Rais Jakaya Kikwete ametoa hati za uraia wa Tanzania kwa wakimbizi 162,156 kutoka nchi jirani ya Burundi na ambao wameishi nchini kwa miaka 42, tangu mwaka 1972.
Alitoa
hati hizo juzi mjini Tabora, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi ya
siku mbili kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo.
Kikwete
alitoa hati hizo kwa wakimbizi 19 kwa niaba ya wenzao katika shughuli
iliyohudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mathias Chikawe.
Wengine
waliohudhuria ni Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wakimbizi
nchini na Mabalozi wa Uingereza, Canada, Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya,
Ireland,Ubelgiji na Mwakilishi wa Ubalozi wa Japan pamoja na Askofu
Mkuu, Jimbo Kuu, Kanisa Katoliki la Tabora, Paul Ruzoka wa Jimbo Kuu la
Kanisa Katoliki la Tabora..
Shughuli
hiyo ilikamilisha mchakato ulioanzishwa na Rais Kikwete mwaka 2007
wakati alipoamua kuwapa wakimbizi hao wa Burundi uraia wa Tanzania baada
ya kuwa wameishi nchini kama wakimbizi tangu walipoingia kwa mara ya
kwanza mwaka 1972 kutokana na machafuko katika Burundi. Wameishi katika
kambi za ukimbizi katika Wilaya ya Kaliua, Mkoa wa Tabora.
Akizungumza
katika shughuli hiyo, Mwakilishi wa UNHCR katika Tanzania, Joyce
Mends-Cole alisema Tanzania imekuwa nchi ya kwanza katika historia ya
dunia kwa kutoa uraia kwa watu wengi kiasi hicho na kwa wakati mmoja.
Naye
Balozi wa Ireland nchini, Fionnula Gilsenan, akizungumza kwa niaba ya
Mabalozi wenzake aliisifu Tanzania na kumpongeza Rais Kikwete kwa uamuzi
wa kutoa uraia na hati za uraia akisema; “kitendo hiki ni kikubwa na
kizuri sana.
“Mheshimiwa
Rais umefanya kitu kikubwa mno. Hili ni jambo kubwa na wewe mwenyewe
umeshuhudia furaha ya watu hawa. Umesikia nyimbo zao za shukurani kwako
na kwa serikali.”
Akizungumza
na raia hao wapya wa Tanzania, Rais Kikwete alisema kuwa matarajio yake
na yale ya Watanzania ni kuwaomba raia wapya ni kuwaona wakitimiza
ahadi yao kwa nchi yao kwa kuwa raia wapya.
“Shughuli
hii ni kutimiza tu mchakato kwa sababu hili la uraia wenu tulilimaliza
siku nyingi. Matarajio yangu na yale ya Watanzania wenzenu ni nyie
kutimiza ahadi ya kiapo chenu cha kuwa raia wema wa nchi yenu.
Heshimuni kiapo chenu.”
Hizi ndio sehemu 12 zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, Bonyeza Hapa chini== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO CHAFU YA AGNESS MASOGANGE== >