Habari Kali
Loading...

INASIKITISHA SANA...!! BASI LA MORO BEST LAUA 17

Mbinu Za Kumfikisha Kileleni Mwanamke Mwenye Makalio Makubwa Kwa Haraka, Bonyeza Hapa chini== >

WATU 17 wamefariki dunia na wengine 56 kujeruhiwa baada ya Basi la Kampuni ya Moro Best, kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa limebeba mabomba makubwa yaliyokuwa yakisafirishwa kwenda nje ya nchi.

Akizungumza na Majira kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, David Misime, alisema ajali hiyo ilitokea jana saa 2 asubuhi katika Kijiji cha Panda Mbili, Wilaya ya Kongwa, kilometa 100 kutoka Dodoma Mjini.

 

Alisema ajali hiyo ilihusisha basi lenye namba T 258 ARV ambalo lilikuwa likitoka Mpwawa kwenda Dar es Salaam na lori lenye namba T 820 CKU na tela lake namba T 390 CKG, ambalo lilikuwa likitoka Dar es Salaam kwenda Dodoma.

“Dereva wa lori Gilbert Nemanya alitaka kulipita gari lingine ndipo akakutana na basi hilo uso kwa uso hivyo mabomba yalifyatuka na kuanza kuwadondokea abiria baada ya ajali,” alisema.

Kamanda Misime alisema dereva wa basi hilo Said Lusogo na kondakta wake Omari Mkubwa walifariki papo hapo na dereva wa lori, Nemanya na tandiboi wake Mikidadi Zuberi nao walifariki papo hapo.

“Kati ya watu 17 waliokufa, wanaume 12 na wanawake 5... idadi ya vifo inaweza kuongezeka kutokana na baadhi ya majeruhi kuwa na hali mbaya wakiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Mkoa na wengine Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa,” alisema.

Alisema hadi jana, tayari maiti 11 zimetambuliwa na ndugu zao ambapo taratibu zingine za kuitambua miili mingine zinaendelea.

Kamanda Misime aliyataja majina ya marehemu waliotambuliwa kuwa ni Melina Maliseli, Christina (jina moja), Wilson Suda, Mark Massawe, Gabriel Mejachiwipe na Justine Makasi ambao wote wakazi wa Mpwapwa.

Wengine ni Nassib (jina moja) mkazi wa Kongwa, Omar Mkubwa (kondakta wa basi) na utingo wa lori hilo aliyefahamika kwa jina la Mikidadi Zuberi.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Ezekiel Mpuya alisema hadi jana mchana, hospitali hiyo ilikuwa imepokea majeruhi 21 kati yao wawili walifariki baada ya kufikishwa hospitalini hapo.

“Majeruhi waliobaki ni 19 lakini wawili hali zao sio nzuri,”alisema Dkt. Mpuya ambapo mmoja wa abiria aliyenusurika kifo katika ajali hiyo, aliyejitambulisha kwa jina moja la Mohamed, alilalamikia mwendo kasi wa dereva wa basi.

“Hili basi lina tabia ya kufukuzana na basi la Kampuni ya Al-Seidy linalokwenda Mpwapwa likitokea Dar es Salaam lakini kwa leo (jana),

Al-Saedy liliondoka saa 12 alfajiri na hili la kwetu liliondoka saa 12:10 wakati ajali inatokea, mimi sikusikia kitu badala yake nimejikuta nipo hospitali,” alisema Mohamed.

Kamanda Misime aliwaonya baadhi ya madereva wenye tabia ya kuyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari na kusababisha vifo na vilema vya abiria wasio na hatia kutokana na uzembe.

“Si jambo jema kwa dereva ambaye anajua yupo makini kulipita gari lingine bila kuchukua tahadhari...huku ni kuendelea kukaidi sheria za usalama barabarni na kusababisha vifo vya wananchi kwa uzembe,” alisema.

-MAJIRA

Hizi ndio sehemu 12 zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, Bonyeza Hapa chini== >


Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO CHAFU YA AGNESS MASOGANGE== >

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Newer Posts Older Posts
© Copyright ZEE LA UDAKU | Designed By Code Nirvana
Back To Top