MCHUNGAJI Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, jana amehojiwa kwa saa tano na kutoka katika Kituo Kikuu cha Polisi, Dar akiwa chapachapa kwa jasho ndani ya koti kufuatia yale madai ya kumtolea maneno yenye kuudhi, Askofu wa Kanisa la Romani Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo.
Awali Gwajima aliwasili kituoni hapo saa 1:15 asubuhi akiwa ameongozana na baadhi ya wachungaji wake bila mwanasheria wake, John Mallya ambaye alifika baadaye.
Gwajima aliingia moja kwa moja lango kuu la kituo hicho na kuingizwa kwenye chumba maalum ambacho Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Suleiman Kova hukitumia kuzungumza na waandishi wa habari.
WAUMINI WAWASILI
Wakati Gwajima akianza kuhojiwa maswali ambayo yalidaiwa ni nje ya matarajio, baadhi ya waumini wake nao waliwasili na kusimama jirani na kituo hicho huku wakikutana na onyo kali ya askari kwamba, hawatakiwi kufika kwenye kituo kabisa.
ULINZI MKALI
Maafande wa kituo hicho waliovalia sare na wale wa jiji wakiwa na bunduki waliweka uzio kwa kusimama mbele ya kituo wakiwaangalia waumini wa Gwajima ambao muda mwingi walionekana kuwa watulivu na kusali chini kwa chini.
MWANAMKE WA AJABU AIBU
Wakati, mapaparazi na watu wengine wakiendelea kusubiri nje, ghafla aliibuka mwanamke mmoja aliyekuwa amevaa gauni jeupe akiwa na mtoto mgongoni. Mkononi alishika kipaza sauti.
Mwanamke huyo alianza kusema maneno yanayohusiana na kuwataka watu kuondoka eneo hilo na kurudi kanisani huku watu wakijiuliza alitumwa na nani kutoa agizo hilo.
Uwazi Mizengwe liliwauliza baadhi ya waumini kama wanamtambua mwanamke huyo ambapo karibu wote walikana siyo mwenzao.
WAUMINI WAONDOKA
Hata hivyo, baadaye, mmoja wa wachungaji wa kanisa la Gwajima aliwataka waumini hao kuondoka eneo hilo la kituo na kuelekea kanisani, Kawe, Dar na mambo mengine wangejulishwa huko.
GWAJIMA ATOKA AKIWA AMESHIKWA
Saa 6: 47, Gwajima alitoka ndani ya kituo hicho akiwa na wachungaji wake na mwanasheria. Gwajima alishikwa mkono na mchungaji mmoja huku akionekana kutembea kwa shida kidogo, jasho likimchirikiza.
“Kwa muda aliokaa mle ndani ilikuwa ni lazima kile kijasho kimtoke, ni lazima atakuwa amebanwa kwa maswali mengi na magumu,” alisikika akisema mmoja wa waumini aliyekuwa eneo hilo.
ALICHOKISEMA KWA WAANDISHI
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kilichojiri chumba cha mahojiano, Gwajima alisema:
“Mahojiano yalikuwa mazuri na mengi zaidi mwanasheria wangu atazungumza na nyie.”
MWANASHERIA SASA
Mwanasheria wake alipotegeshewa vipaza sauti vya vyombo mbalimbali vya habari alikuwa na haya ya kusema:
“Kwa ujumla maswali mengi yalikuwa nje ya suala la Pengo. Amehojiwa maswali mengi yakiwemo ndugu zake waliokufa na walio hai, wanaofanya kazi na wasiofanya kazi na wazazi wake.
“Tumetakiwa kurudi tena Aprili 16, mwaka huu pamoja na vielelezo kumi. Vielelezo hivyo ni hati ya usajili wa kanisa, majina ya bodi ya kanisa, majina ya wadhamini, muundo wa kanisa, waraka wa maaskofu, nyaraka za helikopta, mali na nyumba.
“Pia tumetakiwa siku hiyo kuja na returns za kanisa (mrejesho wa uendeshaji wa kanisa), idadi ya matawi ya makanisa kwa nchi nzima pamoja na mpigapicha wake wa video.”
MASWALI NJE YA ASKOFU PENGO
Hata hivyo, mwanasheria huyo alisema kuwa, anakusudia kesi hiyo itakapofika mahakamani atapinga mteja wake kuulizwa maswali nje ya madai ya awali ya kumkashifu Askofu Pengo.
Baada ya Gwajima na watu wake kuondoka, Uwazi Mizengwe lilikwenda kanisani Kawe ambapo liliwakuta waumini wachache wakiwa hawajui kinachoendelea.
Hizi ndio sehemu 12 zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, Bonyeza Hapa chini== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO CHAFU YA AGNESS MASOGANGE== >