Habari Kali
Loading...

UNYAMA...!! IS WAUA RAIA 300 WA YAZIDI NCHINI IRAQ

Raia wa Yazidi waishio nchini Iraq.
KUNDI la wanamgambo wa Islamic State limewaua mateka takribani 300 ambao ni raia wa Yazidi kaskazini mwa Iraq.
Makamu wa rais nchini Iraq, Osama al-Nujifi ameyalaani mauaji hayo akiyataja kuwa ya kikatili.

Taarifa zimeeleza kuwa watu hao waliuawa katika wilaya moja iliyo magharibi mwa mji wa Mosul siku ya Ijumaa.
Wanamgambo wa Islamic State walithibiti maeneo yaliyo kaskazini mwa Iraq kwa karibu mwaka mmoja uliopita ambapo waliwaua na kuwashika mateka maelfu ya watu wa Yazidi wakiwaita makafiri.
Chanzo: BBC

UNYAMA..!! ISIS WAENDELEA KUFANYA MAUAJI YA KUTISHA HUKO SYRIA NA IRAQ..TAZAMA PICHA HAPA

Mpiganaji wa ISIS akinyanyua tofali la zege kumpiga mmoja wa wanaume waliokamatwa kwa kuua wanawake.
Adhabu ya kuwapiga mawe wanaume waliokamatwa kwa mauaji ya wanawake watatu ikiendelea huko Iraq.
Mmoja wa watuhumiwa wa uchawi akiwa tayari kuchinjwa na Kundi la ISIS huko Raqqa, Syria.
Mtuhumiwa mwingine wa uchawi naye akiwa tayari kuchinjwa na ISIS.
Kabla ya kuuawa watuhumiwa hao walisomewa mashtaka yao na mmoja wa wapiganaji wa ISIS.
Picha ya mashoga wawili waliowekwa mitandaoni na Kundi la ISIS kabla ya kuwapia mawe hadi kufa.
Mashoga hao wakipigwa mawe hadi kufa na wapiganaji wa ISIS huko Syria.
WAPIGANAJI wa ISIS wamefanya mauaji ya kutisha kwa mateka wawili wa kiume waliotuhumiwa kuwaua kwa kuwapiga virungu wanawake watatu huko nchini Iraq.
ISIS waliwapiga watuhumiwa hao kwa matofali ya zege kichwani hadi kufa ikiwa ni adhabu kwa kitendo chao cha kuiba na kuwaua wanawake watatu. Tukio hilo limefanyika katika Mkoa wa Nineveh huko kaskazini mwa Iraq.
Katika tukio lingine lililowekwa katika mitandao ya kijamii wiki hii linaonyesha picha za wanaume wawili wengine wakichinjwa na kundi hilo la ISIS katika Kijiji cha Jarnyah, Magharibi mwa Raqqa nchini Syria.
Wanaume hao wanadaiwa kuuawa baada ya kukamatwa wakijihusisha na vitendo vya kishirikina.
Wanaume hao waliokuwa wamefungwa vitambaa usoni wanaonekana wakiwa wameweka vichwa vyao juu ya magogo huku mapanga yakiwa kwenye shingo zao na wananchi wakishuhudia tukio hilo.
Wiki iliyopita, picha za wapiganaji hao wa ISIS wakiwapiga mawe hadi kufa mashoga wawili huko Syria nazo zilionekana kwenye mitandao ya kijamii.
Kabla ya kuwaua mashoga hao, ISIS waliachia picha zilizokuwa zikiwaonyesha mashoga hao wakiwa wamekumbatiana na kuwaambia kuwa wamewasamehe dhambi zao kabla ya kuwapiga kwa mawe hadi kufa.

UNYAMA...!! MUUGUZI AMCHAPA MJAMZITO VIBOKO..NI WAKATI WA UCHUNGU WA KUJIFUNGUA, MTOTO AFIA TUMBONI.

Muuguzi mmoja wa zahanati ya Muungano, Chamwino, mkoani Dodoma, amekumbwa na kashfa nzito baada ya kudaiwa kumchapa viboko mama mjamzito, wakati akiwa katika hali ya uchungu wa kujifungua na kusababisha mtoto aliyetaka kujifungua kufariki akiwa tumboni.

Aidha, mama huyo ambaye kwa sasa amelazwa katika chumba cha uangalizi maalumu (ICU) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, hali yake inaelezwa kuwa mbaya.

Mwanamke huyo, Mariamu Maroda, anadaiwa kulazwa kwenye chumba hicho kwa zaidi ya wiki moja, ambapo pamoja na kufanyiwa upasuaji, hakufanikiwa kupata mtoto wake akiwa hai.

Akisimulia mkasa huo, mama mdogo wa Maroda, Joyce Charles, alisema Aprili 3, mwaka huu Saa 12:00 jioni, walimpeleka zahanati ya Muungano akiwa na dalili za kujifungua na kupokelewa na muuguzi aliyemfahamu kwa jina la Lucy.

“Nilishuhudia Lucy akimchapa Maroda viboko kwenye mapaja na mgongoni, akisema ana uwezo wa kujifungua lakini anadeka tu, nilishindwa kuingilia nikihofia asimdhuru zaidi mwanangu, ila nilihuzunika sana,” alisema.

Alisema muuguzi huyo alitumia fimbo tatu kumchapa mgonjwa wake, ambazo alikuwa akizitumia kila moja inapovunjika. Alisema fimbo hizo zilipomalizika, alianza kumfinya kwenye mapaja kwa kutumia rula.

“Kesho yake saa 12:00 alfajiri, huku hali ya mgonjwa ikiwa mbaya, walitupatia gari likatupeleka hospitali ya Mvumi Misheni, ambako walisema hali aliyokuwa nayo mgonjwa wasingeiweza na kutuelekeza tumpeleke hospitali ya rufaa, lakini walimpa mgonjwa chupa mbili za damu,” alisema.

Alisema Maroda alifikishiwa chumba cha upasuaji na kisha alilazwa wodi namba 17, lakini miguu na tumbo vilianza kuvimba na alipochunguzwa ikabainika ana usaha tumboni, hivyo aliamriwa arudishwe kwenye chumba cha upasuaji.

 “Yaani ukimuona, mwilini ana alama za fimbo na kufinywa. Sasa walipomfanyia upasuaji kwa awamu ya pili, alipelekwa ICU mpaka hivi tunavyozungumza ni zaidi ya wiki moja,” alieleza Charles.

Viongozi wa Hospitali ya Rufaa, wenye mamlaka ya kuzungumzia suala hilo walionekana ‘kurushiana mpira’ walipotakiwa kuelezea suala hilo. Hata hivyo, Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anatoria Mkindo, alikiri kuwepo kwa mgonjwa huyo.

Awali Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Zainab Chaula, alisema hakuwa na taarifa za kina kuhusu Maroda.

Mkindo alisema walikuwa wameagiza Ofisi ya Mganga wa Wilaya wa Chamwino, kuwapelekea taarifa kuhusu suala hilo.

Alisema pia wametaka Ofisi ya Mganga Mkuu wa mkoa, ifahamishwe hatua zilizochukuliwa dhidi ya mtumishi aliyedaiwa kumchapa viboko mjamzito huyo.

“Mimi sio msemaji, anayetakiwa kuwapa taarifa kamili ni RMO (Chaula) kwanini awalete kwangu, nilichowaeleza ni ambacho nafahamu lakini siyo msemaji, nashauri muende ofisini kwa matroni wa hospitali mtapata taarifa kamili,” alisema.

Afisa Muuguzi wa ICU, Christina Mlumba, alisema, Maroda alipelekwa ICU baada ya kufanyiwa upasuaji na kwamba hali yake inaendelea vizuri.

Mdogo wa Maroda, Silika Mkwawi alivieleza vyombo vya habari kuwa ingawa hakuingia kwenye chumba cha kujifungulia katika zahanati ya muungano, dada yake alipotolewa nje, muuguzi alimueleza kuwa alimchapa fimbo mbili tu, kwa sababu ya kudeka kwake.

UKATILI...!! VIDEO: HOUSE GIRL MWINGINE ANASWA AKIMFANYIA UNYAMA MTOTO WA BOSI WAKE!

dsc_9730
Mwaka jana kuna tukio lililoshtua wengi duniani na kuzungumziwa sana kwenye vyombo vya habari kuhusu msichana Jolly Tumuhiirwe wa Uganda, aliyemfanyia ukatili mtoto wa bosi wake Arnella mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu kwa kumpiga vibaya baada ya kukataa kula chakula.
Wakati hilo halijasahaulika tukio linalokaribia kufanana na hilo limetokea tena Kenya.. msichana ambae anafanya kazi za ndani amekutwa akilazimisha kumnyonyesha mtoto wa bosi wake.
Msichana huyo Grace Mwikali Mwema amekutwa akifanya kitendo hicho siku mbili tangu aanze kazi japo jaribio lake halikufanikiwa kwa kuwa mtoto alikataa kunyonya.
Mama wa mtoto huyo amesema aligundua kitendo hicho kutokana na camera aliyoitega nyumbani kwake na akuunganisha na simu yake ya mkononi.
Msichana huyo anashikiliwa na Polisi akisubiri kupandishwa kizimbani.
Hii ni video ambayo inaonesha tukio lote…

UNYAMA...!! MWANZA: MAMA AJIFUNGUA MTOTO, AMTUPA DAMPO! NA KUKIMBIA!

Wakazi wa Mkuyuni jijini Mwanza wakiwa katika eneo alilotupwa mtoto wakisubiri polisi.
Polisi akishirikiana na wananchi kuuchukua mwili wa mtoto huyo katika jalala alipotupwa na mama yake mzazi.
...wakisaidiana kuubeba mwili wa mtoto.
...wakielekea kwenye gari la jeshi la polisi....wakiupakiza mwili kwenye gari la jeshi la polisi.
...wananchi wakitaharuki kutokana na kitendo hicho cha mama kumtupa mwanaye dampo.
Mwili wa mtoto huyo ukiwa kwenye gari la polisi.
...gari la polisi likiondoka katika eneo la tukio.
...wananchi wakisambaa kutoka kwenye eneo la tukio.
Wananchi wakijadiliana baada ya tukio hilo.
Na Johnson James, GPL / Mwanza
MAMA mmoja mkazi wa kata ya Mkuyuni-Sokoni wilayani Nyamagana jijini Mwanza (jina lake halikufahamika mara moja) amejifungua mtoto wa kiume na kisha kumtupa kwenye shimo la kutupa taka (jalala) eneo a Mkuyuni jijini hapa.
Akizungumza na waandishi wa habari, mmoja wa watoa taarifa kwa viongozi wa serikali aliyetoa sharti la kutotajwa jina lake amesema:
“Mimi ni mfanya usafi hapa Mkuyuni, wakati ninaenda kumwaga uchafu pale dampo nikakuta kitoto kichanga kimetupwa maeneo hayo ndipo nilipoenda kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Mkuyuni-Sokoni ili wafanye utaratibu wa kukitoa hapo:”
Naye mwenyekiti wa mtaa wa Mkuyuni, Godwin Peter  Kyangara,  amesema: “Mimi nimeletewa hizi taarifa za mtoto huyu aliyetupwa maeneo haya mida ya saa 2:30  asubuhi, baada ya kupokea taarifa hizo ikabidi nikatoe taarifa kwa Jeshi la Polisi ndipo walipokuja kuuchukua mwili wa mtoto huyo.”
Inasemekana kwamba mtoto huyo alikuwa tayari ana umri wa miezi tisa hivyo mzazi wake alikuwa tayari amejifungua ndipo alipoamua kumtelekeza kwenye shimo hilo la kutupa takataka.
Kwa upande wake, diwani wa kata ya Mkuyuni, Charles Fashion, ameeleza kuwa ameshangazwa na kitendo hicho cha mwanamke kujifungua mtoto na kumtupa jalalani ambapo alisema inabidi atafutwe na apewe adhabu iwe fundisho kwa akina mama wengine wenye tabia kama hizo katika jamii.
Aidha, Jeshi la Polisi jijini Mwanza limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa bado juhudi za kumtafuta mwanamke huyo aliyetenda unyama huo zinaendelea ili afikishwe mahakamani  kujibu mashtaka yanayomkabili.

ATIWA MBARONI BAADA YA KUNASWA AKIFANYA MAPENZI NA MBWA

MbwaSaa chache baada ya kupata stori kutoka Kenya iliyohusiana na mtu mmoja kukamatwa akituhumiwa kumbaka kondoo, mwingine tena ameingia kwenye headline baada ya kukamatwa kwa kosa la kumbaka mbwa.
Hii inatoka Miami, Florida ambapo jamaa mmoja Jonnie Boggess mwenye umri wa miaka 47 alikamatwa na kufunguliwa mashtaka ya ukatili dhidi ya wanyama baada ya kufanya mapenzi na mbwa.
Akijitetea kutokana na kufanya kosa hilo, Boggess amesema alikuwa sahihi kufanya mapenzi na mbwa huyo kwa kuwa mbwa alikuwa amefikia uzito wa kilogramu 19, na alifanya kitendo hicho ‘polepole’ na haikuwa mara kwanza kufanya hivyo kwa kuwa anampenda sana mbwa wake huyo.
Muda mfupi baadaye jamaa huyo alianza kujutia alichokifanya na kudai haikuwa akili yake ila ni kwa sababu ya pombe, kitu ambacho majirani zake walikanusha na kusema kuwa hiyo ilikuwa kawaida ya jamaa kufanya mapenzi na mbwa.

UKATILI...!! MUME AMLIPUA MKEWE KWA PETROLI


Na Igenga Mtatiro, Butiama
Mwanamke mmoja, Kudra Janja  mkazi wa  Kijiji cha Bwai, wilayani Butiama mkoani Mara amelipuliwa kwa petroli na mumewe, Simon Otieno  kwa kile kilichodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.Katika tukio hilo pia mtoto aliyejulikana kwa jina la Tatu Simon (1) alifariki dunia muda mfupi baada ya kuungua kwa moto katika unyama huo uliofanywa na baba yake mzazi.

Habari kutoka katika kijiji hicho zinasema kwamba mume wa mama huyo, Simon aliamua kuwamiminia petroli mke na mtoto wake kupitia dirishani kisha kulipua kwa moto chumba ambacho wawili hao walikuwa wamelala Machi 31, mwaka huu.
Kudra ameungua vibaya mwili mzima na alilazwa katika Hospitali  ya Mara na baadaye kuhamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Mwanza wakati mtoto wake alikutwa ndani ya nyumba hiyo akiwa ameungua vibaya na baadaye kufariki dunia.
Mama mdogo wa Kudra  aliyejitambulisha kwa jina la Bahati Magesa aliliambia gazeti hili kuwa tukio hilo lilitokea nyumbani kwa mjomba wao saa 10 usiku.“Kisa cha tukio hili ni ugomvi wa siku nyingi unaotokana na wivu wa mapenzi kwa watu hawa ambao wameishi pamoja kwa muda wa mwaka mmoja tu,” alisema Bahati.
“Otieno alikuwa akimtuhumu mke wake kwamba alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na watu wengine lakini baadaye ugomvi huo uliisha na wakawa wanaendelea na maisha yao vizuri.“Baada ya tukio hili Kudra ambaye ni mtoto wa dada yangu aliniambia kuwa mumewe aliingia ndani akiwa na dumu la petroli na alipomuuliza la nini alimuambia alale, halimhusu.
“Baadaye alimwaga mafuta dirishani akachukua kibiriti na kutoka nje akawasha na kuacha mlipuko mkubwa na yeye kutokomea kusikojulikana.“Baada ya moto kulipuka, Kudra alipiga yowe ndipo mjomba wake, Obadia Janja alikimbilia na kwenda kumuokoa na akamtoa nje na mtoto wake wakati moto unawaka kwa kasi.
“Mama alikuwa ameungua mwili mzima na mtoto aliungua vibaya sana na baada ya muda mfupi aliaga dunia,” alisema Bahati.Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Philip Kalangi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
 “Tumeanza kumtafuta Simon Otieno ambaye amefanya tukio la kinyama na linapaswa kulaaniwa na kila mmoja. Ninaiomba jamii kuacha kujichukulia sheria mkononi,” alisema Kamanda Kalangi.

UNYAMA..!! MAMA AWAFUNGIA NDANI WATOTO WAKE WATATU KWA MIAKA 10



Ni mambo ya kushangaza sana ambayo yamenaswa na Gazeti la Uwazi  katika Kisiwa cha Mafia Mkoa wa Pwani ambapo mwanamke mmoja aitwaye Mwasiti Ally wa Kijiji cha Kanga, amewafungia wanaye watatu kwa miaka kumi ndani ya chumba kimoja kwa madai kuwa ni wagonjwa wa akili.

Uwazi lilipata habari hizi kupitia kwa watu waishio Mafia na kuamua kufunga safari hadi kisiwani humo kufuatilia tukio hilo la aina yake.
 
Baada ya kufika Mafia mjini, Uwazi liliendelea na safari ya umbali wa kilomita 40 kutoka mjini hadi kwenye kijiji hicho kwa ajili ya kuthibitisha madai hayo ya kushangaza.
 
Kabla ya kuzungumza na mama huyo, Uwazi lilibahatika kuwapata majirani ambapo mmoja wao alisema watoto hao ambao ni baba mmoja, mama mmoja, walianza kuwa katika hali ya kushangaza kiakili mwaka 2001.
 
“Alianza mtoto mmoja ambaye ni wa kwanza kuzaliwa. Cha ajabu, kila mwaka mwingine akafuatia hadi wa tatu. Jambo hilo liliishangaza familia na hata sisi majirani,” alisema jirani mmoja.
 
Naye mama mzazi wa watoto hao akizungumza na Uwazi alisema: “Ni kweli watoto wangu hawa wana matatizo ya akili, hawako sawa. Nateseka nao sana.
  
“Ilikuwa mwaka 2001, binti yangu mkubwa, Muhadia Juma (pichani) ndiye alianza, tukajaribu kumfikisha hospitali lakini hakuwa vizuri.
 
"Mwaka 2002 akafuatia mdogo wake aitwaye Ally Juma. Nikashangaa ni nini? 
  
“Nikiwa nahangaika nao hawa, mwaka 2003 akafuatia mdogo wao, anaitwa Mzee Juma. Nilizidi kuchanganyikiwa kabisa.”

Mwanamke huyo alisema amejaliwa kuzaa watoto saba, watatu ambao wote ni wakubwa ndiyo wamepatwa na matatizo ya akili na wanne ambao ni wadogo wapo sawa na wameolewa wakiendelea na maisha yao ya ndoa.

Akiendelea kuzungumza na Uwazi, mwanamke huyo ambaye ni mjane alisema baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya alianza kutafuta watu wa kumsaidia ambapo alizunguka kwa waganga mbalimbali wa kienyeji akiamini wanaye hao wamerogwa.
 
“Nimehangaika sana ndugu mwandishi lakini kikubwa kwa watoto wangu wana matatizo ya akili hadi hivi sasa nimekwishafika sehemu mbalimbali, ikiwemo Hospitali ya Wilaya ya Mafia lakini hakuna mafanikio,’’ alisema mama huyo.
  
Hata hivyo, aliongeza kusema kuwa tangu mwaka 2003 aliona imeshindikana na watoto hao wanazidi kufanya mambo ya ajabu ikiwemo kuwaogopa watu, kuchekacheka, kula kwa fujo na kutojijali pia kukimbilia eneo la baharini.

Mwasiti alisema muda wote huo alikuwa akiishi nao nyumba moja lakini ilipofika mwaka 2005 aliamua kuomba msaada kwa watu ili wajengewe kijumba chao waweze kuishi humo wenyewe ambapo ilimlazimu awafungie ndani hadi hivi leo.
 
Wote wamebadilika na kuwa na afya mbaya huku kucha za mikononi na miguuni kurefuka sana, nywele zimekua ndefu kiasi cha kutisha na sura zao kuonekana kama za misukule na kuwa kama walemavu wa miguu. Lakini mama mtu anatoa sababu ya kuwafungia:

“Sababu kubwa ya kuwafungia ndani tangu mwaka 2005 ni usalama wao. Niliamini kwa kuwaachia tu wangeweza hata kupotea.
 
“Miezi ya hivi karibuni nilishanga sana kumwona Muhadia ana ujauzito, aliyempa ni Mzee ambaye kidogo bado anajiweza kinguvu."
  

Mama huyo alisema baada ya kubaini Muhadia kupata ujauzito, familia ilijitahidi kuwa naye karibu hadi siku ya kujifungua ambapo alijifungua mtoto wa kiume  na kupewa jina la Hassan Abdallah (Abadallah si baba).

Inadaiwa kuwa, siku ya uchungu wa Muhadia, familia ilishirikiana na uongozi wa kijiji wakafanikiwa kumpeleka katika hospitali ya wilaya ambapo alijifungua salama.Baada ya kujifungua, Muhadia alirudishwa kijijini lakini baada ya siku 21, mtoto Hassan alifariki dunia na kuzikwa kijijini hapo.
 
Naye mjumbe wa mtaa aliyejitambulisha kwa jina la Mzee Seleman alipoulizwa kuhusu hali ya familia hiyo alisema ni kweli mjane huyo amekuwa akiishi na watoto hao kwa shida sana zaidi ya miaka kumi sasa tangu walipoanza kupata matatizo.
  
“Watoto wale wanamsumbua sana mama yao, wamekwisha changiwa fedha kwa ajili ya matibabu ya matatizo waliyonayo lakini hadi leo hakuna mafanikio kama unavyowaona,’’ alisema mjumbe huyo.
 
“Inawezekana wakipata msaada hata kama akili hazitakuwa sawa lakini afya zao zitaimarika kwani kwa sasa kila kitu wanafanyia mlemle ndani, ikiwemo kujisaidia.
  
 “Hakuna mtu mwingine anayeweze kuingia katika chumba walichofungiwa zaidi ya mama yao mzazi tu,” alisema mjumbe huyo.
 
Kwa hali ya familia hiyo, kunatakiwa nia ya makusudi kwa serikali, taasisi na watu binafsi kwenda kutoa elimu za kijamii ikiwemo kuishi na watu wenye ulemavu na kadhalika, kwani inaonekana elimu bado ni tatizo kwa eneo hilo kiasi kwamba, kuwafungia wagonjwa hao ndani haionekani kama ni suala linaloweza kumfikisha mtu kwenye nyombo vya sheria.
 
Ushahidi wa uduni wa elimu unaonekana hata kwenye kujua mambo muhimu. Mfano, mwanamke huyo hajui tarehe, mwezi na mwaka wa kuzaliwa mtoto wake hata mmoja kati ya watoto wote saba!

Chanzo:  Gazeti  la  Uwazi/Gpl

AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 30 JELA BAADA YA KUMBAKA MTOTO WA MIAKA 3

Wilson Saimon ‘Babu Nyemeni’ (21), mkazi wa Kijiji cha Mgeta wilayani Mvomero mkoani Morogoro aliyehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kudaiwa kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka mitatu.
DUSTAN SHEKIDELE-MOROGORO
USHIRIKINA? Katika hali ya kushangaza, Wilson Saimon ‘Babu Nyemeni’ (21), mkazi wa Kijiji cha Mgeta wilayani Mvomero mkoani Morogoro yamemkuta baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kudaiwa kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka mitatu.
Mama wa mtoto aliyebakwa.
Babu Nyemeni anadaiwa kufanya unyama huo mwishoni mwa mwaka jana, nyumbani kwa Angel Bosco ambaye alikuwa amekwenda kuimba kwaya kanisani na kumuacha nyumbani mtoto huyo (jina tunalihifadhi) akiwa na mfanyakazi wake wa ndani.
Wilson Saimon akiwa mikononi mwa Polisi.
Akisoma hukumu ya kesi hiyo katika Mahakama ya Wilaya ya Morogoro, Hakimu Mkazi, Regina Futakamba alisema siku ya tukio mtuhumiwa huyo ambaye ni jirani yake Angel, alimuomba mtoto huyo kwa mfanyakazi wa ndani na kumwambia anakwenda kumnunulia pipi, mfanyakazi alimkubalia ndipo alipokwenda kumbaka kichakani, jambo ambalo mtuhumiwa huyo alilikiri mahakamani.
Alisema mtoto huyo alikutwa katika kichaka kilicho nje kidogo ya kijiji hicho akiwa analia kwa maumivu ndipo walipompeleka kwenye Zahanati ya Mgeta alikobainika alibakwa na kuharibiwa sehemu za siri.
Hakimu Regina alisema kutokana na kosa hilo, mtuhumiwa alitakiwa kufungwa kifungo cha maisha lakini alitoa nafasi kwa mtuhumiwa kujitetea ambapo alijitetea na hakimu kumpunguzia adhabu hiyo kwa kumfunga miaka 30 jela ili iwe fundisho kwa wengine.
Wakizungumzia tukio hilo, baadhi ya wananchi wa Mgeta walilihusishwa tukio hilo na imani za kishirikina kwani walisema walishangazwa na mtuhumiwa kumbaka mtoto mdogo kiasi hicho.
“Mh! Hii nahisi inawezekana kadanganywa na waganga kwamba atembee na mtoto mdogo ndiyo apate utajiri maana haya mambo nayo yapo,” alisema mkazi mmoja wa Kijiji cha Mgeta.

Ukatili: Mwanaume Amwekea Mkewe Gundi ya Super Glue Sehemu za Siri Kufuatia Wivu wa Mapenzi.

Katika hali ya kushangaza mwanaume mmoja amwekea mkewe gundi ya super glue sehemu za siri kufuatia wivu wa mapenzi.
Vitendo vya uzalilishaji na unyanyasaji dhidi ya wanawake vinaendelea kushamili licha ya jitihada zinazoendelewa kufanywa na serikali na umoja wa mataifa kupinga unyanyasaji na ukatili dhidi ya wanawake .

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 40 kujitokeza hadharani siku ya jana na kusema kuwa kamwe hataweza kushiriki tendo la ndoa katika maisha yake baada ya mumewe kumuwekea gundi aina ya super glue mwanamke huyo aliendelea kulalamika kuwa mwanaume huyo aliendelea kufanyia videndo hivyo mara kwa mara,

kila inapofika tarehe 3 mwezi wa 9 huwa anapata maumivu makali anakumbuka unyama aliofanyiwa na muwe wake huyo. aliendelea kueleza kuwa huwa anapata maumivu makali wakati akienda haja dogo. hadi sasa hivi mume wa wanamke huyo hajawahi kukamatwa kwa kitendo hiki alichokifanya amekimbilia sehemu ambayo haijulikani aliko. 
Mwanamke huyo anasema ana hofu endapo mume huyo akirejea tena au wakirudiana tena anaweza akamchinja.

Bonyeza HAPA kuangalia taarifa hiyo ikirepotiwa na kitua cha AZAM TV

UNYAMA..!! AMUUA MKE WAKE KWA KUMKATA NA MAPANGA HUKO SHINYANGA!


Mwanamke mmoja amefariki dunia mkoani Shinyanga, aitwaye Vumilia Kulwa (21) baada ya kuuawa na mumewe akiwa nyumbani kwa wakwe zake.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Shinyanga, Justus Kamungisha, amesema mwanamke huyo mkazi wa kijiji cha Mwongozo kata ya Mwenge tarafa ya Nindo wilayani Shinyanga, ameuawa na mumewe, Singingi Luyengeja (30) baada ya kumkata panga kichwani na kufa papo hapo.
 
Kamanda amesema chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa mapenzi baada ya Luyengeja kusadiki mkewe amekuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine ambaye hajafahamika jina lake wala makazi.
 
Amesema baada ya mauaji hayo yaliyofanyika nyumbani kwa wazazi wa marehemu, mtuhumiwa ametoroka kusikojulikana na polisi wanaendelea kumtafuta.
 
Kamugisha amesema mwanaume huyo akipatikana atafikishwa katika vyombo vya sheria ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.

BABA ATIWA MBARONI KWA KUWABAKA WATOTO WAKE!

Rahma Mashamu ambaye ni mama mzazi wa watoto wawili mmoja wa miaka 11 na mwingine 15 wanaodaiwa kubakwa na baba wa watoto hao akilia kwa uchungu wakati akihojiwa na waandishi wa habari kuhusiana na tukio hilo, wilayani Kibaha mkoani Pwani.
-------
Mkazi mmoja wa Miembe Saba wilayani Kibaha mkoani Pwani amekamatwa na polisi akituhumiwa kuwabaka watoto wake wawili wadogo kwa zaidi ya miaka miwili sasa.
 
Habari zilizotufikia, zilisema kuwa katika tukio hilo ambalo limethibitishwa na polisi na watoto wenyewe, baba huyo alianza kuwafanyia binti zake vitendo hivyo mwaka 2013 kwa siku ambazo mkewe ambaye nimama wa wasichana hao hakuwapo hadi usiku wa Machi 19, mwaka huu. Kwa sasa tunayahifadhi majina ya familia hiyo.
 
Watoto hao mmoja mwenye umri wa miaka 15 anayesoma darasa la saba na mdogo wake mwenye umri wa miaka 11 aliyeanza kubakwa akiwa darasa la tatu.
 
Kwa mujibu wa watoto hao, baba huyo alikuwa anamuita mmoja wa watoto wake chumbani kwake na kumtaka alale na mdogo wao wa kiume wakati huo akiwa na mwaka mmoja na binti akipitiwa na usingizi humvua nguo za ndani na kumwingilia huku akimtaka kukaa kimya na kuvumilia maumivu.
 
Mke wa mtuhumiwa huyo, ambaye amekuwa akizimia mara kwa mara kutokana na kulia baada ya kubaini mchezo huo, alisema aligundua watoto wake wanabakwa Ijumaa iliyopita baada ya mmoja wa mabinti zake hao kumweleza kuwa baba yake alikuwa amembaka Machi 19, mwaka huu.
 
Alisema kabla ya binti huyo kumweleza hivyo, alimwomba asimpige kwani kuna kitu anataka amweleze, japo ni kibaya lakini yeye amechoshwa na kimekuwa kikimuumiza kichwa.
 
“Alisema kila ninapokwenda katika biashara zangu, anatamani nisiwe ninawaacha hapo, nikamwahidi sitamfanya kitu ili mradi aseme ukweli tu,” alisema mama huyo.
 
Baada ya kuhakikishiwa kulindwa, ndipo binti huyo aliposimulia jinsi ambavyo baba yake amekuwa akiwafanyia na kuwatishia wakipiga kelele atawaua.
 
“Niliposikia mwili ulisisimka na ghafla binti yangu mwingine naye akatokea akilia na kuniambia, ‘hata mimi baba ananifanyiaga hivyohivyo kila siku unapokuwa umepeleka mboga sokoni Kariakoo,”alisema mama huyo.
 
Mwanamke huyo ameomba sheria ichukue nafasi yake katika tukio hilo kwa kuwa ni la kinyama na pia wataalamu wa saikolojia wamsaidie binti yake mdogo wa darasa la tano kwani yeye ameathirika zaidi.
 
Daktari aliyewapima watoto hao, ameshauri binti huyo mdogo apate ushauri zaidi ili kurudisha akili yake katika hali ya kawaida.

Simulizi za watoto
Wakizungumza nyumbani kwao jana watoto hao, walisema baba yao alikuwa akiwatishia kuwakatakata kwa panga au kuwakaba koo humohumo chumbani endapo wangethubutu kumweleza mtu yeyote kitendo wanachokifanya.
 
“Tulikuwa tumeingia kwetu kulala na wadogo zangu, nikasikia ananiita nikambembeleze mtoto eti anamsumbua, nilikwenda nikambembeleza  akalala, wakati nashuka kitandani kurudi chumbani kwetu baba akanivuta kwake akanivua, akasema anachokifanya ni suna kwa hiyo hataki kelele, akisikia atanikaba nife.”
 
“Niliumia sana na asubuhi mama alirudi nikajitahidi kweli asijue na hata shule sikwenda, jioni mama aliondoka tena baba hakuniita siku hiyo lakini baada ya siku tatu aliniita tena ikawa vilevile navumilia. Siku zilivyozidi unaweza kukuta kwa wiki naitwa hata mara nne siku ambazo mama hayupo nyumbani,” alisema.
 
Watoto hao walieleza kuwa baadaye baba huyo alihamia kwa binti mdogo kwa staili ileile na kila mmoja alikuwa akiitwa kwa zamu na kwa vile kila mmoja alijua ni siri yake na baba.

Kutonaka na woga wa kuuawa, hakuna aliyemweleza mwenzake hadi katikati ya mwaka jana mmoja wao alipomweleza mwenzake na baadaye kumweleza mama yao.
 
“Baba alikuwa anasema atatuua bila hata mtu kujua na tutaozea shambani, hata nikiwa katika siku zangu baba ananiingilia hivyohivyo, naugua kila mara UTI, mdogo wangu naye kila mara UTI, tukaamua liwalo na liwe kama kufa basi ila mama ajue,” alisema mtoto huyo huku akibubujikwa na machozi.
 
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Miembe Saba, Hamis Shomari alisema kabla ya kupelekwa kituo cha polisi Kongowe Jumamosi iliyopita, watoto hao waliitwa shuleni hapo na kuhojiwa kila mmoja peke yake na wote walikiri kuanza kubakwa mwaka 2013 na baba yao na kwamba tabia hiyo iliendelea hadi Machi 19 usiku alipobakwa binti mdogo kwa mara ya mwisho na Machi 20 walipoamua kumweleza mama yao.
 
Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Ulrich Matei alisema wanamshikilia mtuhumiwa huyo na kwamba wasichana hao wamefanyiwa vipimo mbalimbali na majibu ya daktari yamethibitisha kuwa wamebakwa na sehemu zao za siri  zimeharibiwa, hivyo wanaendelea na matibabu.

Credit:  Mwananchi

Mbaroni kwa kukutwa na Viungo na Mifupa ya Albino!


WATU wawili wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Kagera kwa kosa la kukutwa na viungo mbalimbali vya mwili ikiwemo mifupa mitatu ya mtu mwenye ulemavu wa ngozi (albino).
 
Kamanda wa Polisi mkoani Kagera Henry Mwaibambe alisema kuwa tukio hilo limetokea juzi katika kijiji cha Kyota kata ya Kimwani wilayani Muleba mkoani humo baada ya jeshi hilo kuweka mtego kwa watuhumiwa hao ambao walikuwa wanatafuta wateja wa viungo hivyo.
 
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni James Rutozi (66) mkazi wa Kimwani ambaye ndiye aliyekuwa anahifadhi viungo hivyo na Emanueli Kaloli (50) ambaye pia ni mkazi wa Kimwani aliyekuwa anatafuta mteja wa viungo hivyo.
 
Alisema mara baada ya kupata taarifa kuwa kuna watu wanauza viungo hivyo kwa Sh milioni 3 waliweka pesa za mitego na kujifanya wao ni wateja na ndipo walipowakamata watuhumiwa hao wawili ambao walikutwa na mfupa mmoja na walipowabana zaidi ndipo walitoa mifupa miwili.
 
Alisema mnamo mwaka 2006 katika kijiji cha Rushwa kata ya Mushabago wilayani Muleba, Zeulia Jestus akiwa na miaka 24 mwenye ulemavu wa ngozi (albino) alifariki dunia muda mfupi baada ya kujifungua na ndipo watuhumiwa hao walifukua kaburi hilo mwaka 2008 kwa maelekezo ya mganga wa jadi.
 
Alisema pia walipotaka kujiridhisha jeshi hilo liliomba kibali mahakamani ili kufukua kaburi hilo mnamo Machi 23, mwaka huu lilipofukuliwa liligundulika kuwa viungo hivyo vimetolewa katika mwili wa marehemu huyo.
 
Aidha, jeshi hilo linamtafuta mganga wa jadi aitwaye Mutalemwa Revocatus ambaye ametoroka kabla hajakamatwa ambaye ndiye aliyewashawishi wafukue hilo kaburi na kuwapa dawa ya kinga ili wasidhurike wakati wanafukua.
 
Aliongeza kuwa mnamo mwaka 2008 wananchi wa kata hiyo ya Mushabago walitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi kuwa kaburi alilozikwa marehemu Zeulia lilifukuliwa na watu wasiojulikana baada ya kugundua tukio hilo.

Mwanaume wa Miaka 45 Ahukumiwa kifungo cha maisha Jela kwa kosa la Kumbaka Mtoto wa Miaka Minne


Mwanaume mmoja Yusufu Chatambala (45) mkazi wa Kijiji cha Makutupa Kata ya Lupeta Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma, amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kukiri kosa la kumbaka mtoto mdogo mwenye umri wa miaka minne.
 
Mwendesha mashtaka wa polisi Godwill Ikema ameiambia mahakama ya Wilaya ya Mpwapwa kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Feb 20 mwaka huu majira ya saa 12 jioni katika kijiji cha Makutupa kilichopo Wilayani Mpwapwa ambapo alimbaka mtoto mdogo wa kike mwenye umri wa miaka minne (jina limehifadhiwa).
 
Mwendesha mashtaka huyo amesema kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo kinyume cha sheria za nchi chini ya Kifungu namba 130 (1) 2 (a) na 131 (1) cha Kanuni ya Adhabu kama kilivyofanyiwa mapitio mwaka 2002.
 
Amesema kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo baada ya kumkamata alipokuwa akicheza na watoto wenzake jirani na nyumbani kwao kisha kumpeleka kwenye shamba la mahindi kisha kumbaka mtoto huyo na kusababishia majeraha na maumivu makali.
 
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpwapwa Paschal Mayumba alimtia hatiani mtuhumiwa huyo jana baada ya kukiri kutenda kosa hilo.
 
Akisoma hukumu hiyo, hakimu Mayumba amesema Mahakama inamhukumu kwenda jela kifungo cha maisha kwa kosa la kubaka mtoto ili iwe fundisho kwake na kwa wengine wanaotenda makosa kama hayo.

Mume Ajinyonga kwa kamba ya katani hadi kufa baada ya KUMUUA Mkewe kwa kumchinja Shingo..

MWANAMUME mwenye umri wa miaka 30 amejinyonga kwa kamba ya katani hadi kufa baada ya kumuua mkewe kwa kumchinja shingo kwa kisu kutokana na kile alichodai kuwa ni kudharauliwa na mkewe. 
 
Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela ambaye amemtaja mwanamume huyo kuwa ni Ramadhani Abdallah, mkulima na mkazi wa kijiji cha Makale katika kata ya Mitundu, tarafa ya Itigi wilayani Manyoni anayedaiwa kumuua mkewe, Amina Waziri (30).
 
Katika tukio hilo la Oktoba 20 saa 9.15 alasiri, Kamanda Kamwela alidai kuwa Ramadhani baada ya kuhakikisha kuwa mke wake amekufa, alichukua kamba ya katani na kujitundika kwenye moja ya kenchi ya nyumba yao na kujinyonga hadi kufa.
 

“Kabla ya kujinyonga, Ramadhani aliacha ujumbe mfupi usemao kuwa amechukua hatua hiyo ya kukatisha maisha yake na mke wake kutokana na mkewe huyo kushirikiana na kaka zake kumuoza binti yake wa kufikia bila ridhaa yake,” alisema Kamanda Kamwela.

UNYAMA! WAZAZI SOMENI HABARI HII YA KUSIKITISHA HAUSIGELI ALIVYOMFANYIA MTOTO

Unyama! Dada wa kazi (hausigeli), aliyetajwa kwa jina moja la Rachel, mkazi wa Tabata-Shule jijini Dar, anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuchukua kisu jikoni kisha kumchomachoma nacho mtoto, Samwel John (4) anayeishi nyumba ya jirani.
Mtoto, Samwel John akiwa na maumivu makali aliyoyapata baada ya kujeruhiwa kwa kisu.
Akizungumzia mkasa huo kwa masikitiko makubwa uliojiri hivi karibuni maeneo hayo, baba mzazi wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la John alisema kuwa, siku ya tukio hilo alimuona hausigeli huyo akiwa amemshika mkono mwanaye huku akiwa na majeraha kwenye jicho na kichwani.
Alisema alipomuuliza nini kimetokea, hausigeli huyo alimjibu kuwa mtoto Samwel aligongwa na pikipiki.
John alisema kwamba, hausigeli huyo alimwambia kuwa mtoto alikuwa amegongwa na pikipiki lakini mtoto alikataa huku akimnyooshea kidole yule dada wa kazi.
Baadhi ya majeraha ya kichwani aliyoyapata mtoto John.
“Nilikuwa nashangaa maana kila hausigeli huyo akizungumza kuwa mtoto amegongwa na pikipiki, mwanangu alikuwa akimnyooshea kidole na kusema kuwa yeye ndiye amemuumiza,” alisema mzazi huyo.
Mzazi huyo aliendelea kusema kwamba, baada ya kuona hivyo alimshika mkono mwanaye hadi kwenye nyumba ambayo anafanya kazi msichana huyo huku mtoto huyo akimuongoza chooni ambapo alikuta damu nyingi zimetapakaa.
Alisema kuwa alipoona hivyo ilibidi amchukue mwanaye na msichana huyo hadi polisi kwa ajili ya kupata PF-3 kwa ajili ya matibabu.Kwa upande wake hausigeli alipoulizwa ni kwa nini alifanya kitendo cha kinyama kiasi hicho alisema kuwa alikuwa akitamani kumtoa jicho mtoto huyo.
Wananchi wakishangaa unyama alioufanya hausigeli huyo.
“Alisema kuna shetani au roho ilikuwa ikimtuma amng’oe macho mwanangu,” alisema baba huyo.
Baada ya kujieleza, hausigeli huyo alitupwa korokoroni nyuma ya nondo za mahabusu kwa kitendo alichokifanya ambapo hadi gazeti hili linaanua jamvi maeneo hayo alikuwa kwenye Kituo cha Polisi cha Tabata akisubiri sheria ichukue mkondo wake.

UNYAMA..!! Video: Ampiga mawe binti yake hadi kufa kwa kosa la kufanya mapenzi kabla ya ndoa!!



Mfuasi mmoja wa kundi la ISIS la Syria ameungana na wanajeshi kadhaa wa kundi hilo kufanya mauaji ya kinyama kwa kumpiga mawe binti yake wa kumzaa hadi kufa baada ya kugundulika kuwa alizini.
 
Kundi la ISIS limeachia video inayoonesha tukio hilo la kusikitisha linaloelezwa kufanyika katika jiji la Hama nchini Syria.
 
Katika video hiyo iliyoripotiwa pia na mtandao wa Mirror wa Uingereza, msichana huyo anaonekana mnyonge akimuomba msamaha baba yake, “tafadhali baba….nisamehe.” Lakini baba yake anasikika akisema, “mimi sio baba yako tena.”
 
Aliongeza kuwa anatumaini adhabu anayompa binti yake itakuwa fundisho kwa wanawake wengine.
 
Baba huyo alioenekana akiwageukia wapiganaji wa ISIS na kuwapa ishara kuwa adhabu ianze, na mwisho yeye anaonekana akiwa na jiwe kubwa zaidi lililoutoa uhai wa binti yake.

Unataka  kuiona  Video? Inatisha  lakini, itazame  hapo  chini.

Older Posts
© Copyright ZEE LA UDAKU | Designed By Code Nirvana
Back To Top