama  zote  za barabarani ni msaada kwa maisha  yako lazima  uziheshimu
 Kona  zote ni hatari kwa usalama  wako hivyo  usihame saiti  yako ili  kukimbia ajali.
 Lazima  unapotaka  kulipita gari la  mbele uwe una uwezo wa kuona mbali  zaidi ya mita  100 ama  zaidi.
 Dereva makini halipiti gari  la  mbele katika  kona

Kumbuka  ni  heri  kuchelewa  ukafika  salama  kuliko kuendesha kwa haraka na ukafika majeruhi ama maiti tambua Taifa  linakuhitaji familia  inakuhitaji na  wewe  dereva ni msaada wa abiria  wote katika gari lako  na  msaada wa maisha  yako jitambue ,watambue abiria  wako , jilinde utulinde  abiria  wako maisha  yako   ni yetu na uhai  wako ni tegemeo letu epuka ajali zingatia sheria  za barabarani. IMETOLEWA NA MATUKIODAIMABLOG

BREAKING NEWZ: AJALI YAUA MMOJA, 25 WAKIJERUHIWA NZEGA!


Basi la abiria la Jordani baada ya kupinduka wilayani Nzega leo.
Mashuhuda wa ajali hiyo wakiwa eneo la tukio.
Marehemu katika ajali hiyo akiwa amelaliwa na basi hilo.
MTU mmoja amefariki dunia huku 25 wakijeruhiwa katika ajali ya basi la abiria la Jordan lililopinduka leo wilayani Nzega, mkoani Tabora.
Basi hilo lilikuwa likitokea mkoani Mwanza kwenda Arusha na limepinduka majira ya saa nne asubuhi.

AJALI HIZI, KUNA KITU..SIO BURE!


Ajali iliyohusisha basi la kampuni ya Nganga na Fuso yakiwaka moto.
KWANZA kabisa tumshukuru Mungu kwa kutuweka hai, hakika yeye anastahili kuabudiwa kila siku.
Baada ya kusema hayo nianze kwa kuwataka wasomaji wangu kutafakari kwa kina hizi ajali za mabasi zinazotokea mara kwa mara katika barabara za nchi yetu.

Kwa muda wa siku zisizozidi kumi na nane zimetokea ajali mbaya tatu za mabasi na kusababisha Watanzania wenzetu zaidi ya ishirini kupoteza maisha.Kule Mkata, Handeni Tanga watu kumi walifariki dunia baada ya mabasi kugongana na njia ya Mikumi, Morogoro mabasi yaligongana na watu wawili waliaga dunia na kuacha wengi wakiwa majeruhi.
Jumapili iliyopita katika eneo la Ruaha Mbuyuni basi liligongana na Fuso na kusababisha watu kadhaa kufariki dunia na wengine kujeruhiwa. Sasa tuseme basi na kuepuka ajali za kizembe, inawezekana.Wakuwalaumu katika ajali hizi ni madereva wetu wanaopewa dhamana ya kusafirisha abiria. Nasema kuna kitu, bila kumung’unya maneno niseme ukweli tu kwamba baadhi ya madereva ni walevi.
Hili ninalolisema polisi ni mashahidi kwa sababu baadhi yao wamewahi kuwakamata madereva wa mabasi wakiwa wamelewa na kuwakataza kusafirisha abiria.Zoezi hilo linatakiwa kuwa la kudumu, kwa sababu tunajua wazi kwamba sasa hivi hakuna utaratibu wa vinywaji vikali kuuzwa na kununuliwa kwenye baa, viroba vinauzwa kila mahali, stendi za mabasi ya kwenda mikoani na hata zile stendi za daladala, Bajaj na bodaboda.
Ukweli ni kwamba madereva wa vyombo vya moto baadhi yao wanafanyakazi wakiwa wamelewa.
Ipo haja kwa jeshi la polisi kupitia kikosi chake cha usalama barabarani kuliangalia hili kwa sababu ni wazi kwamba watu wengi wanafariki dunia na wengine kupata vilema vya maisha kutokana na uzembe wa mtu mmoja tu, dereva.

Ipo haja ya kuhakikisha madereva wote wanapimwa ulevi, siyo mwanzo wa safari tu bali hata kwenye vituo vingine njiani kwa sababu baadhi ya madereva hufungasha viroba kwenye mabegi yao na kunywa njiani, hivyo kuhatarisha usalama wa abiria na mali zao.
Lakini pia kuna baadhi ya madereva wa mabasi na malori ambao hawazingatii sheria za usalama barabarani kwa ‘kuovateki’ magari kwenye kona au mlimani, hawa nao ni wazembe na uzembe wao husababisha maafa.
Madereva wote wa aina hii wanapogundulika ni vema serikali ikawafungia kuendesha vyombo vya moto badala ya kuwatoza faini kwa sababu makosa wanayoyafanya ni kisababishi cha vifo kwa watu wasio na hatia.

Nimuombe Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Barabarani Tanzania, DCP Mohamed Mpinga kuwa mkali kwa askari wanaowaachia madereva walevi na wanaokiuka sheria za usalama barabarani.Sipendi kumfundisha kazi lakini ipo haja sasa kuhakikisha yeye mwenyewe na maofisa wa ngazi za juu wa kikosi chake wanafanya ukaguzi wa kushitukiza ili kukomesha uzembe huo.
Yeyote anayezembea katika hili achukuliwe hatua stahiki kwa sababu ambazo nimezitoa hapo juu, hakika tumechoshwa kushuhudia wananchi wasio na hatia wakifariki dunia kwa uzembe wa wachache.
Older Posts
© Copyright ZEE LA UDAKU | Designed By Code Nirvana
Back To Top